Originally Posted by LAMPARD Ndugu Hussein M Bashe naona umejitahidi sana kujitetea vizuri i think unasiasa za VISASI/CHUKI/KIGAIDI KAMA MAGAIDI WENGINE sina shaka katika hilo kwa jinsi ulivyojieleza kabla sijakufamisha kidogo SIASA HIZI ZA CCM NA WAPINZANIA, find any book written by MARIO PUZZO kisome ukielewe na ujikosoe mwenyewe kwa hayo uliyoyaeleza then u will change by being a good politician katika siasa za kiafrika.
Bashe naomba nikuulize where were u 1995? unamjua mtu aliyekuwa akiitwa BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE? unaposema utamuunga mkono LOWASA mjue kwanza BABA WA TAIFA LA TANZANIA ndio uzungumze huo upuuzi wako, mwalimu nyerere ukaweza kumsoma na kumjua u will be in a safe side, katika wanasiasa ambao wanawaza kuwa rais wa Tanzania siku za mbele LOWASA NI MMOJA WAPO, WAPO NA WENGINE LAKINI KATIKA HAO WOTE ni yeye alikuwa mmoja wa WASISI WA G-55 ndio maana nakwambia msome kambarage BABA WA TAIFA LA TANZANIA.
Nimezungumza hilo la G-55 katika siasa za leo walikuwa wengi lakini wengi washajiachilia na siasa hizi za sasa maana ni za kizazi cha DOT.COM, sasa jua huyo unayetaka kumsimamia alikuwa ni mmoja wa hilo, unataka mpaka tumfufue Nyerere aje akuambie wewe HUSSEIN M BASHE ujue hilo? mimi naendelea kuamini kila aliyekataliwa na BABA WA TAIFA KATIKA TAIFA HILI LA TANZANIA HAWEZI KUNEEMA NA KUINGIA IKULU HATA SIKU MMOJA DAIMA MILELE AMINA. Umemtaja mzee Malecela vema hata yeye alikataliwa na Baba wa Taifa asingeweza kuigusa ikulu, nchi hii ingewaka moto , IKULU NI MAHALA PATAKATIFU SIO KILA MTU ANAWEZA KUKAA PALE KUWATUMIKIA WATANZANIA.
BASHE nakuuliza swali jingine unadhani kwani mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE alimkataa EDWARD maana yeye kwakwe walikuwa watoto akiwaita kwa majina yao , unadhani ni kwanini alimkataa? naomba jibu katika hili......unadhani waTanzania hawajui hili? unajua miiko ya uongozi HUSSEIN M BASHE? historia ya Tanzania ina mambo mengi kuliko nchi yeyote AFRIKA MASHARIKI kama ulikuwa hujui hili jua kuanzia leo.
Bashe jua kwamba BABA WA TAIFA KATIKA KILA ALILOLISIMAMIA KATIKA UHAI WAKE WAPO WATANZANIA WATAYAHESHIMU MAWAZO YAKE DAIMA MILELE, HASA KATIKA KUWAPATA VIONGOZI WA TANZANIA......................katika ninayoamini kama angelikuwa hai Kambarage LOWASA ASINGELIKUWA WAZIRI MKUU, nataka ujue waliokufa wamekufa kiwiliwili roho zao ziko hai na zinaona ndio maana yalitokea yaliyotokea DODOMA 2008 mwezi wa pili.
kuna kukataliwa na kuambiwa bado hujatosha wakati ukifika utapata, sasa LOWASA UNAYETAKA WEWE AWE KIONGOZI WA TANZANIA ALIKATALIWA NA JEMEDARI WA NCHI HII, JAKAYA ALIAMBIWA SUBIRI hakukataliwa wewe haya huyajui................jua kuanzia sasa aliyejitolea uhai wake kuwatumikia waTanzania kiukweli? aliyeacha kazi yake ya mshahara kulikomboa Taifa lake, aliyenusurika kifungo kwa ajili ya uhai wa nchi yake. hayo ni machache tu nakupa kijana Bashe, soma historia ya nchii uijue vizuri usidanganywe na siasa za akina LOWASA,CHENGE, ROSTAM wakidhani vijana wengi wa leo hawajui nchi yao mnajidanganya nyie very funny kumtetea LOWASA bila HAYA AU AIBU katika mipaka ya Tanzania.
narudia tena katika hizi harakati za leo ni yeye peke yake aliyekuwa member wa NEC 1990s-19952s ambaye anapanga kila njama za kuingia IKULU 2015, nakwambia itapasuka ikulu ile vipande vipande na waTanzania tutasali sala hazijawahi saliwa popote ACHA ILE SALA ALIFANYA GOVONOR EDWARD TWINNING ALIPOFUNGA NJIA WANANCHI WASIPITE KIVUKONI PALE, ilimlazimu govonor kwenda kwa SHEIKH IDRISA kuomba, duru zinasema alipiga magoti na kuomba maana ilinyesha mvua haina kikomo maji yalijaa ikulu sehemu nyingine zikiwa salama, sheikh Idrisa leo ndio ule msikiti wa Idrisa unaitwa jina lake.
Hussein Bashe soma siasa ya Tanzania penda kuperuzi mambo yalivyokuwa na yalivyoleo, huwezi leo kutetea waTanzania kwa yanayotokea wakati katika vikao vya chama na jumuiya unacheza karata zako za kuwatetea MAFISADI, liko wazi katika kikao cha DODOMA CHA UVCCM ulikuwa kinara wa kutete mafisadi, kwani hujui VIJIWENI, MISIKITINI, MAKANISANI, VITUO VYA DALADALA, MIJINI NA VIJIJINI KILA MTU ANASEMA LOWASA.......LOWASA......kwa ubaya wa UFISADI, imeenda mbali zaidi ikisemwa hata baadhi ya viongozi wa serikali wanakwamisha maendeleo ya nchi wakipata order toka kwake maana ndio aliowapigia debe kupata hizo nafasi,.
japo naamini mambo yameanza kabadilika sasa, naamini tutaenda pazuri kadri siku zinavyokwenda.
mwisho niseme ni haki yako kikatiba kuunga mkono unachokiamini