UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina

UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina

Hoja yangu ni kwamba mawazo au maoni ya Mwl Nyerere siyo msaafu, lakinilazima tuendelee kumuenzi na kumuheshimu siku zote, lakini kufanyia tathmini za kina mambo aliyofanya ili utusaidie kwenda mbele. Hayo mengine nadhani siyo thread yake hii
Nani kasema eti ni lazima tuendelee kuwaenzi wezi?? Halafu siku zote??? Endelea wewe.
 
- Mkuu ninaamini sana maana majuzi kuna mjumbe mmoja wa NEC ya CCM, alikuwa ananiambia bila uoga wala aibu kwamba Lowassa is the next President, well over our dead bodies!

- Hivi hapa JF kuna mliowahi kusikia jinsi Lowassa na kundi lake walivyojaribu kila mbinu kuikwamisha ripoti ya Mwekyembe isifike bungeni? Zile Millioni 4 walizokuwa wakipewa wabunge kuikataa ile ripoti zilikua zinatolewa na nani? Kwenye ripoti ya Mwekyembe, alisema wazi jinsi walivyojaribiwa kupewa magari na majumba ili wapindishe ukweli ni nani aliyetaka kuwapa magarii na nyumba?

- Hivi mnajua kwamba at one point Lowassa na kundi lake walitengeneza ripoti ya siri ambayo waliitaka isomwe badala ya ile original ya Mwakyembe, ikabidi Mwakyembe ajfiche usiku wa kuamkia kwenda bungeni maana walikuwa wakijaribu kila njia kumshambulia ili wachukue ile original ripoti, sasa leo hapa tuna mtu anayejisema wazi kwamba ni mtu wake, na kuna some of us tunataka kudanganyika na maneno machache matamu aliyoyaweka kuficha makucha yake ya kweli?

Well, this is JF sio wote hapa wasahaulifu!, na akirudi tena basi tutaenda kufukua archives zote za Richimonduli zipo humu! Halafu atuambie jinsi Lowassa alivyo malaika wa Mungu!

Phweeeeew!


FMes!

Hapo kwenye red hutaki au unabisha? Lowassa is the NEXT PRESIDENT OF UNITED REPUBLIC OF TANZANIA ka hamtaki badilisheni uraia. Lowassa is the hardworker more than JK ndo maana mkasukia zengwe sababu mlijua atamfunika mzee mkubwa, hata sasa ushahidi upo si unaona sasa serikali inavyowayawaya Lowassa angekuwa bado waziri mkuu haya usngeyasikia, kusingekuwa na migomo vurugu wala nini sababu he knows what he is doing. Kuhusu suala la Richmond ni kosa la mfumo, vigogo wangapi wanacheza deal za kuwaibia watz ila wanapeta, afu hiyo issue hata mkulu anahusika mbona hamsemi mkaamua kumwangushia Lowassa jumba bovu kwa sababu mnazozijua nyie na unafiki wenu! EEEH? mlizani mnatoa kafara eeeh fikirini tena. Mbona ubilionea wa riz1 hamuusemi. hiyo Ndo fact Lowassa is the next Prezidaa la sivyo is the end of CC M
 
Hapo kwenye red hutaki au unabisha? Lowassa is the NEXT PRESIDENT OF UNITED REPUBLIC OF TANZANIA ka hamtaki badilisheni uraia. Lowassa is the hardworker more than JK ndo maana mkasukia zengwe sababu mlijua atamfunika mzee mkubwa, hata sasa ushahidi upo si unaona sasa serikali inavyowayawaya Lowassa angekuwa bado waziri mkuu haya usngeyasikia, kusingekuwa na migomo vurugu wala nini sababu he knows what he is doing. Kuhusu suala la Richmond ni kosa la mfumo, vigogo wangapi wanacheza deal za kuwaibia watz ila wanapeta, afu hiyo issue hata mkulu anahusika mbona hamsemi mkaamua kumwangushia Lowassa jumba bovu kwa sababu mnazozijua nyie na unafiki wenu! EEEH? mlizani mnatoa kafara eeeh fikirini tena. Mbona ubilionea wa riz1 hamuusemi. hiyo Ndo fact Lowassa is the next Prezidaa la sivyo is the end of CC M

Hehehheh wakimwaga mboga nanyi mnamwaga ugali! Safi sana
 
IKULU NI MAHALA PATAKATIFU SIO KILA MTU ANAWEZA KUKAA PALE KUWATUMIKIA WATANZANIA.

