UVCCM: Maoni juu ya Reform [Survey] | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM: Maoni juu ya Reform [Survey]

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maxence Melo, Jul 18, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Mtakumbuka mnamo mwezi Machi/Aprili (kama sijakosea) mwenyekiti wa kamati ya Mabadiliko UVCCM Hussein Bashe aliahidi kutuomba JF ushauri juu ya reforms ndani ya chama.

  Ametuomba kumpa ushirikiano (kama huna mapendekezo, bora usiandike) katika hili na hivyo naleta rai kwenu ambao mngependa au mpo tayari kutoa ushirikiano kwake (positive and negatives bila kujali itikadi za vyama) juu ya masuala yafuatayo:

  • Ni yepi mangufu ndani ya UVCCM katika:

  • Muundo
  • Mfumo wa upataji viongozi
  • Mfumo wa mawasiliano wa UVCCM
  Maeneo haya matatu ndiyo kaomba tumpe maoni lakini anakaribisha maoni hata kwa mapungufu mengine (not limited) kwa uwazi bila kubanwa na hayo matatu juu, ili ayawasilishe na atakiri ni ya wana JF na anaomba wale ambao wangependa kumtumia maoni personally na si kuandika kwenye thread hii (ambayo watajitahidi kuifuatilia kwa karibu) amwandikie - maoniuvccm@yahoo.com au hussein@newhabari.com
   
 2. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Maxence Melo

  Kabla sijatoa mapendekezo bora unayoyataka tuwekane sawa kwanza hiyo 'bora' unaipimaje maana mtoa hoja anaweza kuona mawazo yake ni bora kumbe kwako si bora, kwa vile umesema unahitaji mawazo yeyote yawe positive au negative mimi ninayo mapendekezo bora lakini negative je yatakufaa.

  Naomba hii post yangu isiwe kati ya mapendekezo yasiyo bora.
   
 3. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ufisadi na ukosefu wa uzalendo kushabikia pumba ndio hasa chanzo cha ubovu wa UVCCM; mengine yanakuja tu; muundo hata uwe mzuri; mfumo hauwezi k uwa mzuri kama kuna ufisadi; hata mawasiliano yanakuwa blocked na ufisadi; tatizo wanataka wavune sawa na wazee hivyo kusahau majukumu ya msingi na wanarubunika sana na wagombea wenye nguvu huwa buruza kama wanavyotaka; so Waache ufisadi ndio watapata wanachotaka otherwise uongozi ni kwa watoto wa vigogo tu na wenye majina Makamba/Jakaya/Kawawa/Karume/Nauye/ etc; hakuna u chungu wajivue gamba kwanza ndio wataweza kuaminika
   
 4. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu, nimemuelewa Maxence. Anamaanisha kama huna mapendekezo ni afadhali usiandike kabisa. Neno 'bora' limetumika kama 'afadhali'. Jaribu kurejea tena kusoma, ni makosa ya uwasilishaji tu.
   
 5. eyetyna

  eyetyna Senior Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kama mimi ninamawazo na ni NEGATIVE............................na nijuavyo mimi ni kwamba mawazo yenye NEGATIVE sikuzote ndio mawazo mazuri kuliko yale ya kwamba mnafanya vizuri HONGERENI AMA SAFI SANA,SASA sijui mtakubali nichangie?
   
 6. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona ametulimit kutolea maoni hayo mambo matatu tu,
  hayo maeneo wala sio yenye matatizo makubwa sana by the way.

  Naomba Muongozo wako kama tuko huru kutoa ukweli wa moyoni mwetu,

  Ila nisiwaache bila maoni. Maoni yangu ya makubwa ni kama ifuatavyo
  1. Kikwete aondolewe uenyekiti wa CCM Taifa
  2. Kikwete aondolowe uenyekiti wa CCM Taifa
  3. Kikwete aondolewe uenyekiti wa CCM Taifa
  4. Anzisheni UVCCM Alumni
  5. Fanyeni appointment ya external auditors kutoka kwenye the top five list, wawe wanakagua
  hesabu zenu na audit reports ziwe wazi wa wananchama wenu wote, mkitaka ziwe public
  the better. Kama hesabu zenu zinafanyiwa ukaguzi pamoja na CCM basi waombeni hao
  jamaa wafuate ushauri huu for the best of your interest.
  6. Tekelezeni sera za Chama na sio watu fulani fulani.
  7. Acheni kutegemea taasisi au favor zozote kutoka serikalini.
  8. Kwa vitendo, hakikisheni kwamba mnakuwa mfano wa kufuata kwa utiifu mkubwa sana
  sheria zote za nchi.

  Nitaendelea.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kiukweli UVCCM imekuwa kama ni mlango wa watoto wa matajiri au wenye ELIMU watoke vp ndo muundo wake ulivyo sio chama cha kulea vijana wa wakulima na wafanyakazi kama ilivyo undwa hapo zamani.

  Hawa watoto wa wenye pesa na ndo wenye nguvu waachie madaraka kwa watoto wa wakulima na wafanyakazi tatizo ni moja na wao wanadai kuwa wana haki ya kuingia kwenye siasa lakini njia wanayo tumia sio sahihi wanamwaga pesa ili kushawishi wapiga kura siku hizi haziangaliwi sera zinaangaliwa pesa hata kama una sera nzuri kiasi gani lakini huna pesa ni ndoto kupata wadhifa hapo UVCCM.

  Naona pendekezeko ni bora UVCCM irudi kama zamani ilivyo CCM, irudi kwa wanyonge wenye pesa wapigwe vita wasiwanie uongozi.
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  UVCCM wafanye Outreach kwa Ratiba maalumu. Wawe Independent katika kuendesha mabaraza yao na wafanye kazi kwa karibu zaidi na secretariet ya chama chao.

  Uwakilishi wao kwenye kamati kuu ya chama inabidi uongezeka kwa kuzingatia population kubwa ya watanzania ambao ni vijana

  Waache kuumarisha magenge ya kihuni na badala yake wawaeke mechanism ya kulea viongozi wa sasa na wa baadae.

  Kwa kuwa wana vitega uchumi vya kutosha, basi waanzishe vyuo vya kufundisha makada wao kutoka sehemu zote Tanzania na kuwaingiza kwenye majimbo na wilaya

  Tungeni katiba yenye mwanya wa watu kuunda petition pale wanapoona viongozi wao wajuu wanaenda vibaya au kuwa na mwelekeo wa kutumiwa na watu nje ya umoja wa vijana.

  Tafsiri Itikadi yenu na muelekeze katika mitaala ya chuo mtakachoanzisha.Tumieni mtaji mkubwa mlio nao kiuchumi kuwekeza na kushinikiza utungaji wa sera zenye maslahi kwa vijana na muwe sharp kuji-associate na hizo sera

  Wape umoja wa vijana meno ya kukosoa hata viongozi hadharani na kuwapa nguvu ya kushinikiza kujiuzulu kwa viongozi goi goi ili kurejesha heshima,nguvu na mvuto wa Umoja wenu

  Kwa sababu nimepita tu haraka haraka nikaona nitoe mapendekezo ya dhati kabisa labda nikipata muda baaade nitatoa mchango wangu.

  Siasa si uadui
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  [1] UVCCM ni daraja la watoto wa vigogo kupewa vyeo ndani ya Chama na serekalini.

  [2] UVCCM inatumiwa na baadhi ya wanasiasa kuwapaka matope bila sababu za msingi

  [3] UVCCM imepoteza mwelekeo kama kilivyo chama cha mapindunzi.

  [4] UVCCM imeacha kazi yake kuu ya kuwapika na kuwaandaa vijana kushika madaraka badala yake imekuwa ikiandaa wezi wa mali ya umma na mtetezi wa mafisadi eg Lowassa,Karamagi,Rostam Azziz na nk.Wakati huo huo UVCCM imekuwa mstari wa mbele kuwapiga vita watetezi na walinzi wa mali za umma eg Sitta,Sendeka,Magufuli na nk.
   
 10. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Safi sana Max......Ukweli ni kwamba UVCCM inahitaji marekebisho makubwa sana....
   
 11. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  NAHISI UKO SAWAA.......Lakini unadhani watasikiliza haooo??/!!!..UNDENI CCM mpyaaa.... yenye watu wapya... tatizo top rank mnarithishana....tena hawana elimu.... utasikia kasoma India, USA..... ni scraperz..... nahsi ni CHHAMA CHA KIKOO 2015
   
 12. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Samahani ila ndio mchango wangu.

  Moja...uvccm ni taasisi ya watoto wa matajili, watoto wa viongozi na watoto wa wafanyabiashara wakubwa. Hili mliangalie upya.

  Pili...uvccm iache makundi na siasa za majungu. Kwanini watumiwe na wanasiasa wakubwa? Huyo bashe mwenye yuko ndani ya hayo makundi. Je, anaweza akatatua mgogoro wakati naye ni tatizo?

  Tatu....maadili ya uvccm hayapo je mna mpango gani wa kuwapa mafunzo ya uongozi hawa vijana wawe na nidhamu?

  Haya yanatosha
   
 13. Mkenazi

  Mkenazi Senior Member

  #13
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  1.Tatizo lenu mna lengo la kutawala tu
  2. Mnakula matunda ya mfumo wa baba zenu (Shule ya kata).
  3. Lete umeme, maji elimu n.k
  4. Msitegemee kuwa kama mlivyokuwa enzi za chama kimoja.
  5. Mlizunguka nchi nzima kumweka rais wa sasa mnataka nini tena?
  6. Mna udini na ukabila - Rejea kauli ya Nape kwamba yeye sio mchaga.
   
 14. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Vunjeni kabisa na muanze usajili upya bila kuwa na upendeleo wala uroho wa madaraka ya ukuu wa wilaya.
   
 15. p

  politiki JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  solution ya matatizo yenu ni moja tekelezeni ahadi zenu mlizozitoa kwa wananchi na pia ku introduce mfumo wa kuweza wa recall viongozi wabovu na siyo kusubiri muda kwisha.

  Kwa maana hiyo itaruhusu uharibifu kuwa mkubwa zaidi mtu akiondolewa na wananchama wote hakutakuwa na ugomvi lakini mtu akiondolewa na mtu au uongozi mara nyingi uzalisha majungu na makundi kwenye taasisi yeyote ile.
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Binafsi ninayo mapendekezo positive mengi sana ila siwezi kuwapatia CCM na watoto wao (Mafisadi baba na mafisadi watoto)!... Naweza na niko tayari kutoa si maoni tu ila hata damu yangu kuijenga Tanzania na siyo hizi taasisi za ufisadi, wizi, utapeli, ubaguzi na kila aina ya uchafu.

  Ushauri wangu muhimu ni kwamba wale wote wanaipenda Tanzania (kama ba Bashe yumo) waachane na upuuzi huu wa kuziba nyufa wakati nyumba imeshaporomoka 45 degrees. Warudi kundini tuongee jinsi ya kuijenga Tanzania mpya, yenye manufaa kwa kila mtanzania na siyo kwa matapeli wachache.

  Nisameheni kama haya siyo maoni yaliyotegemewa (kwa mujibu wa mleta maombi, ... C/o Max)!!!
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Max, SALAM SANA TOKA QUITO

  kiutalaam nafahamu kwamba hoja open-ended kama hii italeta mkanganyiko na tawala za hisia kuliko structured and constructive feedback

  nashauri kwa kuanzia tu, tengenezeni dodoso (kuna wataalam) ambao wataangalia muundo wa UVCCM wa sasa na wachangiaji watachangia kutokana na muundo, lakini mkiileta kama ilivyo naweza kusema mapungufu hata yasiyo na tija kwa chama chenu mf. kiongozi fulani alilewa wakananiliu, au nachukia sana ile unifomu yenu, punguzeni kanga na vitenge etc

  any system review must have tools to do the job and not the way you approach.... HILO NDIO BORESHO LANGU!!!
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kamanda, hayo marekebisho yaanze hata na namna approach ya improvement ilivyoletwa hapa jamvini

  BTW, hivi mnajua vikao vya UVCCM vimekua kama vijiwe vya kucheki mademu na kutafuta kujipendekeza kwa vigogo??
   
 19. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #19
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  MTM,

  Ahsante kwa ushauri.

  Ntaambatanisha na survey link UMEME UKIRUDI
   
 20. G

  Godwine JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Cha msingi wasipoteze muda wachukue muundo wa BAVICHA nao wabadili kidogo nadhani utawafaa sana
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...