Utumbuaji: Tuache Siasa Kwenye Professionalism, Sio Kila Mtumbuliwa ni Jipu!

Sasa yule wa ewura anabakije kwenye kiti cha kuzunguka? Hivi taasisi ile Ina tija kweli kwa uchumi wetu? Hivi kama hakuna vya kuongeza au kupunguza wana jukumu jingine? Siuoni umuhimu wao na ni bora ingeundwa ewura ya kuwatch bei ya unga na maharage sokoni.
 
Proffessionalism/taaluma ni nini? taaluma isiyotoa suluhisho kwa matatizo Wanainchi inatufaidi nini sisi Wanyonge?

Kupandisha bei ni njia ya mkato tu ya kutatua tatizo na uvivu wa kufikiri, ifike mahali Wasomi wawe na msaada/ufumbuzi na sio shortcut za kuwapandishia Wanyonge gharama za maisha yao.
 
Wanabodi,

Hili ni angalizo tuu kuhusu utumbuaji majipu wa rais Magufuli, sio kila mtumbuliwa ni jipu, wengine wanatumbuliwa kwa circumstances tuu, wengine wanatumbuliwa for political capitalisation tuu na wengine kweli ni majipu hivyo wanatumbuliwa kihalali.

Hili la kuwatumbua watu maprofession tena wenye weledi wa hali ya juu katika professionals zao for political capitalization, ni udhalilishaji wa hali ya juu wa professional za watu.

Hii ni kufuatia tetesi ya utumbuaji mwingine wa maprofessionals unaotarajiwa kufanywa na Mhe. rais any moment from now.


Nasisitiza Tanzania ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima tuwe wakweli kwa kuacha kuingiza siasa kwenye taaluma za watu, kama gharama za uzalishaji umeme per unit ni Kubwa kuliko tozo ya umeme, ukweli ni kwamba umeme lazima upende bei tutake tusitake, hili la Tanesco kuendelea kulishwa kwa spoon feed na serikali huku ikilazimishwa kuuza umeme kwa bei ya hasara, sio sustainable na ni short lived! .

Ili Tanzania tuweze kupiga hatua za kweli za maendeleo na kusonga mbele ni kwanza lazima tuwe wakweli, na pili tuache siasa kwenye kila kitu! .

Let's stop politicizing everything, politicians do politics and leave professionals Alone! .
Heri ya Mwaka Mpya.
Paskali
Lazima alie tumbulia ni ndugu yako kama sio mjomba ako basi baba ako mdogo,kama unakabidhiwa shilika kubwa kama Tanesco afu unakosa ubunifu ni vipi usitumbuliwe?? Hebu kua serious bhana.
 
Kwanza sitaki bei ya umeme ipande.. Umeme wenyewe usiokuwa na uhakika, bei ghali halafu upande tena?? Hapana

Ila sitaki kuamini kuwa eti "mtu mmoja" kwa cheo chake anaweza kupandisha bei ya umeme na ikawa kweli... Upandishaji wa bei ya umeme hauwezi kuwa maamuzi ya mtu mmoja. Something fishy here..
 
Muda ndio msemakweli naomba mungu anipe umri na afya ikifika mwaka 2020 nione uchumi wa tz maana sio jitiada za kusonga mbele zaidi ya visasi,udini,ukanda,ukabila
 
Hiyo mikataba hovyo ya IPTL inayoi cost Tanesco..walioshiriki si tunawajua?...bunge lika kaa...wakawajibishwa na kuwajibika...wamerudishwa madarakani..ni waziri tena..huyo huyo anayesema pesa za escrow ni za iptl...anaelewa ni kwa kias gan tanesco wana struggle...leo kappunga maamuzi ya tanesco...nashauri vunja na ewura kabisa sizonje..walihusika pia..
 
No sikutaka umeme upande bei, bali Tanesco na Ewura ni taasisi ya serikali yenye serikali ambayo ni regulatory yenye mandate yake, autonomy yake na independence yake ambapo serikali ina jicho na mkono wake pale kwa mtindo wa eyes on hands off, serikali kujua kila kilichokuwa kinafanyika hatua kwa hatua, lakini maamuzi yalipofikiwa kwa kufuata taratibu zote ndipo serikali hiyo hiyo inaibuka na eyes on hands on kusimamisha.

Ningekuwa mimi bosi wa Tanesco na Ewura, ningeziandika barua za kumbwagia kazi yake jana ile ile ili Jumatatu asubuhi angezikuta mezani kwake kuliko kusubiri kutumbuliwa kwa aibu na udhalilishaji.

Hili la kupanda umeme hakuna kitu ambacho Prof. Muhongo na rais Magufuli walikuwa hawajui kwa sababu maamuzi yoyote ya kuomba kupandisha umeme yanatoka kwenye bodi ambapo bodi zote zina waserikali, mtu wa ikulu, ambao wote waliripoti hivyo wanajua kila kitu bali kudhalilishana tuu


Paskali

Mkuu, kheri ya mwaka mpya.

Hivi unafahamu unachokiandika hapa na unakisikilizia kweli?

Ummesikia raisi JPM alichokisema leo Kanisani Bukoba?
 
Mods huu uzi uunganishwe na ule uzi wa Magufuli au la sivyo nyuzi zetu zilizounganishwa zifumuliwe na kurejeshwa kuwa nyuzi zinazojitegemea....

EWURA wana sifa moja tu....kupandisha bei ya umeme na mafuta.....

Bwana @Pasco na aliyekutuma uje kumtetea hebu njooni na evidence ya kiasi halisi cha gharama ya kuzalisha unit moja ya umeme.

Mtueleze ni lini hizi production costs zilipanda?

Ni kipi kilichopandisha hizo production costs??

Production costs zilipanda kwa kiwango cha asilimia ngapi?

Upandishwaji wa asilimia 8 unamaanisha nini vs ule wa aslimia 18??

Tanesko haipati ruzuku yoyote kutoka serikali kuu??

Madeni yaliyolipwa kwa Tanesko kwa kiwango kikubwa kutoka taasisi za umma kama hospitali yametumiwaje??

Fedha inayokatwa kwenye mauzo ya luku kwenda EWURA inatumika kwa ajili ya nini haswa??? Uongezekaji wa bei ya umeme au mafuta unawafaidishaje EWURA and specifically mabosi wa EWURA?


Mwisho kabisa....tuwekee CV za hao mabosi wa EWURA tuone weledi wao katika Electricity pricing ili kweli uwe na angle ya kuwatetea kama proffesionals.
Capacity charge ya iptl...mbona wazir aliyeko madarakan aliwajibika..then.. karudi kama vile iptl hakuhusika?...hajui mzigo wa tanesco na mikataba mibovu ilhali serikali inasema pesa za escrow ni za singh sio serikali...kuna double standards za uongozi?... ...kweli siasa ikizid ni vituko...sema mnajionesha wazi wazi namna gani mlivyo!
 
Tunauzunguka mbuyu na mchawi tunamjuwa. Escrow, escrow ni kilio na bwana mkubwa keshasema hafukui makaburi sijui tanesco hilo deni watalipaje ngoja tumuone huyo DG mpya aliyeletwa.
 
No sikutaka umeme upande bei, bali Tanesco na Ewura ni taasisi ya serikali yenye serikali ambayo ni regulatory yenye mandate yake, autonomy yake na independence yake ambapo serikali ina jicho na mkono wake pale kwa mtindo wa eyes on hands off, serikali kujua kila kilichokuwa kinafanyika hatua kwa hatua, lakini maamuzi yalipofikiwa kwa kufuata taratibu zote ndipo serikali hiyo hiyo inaibuka na eyes on hands on kusimamisha.

Ningekuwa mimi bosi wa Tanesco na Ewura, ningeziandika barua za kumbwagia kazi yake jana ile ile ili Jumatatu asubuhi angezikuta mezani kwake kuliko kusubiri kutumbuliwa kwa aibu na udhalilishaji.

Hili la kupanda umeme hakuna kitu ambacho Prof. Muhongo na rais Magufuli walikuwa hawajui kwa sababu maamuzi yoyote ya kuomba kupandisha umeme yanatoka kwenye bodi ambapo bodi zote zina waserikali, mtu wa ikulu, ambao wote waliripoti hivyo wanajua kila kitu bali kudhalilishana tuu


Paskali
Kweli nimeamini wewe ni NJAA kama alivyosema rais. Unatetea ongezeko la umeme au ulikuwa unapata mgao. Waziri ameshatoa makosa yaliyofanywa na TANESCO na EWURA hawakupeleka taarifa hadi wanaongeza rate bado unatetea tuuuu!!!
 
Muhongo kasema hivi hawa Tanesco wamegawana Bonus zinazofikia 60m kila mmoja, Uongozi wa juu na 40m kila mmoja kwa wanaofuatia, kawaambia Pesa hiyo irudishwe. Hiyo mbona hamsemi?
Hawa ni Wasomi Mizigo ambao Degree na PhD zao hazitunufaishi huwezi kua na mamlaka kama ewura ambayo kazi yake ni kupandisha tu UMEME na MAJI ifutwe tu inamanufaa gani kwa mtanzania?

Watumbuliwe tu kama wewe Paskali una uchungu na hao jamaa zako kwa vipindi unavyotayarisha watafutie kwa kwenda hatuwataki.
Hii Pascal hawezi changia, ana makengeza ya kuona mazuri yanayofanywa
 
Hivi ni sahihi kila anaetenguliwa kukaa kimya bila nae kujitokeza hadharani na kueleza ya upande wa pili?

Hivi wote ambao nafasi zao zimetenguliwa kila mmoja alikuwa ana makosa?

Mh.sana yeye yuko sahihi kila siku katika maamuzi yake?

Hivi yule alietenguliwa siku za nyuma na baade kuteuliwa kushika wadhifa mwingine si ushahidi kuwa kuna baadhi wanaonewa?

where is natural justice?

Hivi watu hawa kama wananung'unika mioyoni mwao,bwana mkubwa atafanikiwa?

Kila mtu akikunung'unikia kweli utafinikwa?

Asipofanikiwa bwana mkubwa,sisi wote hatuna hasara?
 
Kwa style hii km mungu angekuwa na maamuzi km haya basi hakuna binadamu angebakia ktk ulimwengu huu hvyo mungu akazd kutupatia muda wa kutafakari na kumrudia tena kwa lengo la kwamba tumuombe msamaha pale tulipo kosea
 
Back
Top Bottom