Ndugu Hussein Mohammed Bashe bado ananipa wasiwasi kuwa hali za mivutano kule Nzega hajazimaliza............naendelea kuamini hivyo? i know politics na nimesomea and i know what i mean by saying that, kwanza naomba ukane hadharani huna jeraha,vita, kisasi kwenye nafsi yako juu ya uchaguzi wa jimbo la Nzega na mtu yeyote. na hili linalozunguka sasa kwamba ukishindwa wewe kurudi jimboni nzega mnamuanda kijana mwenzio SALIM ALLY wa UDSM kuja kuchukua jimbo 2015 je hili ni kweli?.
-umezungumza kuhusu uchaguzi na wanaccm 2015, mbona wewe tayari unakundi lako kwa ajili ya LOWASA AMA NCHIMBI kuwa rais baada ya Jakaya? mbona unaongoza zengwe la kumuingiza JAMAL KASSIM kuwa mwenyekiti wa Taifa UV-CCM na katika hilo wewe ukiwa kama mhasibu wa kutunza pesa za kampeni na kuwagawiya wapiga kura? sijui unapozungumza hayo unadhani unayofanya wewe wananchi hawaoni ama hawaelewi? na hili mnalopanga la mdogo wako IBRAHIM MOHAMED BASHE kuwa Rais wa UDOM mmefikia wapi? maana naona maandalizi ni makali sana, JUA TU KWAMBA KILA MNALOFANYA NA KUNDI LAKO LINAFAHAMIKA ila natakakusema tu huo ndio mwisho wenu wa kufanya haya madudu yoooooooooooye...yoooote so kila mnaloona mnaweza kufanya fanyeni after muda fulani ndio mwisho wa kundi lenu wote kuwalaghai WATANZANIA.
-UVCCM ambayo wewe ni mjumbe mnakazi kubwa sana kuibadilisha, ila nadhani ndio mnakamilisha muda wenu wa umri kikanuni sitegemei mnaweza CHAKACHUA TENA UMRI MRUDI HAPO, malizeni muda wenu waingine VIJANA WANAOWEZA FANYA KAZI SAWA SAWA KWA MASLAHI YA VIJANA WA TANZANIA, naamini nusu yenu mnaondoka 2012, japo mnapiga debe suala la umri liongezeke ili muendelee kukaa hapo UVCCM kwa maslahi ya kundi lenu, enough is enough.
Ndg yangu Lampard acha Upotoshaji,
Nikujibu kwa Ufupi:
Sikweli kuwa nina mdogo wangu aneitwa IBRAHIM anaesoma UDOM, mdogo wangu Ibrahim amemaliza Mzumbe na sasa yupo Mtaani akitafuta ajira kama Vijana wengine wa Kitanzania.
Hoja ya kwamba nina jeraha, ama kinyongo, ama chuki nayo ni Upotoshaji. Sina kinyongo that's why nilirudi Jimboni kumsaidia aliyeteuliwa ili chama changu kishinde, this tells a lot. Nadhani waliokupa taarifa hizi wamekupotosha. Lakini haina maana nimesahau yaliyotokea na wala sipo hapa kujadili uhalali wa hoja iliyotumika kutoniteua, bali nikuthibitishie sina kinyongo lakini siwezi kusahau kama ambavyo sijasahau matukio. Ya 2007, Kizota pale jina na kura nilojipigia zilipopotea kimuujiza. Sitasahau ya 2005 Nzega ktk kura za maoni na mimi kuwa Mshindi wa Tatu, sitasahau ya 2008 Dodoma, yote haya yamekua sehemu ya Historia yangu hayatafutika lakini sina kinyongo.
2010 nilimsaidia mbunge wangu kwani niliamini si yeye wala Chama (taasisi) walionikosea that's why mimi na team yangu ilimsaidia Kigwangalla.
Hoja yako kuwa ninamuandaa SALUM ALLY ni hoja potofu, 2015 kama nilivowahi kusema nitarudi kugombea Jimbo la Nzega na hivi sasa naendelea kutekeleza ahadi nilizotoa 2010 kwani wana Nzega walinipa kura 14,420 kati ya kura 19,000 zilizopigwa.
