UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina

UVCCM: Hussein Bashe amjibu Nape kiaina



-Katika hili tafsiri ya nani kalala na nani kaamka ni subjective inawezekana wewe ukawa na usingizi mzito wakati ukihisi umeamka,hotuba yangu inawezekana usiipende sana lakini hayo ni mawazo yangu ambayo wewe pia unayako ,haki uliyonayo wewe kuyapinga yangu,ni haki hiyo hiyo niliyonayo mimi kukataa mawazo yako,si lazima tufikiri sawa,tuamue sawa,ikitokea hivo wote tutakuwa na matatizo,na si lazima hapa katika forum tukawa
wote na mtazamo unaofanana,na si lazima ukalazimisha nione unachoona na mm silazima nikakulazimisha ukaona ninachoona.

Nilisema tuufunge mjadala huu hapa kwani muda wa mjadala juu ya swala hili si sasa na tusipoteze nguvu nyingi sasa kujadili haya mambo,2014 tutakutana jamvini kujadili nani anafaa kuwa Rais wa Nchi yetu regadless anatoka wapi,sasa tutumie muda kujadili BEI MCHELE,BEI SEMBE,AJIRA,STABILITY YA UCHUMI WETU,UMOJA WA KITAIFA,KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA,NAULI ZA DALA DALA ZINONGEZEKA WAKATI VIPATO VYETU BADO DUNI,BEI ZA MAFUTA,TATIZO LA UMEME(Wewe hili hulifahamu bcs utotoni ulikaa upanga,unatumia jenereta,na sasa ukirudi likizo unatumia jenereta nyumbani na huko ulipo hamna mgao wa 16hrs) na kwa sisi wana CCM namna gani tunakisaidia chama kutekeleza majukumu yake kupitia serekali ili kuleta TIJA katika maisha ya watanzania ,haya ya lowasa na wengine si ya tija kwa sasa.Matatizo yetu hapa nyumbani ni ya msingi sana kuliko kujadili hayo unayotaka sasa tuyajidili.

Mwisho inawezekana ulitarajia nifikiri kama wewe ambae umekulia ndani ya mfumo huu,ume enjoy matunda na sasa upo nje ya nchi ukiwa hujui bughudha za daladala,hujui tatizo la mgao ulitaka niimbe ngonjera zako, nimalize kwa kusema tena Turudi katika msingi wa mjadala wangu,nilichosema ninakiamini,nitakisimamia sitabadili msimamoa katika hilo unless kuwe na Tangible Facts juu ya yale uliosema,Kuhusu kuandikiwa hotuba ni vizuri umesema hunifahamu kwahiyo kama walivosema wahenga USILOLIJUA NI USIKU WA GIZA,so nivizuri ukapata muda kidogo kunifahamu na hilo utaweza tu kama utajipa muda kunifahamu.


- Well, siwezi kuwa kwenye usingizi wa aina yoyote, I mean how can kiongozi wa taifa wa stature yako akaja hapa JF kumlilia mwananchi kama mimi aliyelala usingizi, huoni kwamba wananchi walio macho watashindwa kubaini kati yangu na wewe nani yuko usingizini? ha! ha! ha! ha!

- Ni kweli kabisa kama mwanachi nina haki ya kukuuliza wewe kiongozi uliyefukuzwa mara mbili, Moral Authority ya kutoa hotuba za kuelimisha wanachama wa chama kilichokufukuza uongozini mwake umeitoa wapi? Waannchi wengi wamekuuliza maswali humu mbona huwajibu, ila umenikomalia mimi mwananchi niliyelala usingizi? ha! ha! ha! ha! ha! ha! Unajua una hoja zinachekesha sana! ambazo ninaweza kuzijibu bila hata kufikiri sana!

- Tuufunge mjadala maana sasa unakugusa pabaya sana, hapana hapa tunaelimishana na kuelimisha taifa, waannchi wanajionea ni kwa nini hili taifa limedumaa ni kwa sababu ya kuwahi kuongozwa na watu kama wewe, unayeamini kwamba wananchi wana shida ya umeme, lakini wewe utampigia kura Lowassa aliyewaletea hilo hilo tatizo la umeme, Bashe watu kama nyinyi ondokeni huko kwenye siasa za taifa maana wewe na hao MAPACHA WATATU tayari Mmeshindwa, waachieni wengine sasa, I mean mimi hata nikiwa anything sio kiongozi na wala sikutoa hotuba anywhere na kuwadanganya wananchi kwa maneno ambayo mimi mwenyewe nikiwa kiongozi nimsehindwa kuyatimiza,

- Bashe mimi ni mwananchi ni haki yangu kukuuliza maswali ya msingi reardless of who is my father au mother, tizama kwenye hoja zangu ni wapi nimeuulizia kuhusu baba yako au mama yako, wewe hoja ya kwanza Mama Kilango, Malecela! badala ya kusimamia hoja zako mwenyewe ulizozitoa kwenye UV-CCM na kuwalipa media wa kupambe, sasa ukaona na huku JF nako unaweza kupambwa hapa hatupambi mtu, umetoa hotuba umeileta hapa sasa simama hapa ujibu maswali waliyoshindwa kukuuliza kule UV-CCM kwa sababu ya kuwaogopa wanaokutuma MAPACHA WATATU,

- Bashe siasa za kisasa ni hoja, sio manguvu na hasira, mimi sio kiongozi mwenzio wewe ndio mwenye burden of the proof ya kuonyesha kwamba una uwezo wa uongozi, nilitegemea utaonyesha uwezo wako wa kuongoza mpaka wananchi tuamini kwamba ulionewa kwenye kufukuzwa, lakini kwa haya yote uliyoyasema hapa kwenye hii thread, naomba nikwambie kwamba huna uwezo wa kuongoza wala kutafuta maoni ya aina yoyote kwa taifa, na ndio maana hili taifa tumekwama sana, I mean kiongozi wa stature yako anashindwa kujibu hoja za hotuba yake mwenyewe, badala yake unanijibu mwananchi kama mimi ninayekuuliza ishus za baba, mama na location yangu? Damn maan!

Ahsante Sana Mheshimiwa na Mungu Aibariki JF, maana huko kote umesfiwa sana sasa hapa tunakuomba ubebe msalaba wako unalilia baba na mama zetu wananchi na location zetu, kweli hili taifa sijui tulilogwa na nani, I mean can you imagine Trump anamuuliza Obama cheti cha kuzaliwa, halafu Obama anaaanza kumjibu kwamba wewe umezaliwa kwenye utajiri hujui lolote kuhusu umasikini? ha! ha! ha! ha! ha! ha!, Only in Tanzania!

William @ NYC, USA.




 
Du! This is very interesting!!!!!!

Lampard = Hkingwangalla in real life (Au mnataka nitoe ushahidi?). Lampard anamcriticize Bashe tena anaingia personal ile ya ukweli ukweli, the same Lampard in the pen name anajitokeza kwa jina halisi la Hkingwangalla na kumsifu Bashe. Eti hawa ndiyo vijana wa CCM wa kutuletea maisha bora kwa kila mtanzania. Thubutuuuu!

- Duh! noumaaaaa!

Willie @ NYC, USA.
 
Ukisoma taarifa ya richmond hakuna mahali ambapo unaona Low kasemwa bali preamble ambayo nayo imejaaa maneno ya kusikika na kuumwa sikio ambayo katika kamati inayo shughulikia mambo chini ya kiapo haipaswi kufanya hivyo na kuweka ni sehemu ya ripoti.
Mzee Lowasa umeifanyia kazi kubwa sana nchi yetu lakini ni vile watu hawaoni basi mmemchafua bila kujielewa kwa kutumika na wanasiasa uchwara, kuna marafiki zangu maDC wanasema kuwa tangu Low ametoka na wao wanajisikia wako likizo.Naweza kusema kuwa hakuna mwanasiasa ndani ya ccm au waziri yeyote anaeweza kusema kuwa ana uwezo wa kiutendaji kama wa Lowassa.Siasa haina uwezo wa kutoa kiongozi bora na ndio maana mimi sitaki kugombea siasa za tanzania.Siku moja historia itamuhukumu Lowasa kwa haki na itabaini wala haikuwa ajali ya kisiasa bali mpango kamili wenye nia ya kumfanyia political murder.Ole wenu siku aamue kutoka ccm kama mtaweza kusimama tena .aluta continua


  • Ukisoma taarifa ya richmond hakuna mahali ambapo unaona Lowasa kasemwabali preamble ambayo nayo imejaaa maneno.
Kwa kizungu wanasema hukusoma ripoti btn the lines. Hata mtu wa kidato cha Nne angejua tu. Otherwise ulisoma ripoti ukiwa biased. Mwananchi yeyote neutraal na hawakutaka kumvua nguo la sivyo hata Pension yake ya UPM angeilia segerea

  • Mzee Lowasa umeifanyia kazi kubwa sana nchi yetu
Kazi kubwa zipi hizo ebu taja mbili tu ???? Alafu Kwani yeye ni expatraite wa nje. Ni wajibu kukiogozi yeyote. Hatu exepect kazi ndogo kwaiongozi yeyote ni CCM tu ndo inalet down taifa. Lowasa hajafanya kazi. yeye na Jk ni watu wa kucheza na media tu. Tena Lowasa anazidiwa na Pinda the only diffrence pinda hana tamaa ya madaraka ndio maana yeye hangaiki sana na media kupamba habari zake. na cha muhimu ni muaminifu na mzalendo kwa taifa

  • Kuna marafiki zangu maDC wanasema kuwa tangu Lowasa ametoka na wao wanajisikia wako likizo.
Hao marafii zako hawakuepewa U DC kwa uwezo wao bali waliepwa kwa urafiki . Ni aibu sana wewe kuandika haya. DC anataka asukumwe kama gari bovu???!!!!!. Yaani wao motivation ya wao kuwa DC mpaka Lowasa awe PM. Kumbe sifa za uchapakazi wa Lowasa ni sababu ya kukimbizana na ma dc wabovu. teh teh teh. Waulize hao marafiki zako Vip Lowasa angekuwa Rais alafu PM akawa JK . Je wangejisikia wako maternity leave

  • Naweza kusema kuwa hakuna mwanasiasa ndani ya ccm au waziri yeyote anaeweza kusema kuwa ana uwezo wa kiutendaji kama wa Lowassa
Hahahahhaa Aiseeeee utendaji gani sasa kama ofisi yake imeweza kuingia mkataba kampuni hewa. Katika karne hii ya Dotcom jiulize kwa nn huyu mtedaji na watu wake walishindwa hili? Nakuambia tena Lowasa hamzidi hata Pinda sana sana ni kutumia magazeti. Labda kama unamliganisha Lowasa na mwenzake JK. maana wote ni wasanii

  • Siasa haina uwezo wa kutoa kiongozi bora na ndio maana mimi sitaki kugombea siasa za tanzania
Aiseee kumbe yote uliyokuwa unaongea kuhusu Lowasa ilikuwa nini :A S-confused1:
A%20S-confused1.gif


Mkuuu kifupi ondoa propaganda za kusema hakuna kama Lowasa.
 
Heshima kwako Hussein Bashe.

Kwanza naomba kukupongeza kwa kuja jamvini na kujibu baadhi ya hoja na kutoa ufafanuzi katika masuala mbali mbali.Nikiri umejitahidi kujenga hoja lakini pia nikiri lugha unayotumia haifai kabisa ndani ya jamii iliyostaharabika,imejaa dharau,kiburi na zaidi ya yote inakatisha tamaa.

Umekiri mwenyewe umechezewa rafu kibao ndani ya chama chako baya zaidi umeonyesha dhahiri wewe ni mtu wa visasi na vinyongo.Vipi mambo uliyotendewa miaka mingi nyuma hutaki kusahau ? Labda imani na asili yako imekufunza hivyo,ukitendewa jambo baya siku zote ni lazima ujifunze kusamehee na kusahau.Ni uzushi na ubazazi kusema umesamee jambo fulani lakini huwezi kusahau.

Unakiri Lowassa akigombea urais utamuunga mkono hakika kati ya mambo ya kipumbavu uliyowahi kukiri hadharani hakuna kama hili na ikiwa msimamo wako ni huu hakika waliokunyima nafasi ya kugombea ubunge hawakufanya kosa kabisa walikuwa sahihi na ikiwa watakufanyia tena mwaka 2015 watakuwa wamelitendea taifa letu changa jambo jema.

Nikiri mwamzoni nilidhani Bashe ni miongoni mwa vijana wanaoweza kulisaidia taifa lakini baada ya kupitia andiko lako nimegundua hufai hata kurejeshewa uraia wa Tanzania.Vijana wa aina yako ndio wameifikisha Somalia hapo ilipo sasa [kukumbatia magaidi na wezi wa mali za umma]

Mwisho Mungu hawezi kuibarikia Tanzania wala Afrika kama tutawatukuza wezi na mafisadi.

Naomba kuwasilisha.

- Mkulu Ngongo Salute!

William @ NYC, USA.
 
Hii nchi itakuwa na laana kwa kweli,eti nani asiejua kuwa swala zima la ngonjera za mwakyembe dhidi ya lowasa ni siasa za makundi ambazo hatimaye chadema wakazibeba kumshambulia lowasa kwa kuwa vita vya panzi ni furaha ya kunguru......mwakyembe hawezi kumtendea haki edward kwa ukweli mmoja kuwa bado ana uchungu sana kundi lao kuanguka kwenye uchaguzi wa mwaka 2005, na majembe yao dhidi ya low yalianza toka gazeti la radi alilokuwa akiandika na kundi lao kwenye uchaguzi uliopita wa ndani ya chama yani 2005
Ukisoma taarifa ya richmond hakuna mahali ambapo unaona Low kasemwa bali preamble ambayo nayo imejaaa maneno ya kusikika na kuumwa sikio ambayo katika kamati inayo shughulikia mambo chini ya kiapo haipaswi kufanya hivyo na kuweka ni sehemu ya ripoti.
Mzee Lowasa umeifanyia kazi kubwa sana nchi yetu lakini ni vile watu hawaoni basi mmemchafua bila kujielewa kwa kutumika na wanasiasa uchwara, kuna marafiki zangu maDC wanasema kuwa tangu Low ametoka na wao wanajisikia wako likizo.Naweza kusema kuwa hakuna mwanasiasa ndani ya ccm au waziri yeyote anaeweza kusema kuwa ana uwezo wa kiutendaji kama wa Lowassa.Siasa haina uwezo wa kutoa kiongozi bora na ndio maana mimi sitaki kugombea siasa za tanzania.Siku moja historia itamuhukumu Lowasa kwa haki na itabaini wala haikuwa ajali ya kisiasa bali mpango kamili wenye nia ya kumfanyia political murder.Ole wenu siku aamue kutoka ccm kama mtaweza kusimama tena .aluta continua

Endelea kuota na EDWARD wako, huyo kishapigwa chini tafuteni mwingine mumpigie kampeni, huyo hauziki kwa watanazania wa leo....Hata leo mshauri atoke CCM uone nini kitatokea kama siyo kujibu kesi moja baada ya nyingine, nyambaf kabisa!!!....eti Lowassa this, Lowassa that, hebu mshaurini atoke LEO CCM tumuone huo ubavu wake akiwa nje.... Jitu halina huruma na watanzania halafu leo anatokea mtu kumtetea hapa eti kwa vile kaahidiwa kacheo au kabahasha ka khaki, inakera sana!
 
Huna lolote wewe! utamdanganyanani kwa hii mikwara yako ya kujifanya unaijua historia ya nchi hii? unamaneno meeengiiiii ya unafiki wa kujifanya unajua kila kitu! u ar u by the way? kwahiyo unataka kutuambia nchi hatakuja kutawaliwa na chama chochote isipokuwa chama cha magamba? eti oooh kuna babu wa pemba na bibi wa ilala! who are they by the way? wao ni miungu? wao ndiyo waliiumba Tanzania? eti oooh naijua siasa za Tanzania kwa miaka 10! so what? unamtisha na kumlingishia nani? Hivi majimbo ya mbeya,iringa,musoma,kawe,ubungo,mwanza,moshi,arusha,singida na maswa yalipoangukia kwenye mikono ya wapinzani,wewe ulikuwa wapi? hao babu yako wa pemba na bibi wa ilala walikuwa wapi? Mkuu jitahidi kusoma alama za nyakati! hiki ni kizazi cha nyoka a.k.a kizazi cha dot.com....humdanganyi mtu hapa kwa historia yako ya wana magamba. Hivi ujui ccm inaelekea kufa na kutokomea mithili ya KANU ya kenya? keep waiting mkuu....

Hahahahahhah!! This is a winner, asante sana mshikachuma!!

Eti tukitaka kujua history tumtafute bibi wa Ilala na Babu wa Pemba!! Ina maana wamekula memory stick ya historia ya TZ ???

Kama historia yetu haijawa documented kwenye vitabu na maonyesho basi we r goners!! Hatuwezi kurely on porojo za bibi wa Ilala na babu wa Pemba who are not even historic figures like kina Sykes, bibi titi etc...


Mtu akishachafuka na kuanza kuchafua wenzake, sio tu kuwa anasafishika bali anaendelea kutokota topeni na anaowasafisha...

So Bashe get it from me, u r not clean, Lowassa is not clean and there is nothing u can say or do to convince(sp) me otherwise!!

Mshikachuma nimefurahia uchambuzi wako kwakweli, magamba should get out!
 
Kama anayo mivutano Nzega basi ni kawaida ya mizengwe ya CCM huko sina kauli nako. Huyu bwana ametumia sawasawa kutoa elimu ya uraia sio kwa vijana tu, bali pia kwa manape wake na maridhi1 et al. Huo uasili wa Somalia ndio ukabila anaousemea Bashe tusiende huko tukakosa uelekea.

JF ni platform imara ya wanaofikiria kwa kina, kama ni kusemana kwamba sio watanzania basi watu wote walioko mipakani mwa Tanzania sio wananchi wa Tanzania, hata JKN alishasemwa sana utusi wake. Mbona Kinana mmemuachia tum, kwani usomali wake una rangi ya kuwavutia?

Mtu akifanya kazi vizuri kwa manufaa ya wengi mtieni moyo asonge mbele. Maendeleo yakija hayataishia kwenye viunga vya ukoo wake tu. Kwani Chenge ni Msomali anapotuibia vile?

Lowasa je, ni Mkenya? Rostam naye ni Mtanzania ila tabia yake ndio imekosa Utanzania. Kama CCM wangekuwa wanajianika na kufanya hivyo basi hata vyama vya upinzani visingekuwa na nafasi.

Lakini kwa kuwa wanadhani wao ndio vijogoo peke yao, watakula jeuri yao.
 
Waliotoa ujumbe wa kweli kama msomali huyu ndani ya sisiemu ni weng,lakini utekelezaj hakuna!so tusitarajie jpya
 
Hana lolote huyu anapiginia tumbo lake, unategemea Bashe acritise RA, atakula wapi, ni front tu ya kusifisha njia ya boss wake ili waendelee kupeta.
 
SHALOOM JF,

Nimevutiwa na mjadala huu na mnyukano wa BASHE na WILLIAM mnyukano ni mzuri sana unapotoka kwa watu wa MAGAMBAAAAAA HAHAHAHAHAHA.

Nimeamua kuja hapa na mimi kuonyesha ninchokifahamu kuhusu viongozi hawa wawili yaani BASHE na mzee wa TINGA TINGA.

Pia kumueleimisha william na mwisho kumpa ushauri wa bure bashe na maisha yake ya CCM ya baadae kama ambavyo tulimshauri wana mzumbe wenzie tulipokutana nae mwaka jana baada ya kuchakachuliwa.



- Mheshimiwa Bashe, heshima yako sana; kwanza kabisa ningekuomba ufungue mjadala wa Malecela, ili tuweze kujadili huu mjadala wako bila ya kutoka nje ya mada:

HOWEVER nitajaribu kukusaidia kwa kutoka nje kidogo ya mada: Malecela amekua kiongozi wa taifa toka akiwa na umri mdogo sana wa miaka 22, alianza na u-DC Tukuyu, sasa tizama kwamba katika miaka yote ya utumishi wake kwa taifa wewe na wanaokutuma hapa yaani MAPACHA WATATU, mlichonacho ni EPA over him?

Kwa hiyo unasema Malecela amekuwa muaminifu huko nyuma kote, isipokuwa akiwa mwishoni mwa utumishi wake kwa taifa, ndio kwa mara ya kwanza taama ya kuiba tena EPA ndio ikamshika?

ha! ha! ha! ha!

*Nianze na William kwanza nishukuru kufahamu huyu ndie william ambae ni mtoto wa mzee Malecela hapa suala la uadilifu la mzee wako lipo katika mashaka kama alikuzaa wewe nje ya ndoa yake (nakubaliana na hoja ya bashe kwamba wewe ni zao la kiongozi asiye muadilifu).

Tuhuma ingine ni kashfa ya helkopta feki ambazo VITHILANI ambae ni family frieand wenu mimi nikiwa ofisi ya waziri mkuu nakumbuka kupitia kamati ya ulinzi ya Bunge ambayo mzee wako alikuwa anaiongozi walishauri serekali tuingie mkataba huo ambao ni kilio kwa taifa letu. Itakumbukwa wafadhili wakuu wa kampeni za 2005 za baba yako ni VITHILANI, JITU PATEL, NA SHIVACOM, hii nituhuma ingine.

Ipo ingine inayomuhusu mzee wako inayohusiana na kina mama pale CCM na UWT nakumbuka mimi nikiwa na msafara wake yeye kama makumu mkiti ugomvi uliotokea Rukwa baada ya katibu wa UWT na afisa idara ya siasa na itikadi aliekuwa mwanamke kupigana na sisi wasaidizi kutafuta njia ya kuficha aibu hiyo.

Si hilo tu tunakumbuka mgogoro wa mzee wako na viongozi kina LONDA na Mzee mkali juu ya ANNE KILANGO,zipo tuhuma wakati wa mwalimu wafanyakazi wa TTCL walirekodi tape sita tofauti za mzee wako akitumia simu ya serekali kutongoza kina mama.

Haya ni baadhi ambayo tunayaweka hapa ,zipo tuhuma ambazo mwalimu mwaka 1995 alimwambia mzindakaya baada ya kupewa landrover 110 na fedha ambazo Malecela alipokea toka kwa viongozi wa nje kuisaidia ccm akazitia kibindoni,
KIJANA USIRUDIE TENA KUTOA KAULI KAMA HIYO HAPO JUU NA KUSEMA JE NI EPA TUU ZIPO NYINGI YA EPA NI NDOGO.

- Bashe wizi wa mali za umma ni tabia ya kwenye damu, kitabu cha Mwalimu ninacho na inaonejkana hujakisoma, ungekisoma ungejua kwamba Mwalimu hakuwahi kumtuhumu Malecela kwa kuiba anyting, lakini niambie ni mwananchi gani wa taifa hili asiyejua Mwalimu alisema nini kuhusu Bosi wako Lowassa? Alisema ni mwizi infact alimfananisha na Escobar yule M-Colombia wa maunga, amabye kazi yake ilikuwa kuuza unga na kujenga majumba, Mwalimu alisema Lowassa ni sawa yule jambazi Escobar kwa sababu Lowasaa akiwa Waziri wa Ofisi Ya Waziri Mkuu, aliiiba hela za magari ya wabunge na kujenga kijiji cha kukodi kule Arusha.

*Hili sitaki kulisemea sana kitabu cha mwalimu kiko wazi kabisa na sijui kama bashe hajasoma mm si msemaji wake,bali BASHE anauhalali wa kukitumia kuonyesha maovu ya MALECELA,mwalimu alitumia LUGHA za heshima kusema ni namna gani PM alishindwa kumshauri RAIS (MZEE MWINYI) itakumbukwa wahindi waligeuza ikulu baraza lao lakupigia soga,wahindi walivopora nchi,malecela alivuitumia nafasi yake kuifanya mamlaka dhaifu,huu ni usaliti mkubwa lkwa TAIFA HILI kuliko tuhuma zozote ambazo ziliwahi kutokea,tunajua ushiriki wa wale wahindi walioibia BOT kupitia BABA yako.KIJANA USIRUDIE.


- Kuhusu wewe sikufahamu vizuri lakini sio siri kwamba uko kwenye payroll ya nani kwa maneno yako hapa maana yanajisema wazi sana! CCM walikufukuza uongozi kwa sababu ya kutokuwa na maadili, halafu wakakuondoa kwenye kuogmbea ubunge kwa sababu huna maadili, baba yako simjui, lakini at least taifa hili lina ushahidi wa kutosha kuhusu matendo yako mabovu ukiwa kiongozi, ndio maana wakakuondoa kwenye uongozi, na sasa naona unajaribu sana kurudishwa na MAPACHA WATATU kwa sababu huku UV-CCM ndiko peke yake bado mna mikono yenu na mnajaribu kiola njia kuishikilia kwa nguvu, lakini tumeshagundua janja yenu.

*Mimi nimekuwa mwalimu wa BASHE ninamfahamu uwezo na MAPUNGUFU yake,nimekuwa makao makuu ya CHAMA ninafahamu historia ya CHAMA na VIONGOZI ,kwa watanzania wote wanaelewa,BASHE HAJAWAHI KUFUKUZWA CCM hata mara moja,inawezekana hufamu mambo mengi ya nchi yetu ndicho kilichokupelekea kumtuhumu kwamba aliwahi kufukuzwa,kama mtu mmoja alishasema watu hukurupuka juu ya jambo bila kupat taarifa,swala la bashe kuondolewa kuwa mgombea ubunge kwa TUHUMA kwamba si RAIA hii ilikuwa ni aibu kubwa kwa chama na serekali walikurupuka na baada ya siku 3 waligundua walikosea,na hapa ninampongeza kijana huyu kwa kukaa kimya na kuficha AIBU ya mzazi wake na kuamua kurudi kukisaidia chama chake nzega,ingawa sisi wana mageuzi tulimtuhumu sana kwa hilo.

Nikusahihishe HUSSEIN M BASHE hajawahi kufukuzwa ccm kwa kosa lolote,na nimefatilia hili kujiridhisha.


- Bashe mimi sio kiongozi, wewe ndiye kiongozi katika umri wako huo mdogo tayari umeshafukuzwa sehemu mbili muhimu za uongozi wa taifa, sasa unataka nini tena? Moral authority ya kukusanya maoni kuhusu UV-CCM taifa umeipata wapi? Umepewa na hawa MAPACHA WATATU, Moeral authority ya hiyo hotuba yako umeitoa wapi? only in Tanzania, ambapo kiongozi anaweza kufukuzwa mara mbili kwenye taifa na bado akaweza tena kwenda kutoa hotuba kwa ukali, akijidai kujua sana matatizo ya UV-CCM, huku tayari akiwa ameshaharibu mara mbili, unasema ninahitaji kuishi Tanzania kujua haya kwamba huna uwezo wa uongozi na huna Moral authority ya kukusanya maoni yoyote, labda ya namna ya KUWASAFISHA MAPACHA WATATU, kama unavyoonekana kujitahidi sana, you almost did it here, lakini pale uliposema lowassa anafaa na utampigia kura ndipo ulipoharibu!

*Naona kijana hili umelirudia la kufukuzwa nimekueleza na ni vizuri ukakiri kuwa bashe hajawahi kufukuzwa popote ndani ya chama,inawezekana walokupa taarifa wamekupotosha bahati mbaya ama makusudi,nikushauri pia kijana inawezekana kweli lowasa hafai kama ambavyo mwalimu alimuona MALECELA HAFAI lakini kina VITHILANI,na wengine waliona anafaa hayo maono yake na nimepitia hotuba yake sijaona wapi katika hotuba alotoa uvccm akisema lowasa anafaa angetumia hapo tungelimshamngaa BASHE,KAMA ni mawazo yake na si ya uvccm na hajawataka uvccm wamuunge mkno lowasa sioni tatizo liko wapi,kama ambavyo wengi waliona si TATIZO MKAPA ALIPOAMUA KUMKATA MALECELA yeye aliamini hafai na anaefaa ni JK.

- Infact, nina wasi wasi sana na elimu yako pia, maana ungekua nayo basi ungeelewa kwamba hapa JF wananchi tupo huru sana sio kama huko UV-CCM ulikowakomalia na B/S tupu ambazo wewe mwenyewe zimekushinda kuzitimiza kwenye uongozi ndio maana twice umefukuzwa na taifa, I understand kwamba umekuja na watu wako wengi with you hapa JF nilishafahamishwa mapema maana kwenye hayo makundi yenu huwa hamna siri, karibu sana isipokuwa nikutahadharishe one thing, maandishi hayafutiki, na mimi sio kiongozi wala sigombei nafasi yoyote ya taifa so sina anything to lose kwa kulumbana na hoja zako mbuzi sana, HOWEVER NITAKUJIBU MPAKA WANANCHI WAJIONEE WENYEWE UTUPU WAKO WA HOJA, AMBAO UNATHIBITISHA KWAMBA CCM WALIPOKUFUKUZA NAFASI ZAO ZA UONGOZI WALIKUWA RIGHT 100%, I mean wananchi hawana umeme, Tanzania tunalipa Billions zetu za kodi kwa ajili ya umeme ambao haupo, wewe unasema the master minder wa hii National demise utampigia kura maana kama ana makosa kwa nini hajachukuliwa hatua?

*Hili sitalitolea majibu kwani inawezekana taarifa ulizonazo kuwa watakuja hapa JF wengi ni za uhakika,lakini ninachofahamu BASHE JF sio mgeni ni member wa siku nyingi kama ambavyo tulisoma katika gazeti la MWANAHALISI (NADHANI UNALIFAHAMU TUNALIHESHIMU SANA HAPA TANZANIA) Mtua aneitwa MAX aliongea akawataja wana CCM wakwanza kujiunga hapa ni BASHE na NAPE ,unaposema bashe unamkaribisha nimeshangaa kidogo labda na hili umepotoshwa.

Taarifa kwamba amefukuzwa hiyo 100%umepotoshwa na bashe angetakiwa kuja kulijibu hili kiufasaha,swala la ELIMU binafsi nimekuwa mwalimu wake sina shaka juu ya elimu ya BASHE na uwezo wake wa uongozi kitu pekee ambacho nafahamu kuwa ni tatizo lake anatabia ya kusimamia anachikiamini hata kama atabaki peke yake,na mara zote huyu jamaa si NDIO MZEE,kwa tunaofahamu historia za siasa za nchi hii watakumbuka 2007,chaguzi za chama kilichomgharimu ni yeye kupingana na viongozi wa kitaifa na mkoa wake juu ya nani anaefaa kuwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa tabora,akisimamia kumuuonga mkono MZEE ANAEITWA JUMA NKUMBA wakati mtandao ukisema hafai kwakuwa NGUMBA aliwapinga ,nikiwa idara ya uchaguzi CCM makao makuu na Mzee CHIZIII tulimshauri bashe akae mbalina uchaguzi ule akasema atasimamia anachoamini bila kujali nani anampinga huyo mzee.tunafahamu kilichotokea
.

- Lakini unashindwa kujibu swali dogo sana kwamba kwa nini bosi wako unayejaribu sana kumsafisha hapa Lowassa alikimbia kule Bungeni U-Waziri Mkuu bila kufukuzwa?

*Hapa kuna upotoshaji,BOSI WA BASHE si LOWASA tunafahamu si muajiriwa wake,kama tafsiri ya BOSI inatafsiriwa kwa yeye kusema anamuunga mkono lowasa basi umepotosha kija ukweli wa tafsiri hii,balitukijadili kwanini lowasa hakujitetea,inahitaji muda mrefu kulijadili hili kijana muulize mzee malecela ,mwakiembe,samwel sita,wanajua ukweli wa hili,na siku ukimuona MH KIKWETE huko ulaya muulize atakueleza ni SIRI NZITO YA TAIFA LETU.

*ndg wiliamu usinichukulie kama msemaji wa bashe,usinichukulie nimenunuliwa kwani hapa nimeona tayari kila anaekuwa na mtazamo tofauti amenunuliwa.
 
Endelea kuota na EDWARD wako, huyo kishapigwa chini tafuteni mwingine mumpigie kampeni, huyo hauziki kwa watanazania wa leo....Hata leo mshauri atoke CCM uone nini kitatokea kama siyo kujibu kesi moja baada ya nyingine, nyambaf kabisa!!!....eti Lowassa this, Lowassa that, hebu mshaurini atoke LEO CCM tumuone huo ubavu wake akiwa nje.... Jitu halina huruma na watanzania halafu leo anatokea mtu kumtetea hapa eti kwa vile kaahidiwa kacheo au kabahasha ka khaki, inakera sana!

Hapo kwenye Red Ina maana Lowassa hapelekwi mahakamani pamoja na makosa yote aliyonayo kwa vile yuko CCM?
 
very interesting, malecela ana m challenge Bashe kwa kuongelea mambo binafsi kabla hajamaliza na yeye anamshughulikia bashe kwa mambo binafsi, na nilichokiona mdogo wangu malecela nae na hasira nzito inawezekana ni baada ya baba yake kunyukwa vibaya alipoiota ikulu hivyo nae ana fanya lile lile tukose wote, moral authority ya mawazo hayo kwa michango yako unaitoa wapi? kwa wale wasiofahamu tu ni kwamba pamoja na mapungufu yote ya EL hajapatikana Pm hadi leo ukimtoa Moringe aliyefanya kazi na serikali ikawa na heshima kabla ya mbinu chafu za richmond hazifanya kazi yake!
 
SHALOOM JF,










.

*Mimi nimekuwa mwalimu wa BASHE ninamfahamu uwezo na MAPUNGUFU yake,nimekuwa makao makuu ya CHAMA ninafahamu historia ya CHAMA na VIONGOZI ,kwa watanzania wote wanaelewa,BASHE HAJAWAHI KUFUKUZWA CCM hata mara moja,inawezekana hufamu mambo mengi ya nchi yetu ndicho kilichokupelekea kumtuhumu kwamba aliwahi kufukuzwa,kama mtu mmoja alishasema watu hukurupuka juu ya jambo bila kupat taarifa,swala la bashe kuondolewa kuwa mgombea ubunge kwa TUHUMA kwamba si RAIA hii ilikuwa ni aibu kubwa kwa chama na serekali walikurupuka na baada ya siku 3 waligundua walikosea
Nikusahihishe HUSSEIN M BASHE hajawahi kufukuzwa ccm kwa kosa lolote,na nimefatilia hili kujiridhisha.




*Naona kijana hili umelirudia la kufukuzwa nimekueleza na ni vizuri ukakiri kuwa bashe hajawahi kufukuzwa popote ndani ya chama,inawezekana walokupa taarifa wamekupotosha bahati mbaya ama makusudi,nikushauri pia kijana inawezekana kweli lowasa hafai kama ambavyo mwalimu alimuona MALECELA HAFAI lakini kina VITHILANI,na wengine waliona anafaa hayo maono yake na nimepitia hotuba yake sijaona wapi katika hotuba alotoa uvccm akisema lowasa anafaa angetumia hapo tungelimshamngaa BASHE,KAMA ni mawazo yake na si ya uvccm na hajawataka uvccm wamuunge mkno lowasa sioni tatizo liko wapi,kama ambavyo wengi waliona si TATIZO MKAPA ALIPOAMUA KUMKATA MALECELA yeye aliamini hafai na anaefaa ni JK.


*Hili sitalitolea majibu kwani inawezekana taarifa ulizonazo kuwa watakuja hapa JF wengi ni za uhakika,lakini ninachofahamu BASHE JF sio mgeni ni member wa siku nyingi kama ambavyo tulisoma katika gazeti la MWANAHALISI (NADHANI UNALIFAHAMU TUNALIHESHIMU SANA HAPA TANZANIA) Mtua aneitwa MAX aliongea akawataja wana CCM wakwanza kujiunga hapa ni BASHE na NAPE ,unaposema bashe unamkaribisha nimeshangaa kidogo labda na hili umepotoshwa.

Taarifa kwamba amefukuzwa hiyo 100%umepotoshwa na bashe angetakiwa kuja kulijibu hili kiufasaha,swala la ELIMU binafsi nimekuwa mwalimu wake sina shaka juu ya elimu ya BASHE na uwezo wake wa uongozi kitu pekee ambacho nafahamu kuwa ni tatizo lake anatabia ya kusimamia anachikiamini hata kama atabaki peke yake,na mara zote huyu jamaa si NDIO MZEE,kwa tunaofahamu historia za siasa za nchi hii watakumbuka 2007,chaguzi za chama kilichomgharimu ni yeye kupingana na viongozi wa kitaifa na mkoa wake juu ya nani anaefaa kuwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa tabora,akisimamia kumuuonga mkono MZEE ANAEITWA JUMA NKUMBA wakati mtandao ukisema hafai kwakuwa NGUMBA aliwapinga ,nikiwa idara ya uchaguzi CCM makao makuu na Mzee CHIZIII tulimshauri bashe akae mbalina uchaguzi ule akasema atasimamia anachoamini bila kujali nani anampinga huyo mzee.tunafahamu kilichotokea
.

*Hapa kuna upotoshaji,BOSI WA BASHE si LOWASA tunafahamu si muajiriwa wake,kama tafsiri ya BOSI inatafsiriwa kwa yeye kusema anamuunga mkono lowasa basi umepotosha kija ukweli wa tafsiri hii,balitukijadili kwanini lowasa hakujitetea,inahitaji muda mrefu kulijadili hili kijana muulize mzee malecela ,mwakiembe,samwel sita,wanajua ukweli wa hili,na siku ukimuona MH KIKWETE huko ulaya muulize atakueleza ni SIRI NZITO YA TAIFA LETU.

*ndg wiliamu usinichukulie kama msemaji wa bashe,usinichukulie nimenunuliwa kwani hapa nimeona tayari kila anaekuwa na mtazamo tofauti amenunuliwa.
[/COLOR][/B][/COLOR][/COLOR][/SIZE]

- Ha! ha! ha! ha! ha! ha!, Mheshimiwa Bashe Bashe! ha! ha! ha! ha! ha!, Message sent and delivered, & received!

William @ NYC, USA.
 
Hussein Bashe;

1. Haki na Uhuru wa mimi kumuunga mkono LOWASSA akitangaza NIA, na KUTEULIWA na chama changu ni haki yangu ya Kikatiba.


2. Nikuombe uheshimu haki yangu ya kutoa maoni yangu kama wewe ulivyo.


3. Leo mimi nimejitokeza openly na kusema ninachokiamini sijaongelea suala la whether Lowassa ana tuhuma ama hapana,


4. Leo hapa nimesema ninachokiamin, come out sema kama Lowassa hana sifa niliyotaja then utakuwa na hoja ukinipa sababu za yeye kutokuwa na uwezo wa kuchapa kazi na ukajenga hoja nitakuelewa.