Bashe jua kwamba BABA WA TAIFA KATIKA KILA ALILOLISIMAMIA KATIKA UHAI WAKE WAPO WATANZANIA WATAYAHESHIMU MAWAZO YAKE DAIMA MILELE, HASA KATIKA KUWAPATA VIONGOZI WA TANZANIA.................

Hapo kuwa WATZ wanaheshimu mawazo ya Baba Taifa ni kweli na tupo wengi tunaoheshimu na kufata mawazo na ushauri wake narejea mawazo yake aliyoyatoa katika kikao cha NEC 1995 Dodoma. ''Kiongozi anaweza toka popote pale, lakini kiongozi bora na wa kutumainiwa na Taifa atatoka ndani ya CCM ....... na Watanzania wakikosa uongozi bora ndani ya CCM watautafuta nje ya CCM hapo nilipobold hapo ndo WATZ tumemsikia Baba wa Taifa, since CCM na viongozi wake wamezingua tunatafuta uongozi bora nje, na tutawapata. You were very right indeed
 
BIG UP BASHE! HOTUBA YAKO IMEOGA HALAFU IKAENDA SHULE. Tunajua ccm wapo watu wenye hekima na busara lakini walikuwa wanateswa na unafiki na nidhamu ya woga na sasa kutokana na sintofahamu ndani ya ccm- people are begining to show their true natural colors!
 
Wewe unachuki binafsi.....ingekuwa vema kama ungekuja na logical arguments hapa lakini ulichokujanacho nishutuma ambazo zimeelea na zinakosa mashiko. Bashe kaongea mambo ya msingi sana, na kama wewe ni CCM hiyo ndiyo tiba pekee kwa chama chenu, na sio DRAMA za kujivua gamba. Unachofanya wewe ndio kile alicho address bashe katika hotuba yake acheni kulumbana na kufikiria uchaguzi tu, wakati mna wasahau wanaowachagua na kugeuza majungu mtaji wa kisiasa......jenga hoja kama mwenzio alivyojenga na sio kuja na SIASA ZA MAJI TAKA!
CCM pia tuna tatizo la kutokubali ukweli na uwezo wa mtu hata siku moja huwezi kukubali uwezo wa mtu na badala yake watu ambao wana historia ya ukandamizaji na kupokonya nafasi za watoto wenzao wa tanzania na bado hata wasiwapitie na kuwasaidia baada ya kupora vyeti vyao ndio leo wanahubiri kuwa wanataka kuleta ukombozi wakweli wa mtanzania....angalia mbunge wa nzega chadema walimgundua kuwa ni mtu aliepora jina kijana mmoja aliefauru darasa la saba, na jina kla kweli la mh mbunge ni Said Nassoro, Huyu kigwangwal original ni fundi baskeli.......mwenezi wa cccm pia alipora jina la Mwigulu ambalo mwenye jina sasa ni muuza chumvi na yeye anafaidi maisha.........
 
Eti ni mchapa kazi.mhhhhhh Labda tumuulize Bashe Tofauti yake yeye na Lowasa kisifa za uongozi ni zipi?