Hoja yako ya kuwa mimi nina kundi: Hakuna mwanasiasa asiyekuwa na kundi lake, msingi wa hoja yangu ni kwamba siasa 2015 zinakiumiza chama kwani sasa kuanza mikakati hiyo ni kudhoofisha chama wajibu wangu na wewe na wana CCM wote ni kumsaidia Rais Kikwete kutekeleza Majukumu yake KUFIKIA MATARAJIO ya WATANZANIA; bila ya hivo 2015 CCM haitakuwa na uhalali wa kuchaguliwa, ni wendawazimu kuanza kampeni leo wakati hata nusu ya tearm ya Pili ya Kikwete haijafika. Nikushauri acha mawazo mgando hayo.
Hoja yako kuwa namuunga Mkono Lowassa na Nchimbi kwa URAIS nayo ni upotoshaji. Hawa watu hawajatangaza labda wamekuambia wewe mimi sina taarifa. Ila kama Lowassa atasema anagombea sitasita kumuunga mkono kwani ninaamini katika uwezo wake wa kusimamia na kufanya kazi hilo sina mashaka nalo (ni msimamo wangu binafsi ambao unaweza kuendelea kubaki hivi ama kubadilika kulingana na wakati husika), kama chama kitamteua nitamuunga mkono bila shaka. Lakini sasa sina taarifa hizo.
Hoja ya Jamal nayo ni upotoshaji. Si kweli unalosema, na usimzushie ili aonekane ameanza kampeni mumkate, na mtu anapokuwa na Uwezo ni vizuri mkakubali. Uwezo wa Jamal hauna mashaka, kama chama kitamteua atahukumiwa na wapiga Kura na mimi nitakayemuunga mkono muda ukifika utamjua kwani sina sifa ya Kujificha katika Msimamo wangu.
Ndg yangu,
Hoja yako juu ya umri nikutoe shaka; Mimi ninaheshimu kanuni na taratibu, sina uroho wa madaraka, Kamati yangu haijapewa ktk Hadidu rejea zake hatuna suala 'Umri' kwa hiyo usiwe unahukumu bila Facts.
Pia ninapoongelea hoja ya Urais 2015 ninamaanisha kwamba wana CCM tufanye siasa
'above Group Politics' kwa Maslahi ya Chama Chetu na taifa. Linapokuja suala la nchi ni muhimu kufanya kazi 'Above Party Politics', hii itaisaidia nchi yetu. Nikushauri usipende kuwa kasuku, ongea kitu ambacho unakijua na una Facts zake. Ni rahisi kujua UJINGA wa mtu kupitia maandishi, kwahiyo wanpokupa cha kuongea fanya uchunguzi.
Lampard, nimeona kauli yako unasema kundi letu mtalimaliza; maana yake wewe una kundi unalolinda. Usionyeshe 'ujinga' wako kirahisi hivi. Nchi hii imeumizwa na 'Cheap Politics' ni Vizuri ukaanza kufikiri above Group Politics na Party Politics. Fanya uchunguzi kuwa na Facts kabla hujaongea.
Ndg yangu Lampard,
Nikuombe usiwe miongoni mwa wanaoumiza nchi kwa kufanya siasa ambazo ni 'Based On Speculations'.
Leo nchi yetu imeumia sana kwa aina hii ya siasa, CCM kimekuwa chama ambacho kinaumizwa sana na siasa hizi za Uzushi na Uongo.
Nilivyokusoma unaonyesha wewe ni Mwana CCM mwenye kundi ndani ya CCM. Nikushauri usikubali kila unachoaminishwa. Jifunze kuwa tabia ya kuhoji, why, how, when, which, what... Hii itakusaidia kusimamia unachoamini kwa Hoja.
Nimeona ukijisifia usomi wako wa Siasa; Nikiri inawezekana ni msomi wa siasa, basi anza kuwa 'Mwana Tafakuri' ili usomi wako uwe na Tija. Usikubali kuugua ugonjwa wa kugawanyika kwani ukianza kauli hizi KUNDI LENU na KUNDI LAO na KUNDI LETU, kesho utaingia katika kansa ya Kugawanyika ambayo hutumiwa na wana siasa MUFLISI ambao hujadili na kutazama mambo kwa Msingi wa Ukabila, Dini, Ukanda n.k. Tutaua nchi na chama chetu, waambie walokupa taarifa Next time wakupe Taarifa za kweli.
Mwisho nikuhakikishie: Sina Kinyongo, Sina Hasira bali sijasahau, Nzega 2015 sina ninayemuandaa Nzega bali nitarudi kugombea mwenyewe.
Kila la kheri Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika.