UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zyansiku, May 29, 2011.

 1. Z

  Zyansiku Member

  #1
  May 29, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana Jf

  Jana Mwenyekiti wa Kamati ya REFORMS UVCCM, Hussein Bashe akiwa katika Mkutano Mkuu wa Uvccm Mkoa wa Dar es Salaam, alitoa Onyo kwa UVCCM na Chama Cha Mapinduzi, Bashe alisema Wakati CCM na UVCCM wakisahau wajibu wao kwa Jamii na Kubaki Kulumbana na Kutuhumiana wenzeao CDM wako busy katika kukijenga Chama Chao.

  Bashe alitumia muda Mwingi kueleza kwanini CCM inapoteza uhalali wake, alisema CCM imesahau kutekeleza wajibu wake na hasa Kusimamia SOCIAL JUSTICE, na akasema wasipotekeleza wajibu wao CCM itaondolewa madarakani na watanzania. Bashe alisema watanzania wengi leo wanahali ngumu, Maisha yanazidi kupanda nchi ina Nyemelewa na Njaa.

  Alitoa Mfano kwao Nzega kati ya kata 130 za wilaya ya Nzega kata 90 zina upungufu wa chakula, Bei ya Mchele leo 1600 kipindi cha mavuno Bashe pia alisema leo Nchi ipo ktk Mgao zaidi ya Mika 6 viongozi wanalumbana badala ya kutatua tatizo la Umeme. Bashe alisema Mafuta yanapanda kwakuwa duniani yamepanda lakini ni wajibu wa serekali kutafuta Njia ya kupunguza makali. Maharage 1,500, Sembe 1,000 anashangaa chama hakiibani serikali wako busy kujibizana na Slaa na CHADEMA, alisema wana CCM wengi hawaijui ITIKADI ya Chama Chao inatekelezekaje ktk ulimwengu wa Mfumo wa soko.

  Bashe alionya CCM isipokuwa makini Itaondoka Madarakani na kuwataka vijana wenzie wa UVCCM kuamka na kukibana chama kisimamie serekali ili tuwatendee haki wananchi,Bashe aliwashangaa Viongozi wa Chama chake badala kutumia Muda mrefu kutatua kero za watanzania wao wako BUSY kukomoana na Kutuhumiana Mara. FULANI Fisadi atoke, Fulani CCJ alishiriki kuandaa katiba,alisema watanzania wanataka uhakika wa Ajira, Masoko ya Bidhaa zao,uimara wa Shilingi na Uchumi, kuliko matakwimu ambayo hayaonekani ktk maisha ya kila siku ,Afya ya Uhakika, Maji ya Uhakika sio porojo za fulani fisadi fulani CCJ, Bashe pia aliwaahidi wajumbe hao uhuru wa kutoa maoni na kamati yake haita chakachua lolote .

  Pia katika hotuba yake Bashe alimpa Ujumbe Kijana aneitwa Matefu,kumwambia asikubali kuwa Sauti ya watu Flani lazima ahoji kila anachoambiwa kusema ili hata akisema Basi awe amekiamini na kukijua.

  Bashe alionya Pia Tabia ya Viongozi kutumia UDINI na UKABILA kuhalalisha hoja zao za kisiasa ama kutafuta Political Legitimacy (uhalali wa kisiasa), Bashe alisema Leo kiongozi anakituhumu chama flani kuwa ni cha wachaga alihoji ama chadema tunawatuhumu kuwa ni cha wakristo.

  Jamani huu ni ujuha, wendawazimu na ulevi kwa kijana wa CCM kuongea ama kuwaza haya, Dhambi hii itatuumiza kama Chama na Nchi. Alisema je wachaga na wakristo wote wakihamia chadema itakuwaje, tunataka kuvuruga nchi, ama tunataka kuwaambia watanzania CCM hakitaki wachaga na wakristo, alionya UVCCM wasiongee mawazo hayo dhaifu na Mabovu yasiyo kuwa na mashiko.

  Bashe wakati akifunga Mkutano aliwaahidi vijana yale waliomueleza atayafikisha katika Baraza kuu Bila kuchakachua,Bashe alionya Mfumo mbovu wa chama ambao viongozi wamekaa kiuchaguzi chaguzi utakimaliza chama alisema CCM ni P na Serekali ni Agent,lazima Chama kiisimamie serekali kutekeleza wajibu wake na kuwataka Viongozi wa Chama na Jumuiya kuacha Mara moja Tabia ya Kuchokonoana kwani itavunja heshima ya Chama alitoa Mfano wa kesi ya Mahalu akasema hiyo iwe Shule kwani leo Rais mkapa anatakiwa mahakamani,Rais kikwete anatakiwa mahakamani hii ni aibu

  Alisema Tuwatumikie watanzania tuache kuwa watumwa wa Historia,makosa ya Nyuma yatumike kurekebisha Future. Alisema Urais 2015 usitumike kukimaliza Chama Viongozi watimize wajibu wao waache kuwaza mfumo wa kushughulikiana,alisema Communication Strategy (mfumo wa mawasiliano) wa Chama ni Mbovu Magazeti, Radio za chama hazina Mvuto kwa watu kwakua hatuelezi vitu vya maana zaidi ya Mipasho na Porojo,Watanzania wamechoka kusikiliza Porojo lazima kila Mwana ccm atekeleze wajibu wake kukisaidia chama na si kusaidia kundi lake, aliwataka Vijana waungane kujenga Jumuiya Imara.

  Alisema wasitumie muda Mwingi kujadili chadema tutumie muda mwingi kujenga chama chetu na kutimiza wajibu wetu, alimaliza kuwaasa vijana wasiwaze kuwa CCM ni watawala alisema dhana hiyo ni mbovu,bali alisema dhana sahihi ni kujenga Fikra kuwa CCM ni chama kinachoongoza ni si Tawala. Alisema leo CCM inaimba Nyimbo za Chadema na akasema Tumeingia katika POLITICAL TRAP ya chadema tunafanyia kazi ya kwao na kuacha ya kwetu 2015 tutaulizwa yakwetu tutakua hatuna majibu, alisema CCM tumekua REACTIVE badala ya PROACTIVE,badala ya kuwa Viongozi sasa Tunaongozwa,Tumebaki kuwaza Madaraka Badala ya kuwaza Namna Gani tutamiza wajibu wetu.

  Aliwataka UVCCM kubadilika na kusema Maslahi ya Nchi na Chama yatalindwa kwa sisi kutekeleza wajibu wetu na kuacha UROHO wa Madaraka bila ya hivo tutaivuruga Nchi na Chama chetu alishangaa Tabia sikuhizi ccm kila mtu anasharubu na Kutoa Matamko.

  Alisema Kamati yake itapokea maoni kupitia Email, akatangaza email address (maoniuvccm@yahoo.com) pia ukurusa wa Facebook ( maoni uvccm reforms)pia sms alisema kila wilaya wametuma madodoso 100 ambayo yatajazwa na wana uvccmm alisema watafanya mikutano ya namna hiyo ktk miko kumi na moja watakutana na wasomi wa Vyuo Vikuu.

  Alisema atatumia JamiiForums ataongea na Viongozi wa mtandao huo wapate fursa ya kupokea maoni kwa Njia hiyo, aliwataja viongozi wastaafu wote alisema anawaomba vijana wasigubikwe na ugonjwa wa rushwa na kusema leo kila Mwana CCM hataki kutekeleza wajibu wake mpaka apewe Pesa aliomba Tuweke maslahi ya Chama na kukilinda na Kukijenga Chama Na Nchi yetu.
   
 2. M

  Makupa JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kuna mambo ya msingi sana ameeleza na kama Mkabila Nape akisoma haya maelezo ya Bashe anaweza kubadilisha approach anayotumia kufikisha ujumbe ambayo imekuwa na madhara kuliko kujenga shame on you Nape
   
 3. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hotuba hii imekwenda shule kisawasawa. big up wakuu ripota na bashe
   
 4. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  sikuwahi kufahamu kuwa Bashe ana akili kiasi hiki....huyu jamaa angetufaa sana Cdm....wapi Zito? Tafadhali huyu jamaa tunamwitaji sana.
   
 5. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Msimu wa usajili wa wanasiasa unafungwa lini?
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Amegusia risasi za Arusha , Tarime na sasa Tabora wananchi kupigwa na wengine kuawa ? Maana ni kazi ya CCM hii
   
 7. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, pamoja na kwamba hotuba hii ya Bashe labda (sina uhakika) inalenga kuwatetea mapacha watatu, lakini ameongea vitu vya msingi sana, na nadhani alistahili kuwa mbunge wa Nzega na sio yule Mrundi Kigwangallah.
   
 8. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,775
  Likes Received: 6,108
  Trophy Points: 280
  Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni; hata kama sio raia but excellent Bashe. Ni heri asiye raia lakini mkweli kuliko raia ambaye ni mwongo na mnafiki. Laiti vingozi wa magamba wangekuwa na maono kama hayo! Hata kama ana ajenda nyingine moyoni (ambapo ni Mungu pekee ajuaye), lakini kwa kauli hii nampongeza.

  Magamba, Magamba, Magamba; mbinu zenu chafu za kujaribu kujenga na kupandikiza hoja za kidini, kikabila, na kikanda kwa wengine soon zitawamaliza; time will tell - since 1995 imekuwa mchezo wenu.
   
 9. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Good speech! God bless you ingawa najua hamtayafanyia kazi uliyoyasema.
   
