simba45 mkali
JF-Expert Member
- Oct 15, 2012
- 1,980
- 1,879
Mkuu hapa umeongea kama mchambuzi mbobezi nakupa mkono kwa kutolea ufafanuzi huu utumbuaji ovyo ovyoNo sikutaka umeme upande bei, bali Tanesco na Ewura ni taasisi ya serikali yenye serikali ambayo ni regulatory yenye mandate yake, autonomy yake na independence yake ambapo serikali ina jicho na mkono wake pale kwa mtindo wa eyes on hands off, serikali kujua kila kilichokuwa kinafanyika hatua kwa hatua, lakini maamuzi yalipofikiwa kwa kufuata taratibu zote ndipo serikali hiyo hiyo inaibuka na eyes on hands on kusimamisha.
Ningekuwa mimi bosi wa Tanesco na Ewura, ningeziandika barua za kumbwagia kazi yake jana ile ile ili Jumatatu asubuhi angezikuta mezani kwake kuliko kusubiri kutumbuliwa kwa aibu na udhalilishaji.
Hili la kupanda umeme hakuna kitu ambacho Prof. Muhongo na rais Magufuli walikuwa hawajui kwa sababu maamuzi yoyote ya kuomba kupandisha umeme yanatoka kwenye bodi ambapo bodi zote zina waserikali, mtu wa ikulu, ambao wote waliripoti hivyo wanajua kila kitu bali kudhalilishana tuu
Paskali