Max.....Mimi nina haya machache ambayo nadhani yanaweza kusaidia katika kuireform UVCCM..
1.
Muundo.
Kwa muundo nadhani uliopo si mbaya sana,ila kunatakiwa kuwepo na muundo ufuatao:
i. UVCCM Taifa
ii.Baraza kuu la UVCCM
iii. Sekretarieti ya UVCCM Taifa
iv.UVCCM mkoa
v. Baraza la UVCCM mkoa
vi. UVCCM wilaya
vii. Baraza la UVCCM wilaya
viii. UVCCM kata
ix. Baraza la UVCCM kata
x. UVCCM tawi
xi. Baraza la UVCCM tawi.
2.
Mfumo wa upataji viongozi
Si vibaya UVCCM wakawa na mfumo unaojitegemea wa kupata vioongozi na pia mfumo huo utofautiane na ule wa CCM ambao unakuwa na Mwenyekiti wa taifa,Makamu mwenyekiti wa bara na visiwani,katibu mkuu n.k...Ni vema UVCCM wakawa na Mwenyekiti(kama ilivyo sasa) ambaye
atachaguliwa na mkutano mkuu(Baraza kuu) la UVCCM.Pia awepo Makamu mwenyekiti ambaye pia atachaguliwa na Mkutano mkuu wa UVCCM,
awepo Makamu mwenyekiti mmoja tu na si lazima awepo wa Bara na Visiwani,na si vibaya ikiwa Mwenyekiti atatoka Bara Makamu wake akatoka
visiwani(upande wa pili wa Muungano).Pia awepo katibu mkuu ambaye atateuliwa na Mwenyekiti wa UVCCM taifa na jina lake kuthibitishwa na
mkutano mkuu wa UVCCM badala ya katibu huyo kuteuliwa na mwenyekiti wa CCM Taifa kama ilivyo sasa...Vile vile katibu wa fedha ambaye atateuliwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa miongoni mwa wajumbe wa UVCCM Taifa ambaye kazi yake itakuwa ni kusimamia miradi yote ya UVCCM na pia atakuwa ndiye mweka hazina wa jumuia....Baraza kuu la UVCCM litaundwa na wajumbe ambao watachaguliwa katika ngazi ya wilaya...Pia uchaguzi mkuu wa UVCCM uwe unafanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM na si baada ya uchaguzi mkuu wa CCM...Shughuli za uenezi na uhamasishaji zitafanywa na kitengo maalum ambacho kitakuwa ni sehemu ya idara ya mawasiliano kwa umma....
Ni vema pia UVCCM wakarekebisha katiba yao ambayo ina mapungufu mengi sana na ioneshe hatua(za kinidhmu) ambazo zitachukuliwa kwa wanachama/viongozi wote ambao wataenda kinyume na maadili ya jumuia na CCM,hii ni pamoja kuwakumbatia mafisadi n.k....
3.
Mfumo wa mawasiliano wa UVCCM
Kuwepo na kitengo cha mawasiliano ambacho kitakuwa chini ya Msemaji mkuu(Spokeperson) wa UVCCM..Msemaji mkuu ndiye atakuwa mkuu wa kitengo cha mawasiliano ndani ya UVCCM,yeye ndiye atakuwa mtoaji wa taarifa zote zinazohusiana na UVCCM...
Vile vile kuwepo na majarida mbali mbali yanayonilikiwa na UVCCM ambayo yatatumika kutoa taarifa kwa wanachama pamoja na kufanya kazi ya uenezi wa sera na itikadi za CCM.
Pia kuwepo na tovuti(website) ya UVCCM ambayo pia itatumika kufanya kazi ya kutoa taarifa pamoja na kufanya kazi ya uenezi....Wajivunze kutoka kwa wenzao wa ANC(ANC Youth League) ambao website yao ni nzuri na iko upadated
ANC Youth League
Vile vile si vibaya wakaanzisha vipindi katika redio ya CCM,Redio Uhuru ambavyo vitasaidia kuweka mawasiliano baina yao na wanachama wao...
Ili hayo yote hapo juu yakamilike ni lazima waifanyie marekebisho katiba yao(UVCCM) ili angalau iendane na na hali ya sasa,wanaweza hata kuchukua baadhi ya vitu vilivyomo katika katiba ya ANCYL
http://www.ancyl.org.za/docs/const/2008/constitution2010b.pdf
Aidha ni vema wakaanzisha chuo ambacho kitafanya kazi ya kuwaandaa viongozi wajao wa CCM,na kuwepo na sharti kwamba kila kiongozi wa UVCCM na CCM ajaye ni lazima awe amepitia katika chuo hiki ambacho kitafanya kazi kama kilichokuwa chuo cha(uongozi) chama cha Kivukoni ambacho kilitumika kuwaandaa viongozi mahiri,waadilifu na wenye uchungu na nchi yao.....Chuo hiki kitawaandaa viongozi na makada ambapo pamoja na mambo mengine watafundishwa maadili ya uongozi na hili linaweza kusaidia kuondokana na janga lililopo sasa la kuwa na viongozi wasio na uchungu na nchi yao na ambao wanaweka maslahi yao binafsi mbele kwa kushiriki vitendo vya ufisadi na mambo mengine mabaya ambayo ni kinyume na maadili ya uongozi...