 10. n

  neyro JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 232
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Bashe kanena na ameonesha ukomavu wa kisiasa na kidiplomasia, mimi ningewaomba raia wengine wa Tanzania wasio na asili ya Tanzania na Afrika wafanye yale yenye kujenga nchi ili wote tujue tuko pamoja na sikufanya anachokifanya Pacha, afu akiambiwa si mtanzania ndio maana anatuibia anasema tumeanza ubaguzi.Bravo Msomali Bashe.....
   
 11. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Nyie nani kawaambia sio raia? mama yake mnyamwezi.Unajua hakuna mtu mbaguzi kama mwaafrika sema tu hakujaliwa
   
 12. z

  zamlock JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  safi sana mawazo mazuri ccm wayapokee
   
 13. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ccm inaongozwa na wasomalia,hii ni ndio alshabab yenyewe au?
   
 14. LAMPARD

  LAMPARD Member

  #14
  May 29, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu Hussein Mohammed Bashe bado ananipa wasiwasi kuwa hali za mivutano kule Nzega hajazimaliza............naendelea kuamini hivyo? i know politics na nimesomea and i know what i mean by saying that, kwanza naomba ukane hadharani huna jeraha,vita, kisasi kwenye nafsi yako juu ya uchaguzi wa jimbo la Nzega na mtu yeyote. na hili linalozunguka sasa kwamba ukishindwa wewe kurudi jimboni nzega mnamuanda kijana mwenzio SALIM ALLY wa UDSM kuja kuchukua jimbo 2015 je hili ni kweli?.

  -umezungumza kuhusu uchaguzi na wanaccm 2015, mbona wewe tayari unakundi lako kwa ajili ya LOWASA AMA NCHIMBI kuwa rais baada ya Jakaya? mbona unaongoza zengwe la kumuingiza JAMAL KASSIM kuwa mwenyekiti wa Taifa UV-CCM na katika hilo wewe ukiwa kama mhasibu wa kutunza pesa za kampeni na kuwagawiya wapiga kura? sijui unapozungumza hayo unadhani unayofanya wewe wananchi hawaoni ama hawaelewi? na hili mnalopanga la mdogo wako IBRAHIM MOHAMED BASHE kuwa Rais wa UDOM mmefikia wapi? maana naona maandalizi ni makali sana, JUA TU KWAMBA KILA MNALOFANYA NA KUNDI LAKO LINAFAHAMIKA ila natakakusema tu huo ndio mwisho wenu wa kufanya haya madudu yoooooooooooye...yoooote so kila mnaloona mnaweza kufanya fanyeni after muda fulani ndio mwisho wa kundi lenu wote kuwalaghai WATANZANIA.

  -UVCCM ambayo wewe ni mjumbe mnakazi kubwa sana kuibadilisha, ila nadhani ndio mnakamilisha muda wenu wa umri kikanuni sitegemei mnaweza CHAKACHUA TENA UMRI MRUDI HAPO, malizeni muda wenu waingine VIJANA WANAOWEZA FANYA KAZI SAWA SAWA KWA MASLAHI YA VIJANA WA TANZANIA, naamini nusu yenu mnaondoka 2012, japo mnapiga debe suala la umri liongezeke ili muendelee kukaa hapo UVCCM kwa maslahi ya kundi lenu, enough is enough.
   
 15. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  CCM katika vikao vyao vya kuhujumiana ndo waliotuambia..tena na vyeo wakamvua :) Sie wala tulikuwa hatuna habari yakhe! So walaumu hao haooo.
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mzee umesha muua huyu jamaa .Atakuwa kapata shida na moyo kutaka kusimama .Kweli watu mnajua mambo makuu huyu ndiyo mtuhumiwa Msomali ?
   
 17. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Maajabu sana katika hii nchni yetu! Rais aliwai kusema kuwa huyu Jamaa si Raia tena alitangaza na nchni nzima mkamsikia, Rais haitendei haki nchni yake hata hii tabia ni magamba inapaswa kuondolewa ndani ya CCM na Ikulu inakuwaje Rais useme kitu alafu kionekane kama kituko!

  Ujasiri na Kiapo cha kulinda katiba na mipaka ya Jamhuri ya Tanzania bila woga upo wapi?!
   
 18. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,238
  Likes Received: 931
  Trophy Points: 280
  Bashe ametumika tu kupresent hiyo speech,sababu hiyo speech imemgonga mwenyekiti wao wa Chama na kundi lake linalohubiri kujivua Gamba,hii inadhihirisha kwamba Mapacha watatu ni smarter na wamejipanga kuliko Mwenyekiti na kundi lake.
   
 19. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Lampard umeweka posts tatu zinazofanana hata moja ingetosha,katika hotuba hii kuna machache nimeyapenda kama hili la kukemea ukabila na udini,na pia kusahaulika shida za wananchi.
   
 20. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Suala sijui bashe katumwa anamuongelea nani hili si la msingi, la muhimu ni Ujumbe aliousema una mashiko si mchezo. Saa nyingine hata vichaa na wendawazimu huongea ukweli judge the message not the messenger
   
Loading...