UVCCM: Maoni juu ya Reform [Survey]

UVCCM: Maoni juu ya Reform [Survey]

Status
Not open for further replies.
UVCCM wafanye Outreach kwa Ratiba maalumu. Wawe Independent katika kuendesha mabaraza yao na wafanye kazi kwa karibu zaidi na secretariet ya chama chao.

Uwakilishi wao kwenye kamati kuu ya chama inabidi uongezeka kwa kuzingatia population kubwa ya watanzania ambao ni vijana

Waache kuumarisha magenge ya kihuni na badala yake wawaeke mechanism ya kulea viongozi wa sasa na wa baadae.

Kwa kuwa wana vitega uchumi vya kutosha, basi waanzishe vyuo vya kufundisha makada wao kutoka sehemu zote Tanzania na kuwaingiza kwenye majimbo na wilaya

Tungeni katiba yenye mwanya wa watu kuunda petition pale wanapoona viongozi wao wajuu wanaenda vibaya au kuwa na mwelekeo wa kutumiwa na watu nje ya umoja wa vijana.

Tafsiri Itikadi yenu na muelekeze katika mitaala ya chuo mtakachoanzisha.Tumieni mtaji mkubwa mlio nao kiuchumi kuwekeza na kushinikiza utungaji wa sera zenye maslahi kwa vijana na muwe sharp kuji-associate na hizo sera

Wape umoja wa vijana meno ya kukosoa hata viongozi hadharani na kuwapa nguvu ya kushinikiza kujiuzulu kwa viongozi goi goi ili kurejesha heshima,nguvu na mvuto wa Umoja wenu

Kwa sababu nimepita tu haraka haraka nikaona nitoe mapendekezo ya dhati kabisa labda nikipata muda baaade nitatoa mchango wangu.

Siasa si uadui

hawawezi kuwa independent kwa sababu wao ni tawi katika mti mbovu. Lazima wawe wabovu. Ili UVCCM iwe safi, lazima mti wenyewe uwe safi. Maboresho ambayo wanaweza kufanya, waondoe gamba la kichwani yaani Kikwete. Kisha ndo CCM ifumuliwe upya, mafisadi wote wawekwe kizuizini. Kisha CCM iundwe upya hapo ndipo hayo matawi (UVCCM, UWT, WAZAZI n.k) yataweza kutenda kazi nzuri.

Mimi Quality (Mkuu wa Viwango Tanzania)
 
Tumeimba nyimbo toka tukiwa wadogo ili tuendelee tunahitaji
  1. Watu- watu tupo na hivi sasa tumeelimika kwa kiasi fulani tofauti na miaka ya 1960-1970. Lakini katika watu hao hao tupo wenye matatizo japo wachache ........... nisome baadae
  2. Ardhi- Tunayo ya kutosha labda tatizo haijatumika vizuri. Ardhi yetu imejaliwa madini, mbuga za wanyama, rutuba..............
  3. Siasa Safi- Assuming tuna siasa safi ( sera) toka tukapte uhuru . Kwa nn tuna rudi nyuma. tataizo hapa ni uratibu wa siasa (sera kweye makaratasi) na utekelezaji( implimentation)...........
  4. Uongozi bora- Assuming pia toka tupate uhuru mpaka sasa tuna viongozi bora. Sasa nini imekuwa tatizo? Tatizo laweza kuwa kama tuna kiongozi bora basi hakutumia siasa safi au hakuwa na watu .Au kama alitumia siasa safi na watu wa kutekeeleza siasa zake walikuwepo basi kiongozi alikuwa na mapungufu......... nitafafafanua
  5. Taarifa- (kipengele hii ni mawazo yangu)- Tuko katika karne inayoitwa Digital age . Kumbuka tulianza na zama a mawe, zikaja zama zama za chuma. Hata kwenye vita jeshi haliweiz kufanikiwa kama halina taarifa za adui. Na si kuwa na taarifa inatakiwa taarifa sahiihi ili kufanya maamui sahihi. Wazungu wana msemo Information is power. .... kivipi watendaji na taasisis zote za serikali walishidnwa kujua kuwa rimcmond in brifcase company???!!!!!!!!. Tuko katka zama za sayansi na Teknolojia. communiction should be timely , reliable accurate. but kwa CCM ni business as usual. Na usipokuwa na taaarifa zenye sifa maaamuzi( Decison making) yatayotoka na taarifa hizo ndio kama hivi tunavyoona leo ......... nitatoa mifano

NB
Nitakuwa naandika maoni yangu hapa kadiri navyopata muda kutokana na hayo mambo na kutoa mifano hai na ni vipi CCM inaweza kujitoa shimoni.

Lakini je huyu mgonjwa UVCMM mbona inaonekana wanatofautiana lugha na mzazai wake CCM. atatuthibishia vipi kuwa haya maoni pia yatawafikia na kina Msekwa. Tusije kuwa tuna mwaga maji baharini
 
..nawashauri wafunge tu shughuli zao.

..pia wapendekeze CCM ifunge shughuli za kisiasa nchini.

..CCM imetekwa nyara na majambazi sasa hivi, the changes that have taken place are irrevesible.
 
Kwa mawazo yangu nafikiri tatizo la uvccm si la kimuundo zaidi bali ni la kimfumo zaidi kitu kinachopelekea asilimia kubwa ya viongozi wetu wa vijana kujikuta wanalazimika kufunika kombe mwanaharamu apite na hatimae mradi wao ufanikiwe, vijana wengi wamekua zaidi wapokea maagizo kwa masilahi ya watu fulani, kitu ambacho kwa namna moja kinasababishwa na viongozi wetu wengi wa vijana kujikuta wakijitumikisha wenyewe hasa ukizingatia uchumi wao zaifu, wamegeuka ombaomba, wategemezi, na hivyo kuwa wanafiki, waongo, na mara zote tumewaona wakigeuka wapambe/ kama migambo katika ziara za wakubwa huku wakijipenyezapenyeza ili watambulike kwa dhamira ya kuweza kufikiriwa fikiriwa bila kuzingatia uwezo wao katika utendaji. ndugu yangu bashe ninachofahamu mimi uvccm kwa hapa ilipofika inahitaji bed rest tena icu room, na kama ni kujivua kwa sasa ningependa kushauri isiwe gamba bali ni kushusha ingini na hatimae fundi aone uwezo wa injini na if possible kubadili mpaka shaft siyo tu ringn a piston
 
Nadhani tatizo ni kuwa UVCCM ni sehemu ya chama kilichochoka kifikra, kimfumo, kiitikadi na kimaadili kutokana na kazi kubwa ya kuongoza nchi kwa miaka 50 sasa. Tunawashukuru sana kwa kazi kubwa hiyo na daima tutawaenzi. Ushauri ni kuwa wapumzike sasa kwani kazi waliyoifanya ni kubwa na nzito....INATOSHAAAA...Funda moja tu la ziada.......
 
  • Ni yepi mangufu ndani ya UVCCM katika:

  • Muundo
  • Mfumo wa upataji viongozi
  • Mfumo wa mawasiliano wa UVCCM


Wana JF
this goes esp to UVCCM

Muundo kama Muundo wa UVCCM unaweza ukawa ni mzuri na kuwa na mapungufu madogo hiyo ipo ktkt vyama vingi tu

Ila katika swala la kuandaaa viongozi au upatikanaji wa viongozi ndani ya UVCCM ndipo kuna tatizo kubwa Uadilifu ni zero, Rushwa hapo ndipo imechukuwa 100% nafasi katika hivyo tu tayari mfumo wa kuwaandaa viongozi nani ya UVCCM tayari umeisha chafuka hadi hapo na kusafisha hapo ni kazi ni kutoana kafara amini nawaambieni maana kuvurugika kwa uadilifu na maadili ya uongozi ni kama vile mumeingia vitani wenyewe kwa wenyewe na kuitoa hali iyo ni mpaka mumejikuta mumepukutika wote ndi mshituke ati mwafanya nini? tooo late.

Ni muda sasa kurudisha Uzalendo Uadilifu,Maadili ya uongozi ndani ya UVCCM kwa manufaaa ya CHAMA.

Mfumo wa mawasiliano laziama ujengwe upya kuwe na heshima kuanzia mtu mdogo mpaka wa lika la juu hicho ni chama ni kama taasisi fulani inatikiwa iwe na kanuni na utaratibu wake wa kufwatwa na sio mambo yajiendee kiholela holela tuu ilimradi wewe ni M/kiti you've the last say hapana. Ndani ya UVCCM sasa katika mikoa mingi au Wilaya ukiuliza vikao walivyo kaa kwa ajili ya maendeleo yao au mipango yao hakuna utakuta ni mara baada ya kuchaguliwa kuwa viongozi basi na kikao cha kupitasha wajumbe wa baraza hawakutani tena kwani hawa cha kuongea wao ni kukutana wakati wa Kampeni na uchaguzi ndipo utaona kuna mawasiliano ya vikao huku nyuma walisha sahau kuwa kuna shughuli za kichama zilipaswa kujengwa kwanza ili mkija kwenye chaguzi ndio zitakazo wasafishia njia zaidi kwa wapiga kura lakini matokeo yake ni viongozi wa juu katika UVCCM wanakuala tenda nyingi huko Manicipaa. Yaani uki kaa ukachunguza hii UVCCM unaweza waweka ndani viongozi wote wa UVCCM ni wapo hapo kwa maslahi ya viongozi wa ngazi za juu katika chama CCM UVCCM wamekuwa ni watumwa jamani.
 
Nashauri muundo wa upatikanaji wa viongozi wa UVCCM uanzie chini.
Wakuu,

Mtakumbuka mnamo mwezi Machi/Aprili (kama sijakosea) mwenyekiti wa kamati ya Mabadiliko UVCCM Hussein Bashe aliahidi kutuomba JF ushauri juu ya reforms ndani ya chama.

Ametuomba kumpa ushirikiano (kama huna mapendekezo, bora usiandike) katika hili na hivyo naleta rai kwenu ambao mngependa au mpo tayari kutoa ushirikiano kwake (positive and negatives bila kujali itikadi za vyama) juu ya masuala yafuatayo:
  • Ni yepi mangufu ndani ya UVCCM katika:
  • Muundo
  • Mfumo wa upataji viongozi
  • Mfumo wa mawasiliano wa UVCCM
Maeneo haya matatu ndiyo kaomba tumpe maoni lakini anakaribisha maoni hata kwa mapungufu mengine (not limited) kwa uwazi bila kubanwa na hayo matatu juu, ili ayawasilishe na atakiri ni ya wana JF na anaomba wale ambao wangependa kumtumia maoni personally na si kuandika kwenye thread hii (ambayo watajitahidi kuifuatilia kwa karibu) amwandikie - maoniuvccm@yahoo.com au hussein@newhabari.com
 
Kwa mtazamo wangu ktk muundo uliyopo hauna tatizo, ila tatizo lipo ktk uongozi wao. je wanaufuata utaratibu unaofuata katiba yao?
Hapo ndipo penye tatizo. Ni hiyo yote ni kwa sababu ya kutokuwepo nidhamu na maadili mema ya uongozi,
waanzishe chuo maalum kwa ajili ya kuwafundisha vijana viongozi wao watarajiwa kuhusu maadili ya uongozi na mambo mengi mf demekrasia ya kweli etc.

Miaka ya nyuma palikuwepo chuo cha CCM, kama ninakumbuka vizuri ilikuwa sio rahisi kupewa dhamana ya uongozi kama hakuhudhuria courses zao ktk chuo kile.

Nadhani hapa cha msingi ni kufikiria namna ya kurudisha chuo chao cha CCM, ili kuweza kuondoka na huu uongozi wa sasa, ambao unawapotezea heshima ya kujiongoza pasipo kuingiliwa na viongozi wa CCM Taifa kwa maslahi binafsi.
 
Maoni yangu ya mabadiliko:
1. UVCCM, makada wake warudi Kivukoni wakapikwe!
2. Waachwe kutumiwa kuwahujumu na kuwasafisha watu wao wanaolilia Ikulu!
3. Wazingatie UMRI uliowekwa, na iwe mwiko kwa "kijana" wa miaka 50, kujiweka sehemu ya jumuia!
 
Maoni yaliyoshatolewa yanawatosha, wakayafanyie kazi hayo. Toa hii kitu hapa.
 
nina Mashaka sana na hii move ya BAshe, anyway nina maswali mengi ambayo yananikoroga tu kichwani BAshe anamamlaka gani ndani ya UVCCM akatengeneza hoja bila kuwashirikisha wenzie? na anafanya kazi hii kiofisi ama binafsi? haya mawazo atakayoyapata ana uhakika gani yatapita huko anakotaka kuyapeleka?, hivi ndani ya chama chao walishawahi kukaa na kuliangalia hili na likashingikana mpaka aje JF kuomba ushauri? kwa nini kila kitu kinaonekana ni personal(Hoja ziende kwa bashe na sio UVCCM? na kwa nini ni personal emails tu ndio alizotoa, na ni zake tu bila kuweka emails za wengine?)

Nadhani kuna Chama kipya kutoka CCM kipo mbioni
 
Mapendekezo yangu Bashe awe mwenyekiti ili awaingize Wasomali wenzie na Al-Shabab ndani ya UVCCM....
 
Cha msingi UVCCM ihamasishe maandamano nchi nzima waikatae CCM kwa kushindwa kukilea kizazi cha taifa lenye rasilimali lukuki and thereafter waombe mawazo zaidi
 
Maoni yangu ni kwamba: UVCCM inapendelea watoto wale wazee wanye majina. Wajitahidi katika uongozi waweke na vijana wa walalahoi
 
Naona wanaelekea kufanikiwa kuongeza umri hadi miaka 40 ili warudi tena!
 
tanzania itajengwa nawatanzia wenye nia njema ya maendeleoa, uzalendo ,utu,huruma kwa wenzao wala sio haramu ya mtu kutoka nchi nyingine kuja kuendeleza nchi . chama hakina tatizo lakini viongozi wake ndio makapi hawana utu, uzalendo, hawatumii hekama hata busara kujua kuwa uongozi ni dhamana ya wananchi waliowachangua nakuwapa madaraka ili wasimamie rasrimali za nchi wala si vinginevyo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom