Uvumi wa kuachana na Tanasha; Diamond Platnumz kuongea na waandishi wa habari kesho Serena Hotel

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Diamond amepost kwenye page yake ya Instagram kuwa ataongea na waandishi wa habari kesho huku kukiwa na uvumi wa utata kwenye mahusiano yake.

Inasemeka kuwa Diomond na Tanasha wapo kwenye mgogoro mzito na ikidaiwa kuwa penzi lao limefika mwisho. Je, ndicho kitu ambacho Diamond anataka kukizungumzia kesho kwa waandishi wa habari?

Jambo hilo bado limewaacha watu wengi na maswali kama ni kweli wameachana au ni uvumi wa watu, naamini kesho watapata majibu juu ya utata uliopo kwenye mahusiano ya wazazi wenza hawa.

Mond.jpg
 
kwani ni couple ya Taifa? Atazungumzia uchmi na maisha yetu? Au maisha binafsi.
 
Hiyo ni kutafuta tension ya watu.
Hawezi kuzungumzia mahusiano,anaenda kukuza biashara yake ya muziki. Ametumia hiyo chance ya kupata wafuatiliaji zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisaa anataka capitalise hali ya mambo ilivyo ili kupush biashara, kama ambavyo Ali Kiba alivyoweka watu na hamu kusikia na kuona press conference ya kile alichokiita,"TAMKO RASMI" baada ya trending story ya kumjibu Diamond, watu wakadhani ni tamko dhidi ya Diamond kumbe ni music tour yake, "ALI KIBA UNFORGETTABLE TOUR".
 
Diamond ni mjanja hawezi kuzungumzia mambo yake ya mahusiano Kama watu watavyofikiri hapo Sana Sana atazungumzia labda Kuna kitu WASAFI media wanafanya announcement ya Jambo Fulani au masuala mengine ya biashara au Jambo la label yake ya WCB.So anatumia Huu mwanya wa watu kuzungumzia mahusiano yake kufanya mambo yake ya biashara iende.
 
Diamond amepost kwenye page yake ya Instagram kuwa ataongea na waandishi wa habari kesho huku kukiwa na uvumi wa utata kwenye mahusiano yake.

Inasemeka kuwa Diomond na Tanasha wapo kwenye mgogoro mzito na ikidaiwa kuwa penzi lao limefika mwisho. Je, ndicho kitu ambacho Diamond anataka kukizungumzia kesho kwa waandishi wa habari?

Jambo hilo bado limewaacha watu wengi na maswali kama ni kweli wameachana au ni uvumi wa watu, naamini kesho watapata majibu juu ya utata uliopo kwenye mahusiano ya wazazi wenza hawa.

Ataongea kuhusu maswala ya kombe lao la mpira wala hata sio mambo hayo
 
Diamond hata ajitetee vipi. ukweli nikwamba ni Muharibifu kama walivyo wengine tu ,..yaan wanawake wote hao alikua nao..alowazalisha, hajapatikana hata wife material mmoja??
 
Back
Top Bottom