5. Tusipige porojo eti Lowassa alimfata Rais na kubembeleza, Kama Lowassa anahusika na Richmond apelekwe mahakamani, hakuna anayemtetea na wala hilo halina mjadala; mahakama itaamua,


6. kama Lowassa ni mwizi basi ni udhaifu wa mamlaka kutowakamata wezi na kuwapeleka mahakamani. Kama una ushahidi peleka katika authority uje hapa utueleze umepeleka ushahidi wa wizi wa Lowassa na hata mimi nitakuona hero!


7. Tujadili facts mkuu, tusiingilie uhuru wa mtu kuchagua. Nimesema wazi kama chama kitamteua nitampigia kura na nimetoa sababu yangu, na si Lowassa pekee,


8. Tusipoteze muda mwingi kujadili LOWASSA, huyu kama ana madhambi yake mamlaka husika zitachukua hatua zinazostahili. Nchi yetu ina bahati mbaya tumekumbwa na ugonjwa wa unaoitwa ‘LOWASSA',


9. Nikutoe shaka juu ya jambo moja: Ssina historia ya kuficha wala kutafuna maneno katika jambo ninaloliamini, .[/FONT]


10. Nimalize kwa kusema LOWASSA akiteuliwa na kupitishwa na chama nitamuunga mkono


11. Mimi nimesema msimamo wangu na kwa jina langu, wewe come out and sema msimamo wako.



Hussein


- Kwa kweli Mheshimiwa sana Bashe, umesikika na kueleweka sana, karibu sana tukate ishus na tuelimishane zaidi na UBARIKIWE SANA NA MUNGU WA MBINGUNI!

william @ NYC, USA.
 
Bashe: Nikutoe shaka juu ya jambo moja: Sina historia ya kuficha wala kutafuna maneno katika jambo ninaloliamini

Mjadala umefungwa au! Nachangia kidogo nikiwa nje ya 'family feud'

Ndugu Bashe, Naomba unishahihishe kama nitakuwa nimeelewa baadhi ya mambo kinyume, lengo langu ni kupata ufafanuzi ili kuondoa maneno yasiyo na uthibitisho au utata.
Kwa vile umejitokeza nashukuru endapo utajibu hoja hapo juu na zitokanazo na thread.

1. Wewe umezaliwa Nzega umekulia na kusomea Tanzania ukitumia respources zote kama raia.
Mwaka 2009(kama sijakosea) ukiwa unajiandaa kugombea ubunge ulienda mahakamani ili kupata uraia wa Tanzania.

Swali: Ukiwa unajiamini, ni kwanini ulienda kuomba uraia ili hali ukijua wewe ni raia? Je hapo si kutafuna maneno. Je unajiamini kwa lipi endapo hukuweza kujiamini kwa yanayokuhusu.

2. Kama unajiamini, katika hotuba yako umetumia maneno ' CCM kutokuwa na social justice'.
Tafadhali tufanunulie ni social justice ipi na ushahidi gani unao wewe wa kuonyesha kuwa
social justice haipo ndani ya chama chako.

3. Katika hotuba yako umesema kuwa CCM isijiingize katika majadiliano kama kudai watu fulani
ni mafisadi. Umesema CCM ijikite katika kujibu hoja za wananchi.

Swali: a)Unataka umma uelewe kuwa ufisadi si sehemu ya hoja za wananchi na wana CCM?

b)Je si kweli kuwa ufisadi ndio unaoipunguzia CCM umaarufu na kwamba ni muhimu
kuushughullikia.
c)Kama chama chako hutaki kiongelee ufisadi, utawezeja kuendeleza sera za chama huku
kikundi cha watu wachache ndani ya chama kikihodhi chama na serikali kwa maslahi
binafsi ?

Nipo tayari kusahihishwa.
 
Maajabu sana katika hii nchni yetu! Rais aliwai kusema kuwa huyu Jamaa si Raia tena alitangaza na nchni nzima mkamsikia, Rais haitendei haki nchni yake hata hii tabia ni magamba inapaswa kuondolewa ndani ya CCM na Ikulu inakuwaje Rais useme kitu alafu kionekane kama kituko!

Ujasiri na Kiapo cha kulinda katiba na mipaka ya Jamhuri ya Tanzania bila woga upo wapi?!


KAKA HAYO NI MATUNDA YA UPEO MDOGO WA RAIS WETU KUFIKIRI, for a serious president when you talk about something ni kwamba unauhakika nacho na especially intelingisia yako iko makini. Tanzania inteligensia ipo kwenye kuzuia maandamano na si kumpa rais concrete issues azungumze hadharani, waziri anasema si raia, uhamiaji wanasema raia na passport wamempa na rais anakuja kusema sio raia yaani inakereketa kweli kuona how serious the govt is not!! uswahili swahili sijui kwa nini nyerere aliing'ang'ania kyela saa hizi ningekuwa malawi!!
 
Hapo kwenye Red Ina maana Lowassa hapelekwi mahakamani pamoja na makosa yote aliyonayo kwa vile yuko CCM?

Reffer kauli ya Fredrick T. Sumaye - " Ukitaka mambo yakunyookee ingia CCM", end of quote.
 
very interesting, malecela ana m challenge Bashe kwa kuongelea mambo binafsi kabla hajamaliza na yeye anamshughulikia bashe kwa mambo binafsi, na nilichokiona mdogo wangu malecela nae na hasira nzito inawezekana ni baada ya baba yake kunyukwa vibaya alipoiota ikulu hivyo nae ana fanya lile lile tukose wote, moral authority ya mawazo hayo kwa michango yako unaitoa wapi? kwa wale wasiofahamu tu ni kwamba pamoja na mapungufu yote ya EL hajapatikana Pm hadi leo ukimtoa Moringe aliyefanya kazi na serikali ikawa na heshima kabla ya mbinu chafu za richmond hazifanya kazi yake!

- Well, MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA PIA AIBARIKI SANA JF!

William @ NYC, USA.
 
Back
Top Bottom