Hii nchi itakuwa na laana kwa kweli,eti nani asiejua kuwa swala zima la ngonjera za mwakyembe dhidi ya lowasa ni siasa za makundi ambazo hatimaye chadema wakazibeba kumshambulia lowasa kwa kuwa vita vya panzi ni furaha ya kunguru......mwakyembe hawezi kumtendea haki edward kwa ukweli mmoja kuwa bado ana uchungu sana kundi lao kuanguka kwenye uchaguzi wa mwaka 2005, na majembe yao dhidi ya low yalianza toka gazeti la radi alilokuwa akiandika na kundi lao kwenye uchaguzi uliopita wa ndani ya chama yani 2005
Ukisoma taarifa ya richmond hakuna mahali ambapo unaona Low kasemwa bali preamble ambayo nayo imejaaa maneno ya kusikika na kuumwa sikio ambayo katika kamati inayo shughulikia mambo chini ya kiapo haipaswi kufanya hivyo na kuweka ni sehemu ya ripoti.
Mzee Lowasa umeifanyia kazi kubwa sana nchi yetu lakini ni vile watu hawaoni basi mmemchafua bila kujielewa kwa kutumika na wanasiasa uchwara, kuna marafiki zangu maDC wanasema kuwa tangu Low ametoka na wao wanajisikia wako likizo.Naweza kusema kuwa hakuna mwanasiasa ndani ya ccm au waziri yeyote anaeweza kusema kuwa ana uwezo wa kiutendaji kama wa Lowassa.Siasa haina uwezo wa kutoa kiongozi bora na ndio maana mimi sitaki kugombea siasa za tanzania.Siku moja historia itamuhukumu Lowasa kwa haki na itabaini wala haikuwa ajali ya kisiasa bali mpango kamili wenye nia ya kumfanyia political murder.Ole wenu siku aamue kutoka ccm kama mtaweza kusimama tena .aluta continua
 
sikuwahi kufahamu kuwa Bashe ana akili kiasi hiki....huyu jamaa angetufaa sana Cdm....wapi Zito? Tafadhali huyu jamaa tunamwitaji sana.
Nikweli mkuu huyu jamaa ni kichwa si utani Kile kipindi walipo mchakachua huko NZEGA, Zitto alimtatafuta ili ahamie CDM na agombee NZEGA kupitia CDM nahisi kuna ahadi alipewa NA CCM hadi akakataa
 
Kaka Bashe chukua tano, mambo uliyoyasema ni kweli kabisa. Tunahitaji vijana wenye miongozo kam ya kwako. Walitaka kuku maliza lakini haita wezekana.
 
Wewe Bashe ni msomali rudi kwenu somalia unaingia kwenye siasa kwa nguvu kuficha uraia kama A. Kinana alivyofanya kupitia jeshi. Jamani Tanzania tunaenda kubaya sijui wajukuu wetu ikakuwaje miaka hiyo

Nani kakwambia Bashe ni msomali, mama yake ni mnyamwezi. Na Bashe kazaliwa Tabora. Acha ubaguzi ndugu.
 
Lampard, Hongera sana kwa kujua historia ya nchi yetu. Mimi umenijuza mengi. Bila shaka na wewe umo ndani ya UVCCM...!

Hotuba ya Ndg yangu Bashe ni nzuri sana, wengine wamehoji kama ana moral authority ya kuongea alichokiongea, wengine wamehoji kama anajenga ama anabomoa, kama analitetea kundi lake ama 'CCM'. Mimi sipendi nimhukumu, Ndg yangu huyu, kwetu kumoja na mchezo wetu mmoja! Kuna mmoja amenifurahisha sana kwa kusema 'judge the message not a messenger!' Tufanye hivyo na sisi wanaCCM tutakisaidia chama chetu na nchi yetu.

Sitaki kuhoji kama Bashe amemlenga Nape ama la, lakini je Nape naye ana kundi lake ndani ya chama na Kigwangalla naye ana kundi lake ndani ya chama ama la? Kitu kikubwa kuliko sisi sote, kuliko makundi yote ni chama na cha muhimu kwa sasa ni kusafisha nyumba yetu na kuiimarisha zaidi ili tuendelee 'kutawala' (kutawala ni neno lililotumika hapa kisomi kama tafsiri ya 'kushika madaraka', 'to rule') - japokuwa misingi ya uongozi kama ilivyo kwenye katiba ya chama chetu iko wazi na inatutaka viongozi wa chama tuwe 'viongozi' kwa maana anayoitaka Bashe katika hotuba yake!

Kwa kiasi kikubwa, Bashe ameweka mtazamo wa kujenga image mpya ya chama kupitia kutatua matatizo ya wananchi kijamii na kiuchumi. Na huu ni mtazamo ulio kwenye vichwa vya wengi wetu ndani ya CCM, japokuwa kuna wengi pia wana taswira tofauti ya kukirudishia chama umaarufu wake ulioanza kushuka. Nao wana haki ya kufanya hayo.

Wakatabahu,
HK.

- Mungu Aibariki Tanzania!

William @ NYC, USA.
 
Du! This is very interesting!!!!!!

Lampard = Hkingwangalla in real life (Au mnataka nitoe ushahidi?). Lampard anamcriticize Bashe tena anaingia personal ile ya ukweli ukweli, the same Lampard in the pen name anajitokeza kwa jina halisi la Hkingwangalla na kumsifu Bashe. Eti hawa ndiyo vijana wa CCM wa kutuletea maisha bora kwa kila mtanzania. Thubutuuuu!
 
Du! This is very interesting!!!!!!

Lampard = Hkingwangalla in real life (Au mnataka nitoe ushahidi?). Lampard anamcriticize Bashe tena anaingia personal ile ya ukweli ukweli, the same Lampard in the pen name anajitokeza kwa jina halisi la Hkingwangalla na kumsifu Bashe. Eti hawa ndiyo vijana wa CCM wa kutuletea maisha bora kwa kila mtanzania. Thubutuuuu!

Sarakasi hizi na Bashe naye anaingia kwa Zyansiku......mambo juu ya mambo!
 


- Ndg william sikutaka kukujibu ila nikusaidie kwakuwa umekuwa nje ya nchi inawezekana huna taarifa nyingi za hapa Nyumbani,sikumjadili mangula usitafute chaka la kuficha maovu ya Baba yako hili la malecela kuhusika na EPA limeongelewa kwa mud mrefu na Vyombo vya habari hapa Nyumbani,ukiongelea UFISADI malecela nae ni FISADI tena ni miongoni ambao mwalimu Nyerere aliwataja katika KITABU chake alichoandika kuhusu HATMA YA UONGOZI WA NCHI YETU,thats why nilisema tukiongelea swala la UADILIFU wewe BINAFSI NI ZAO LA VIONGOZI WASIO WAADILIFU dont take it personal ,kinachoumiza taifa leo kuna ambao wamekuwa sehemu ya mfumo mbovu ,sehemu ya matokea ya mfumo huo lakini mbele ya PUBLIC wanajionyesha ni watu wema sana kama ulivo wewe,hatuwezi kujadili UFISADI,ama UADILIFU tukakuacha wewe Nje thats why niliamua kufunga mjadala wa LOWASA na kuomba let us not agree on this.


- Mheshimiwa Bashe, heshima yako sana; kwanza kabisa ningekuomba ufungue mjadala wa Malecela, ili tuweze kujadili huu mjadala wako bila ya kutoka nje ya mada: HOWEVER nitajaribu kukusaidia kwa kutoka nje kidogo ya mada: Malecela amekua kiongozi wa taifa toka akiwa na umri mdogo sana wa miaka 22, alianza na u-DC Tukuyu, sasa tizama kwamba katika miaka yote ya utumishi wake kwa taifa wewe na wanaokutuma hapa yaani MAPACHA WATATU, mlichonacho ni EPA over him? Kwa hiyo unasema Malecela amekuwa muaminifu huko nyuma kote, isipokuwa akiwa mwishoni mwa utumishi wake kwa taifa, ndio kwa mara ya kwanza taama ya kuiba tena EPA ndio ikamshika? ha! ha! ha! ha!

- Bashe wizi wa mali za umma ni tabia ya kwenye damu, kitabu cha Mwalimu ninacho na inaonejkana hujakisoma, ungekisoma ungejua kwamba Mwalimu hakuwahi kumtuhumu Malecela kwa kuiba anyting, lakini niambie ni mwananchi gani wa taifa hili asiyejua Mwalimu alisema nini kuhusu Bosi wako Lowassa? Alisema ni mwizi infact alimfananisha na Escobar yule M-Colombia wa maunga, amabye kazi yake ilikuwa kuuza unga na kujenga majumba, Mwalimu alisema Lowassa ni sawa yule jambazi Escobar kwa sababu Lowasaa akiwa Waziri wa Ofisi Ya Waziri Mkuu, aliiiba hela za magari ya wabunge na kujenga kijiji cha kukodi kule Arusha.

- Kuhusu wewe sikufahamu vizuri lakini sio siri kwamba uko kwenye payroll ya nani kwa maneno yako hapa maana yanajisema wazi sana! CCM walikufukuza uongozi kwa sababu ya kutokuwa na maadili, halafu wakakuondoa kwenye kuogmbea ubunge kwa sababu huna maadili, baba yako simjui, lakini at least taifa hili lina ushahidi wa kutosha kuhusu matendo yako mabovu ukiwa kiongozi, ndio maana wakakuondoa kwenye uongozi, na sasa naona unajaribu sana kurudishwa na MAPACHA WATATU kwa sababu huku UV-CCM ndiko peke yake bado mna mikono yenu na mnajaribu kiola njia kuishikilia kwa nguvu, lakini tumeshagundua janja yenu.

- Bashe mimi sio kiongozi, wewe ndiye kiongozi katika umri wako huo mdogo tayari umeshafukuzwa sehemu mbili muhimu za uongozi wa taifa, sasa unataka nini tena? Moral authority ya kukusanya maoni kuhusu UV-CCM taifa umeipata wapi? Umepewa na hawa MAPACHA WATATU, Moeral authority ya hiyo hotuba yako umeitoa wapi? only in Tanzania, ambapo kiongozi anaweza kufukuzwa mara mbili kwenye taifa na bado akaweza tena kwenda kutoa hotuba kwa ukali, akijidai kujua sana matatizo ya UV-CCM, huku tayari akiwa ameshaharibu mara mbili, unasema ninahitaji kuishi Tanzania kujua haya kwamba huna uwezo wa uongozi na huna Moral authority ya kukusanya maoni yoyote, labda ya namna ya KUWASAFISHA MAPACHA WATATU, kama unavyoonekana kujitahidi sana, you almost did it here, lakini pale uliposema lowassa anafaa na utampigia kura ndipo ulipoharibu!

- Infact, nina wasi wasi sana na elimu yako pia, maana ungekua nayo basi ungeelewa kwamba hapa JF wananchi tupo huru sana sio kama huko UV-CCM ulikowakomalia na B/S tupu ambazo wewe mwenyewe zimekushinda kuzitimiza kwenye uongozi ndio maana twice umefukuzwa na taifa, I understand kwamba umekuja na watu wako wengi with you hapa JF nilishafahamishwa mapema maana kwenye hayo makundi yenu huwa hamna siri, karibu sana isipokuwa nikutahadharishe one thing, maandishi hayafutiki, na mimi sio kiongozi wala sigombei nafasi yoyote ya taifa so sina anything to lose kwa kulumbana na hoja zako mbuzi sana, HOWEVER NITAKUJIBU MPAKA WANANCHI WAJIONEE WENYEWE UTUPU WAKO WA HOJA, AMBAO UNATHIBITISHA KWAMBA CCM WALIPOKUFUKUZA NAFASI ZAO ZA UONGOZI WALIKUWA RIGHT 100%, I mean wananchi hawana umeme, Tanzania tunalipa Billions zetu za kodi kwa ajili ya umeme ambao haupo, wewe unasema the master minder wa hii National demise utampigia kura maana kama ana makosa kwa nini hajachukuliwa hatua?

- Lakini unashindwa kujibu swali dogo sana kwamba kwa nini bosi wako unayejaribu sana kumsafisha hapa Lowassa alikimbia kule Bungeni U-Waziri Mkuu bila kufukuzwa?


Mheshimiwa Bashe, karibu sana!

William @ NYC, USA.




 
-Niweke record sawa sawa katika hili sikusema niko hapa kushindana bali nilisema tufunge mjadala huu wa lowasa kwani huu si wakati sahihi wakujadili hoja ya lowasa na nimekuwa clear kwamba tusubiri muda ufike kama atagombea na kuteuliwa binafsi kama mpiga kura nitampa kura yangu unless nipate hoja,sababu za msingi sio hizi hoja zako eti nilienda texas kupiga picha,mara ooh tulipambana kubenea akadhurika tutajuaje kama wewe na wale walioaminisha umma kwamba ni wapambanaji walikuwa sehemu ya mkakati ili mfanikishe mnayotaka basi mumdhuru kubenea ili kujenga imani na kufanikisha mpango wenu.Swala la kubenea kuumizwa kinyama halikuwa jambo jema,lakini ni makosa vilevile kutumia maumivu ya kubenea kuhalalisha ile sinema ya kuigiza.

Usipotoshe watu kwamba nilikuwa nafoka ,usiaminishe watu kwamba wewe ndo unaweza kufikiri kuliko wote waliokuwa katika kikao hicho,usiaminishe umma kwamba waliohudhuria hawana taarifa za kutosha juu ya Taifa lao,kilichokuleta speed hapa si msingi wa mjadala uliokuwepo bali ni swala la kusadikika lililojengwa na LAMPARD na hoja ya Makundi,mimi kundi langu mmelitaja na kulitamka sasa WEWE na LAMPARD kundi lenu ni lipi?mmenihukumu mm nipo kwa maslahi ya kundi flani,je nyinyi mnasimamia maslahi ya kundi lipi?na kundi hilo lipo kwa maslahi ya mtu yupi?


- Well, unasema mpaka leo hujaona hoja wala sababu ya msingi against Lowassa, ni kwa sababu mpaka leo hujaona hoja na sababu ya msingi ya wewe kufukuzwa uongozi wa taifa mara mbili, sasa nyani si kawaida kutoona his behind, I mean wananchi wanahangaika na umeme wa mgawo, wewe unasema huoni sababu za msingi against Lowassa, pamoja na Lowasaa kuondolewa NEC na CC wewe huoni sababu ya msingi against Lowassa, na with all this unaamini kwamba you are good enough kukusanya maoni ya taifa kuhusu UV-CCM?

- Umezoea kuishi kwa kufikiri kwa makundi sasa unaamini kwamba hata wananchi wote wana makundi, maana ndivyo ulivyozoeshwa kufikiri na hao MAPACHA WATATU WALIOKUTUMA UJE HAPA!, mimi sina kundi lolote kundi langu ni taifa langu tu, nimesoma hotuba yako na kuona ni very shallow kwa sababu kwanza umeandikiwa na MAPACHA WATATU kwa nia ya kutaka kuwasafisha, halafu wewe uliwahi kuwa kiongozi mbona huku-implement hayo mawazo unayoweza kuyasema kwa nguvu ukiwa kwa nje? Hawasafishiki wale ndio maana CCM tumewaondoa kwenye NEC na CC, na wewe pia tulikuondoa kwenye nafasi mbili za taifa, simply ni kwamba hamfai na hamsafishiki.

- I understand kwamba umetaja kundi lako la MAPACHA WATATU, mimi sina kundi zaidi ya Taifa na mimi sio kiongozi na wala sigombei anything, ishu yangu ni kwamba umehutubia wananchi wasio na uwezo mkubwa sana wa kufikiri, wangekua nao wangekuuliza wewe mbona umefukuzwa mara mbili na taifa sasa uwezo wa kuwafundisha what is wrong and what is right kwenye ile hotuba yako umeutoa wapi?

- Sasa badala ya kujibu hoja hapa unalilia Malecela! ha! ha!, hapa hamna baba yako wala wa mtu yoyote, hii ndio JF simama hapa ubebe msalaba wako!, Bashe sikutaka kufika kote huku ila ni wewe mwenyewe na washauri wako ndio mmenifikisha, so lest talk! Naona ulifikiri jina la Malecela litakuokoa hapa! ha! ha! ha!ghrrrrrrrr! lahaula! ha! ha! ha!

Ahsante Mheshimiwa!

William @ NYC, USA.





 
Game-of-Thrones-TV-Series.jpg
 
Many thanks Billy! Bashe under the Microscope!! keep bringing many thruths to light.....Pamoja mkulu!
 
Back
Top Bottom