UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina

UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina

Nyie nani kawaambia sio raia? mama yake mnyamwezi.Unajua hakuna mtu mbaguzi kama mwaafrika sema tu hakujaliwa
Hata kama waziri amesema Bashe ni raia sisi kama CCM bado tunamuona si raia" - Luteni (mstaafu) Y Makamba......................:heh:
 
Mheshimiwa Bashe: ninaomba sana nisaidie kujibu huu ujumbe wako kwa sababu no question unaelekezwa kwangu zaidi kuliko uliyetaka kumtumia, na ninaomba sana nikuaminishe kwamba mimi ninasimamia taifa kwanza na sio majungu na hadithi hadithi za mitaani.

1. Sikufahamu sana, lakini kwa maneno uliyoanza nayo umenipa wasi wasi sana na uwezo wako wa uongozi wa juu na hata kufikia kuwa ndiye mkusanyaji wa mawazo ya wananchi on UV-CCM: Hela za EPA zilikuwa ni hela za Mtandao ambao Malecela alikuwa ni their number one enemy, nitakuamini kwamba unasema ukweli iwapo utaonyesha karatasi yoyote ile iliyosainiwa na Malecela kuchukua hela kutoka BOT on the behalf of CCM.

- Unaropoka ropoka kuhusu Mama Kilango na kuvamiwa na majambazi pale Mvomero, hapa ndipo nimekutoa heshima kabisaa kwamba huna maana kabisaa kwa hili taifa, Mama kilango alikuwa akitokea kwangu hapa New York kuchukua malighafi zake za biashara zake, kwenye maduka yake ya Dar na Dodoma, ni kawaida yake kila anapofika huko kugawanya bidha zake kati ya dula lake la Dar na zingine husafiri nazo kwende kwenye duka lake la Dodoma, kwenye lile alikuwa amebeba masanduku ya nguo za biashara na kwenye pochi yake alikuwa na Shillingi laki mbili tu, na hata kwenye kesi mahakamani wale majambazi walikiri kwamba ndizo hela walizozikuta kwenye pochi waliyokimbia nayo, masanduku yalikuwa ni mazito sana yaliwashinda kabisa kukimbia nayo wakayaacha pale pale, sasa unasema Shiilingi laki mbili ndio zinaweza kununua urais wa Tanzania mwaka 2005!

- Halafu kwa taarifa yako kesho yake hawa majambazi walimvamia Makongoro Nyerere na kumpora kila kitu vipi na yeye alikuwa anagawa hela za rushwa wa Urais?

- Una maana Mvomero ndio wanaamua Rais wa Tanzania awe nani kwamba Mama kilango na Makongoro walikwenda kugawa hela pale? ha! ha! ha!

2. Malecela facts na Lowassa ni kwamba wabunge wanne walipokwenda Chamwino kumuona Rais kuhusu kumuokoa Lowassa na Uwaziri Mkuu, Makamba, Ameir, na Kingunge walimtetea Lowassa ni Malecela peke yake aliyegoma kwamba ni lazima aondoke, yes hilo aliniambia, asingeweza kuniambia uongo ambao haukufanyika! Mimi simchukii Lowasaa as a person lakini nina tatizo sana na kazi zake akiwa Waziri mkuu, hasa ninapoona taifa letu linalipa mabillioni ya pesa kwa Umeme ambao haupo nina haki zote za kukemea aliyetufikisha hapo kama ulivyoona kwenye ile topic niliyoianzisha jana ya kujivua.

- Unasema wewe matatizo ya Richmond hayakuhusu maana ni mapungufu ya mamlaka zetu kwa kutokumchukulia hatua and you want to be a leader wa hili taifa?

well, nilitaka kugusa haya tu mkuu sana, ninaamini Mkulu FMES naye atakujibu kama ulivyomu-address kwenye ujumbe wako, karibu sana mkuu, nothing personal ila NI TAIFA KWANZA!


William @ NYC, USA.

You guys dnt personify your arguments...
 
Hawa ni Waarabu wa Pemba wanajuana kwa vilemba. wote ni Magamba a.k.a Mafisadi
 


- Mheshimiwa Bashe, suala la Malecela na Mangula na EPA kusemwa majuzi sana kule Tabora, tulisema wazi lina mkono wa mafisadi baada ya kutemwa NEC na CC, na hapa sasa wewe mwenyewe unathibitishia wazi kwamba ni kweli, Bashe hizi siasa mmejifunzia wapi where unaishia kusema usichotaka kusema? Ha! ha! ha! ha! ha!

- Ndg william sikutaka kukujibu ila nikusaidie kwakuwa umekuwa nje ya nchi inawezekana huna taarifa nyingi za hapa Nyumbani,sikumjadili mangula usitafute chaka la kuficha maovu ya Baba yako hili la malecela kuhusika na EPA limeongelewa kwa mud mrefu na Vyombo vya habari hapa Nyumbani,ukiongelea UFISADI malecela nae ni FISADI tena ni miongoni ambao mwalimu Nyerere aliwataja katika KITABU chake alichoandika kuhusu HATMA YA UONGOZI WA NCHI YETU,thats why nilisema tukiongelea swala la UADILIFU wewe BINAFSI NI ZAO LA VIONGOZI WASIO WAADILIFU dont take it personal ,kinachoumiza taifa leo kuna ambao wamekuwa sehemu ya mfumo mbovu ,sehemu ya matokea ya mfumo huo lakini mbele ya PUBLIC wanajionyesha ni watu wema sana kama ulivo wewe,hatuwezi kujadili UFISADI,ama UADILIFU tukakuacha wewe Nje thats why niliamua kufunga mjadala wa LOWASA na kuomba let us not agree on this.

- I mean unashindwa kuelewa a very simple idea ya hii mijadala JF kwamba sio kushinda ila ni kuelimishana kihoja na wakati ni huu wa sasa, umeenda huko kwenye UV-CCM umewakaripia wee masikini wa Mungu wasioelewa kitu, sasa unakuja hapa unatakiwa kusimamia hoja zako mwenyewe, unalilia Malecela! ha! ha! ha! Malecela ndiye aliyekuambia umtetee Lowassa? Now seriously what Malecela has to do na msimamo kwamba Lowassa ni matatizo ya mamalaka zetu kama ana makosa mbona hawajamshitaki kwenye sheria, kweli this is all you could do kutetea msimamo mzito kama huo?

-Niweke record sawa sawa katika hili sikusema niko hapa kushindana bali nilisema tufunge mjadala huu wa lowasa kwani huu si wakati sahihi wakujadili hoja ya lowasa na nimekuwa clear kwamba tusubiri muda ufike kama atagombea na kuteuliwa binafsi kama mpiga kura nitampa kura yangu unless nipate hoja,sababu za msingi sio hizi hoja zako eti nilienda texas kupiga picha,mara ooh tulipambana kubenea akadhurika tutajuaje kama wewe na wale walioaminisha umma kwamba ni wapambanaji walikuwa sehemu ya mkakati ili mfanikishe mnayotaka basi mumdhuru kubenea ili kujenga imani na kufanikisha mpango wenu.Swala la kubenea kuumizwa kinyama halikuwa jambo jema,lakini ni makosa vilevile kutumia maumivu ya kubenea kuhalalisha ile sinema ya kuigiza.

Usipotoshe watu kwamba nilikuwa nafoka ,usiaminishe watu kwamba wewe ndo unaweza kufikiri kuliko wote waliokuwa katika kikao hicho,usiaminishe umma kwamba waliohudhuria hawana taarifa za kutosha juu ya Taifa lao,kilichokuleta speed hapa si msingi wa mjadala uliokuwepo bali ni swala la kusadikika lililojengwa na LAMPARD na hoja ya Makundi,mimi kundi langu mmelitaja na kulitamka sasa WEWE na LAMPARD kundi lenu ni lipi?mmenihukumu mm nipo kwa maslahi ya kundi flani,je nyinyi mnasimamia maslahi ya kundi lipi?na kundi hilo lipo kwa maslahi ya mtu yupi?


- Ninakushuru sana kwamba umetutaja sana JF kwenye media kwamba utatutumia na tume yako, that is all I see to be good kwenye hotuba zako, otherwise please Brother unahitaji ukarabati hali ya juu sana kuhusu kusimamia hoja zako hapa, sio wote hapa tumelala usingizi kama huko UV-CCM, nimeisoma sana hotuba yako sikutegemea kwamba watu wazima wenye akili timamu walikuwa wamekaa wanakusikiliza mwanzo mpaka mwisho bila hata kukuuuliza maswali!

-Katika hili tafsiri ya nani kalala na nani kaamka ni subjective inawezekana wewe ukawa na usingizi mzito wakati ukihisi umeamka,hotuba yangu inawezekana usiipende sana lakini hayo ni mawazo yangu ambayo wewe pia unayako ,haki uliyonayo wewe kuyapinga yangu,ni haki hiyo hiyo niliyonayo mimi kukataa mawazo yako,si lazima tufikiri sawa,tuamue sawa,ikitokea hivo wote tutakuwa na matatizo,na si lazima hapa katika forum tukawa wote na mtazamo unaofanana,na si lazima ukalazimisha nione unachoona na mm silazima nikakulazimisha ukaona ninachoona.

Nilisema tuufunge mjadala huu hapa kwani muda wa mjadala juu ya swala hili si sasa na tusipoteze nguvu nyingi sasa kujadili haya mambo,2014 tutakutana jamvini kujadili nani anafaa kuwa Rais wa Nchi yetu regadless anatoka wapi,sasa tutumie muda kujadili BEI MCHELE,BEI SEMBE,AJIRA,STABILITY YA UCHUMI WETU,UMOJA WA KITAIFA,KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA,NAULI ZA DALA DALA ZINONGEZEKA WAKATI VIPATO VYETU BADO DUNI,BEI ZA MAFUTA,TATIZO LA UMEME(Wewe hili hulifahamu bcs utotoni ulikaa upanga,unatumia jenereta,na sasa ukirudi likizo unatumia jenereta nyumbani na huko ulipo hamna mgao wa 16hrs) na kwa sisi wana CCM namna gani tunakisaidia chama kutekeleza majukumu yake kupitia serekali ili kuleta TIJA katika maisha ya watanzania ,haya ya lowasa na wengine si ya tija kwa sasa.Matatizo yetu hapa nyumbani ni ya msingi sana kuliko kujadili hayo unayotaka sasa tuyajidili.

- Well, karibu sana mkuu ukweli ni kwamba hapa hatushindani ila tunaweka hoja na wananchi wanaamua mchele na pumba zilipo, ila seriously sikufashamu sana ila sikutegemea this coming from you, wewe mwenyewe kaa chini uangalie hotuba yako na haya majibu yako hapa JF utajionea mwenyewe tofauti ilivyo kubwa sana na ndio inayotupelekea wengine wetu hapa kuamini kwamba ile hotuba hukuandika wewe, anyways karibu sana mkuu tulemishane kuhusu taifa letu, hopefully na wengine kama wewe huko CCM watakuja hapa kusimamia hoja zao, kama ulivyofanya, inatupa nafasi wananchi kuwaelewa vizuri, maana baada ya kukusoma hapa sasa sina wasi wasi kabisa kwamba ukipewa uongozi wa juu nitegemee nini toka kwako!

Mwisho inawezekana ulitarajia nifikiri kama wewe ambae umekulia ndani ya mfumo huu,ume enjoy matunda na sasa upo nje ya nchi ukiwa hujui bughudha za daladala,hujui tatizo la mgao ulitaka niimbe ngonjera zako, nimalize kwa kusema tena Turudi katika msingi wa mjadala wangu,nilichosema ninakiamini,nitakisimamia sitabadili msimamoa katika hilo unless kuwe na Tangible Facts juu ya yale uliosema,Kuhusu kuandikiwa hotuba ni vizuri umesema hunifahamu kwahiyo kama walivosema wahenga USILOLIJUA NI USIKU WA GIZA,so nivizuri ukapata muda kidogo kunifahamu na hilo utaweza tu kama utajipa muda kunifahamu.


MUNGU AIBARIKI JF!

MUNFU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA

William @ NYC, USA.


Hussein M Bashe
 
Nimeona kwa vipindi tofauti, watu wakijajaribu kutumia maoni au mawazo fulani ya mwl Nyerere kujenga hoja zao, ni kweli kabisa kwamba mawazo ya Mwl Nyerere ambaye ndiye muasisi wa taifa letu ni muhimu sana kwenye kuamua mustakabali wa nchi yetu na ndiyo maana maoni yake yametumika kuua ndoto za urais za watu wengi, wakiwamo wakina Mzee Malecela na wengine wengi, akiwemo pia Mark Bomani kwa hoja ya kukataa Rais kutoka sukumaland or kanda hiyo, lakini ikatumiwa hoja ya ujaji wake kumzuia. Tunatakiwa kumuenzi Mwl Nyerere siku zote, lakini tuwe makini tunatumiaje maoni yake. Kwa taarifa ambazo hazipingiki ni kweli kwamba Lowassa alikuwa groomed kiuongozi na Mwl Nyerere kwenye Chama tangu wakati ule akisoma UDSM, na vijana wengine waliokuwa kwenye kundi hilo wakiwemo Kikwete, Kinana, Marehemu Ditoplie na wengineo, na Nyerere huyo huyo alikuwa akimtumia Lowassa kumuwakilisha sehemu nyingi kichama, wakati huo Lowassa akiwa msaidizi wa Marehemu Mzee Kawawa pale Lumumba, lakini baada ya Mwinyi kuingia madarakani 1985 na Mwl Nyerere kurudi butiama, ingawa bado alikuwa anapatikana msasani na safari zake mikutano yake ya kimataifa duniniani, lakini officiially address yake ikawa butiama na tuliona viongozi wengi wakienda huko kwa ushauri wakati ule. Ilianza kuonekana feeling fulani kama Mwl Nyerere amenyangnywa nchi yake aliyokuwa anaipenda, maneno ya mtaani yakawa kwamba Mwinyi alikuwa hamuheshimu tena Nyerere na alikuwa haendi kuomba ushauri wa kila jambo, ghafla uadui ukahamia hadharani na Mwalimu akawa akimtukana Rais mwinyi aliyekuwa Ikulu kwa matusi mengi mengi hadharani. Tutakumbuka alisema unakuwaje Rais ambaye ukifika kitandani nyumbani halafu mkeo anabadilisha maamuzi yako ya nchi - sijui ingekuwa leo tungesemaje?? hehe . Kwahiyo umaarufu wa kisiasa walioupata Lowasa na Lyatonga wakati ule kuelkea 1995 uliasisiwa na kubarikiwa na Mzee Mwinyi, na alichokiona Mwl Nyerere ni kwamba atazidi kupoteza clout yake kwenye maamuzi ya nchi akiruhusu hayo kutokea na ndiyo maana akaanza politcal games zake - hamna anayemzidi hapa Tanzania, akahakikisha anamshawishi Lyatonga kuhamia upinzani NCCR, akijua haiwezekani dola iruhusu nchi ichukueliwe na upinzani kwa wakati ule na Lowasa akaambiwa kwa makusudi kwamba akahukue fomu pamoja na Kikwete - ambaye hakuwa na umaarufu wowote wakati ule, lakini Nyerere akijua kichwani kwake anamtaka nani na hawa wote wakaingia kwenye mstari. Kwa umaarufu wa Lowassa wakati ule, ni ukweli usiopingika kwamba angeenda kwenye mkutano mkuu, angeshinda na angekuwa Rais 1995, kama amabvyo Mzee Malecela angeingia kwenye mkutano mkuu 2005, angesumbua, kwahiyo njia rahisi ya wagombea kama hawa ni kuwakata majina kwenye kamati kuu. Kulikuwa na mvutano mkubwa sana ndani ya kamati kuu kuhusu Lowassa kipindi kile na ikabidi kujenga hoja ya nguvu ili kumzuia, zikaletwa tuhuma za kuchonga ambazio kamati kuu ilitupilia mbali, lakini Mwl Nyerere akatumia VETO kujenga hoja yake na hamna mtu anaweza kumpinga, lakini baada ya pale, kama baba na watoto wake aliowapenda< aliwaita wote mmoja mmoja pale msasani na Lowassa akaambiwa una miaka 42 tu, natambua uwezo wako mkubwa sana, subiri wakati wako utafika, usiwe na papara na siyo hvyo tu, wasaidizi wake wa karibu wanasema Mwalimu alikwenda Geneva na kukutana na kundi la Watanzania waliohoji kutoswa kwa Lowassa, akasema kwenye vijana niliowa-groom, huyu ndiye mwenye uwezo zaidi, ila sasa haikuwa muda wake, niachieni, najua ninachofanya. Kuna mazuri mengi sana na mabaya aliyoyafanya Mwl Nyerere na tunatakiwa kumuheshimu siku zote kwasababu Baba wa Taifa atakuwa mmoja tu kwa Tanzania lakini tusishabikie maoni yake au maamuzi, ni muhimu kuyajadili na kufanya tathmini jinsi ambavyo yatatusaidia kwenda mbele na maendleo ya nchi yetu. Nawasilisha
 
Kwa taarifa ambazo hazipingiki ni kweli kwamba Lowassa alikuwa groomed kiuongozi na Mwl Nyerere kwenye Chama tangu wakati ule akisoma UDSM, na vijana wengine waliokuwa kwenye kundi hilo wakiwemo Kikwete, Kinana, Marehemu Ditoplie na wengineo, na Nyerere huyo huyo alikuwa akimtumia Lowassa kumuwakilisha sehemu nyingi kichama, wakati huo Lowassa akiwa msaidizi wa Marehemu Mzee Kawawa pale Lumumba, lakini baada ya Mwinyi kuingia madarakani 1985 na Mwl Nyerere kurudi butiama, ingawa bado alikuwa anapatikana msasani na safari zake mikutano yake ya kimataifa duniniani, lakini officiially address yake ikawa butiama na tuliona viongozi wengi wakienda huko kwa ushauri wakati ule.

Hahahahah sarakasi hizi! Lowassa na ufisadi wote kweli aje kuwa raisi wa nchi? Hebu acheni mazingaobwe of all the peoples Lowassa kabisa? Kwanza huyu avuliwe Gamba na kufukuzwa CCM ni mwizi na Fisadi.....hatutaki maneno le eti alikuwa groomed na Nyerere hahahahaha kituko hiki. Nyerere huyo huyo alimuuliza kijana mdogo kama wewe umetoa wapi huo utajili ....kifupi hafai hafai kabisa.
 
FMES,

Nikuombe jaribu kuficha hasira zako kwa Lowassa. Haki na Uhuru wa mimi kumuunga mkono LOWASSA akitangaza NIA, na KUTEULIWA na chama changu ni haki yangu ya Kikatiba kama ilivyokuwa haki yako mwaka 2005 kumuunga mkono Mzee Malecela.

Ni kichaa aliyelazwa Mirembe peke yake leo anaweza kumtetea Lowasa

Nikuombe uheshimu haki yangu ya kutoa maoni yangu kama wewe ulivyotoa maoni yako ukitaka wagombea wajitokeze..

Bila kujali chama wagombea wanatakiwa wawe safi lakini sio Lowasa tena

Leo mimi nimejitokeza openly na kusema ninachokiamini sijaongelea suala la whether Lowassa ana tuhuma ama hapana,

Nashangaa sana na kujiuliza kwa nini huwa unaitetea kwa nguvu sana hii Richmond/Lowasa? utakumbuka kwenye kura za maoni Pale Nyasa/Nzega mzee mmoja alikuuliza jambo hili na wewe ulifura mishipa ikikutoka na kumjibu kuwa eti hiyo ni pesa ndogo tu ukilinganisha na pesa iliyotumiwa na kamati ya Mwakyembe, kweli huo ndio utetezi makini?

tukianza kufukua tuhuma hata mzee wako ana tuhuma za kupokea fedha za EPA kupitia Jeetu Patel lakini hakuna aliekutuhumu kwa wewe kumuunga Mkono 2005 na pale Morogoro zilipoporwa na wezi wakati mama Anne Malecela akizileta kugawia wapiga kura.


