SoC02 Uvumilivu ni silaha ya mafanikio katika maisha

Stories of Change - 2022 Competition

Godwin Nyalusi

New Member
Mar 26, 2021
4
2
Habari wanajamii. Natumaini nyote mu wazima.

Kwa majina naitwa Godwin Nyalusi.

Leo hii nimechukua hii fursa na nafasi niliyoipata kuwajuza na kuwashirikisha kile nilicho nacho.

Ni maisha yangu ya kweli kabisa na wala sio stori ya kutunga au kubuni.

Godwin ni kijana aliyezaliwa mnamo tarehe 12/08/1998 katika hospitali ya Agakhan jijini Daresalaam.

Maisha yake ya shule ya msingi
Kwa baraka za Mwenyezi Mungu kijana huyu alizaliwa akiwa na uwezo mkubwa kiakili hasa katika ukuaji wake,
alianza kujua kusoma na kuandika kipindi akiwa na umri wa miaka mitatu (3) ,alipofikisha umri wa miaka mitano(5), alipelekwa shule ili kuanza darasa la kwanza ila suala hilo halikuwezekana kutokana walimu walihitaji mtoto huyu kuanza na elimu ya awali yaani chekechea.

Kutokana na uwezo wake kiakili alipendwa sana na Walimu katiika shule ya msingi Kipunguni B , mnamo darasa la tatu alihamishwa shule na kupelekwa katika shule ya msingi Juhudi.

Kipindi mtoto huyu anasoma shule ya msingi Juhudi alianza kukutana na changamoto kuanzia hapo, shule ya msingi Juhudi imeambatana na shule mbili yaani Ukonga Jeika na Ukonga, shule hizi kwa kipindi hicho zilisifika kwa sifa mbaya hadi kutangazwa maredioni, kwa mfano wanafunzi wa kiume kulawitiana na kulawitiwa, watoto wa kike kubakwa n.k.

Mtoto huyu ilifika siku ,alipata shida ya tumbo la kuhara ,akawa kwa bahati mbaya anajichafua kwenye bukta yake, kwa kuwa mama yake alimpenda sana mtoto huyu basi alikuwa ana mtindo wa kumfulia nguo mtoto huyu.

Katika kufua mama wa mtoto huyu alikuta hilo suala la mtoto wake kujichafua kwenye bukta yake ,yaani alikuta kinyesi kwenye bukta za mtoto wake, basi kwakuwa mama alimpenda mtoto akapatwa na wasiwasi ukilinganisha na taarifa za ile shule, kama nilivyowaeleza hapo juu.

Mama alichukua jukumu la kwenda shuleni kwa mtoto huyu na kuwaeleza walimu, moja kwa moja kama mnavyowajua Walimu hawakuchelewa. Godwin aliitwa na kuanza kuhojiwa kwa ukali ,kutokana na ukali mtoto alishindwa kujitetea vya kutosha ,na vile walimu wakiona mzazi basi hapo mtoto anaweza pewa sifa hata ambazo sio zake.

Kwa ukali na kipigo cha fimbo za kutosha, ilimlazimu Godwin kukubali kuwa alilawitiwa na wenzake tena kwakuwa alikuwa akilazimishwa sana kwa fimbo ilibidi ajitetee kwa kuwataja marafiki zake wa karibu tena wale alikokuwa anaongoza nao akirudi nyumbani.

Mtoto huyu alifanya hivyo ili kuepuka fimbo, bila kujua ilikuwa ni aibu aliyoishi nayo siku zote hapo shuleni.

Toka siku hiyo Godwin alianza kuishi maisha ya peke yake maana marafiki zake walimtenga, alishuka kiuwezo kutoka darasa la tatu mpaka alipofika darasa la saba ndipo kidogo alianza kukaa vizuri kielimu.

Kiukweli hakulawitiwa lakini ilimbidi akubali, siku hiyo kwa mtoto Godwin ilikuwa si nzuri kabisa kwanza alipoteza marafiki zake, alipata aibu, alipata kipigo kizito kwa walimu na vilevile alipata kipigo kizito kwa baba yake alivyorudi nyumbani kwa kosa lisilokuwa la kweli.

kila alipopita Godwin alizungumziwa vibaya na wenzake pamoja na walimu pia akawa sio Godwin yule aliyependwa tena ,bali akawa wa kutengwa na kusemwa kila akionekana,aliishi maisha ya shida kidogo.

Alipofika darasa la saba(7), Mungu sio Athumani, Godwin alirudi katika ubora wake tena akawa anategemewa darasa alilokuwa anasoma hasa katika somo la sayansi na hisabati. Walimu wake walianza kumkubali tena akawa anazidi kuonyesha maendeleo mazuri darasani.

Mama yake kama kawaida alikuwa anampenda sana alipokuja kuulizia matokeo na maendeleo ya mwanawe basi alikutana na misifa kedekede ambayo alikuwa akiisikia wakati mtoto wake yupo shule aliyohamaga yaani shule ya msingi Kipunguni B.

Darasa la saba alifaulu vizuri na akachaguliwa shule ya kuendelea na kidato cha kwanza. Alifanya usahili katika shule nne na zote alifaulu yaani shule ya sekondari Airwing, St.a Anthony,Royols na Visiga..


Maisha yake ya sekondari
Godwin alisoma shule ya sekondari St. Anthony Mbagala.

Maisha yake ya elimu ya sekondari yalikuwa mazuri yasiyokuwa na changamoto zozte zile, alikuwa akifanya masomo yake vizuri na kupendwa na Walimu hata na wanafuzni wake lakini kutokana na lile tukio la shule ya msingi lilikuwa likimuadhiri katika maisha yake yote hata hadi alipokuwa kidato cha kwanza hadi cha nne.

Godwin alikuwa sio mtu wa kujichanganya na wanafunzi wengine kivile, hata marafiki hakuwa nao wengi zaidi ya wale aliosoma nao. Aliishi hivyo kutoka kidato cha kwanza hadi cha nne.

Ukimuona utasema kuwa haongei na ni mpole saana,lakini hali yote hiyo ilitokana na tukio lililomtokea wakati akiwa shule ya msingi.
Alimaliza elimu yake ya sekondari yaani kidato cha nne mwaka 2014, kwa baraka za mwenyezi Mungu alifaulu kidato cha nne..

Baada ya kumaliza kidato cha nne, kidato cha tano alichaguliwa kusoma katika shule ya sekondari MIlambo boys huko mkoani Tabora,alipangiwa mchepuo wa lugha yaani KLF(KISWAHILI,KINGEREZA na KIFARANSA).

Kutokana na alipenda masomo ya sayansi tangu akiwa mdogo, alibadili mchepuo na khamia sayansi yaani PcB(PHYSICS,CHEMISTRY na BIOLOGY).

Kwa bahati mbaya Godwin aliumwa ghafla ugonjwa wa sitifahamu yaani haikujulikana nini hasa kinamsumbua. Ugonjwa huo ulimpelekea hadi kuamishwa shule kutoka shule ya sekondari Milambo boys na kuhamia shule ya sekondari Tambaza. Ugonjwa ulimfanya hadi kupoteza kumbukumbu kabisa lakini haukumsababisha Godwin kuacha shule aliendelea kusoma hivyo hivyo. Ilifikia hatua Godwin kupata sifuri kwenye masomo yake.

Hakika ni jambo lililompa shida na maswali mengi kichwani mwake,wazazi wake walihangaika sana.
Ilifikia kipindi watu walianza kusema yao kama kawaida yao kuwa Godwin amelogwa na mama yake mzazi lakini kwa miujiza Godwin hakuwahi kuweka kichwani maneno yote

Alisoma kidato cha tano mara ya kwanza, alipoona hayupo vizuri akaomba uonogozi wa shule arudie tena kidato cha tano. Hakika huyu alikuwa ni kijana mvumilivu na wa kusaka ndoto zake zilipo.

Lakini hali ilikuwa vilevile aliendelea kupata alama za ajabu na sifuri hazikukosekana na upande wa kumbukumbu ndio ilikuwa shida kubwa maana alianza kusahau hadi watu aliokutana nao na kuongea nao kipindi cha nyuma. Hakika lilikuwa pigo kubwa kwake.

Katika elimu yake ya kidato cha tano na cha sita alipata fedheha ,dharau na kusemwa vibaya mno zaidi ya alivyokuwa shule ya msingi. Wanafuzni wenzake walimuona ni kilaza wa mwisho asiyekuwa na akili kabisa tena wengine wakimuandika vibaya ubaoni, hakika ilimuhitaji kuwa uvumilivu wa hali ya juu kuyashinda yote hayo.

