What do you mean by it is shocking..??? What ignorance are you talking about???.. These people are living naturally, they are not contaminated, they are pure, They live their life happily without frustration. Their hearts are pure, they never think of sex and prostitution as you people who on the other hand call your self civilised because you have wastern Education. Whose civilization is that? is it yours? You ware hijab or Kanzu, is that your civilization? Are you and arab? Stop being an alien to ypur self, this is purely alienation to oneself. Come back to your sense and start to value your african cultrue and norms. Stop embracing other people`s cultures. That is why we will never develop because we dispise our selves, as a result when any tone that is played in America and Europe, we all dance blindly the rhythm that they want us to dance. We dont have anything to call our own because we are mentally colonised. It is hi time that we come to our senses and start valuing what is ours.
Nadhani shida kwa tulio wengi tuliozaliwa hivi karibuni ni kudhani yale tuliyoyakuta wazee wetu wakifanya ni yao na hivyo ni yetu kumbe ni mapokeo. Na historia imepotezwa kabisa ili kujenga dunia mpya.
Kuwa Mkristu au Muislamu si jambo la kujivunia sasa wakati ambapo historia yetu inatuambia kuwa sisi weusi wa Afrika tuliitwa "washenzi" na tusiostaarabika kwa sababu hatukuwa na Dini wakati Mkoloni alipoingia katika nyumba zetu, akatuchalaza mijeledi mbele ya familia zetu na kututawala huku wakikaa katika ardhi yetu na sisi kutupa Biblia na Quran tusome ili tumjue Mungu wa Kweli, Mungu ambaye hata wale waliotuletea dini hawakuonyesha kumheshimu na kumfuta kwa matendo yao wenyewe kutokana na kuwafanya babu zetu watumwa, kuwatumikisha katika mashamaba ya manamba, kuwanyonga kama kuku kwa aibu nk nk.
Leo tunaweza kusimama na kujivunia mila za kimagharibi au Kiarabu na kujiona tumezaliwa upya na kustaarabika kwa kuwa sasa si wale "washenzi" tena ambao tulivaa magome ya miti, tuliabudu katika mila nk nk. Lakini historia yetu itakuja kutusuta kwa kuwa Dunia ile iliyotuona sisi Weusi ni Washenzi inabadilika sasa na kuonekna wapo ndo washenzi zaidi.... wazungu na hao waarabu ambao tunawashabikia sasa ndio wanatembea uchi mabarabarani, ndio wanaoongoza kuwa na mambo ya kifirauni kama biashara ya ukahaba (sasa kwa tovuti); ndoa za jinsia moja, kuingiliana kinyume cha maumbile, nk.
Hawa ndio wastaarabu, ambao wakija Umasaini au kule Umakondeni mnawaona wakinunua nguo za kimasai na vinjago vya wamakonde ili wakavae na kupamba kule kwao, ni hzo mila ambazo pengine zinanunuliwa kwa bei ghari sana leo. Leo ukiwa Ulaya na Marekani katika maonyesho ya sanaa, picha toka Afrika ambazo zinaonyesha utamaduni halisi wa Mtu Mweusi zinauzwa kwa bei kubwa sasa na pengine ni hizo wanazokuja kutupiga bure huku tukiwakenulia meno kwa kuwa akili zetu zishaharibika kwa kuona tu ngozi nyeupe.
Hao waliotuita Washenzi karne chache zilizopita, ndio sasa wanakuja kwetu ili tushirikiana nao kiuchumi na kitamaduni, wanatuolea dada zetu ili tuzae nao tuwe familia ya baba na mama moja, na bado tunadhani wao ni bora kuliko sisi ambao akili zetu zimedumazwa na propaganda zao na kujiona pasipo wao hatuwezi.
Tukielimika sana tusisahau historia yetu, tukaona kiarabu na kizungu ni lugha yetu, hijabu, bikini na jeans ni mavazi yetu ...tende, harua na bugglers ni chakua chetu nk nk..akili zetu zitakuwa zimekwanguka!.