Kama tuhuma hizi ni za kweli basi mshauri Mwenyekiti wako ambaye ndie Rais aagize watu wake haraka afunguliwe mashtaka


Leo hapa nimesema ninachokiamin, come out sema kama Lowassa hana sifa niliyotaja then utakuwa na hoja ukinipa sababu za yeye kutokuwa na uwezo wa kuchapa kazi na ukajenga hoja nitakuelewa.

Kwanza Lowasa alikataliwa na Mwalim kwa utajiri usio na maelezo na mpaka leo hawezi toa maelezo, pili tumemwona kwenye dili la Richmond achilia mbali lile dili lililokwama la kutengeneza mvua na jamaa zake waThailand

Tusipige porojo eti Lowassa alimfata Rais na kubembeleza, go and ask Mr. Malecela and he will give u the facts ambazo wengi hawapendi kusikia. Kama Lowassa anahusika na Richmond apelekwe mahakamani,

Serikali inayoongozwa na CCM ndio inayowajibika kumpeleka Mahakamani na si mwingine

hakuna anayemtetea na wala hilo halina mjadala; mahakama itaamua, kama Lowassa ni mwizi basi ni udhaifu wa mamlaka kutowakamata wezi na kuwapeleka mahakamani. Kama una ushahidi peleka katika authority uje hapa utueleze umepeleka ushahidi wa wizi wa Lowassa na hata mimi nitakuona hero!

Ushahidi gani tena wakati Mwakyembe alimaliza kila kitu?

Tujadili facts mkuu, tusiingilie uhuru wa mtu kuchagua. Nimesema wazi kama chama kitamteua nitampigia kura na nimetoa sababu yangu, na si Lowassa pekee, same applies kwa CDM, wakisimamisha mgombea hawezi kuwa mkamilifu wa kila kitu lakini kila mmoja atahakikisha anampigia kura.

Uhuru gani huo wa kuchagua fisadi?

FMES na Wana JF,

Tusipoteze muda mwingi kujadili LOWASSA, huyu kama ana madhambi yake mamlaka husika zitachukua hatua zinazostahili. Nchi yetu ina bahati mbaya tumekumbwa na ugonjwa wa unaoitwa ‘LOWASSA’, tujadili issues za maendeleo.

Ni kweli cancer hii "Lowasanoma" inahitaji A good amputation including all lymph nodes behind it

Nikutoe shaka juu ya jambo moja: Ssina historia ya kuficha wala kutafuna maneno katika jambo ninaloliamini, kama wewe ulifanya kazi ya kutafuta ushahidi juu ya mkataba mbovu wa Richmond, nikupe hongera ulitekeleza wajibu wako kama RAIA mwema. Kama utaongelea UADILIFU, wewe mwenyewe ni zao la UKOSEFU wa UADILIFU wa Viongozi wetu. Suala la RICHMOND ni udhaifu wa mfumo wetu,

Si kweli kwani Richmond ilikuwa ni uizi wa mchana kweupe kwa kukosa uadilifu wa waajiriwa wa serikali waliotokana na CCM

jambo ambalo mpaka leo linatugharimu kama Taifa. Tumelalamika, tumetuhumu, tumekosoa lakini hatujajadili ufumbuzi wa tatizo lililoleta RICHMOND. Leo ni mwaka wa sita bado tatizo lipo lakini bado tunajadili RICHMOND na LOWASSA.


Na tatizo hili usijidanganye ukifikiri litakwisha bila siku moja wahusika kuwajibishwa ambao ni Lowasa na tajiri yako Rostam

FMES, don't fool people here, tunafahamu why unakuwa na hasira when it comes to LOWASSA. Ni tatizo la familia yenu na ni makovu ya 2005. Nimalize kwa kusema LOWASSA akiteuliwa na kupitishwa na chama nitamuunga mkono asipoteuliwa na asipopitishwa na chama pia nitaheshimu na kufanya maamuzi kutokana na wakati na mazingira ya wakati huo, hiyo ni imani yangu.

Hata Dovutwa naye ana watu waompenda awe kiongozi wetu

Mimi nimesema msimamo wangu na kwa jina langu, wewe come out and sema msimamo wako. Kila mmoja wetu atakuwa na maamuzi yake tuyaheshimu, akini kwa sasa tujadili masuala ya NCHI yetu na tutimize wajibu wetu. Wewe binafsi huna moral authority kuongelea uadilifu bcs your background inaonyesha, lakini hatukuangalii kwa Background yako tunakuangalia wewe na unachosema kwa sasa.


Hussein

Kwa yote uliyosema wenye akili zao umewapa mwanga zaidi kuliko ilivyokuwa hapo nyuma
 
Hahahahah sarakasi hizi! Lowassa na ufisadi wote kweli aje kuwa raisi wa nchi? Hebu acheni mazingaobwe of all the peoples Lowassa kabisa? Kwanza huyu avuliwe Gmaba na kufukuzwa CCM ni mwizi na Fisadi.....hatutaki maneno le eti alikuwa groomed na Nyerere hahahahaha kituko hiki. Nyerere huyo huyo alimuuliza kijana mdogo kama wewe umetoa wapi huo utajili ....kifupi hafai hafai kabisa.

hehehehe, Rev Masanilo, wewe ni senior kidogo, epuka ushabiki na tujaribu kusaidiana kueliminishana humu kwenye forum, argument yangu wala haikuwa kuhusu Urais wa Lowassa, lakini kuna mtu hmu ndani alisema tunauguzwa homa ya Lowassa, tukisikia jina tu, tunafikiria Urais. Kasheshe nzito

Hoja yangu ni kwamba mawazo au maoni ya Mwl Nyerere siyo msaafu, lakini lazima tuendelee kumuenzi na kumuheshimu siku zote, lakini kufanyia tathmini za kina mambo aliyofanya ili utusaidie kwenda mbele. Hayo mengine nadhani siyo thread yake hii
 
hehehehe, Rev Masanilo, wewe ni senior kidogo, epuka ushabiki na tujaribu kusaidiana kueliminishana humu kwenye forum, argument yangu wala haikuwa kuhusu Urais wa Lowassa, lakini kuna mtu hmu ndani alisema tunauguzwa homa ya Lowassa, tukisikia jina tu, tunafikiria Urais. Kasheshe nzito

Hoja yangu ni kwamba mawazo au maoni ya Mwl Nyerere siyo msaafu, lakini lazima tuendelee kumuenzi na kumuheshimu siku zote, lakini kufanyia tathmini za kina mambo aliyofanya ili utusaidie kwenda mbele. Hayo mengine nadhani siyo thread yake hii

Nimerudia tena ulichoandika ! Sina ushabiki na si tabia yangu huwa naandika ninachofikiri. Hiyo grooming ya Lowassa na Nyerere unaweza iweka wazi kwa evidence? Kwa kuwa saidia huyo Edward Lowassa akisimamishwa na CCM nina wahakikishia wapinzani wanachukua uraisi. Hasafishiki kwa kashfa za ufisadi ndugu yangu.
 
Kwa yote uliyosema wenye akili zao umewapa mwanga zaidi kuliko ilivyokuwa hapo nyuma

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha Kaka mpaka leo unakumbuka majibu yangu?na kura alinipa huyo mzee kama unakumbuka maana yake aliridhika na majibu alopata ,usipotoshe sikufura bali nilitabasamu na kuwakumbusha wana nzega jinsi mbunge wetu kaka seleli kamati ilimsaidia angalau akajenga kale kahoteli ketu kazuri kanako itwa RICHMOND pale nyumbani.

Sasa kaka ( S) why hidding ur identity?
 
Acha kujikweza wewe! Mario Puzo the novelist, amendika vitabu 11 kati ya hivyo cha The Gold Father ndicho kilichokuwa maarufu, kumbuka kuna hata sinema yake. Kazi zingine za Mario Puzo ni


  1. The Dark Arena (1955)
  2. The Fortunate Pilgrim (1965)
  3. The Runaway Summer of Davie Shaw (1966)
  4. Six Graves to Munich (1967)

    [*]The Godfather (1969)
    [*]Fools Die (1978)
  5. The Sicilian (1984)
  6. The Fourth K (1991)
  7. The Last Don (1996)
  8. Omertà (2000)
  9. The Family (2001) (kilimaliziwa na mchumba wake baada ya yeye kuwa amekufa Carol Gino)
Asome kipi hapo, achana na blanket statement eti Mario Puzo hakuna mahusiano na siasa zetu za uchwara! Kawadanganye UVCCM si JF

Hivyo viwili mazee ntavipata wapi kwani napenda na wanangu waje wavisome
 
Kuna mambo ya msingi sana ameeleza na kama Mkabila Nape akisoma haya maelezo ya Bashe anaweza kubadilisha approach anayotumia kufikisha ujumbe ambayo imekuwa na madhara kuliko kujenga shame on you Nape
there you are makupa
 
Jitu lisiloonekana aka invisible naomba kama mnaweza hii tread iwe article kwa ajili ya kumbukumbu
 
Siipendi ccm..but katika hili bashe kanena,suala la kuwa katumika kupresent au vp sio la msingi sana,the issue is katoa hotuba ya kweli ambayo kwa mwana ccm makini nakifuatilia na kuifanyia kazi itawapeleka one step ahead.Hata kama ametumwa basi nawapongeza waliomtuma kwa kuandaa speech nzuri na yenye mashiko.Ni ujumbe mzuri kwa nape kama ana akili atajifunza kitu,ni matumaini yangu ataacha uropokaji na kuongea vitu bila kupima madhara yake baadaye.Hongera bashe kwa kutumia muda wako kuandaa hii speech I am looking at the message and not where it comes from.
 
Ndugu Bashe, naomba nitoke nje ya mada kidogo. Hivi unafanyaje kujua ID nyingine za watu? Kuna ID kama mbili hivi ambazo umeziunganisha na nimezifuatilia mtiririko wa maneno na kuona ni kweli ni mtu huyo huyo. Inaboa kuna watu wanajiuliza na kujijibu wenyewe humu.

Nikirudi kwenye mada, hotuba ulioitoa ni nzuri sana endapo tu hakuna ajenda ya siri nyuma ya hotuba hiyo ila ukitaka uonekane mbaya CCM basi we sema ukweli. Vijana wengi walioko CCM wako pale sio kwa sababu ya kuridhika na sera za chama bali kwa maslahi binafsi kutokana na uwezo mkubwa wa chama. Hii ndio sababu hakuna suala la kujitolea kwa chama kama ilivyo miaka ya nyuma. Hata kwenda tu kwenye mikutano ya chama inabidi yatumike malori kwenda kuwachukua na kuwarudisha na kupata chakula, kanga, fulana au kofia kinyume cha hapo haendi mtu.
 
Ndugu Bashe, naomba nitoke nje ya mada kidogo. Hivi unafanyaje kujua ID nyingine za watu? Kuna ID kama mbili hivi ambazo umeziunganisha na nimezifuatilia mtiririko wa maneno na kuona ni kweli ni mtu huyo huyo. Inaboa kuna watu wanajiuliza na kujijibu wenyewe humu.

Jaluo

ID zipi hizo nasisi tuzijue?
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha Kaka mpaka leo unakumbuka majibu yangu?na kura alinipa huyo mzee kama unakumbuka maana yake aliridhika na majibu alopata ,usipotoshe sikufura bali nilitabasamu na kuwakumbusha wana nzega jinsi mbunge wetu kaka seleli kamati ilimsaidia angalau akajenga kale kahoteli ketu kazuri kanako itwa RICHMOND pale nyumbani.

Sasa kaka ( S) why hidding ur identity?

iShh...Personal attack? for red above try it again!
 
Back
Top Bottom