Hali kadhalika Walimu nao walizidi kumsema na kumhisi anafanya makusudi, walianza kumsema kuwa anavuta bangi. Yaani itabidi kama serikali hawa walimu wafundishwe na elimu ya afya ya akili maana angekuwa mwingine asingeweza kuvumilia yale yaliyonipata nikiwa kidato cha tano na sita nilihisi ni mwisho wa Dunia.

Shuleni sikuwahi kumueleza mtu kama nina tatizo la kupoteza kumbukumbu na hata wazazi wangu niliwakatalia kuwaeleza watu kuwa nina tatizo la kupoteza kumbukumbu, kwa imani yangu niliamini ni mapito tu, ipo siku nitakuwa sawa tu ila nilipata changamoto sana nikawa bonge la muigizaji yaani muda wote ni kufurahi hata kama ninalia moyoni lakini nje bonge la tabasamu hadi baadhi ya wanafunzi waliniita mr no fear.

Alifanikiwa kumaliza kidato cha sita mnamo mwaka 2018 katika shule ya sekondari Tambaza. kwa bahati mbaya alifeli


Maisha yake ya chuo
Godwin aliumbwa kipekee sana bado hakukata tamaa katika ndoto zake, aliomba wazazi wake kuendelea na masomo katika elimu ya chuo. Alifanikiwa kupata chuo mkoani mMbeya, Chuo cha Afya St. John.

Kwa miujiza ya mwenyezi Mungu uwezo wa akili yake ulikuwa mara mbili kulinganisha na kipindi kabla hajaumwa na kupoteza kumbukumbu.

Chuoni alikuwa akifaulu vizuri na kila mwalimu aliufahamu uwezo wake wa kichwani tena akapata na nafasi ya kuwa Waziri wa Elimu chuoni, lakini matokeo yake hajawahi kushuka aliendelea kufaulu.

Chuo amesomea kada ya Uuguzi na Ukunga ambapo amesoma kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.

Baada ya kumaliza mwaka 2021, alitafuta sehemu ya kujitolea ambapo alijitolea kwa muda wa miezi tisa(9), kwasasa amepata ajira katika kituo kimoja cha afya mjini Njombe.

Kwa kada yangu hii ya uuguzi na ukunga nimeweza kumhudumia mdogo wangu pamoja na marehemu Baba yangu mzazi, tena nakumbuka wakati nampa huduma alikuwa akinitazama mara mbilimbili yaani alikuwa haamini kama ni mimi. Alikuwa akisema mimi ni professional zaidi ya wale wauguzi wa hospitali aliyokuwa anaenda kutibiwa.


Maisha yake ya mtaani
Godwini sio kijana wa starehe wala mambo ya ujana, kwa mafano bangi n.k.....

Vilevile upande wa marafiki kama kawaida yangu sikuwahi kuwa na marafiki hadi pale nilipofika chuo, kwasasa marafiki nilionao ni wale wa chuoni tu.

Kinachonipa shida kwasasa kama kuna mtu nilionana nae kabla sijaumwa, huyo nitamkumbuka kwa shida sana tena akijifanya ameniona halafu akanichunia atasema nina dharau.


Lengo la kuwaeleza kuhusu maisha yangu
Hiyo hapo juu ni stori yangu halisi ya maisha yangu kabisa kwa njia nilizopitia.

Imani yangu watu watajifunza mengi sana kupitia stori yangu,maana kuna ile hali ya kupanda na kushuka na kupanda tena ukiiweka stori yangu upande wa elimu inaingia hata upande wa biashara inajenga.

Kikubwa tusikate tamaa katika lengo au malengo tuliyonayo kwa changamoto tunazokutana nazo katika kuelekea mafanikio. Hebu tazama ningeamua kuacha shule leo hii nisngeweza kuwa muuguzi na nisingekuwa na kazi labda haijulikani ningekuwaje. Uvumilivu wangu ndio silaha yangu ya pekee maishani mwangu.

Kwa wanaohitaji ushauri au kumpa yale niliyoyafanya wakati wa kuzivumilia hizo changamoto napatikana whatsapp kwa namba 0768237875.

Napenda wengi kuwasaidia wenye changamoto kama yangu, afya au hata nyingine bila malipo yoyote yale kwa ushauri au kuelekezana nini cha kufanya.

Ahsante



 
Back
Top Bottom