Uvumi/Tetesi: Mtoto wa Kikwete (8) kugombea Uenyekiti Chipukizi?

Status
Not open for further replies.

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Uchaguzi wa chipukizi CCM Taifa Unao tarajiwa kufanyika tarehee 29 Dec 2009 Kitaifa mkoani morogoro umethibitisha kuwa famiia ya JK imejipanga kurithishana madaraka ya Nchi ya hii tofauti na Marais waliomtangulia.

Mtoto mdogo wa Kikwete Mwenye Miaka 8 Anagombea uenyekiti wa chipukizi Taifa, Tayari amewaita makatibu wa mikoa na wilaya wa umoja wa vijana nchi Nzima na kuwaeleza Dhamira yake ya kugombea Uenyekiti wa chipukizi Taifa Zoezi ili lilisimamiwa na uongozi wa UVCCM taifa.

Tukio hii linazidi kututisha sisi watoto wa wakulima ikizingatiwa Baba yake ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na ni RAIS wa Tanzania, Mama yake (Salma Kikwete) ni Mjumbe wa mkutano mkuu kupitia wilaya wa lindi, fIrsrt Born wa Kikwete Ridhwan ni mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa , na vilevile ni mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa, Kaka wawili wa mkulu ni wajumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa kupitia Bagamoyo wacha mbali wanafamilia ambao ni wateule wake ktk Nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali eg KAWAMBWA etc.

Je na mimi mkulima wa huku kilombero mtoto wangu ataweza kushindana na mtoto anaeishi ikulu kwa kodi zetu? Dhana ya fursa sawa kwa wote itatimia au mama Ana Mkapa aliondoka nayo nyumba number 1 mtaa wa magogoni?
 
Tatizo si yeye kugombea. Tatizo ni nyinyi makabwela kumpigia kura!

Amandla........
Nadhani tuweze kuzidhibiti njaa zetu kwenye chaguzi mbalimbali sasa kinyume cha hapo familia ya kikwete imeonyesha njia sisi je?

Lakini kwangu mimi tatizo sio kubwa, sisiem ni chama tu kama vyama vingine vilivyopo na vitakavyokuja. Uchaguzi tunao sisi wananchi kwa kuwa sisiem ndio deal basi itakuwa kikwete tupu. Vinginevyo tuchague vyama vingine ili navyo viimarike hatuwezi, tuanzishe vingine sheria inaturuhusu.
 
Wamshukuru sana Kambarage aliyepanda mbegu na kupalilia miche ya amani na utulivu ndani ya mioyo ya Watanzania. Maana kwa Watanzania ni business as usual hakuna anayejali.
 
Ha ha ha ha ha. Mtoto wa nyoka ni nyoka tu. Lakini kweli last born wa Salma na Jakaya ana umri gani?

Mama Salma , kazi unayo.

Hata hivyo, ni uhuru wake kugombea. Hakuna mahali katiba imesema mtoto wa kigogo asigombee uongozi kama amekidhi vigezo. Ni uamuzi wa wapiga kura kumchagua au la. Ila nifahamuvyo watanzania wanasiasa hasa SSM wana woga na wanataka kujipendekeza, hivyo sitashangaa wakimchagua. Yetu macho.
 
Haya bwana, naona hasi wajumbe wa nyumba kumi mnataka kuwa kina kikwete
 
What is this chipukizi issue comming over?, sidhani kama inafikia viwango wa kuwa discussed hapa uwanjani. Leteni vitu vya maana.
 
Taratibu za kupiga kura zipo, sifa zinatakiwa. Kama mgombea amefuata taratibu na ana sifa za kugombea, agombee tu, tatizo nini? Wapiga kura si wanaelewa wanachokifanya, tatizo nini? Mwache!
 
Uchaguzi wa chipukizi CCM Taifa Unao tarajiwa kufanyika tarehee 29 Dec 2009 Kitaifa mkoani morogoro umethibitisha kuwa famiia ya jk imejipanga kurithishana madaraka ya Nchi ya hii tofauti na Marais waliomtangulia
Mtoto mdogo wa kikwete Mwenye Miaka ( Anagombea uenyekiti wa chipukizi Taifa ,Tayari amewaita makatibu wa mikoa na wilaya wa umoja wa vijana nchi Nzima na kuwaeleza Dhamira yake ya kugombea Uenyekiti wa chipukizi Taifa Zoezi ili lilisimamiwa na uongozi wa UVCCM taifa
Tukio hii linazidi kututisha sisi watoto wa wakulima ikizingatiwa Baba yake ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na ni RAIS wa Tanzania,Mama yake (Salma Kikwete) ni Mjumbe wa mkutano mkuu kupitia wilaya wa lindi, fIrsrt Born wa Kikwete Ridhwan ni mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa ,na vilevile ni mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa,Kaka wawili wa mkulu ni wajumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa kupitia Bagamoyo wacha mbali wanafamilia ambao ni wateule wake ktk Nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali eg KAWAMBWA etc
Je na mimi mkulima wa huku kilombero mtoto wangu ataweza kushindana na mtoto anaeishi ikulu kwa kodi zetu? dhana ya fursa sawa kwa wote itatimia au mama Ana Mkapa aliondoka nayo nyumba number 1 mtaa wa magogoni?

Na kama ingekua ni uwezo wake tu angejiita King of Africa, tazama na wanajeshi wenzake aliowaweka serikalini. Absolute JK
 
Taratibu za kupiga kura zipo, sifa zinatakiwa. Kama mgombea amefuata taratibu na ana sifa za kugombea, agombee tu, tatizo nini? Wapiga kura si wanaelewa wanachokifanya, tatizo nini? Mwache!

I say, hapa panatatizo kubwa sana la kisykolojia, ambalo wengi hawalioni. Sio kuhusu mtoto bali kuhusu baba. Mtoto hakutamka mwenyewe kutaka kugombea na wala sijui kama anajua anagombea nini. Hii inaonesha kupenda madaraka na kupenda ukubwa. Na huyo baba kama mtamnyima ukubwa basi atakuwa tayari hata kuuchukuwa kwa nguvu!
Anyway, siamini kama JK na mama JK wanaweza kuruhusu hali hio. Hii yote ni maneno ya wapinzani tu wasiomtakia kheri JK!
 
Mtoto mdogo wa kikwete Mwenye Miaka (8) Anagombea uenyekiti wa chipukizi Taifa ,Tayari amewaita makatibu wa mikoa na wilaya wa umoja wa vijana nchi Nzima na kuwaeleza Dhamira yake ya kugombea Uenyekiti wa chipukizi Taifa Zoezi ili lilisimamiwa na uongozi wa UVCCM taifa

Hivi wanaopiga kura katika huo uchaguzi ni wakina nani? Chipukizi wenzake au wazazi wao? Hao makatibu walioitwa na kukubali kwenda kumsikiliza mtoto wa miaka minane ni wakina nani? Nao wana umri gani?

Kama hii habari ni ya ukweli, basi huyu mtoto ni wa kumuonea huruma. Badala ya kuachiwa afaidi utoto wake anasukumizwa katika jukwaa la taifa! Matokeo yake mara nyingi ni mabaya. Angalia wakina Michael jackson, Tatum O'Neal n.k. Angeachiwa aendelee kuchezea vigari na kupanda miti kama wenzake. Vile vile itamuondolea muda wa masomo. Wakina Clinton na Obama si wajinga kulinda kwa kila hali nafasi ya wanao kuwa watoto!

Amandla......
 
Tatizo si yeye kugombea. Tatizo ni nyinyi makabwela kumpigia kura!

Amandla........



Unawaonea tu hao makabwela.Hivi Tanzania kumeshaanza kuwa na chaguzi huru?Huyo dogo kama ana mwongozo wa baba yake basi ataukwaa tu uenyekiti whether makabwela watapiga kura or not.Kikwete akiwaambia hao UVCCM mtoto wake apitishwe unadhani kuna sisimizi atatia fyoko?
 
hebu tuamke tuache mawazo mnato. hivi kuna mtu anakazwa kugombea? sioni tatizo la mtoto huyo kugombea. suala la kugombea ni suala la kuweza na si suala la nani anatoka familia ipi. kama una mwana na anaweza kuomba kura ruksaaaaaaaa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom