Utumbuaji: Tuache Siasa Kwenye Professionalism, Sio Kila Mtumbuliwa ni Jipu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,685
119,325
Wanabodi,

Hili ni angalizo tuu kuhusu utumbuaji majipu wa rais Magufuli, sio kila mtumbuliwa ni jipu, wengine wanatumbuliwa kwa circumstances tuu, wengine wanatumbuliwa for political capitalisation tuu na wengine kweli ni majipu hivyo wanastahili kutumbuliwa na wanatumbuliwa kihalali.

Hili la kuwatumbua watu maprofession tena wenye weledi wa hali ya juu katika professionals zao, hawakuomba kuteuliwa bali mteuzi ameona wanafaa kumsaidia, ikifika mahali mteuzi akaona hawamsaidii kama alivyodhani, then ni busara kuwarejesha kwa heshima, kule alikowatoa na sio kuwadhalilisha na kuwatumbua for political capitalization tuu kwa kuwafanya ni mbuzi au kondoo wa kafara, (the sacrificial lambs), au kuwafanya "bangusilio". Huku sio kuwatendea haki!, ni udhalilishaji wa hali ya juu wa professional za watu!.

Hii ni kufuatia tetesi ya utumbuaji mwingine wa maprofessionals unaotarajiwa kufanywa na Mhe. Magufuli at any moment from now!.

Wanabodi,

Hizi ni confirmed tetesi, ni tetesi kwa sababu utumbuaji wenyewe bado haujafanyika, na ni confirmed kwa kuwa ni mtumbuaji mwenyewe kasema atatumbua.

Kufuatia sakata la kupandisha bei ya umeme, it is now confirmed beyond reasonable doubt kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Eng. Felichesm Mramba, ambaye kiukweli sio jipu, ila amekalia kuti kavu, na sio huenda akatumbuliwa, bali for sure atatumbuliwa!, it's now just a matter of time! .

NB. Sio kila anayetumbuliwa ni jipu!.

Source ni "The Horses Mouth.

Sikiliza mwenyewe kwa masikio yako.



Utumbuaji huu pia ni uthibitisho as days go by, rais wetu mpendwa Dr.John Pombe Joseph Magufuli is changing for the better kwa kupunguza Utumbuaji wa papara na badala yake he is taking time kutafakari kwa kina ndipo atumbue, all in all, Utumbuaji huu labda pia umepisha tuu kutowaharibia watu sikukuu yao.

Heri ya Mwaka Mpya.
Paskali

Nasisitiza Tanzania ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima kwanza tujenge mifumo, systems, ukimess unajitumbua mwenyewe wala huna haja ya kusubiri kutumbuliwa!. Lazima tuwe wakweli kwa kuacha kuingiza siasa kwenye taaluma za watu, kama gharama za uzalishaji umeme per unit ni Kubwa kuliko tozo ya umeme, ukweli ni kwamba umeme lazima upande bei tutake tusitake, watu walipie kile wanachotumia, Tanzania ni nchi ya ajabu sana!, badala ya kutoa ruzuku kwenye kilimo, ambayo uchumi wa nchi hii unategemea kilimo, unakwenda kutoa ruzuku kwenye umeme!, tena kwa kutegemea kuikopa hiyo ruzuku kutoka World Bank!, ni ajabu sana!.

Hili la Tanesco kuendelea kubebeshwa mzigo wa madeni yasiyo lipika huku ikitegemea kulishwa kwa spoon feed na serikali huku ikilazimishwa kuuza umeme kwa bei ya hasara, inanunua umeme kwa bei kubwa na kuuza kwa bei ndongo, sio tuu its not sustainable but it is short lived na tunajidanganya!. Huwezi kuishi kwa uongo, living a lie!. Live a fake life!.

Ili Tanzania tuweze kupiga hatua za kweli za maendeleo na kusonga mbele, kwanza ni lazima tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu, na pili tuache siasa kwenye kila kitu! .

Let's stop politicizing everything, let politicians do politics kwenye political arena and let professionals do professionalism kwenye issues za professionalism and politicians should leave professionals Alone! .
Heri ya Mwaka Mpya.
Paskali
 
Huyu anatakiwa atumbuliwe kabisa waache kula pesa za mafisadi na kuja kusingizia professional...........

Sasa hivi kuna gesi inazalishwap umeme,Tanesco wamefunga Luku karibu kwa watumia 75% sasa hasara inatoka wapi?.........

Wakati mtu akitaka kuunganishiwa umeme ananunua nguzo,vifaa vyote kama mita ananunua sasa hizo garama zinatoka wapi?......

Mchawi ni Tanesco wenyewe waliokubali kuingiza siasa kwenye professional yao kusaini mikataba mibovu kama kuwalipa watu Milioni 400 kwa siku...........

Huyu mkurugenzi huwezi sema hana maslahi wakati umeme ukipanda na tozo yao kama EWURA inapanda pia....

Hawa ndio walisababisha mafuta ya taa yapande bila sababu eti uchakachuaji...

Uchakachuaji unathibitiwa kwa kupandishwa mafuta ya taa?.......

Halafu kichekesho pesa wanayokusanya yote kwenye mafuta,umeme maji ni pesa ya kugawana tu kula kwenye vikao,posho na kuandaa press kwa ajili ya kutoa matamko......

Huyu anatumwa na wezi na wanyonyaji wenye kampuni za kufua umeme tuwe wakweli hapa Rais akichukua hatua wala siwezi shangaa............

Pasco nakuheshimu sana lakini kama unatetea hawa wasomi wezi sitaungana na wewe...........
 
"Politics is about everything,but everyhing is not politics and making everything politics,amount to make everything a failure".

Katika hili la kuzuia kupanda kwa bei ya umeme kwa umbumbu na ujinga wetu,tunasifia maamuzi haya ya wanasiasa lakini hatujiulizi chanzo cha haya yote ni nini na hii shirika limefikaje hapa lilipo leo hii.

Alafu hivi huu mchakato wa kupandisha bei ya umeme ulikuwa wa siri?

Mbona serikali haikusitisha mapema huu mchakato wa kupandisha bei ambao umetumia fedha za serikali(EWURA) na badala yake wanasubiri dakika za mwisho?

Huku si kutafuta sifa za kisiasa tu?

Hivi tunastahili kupongeza hapa?

Sometimes huwa nawaza sana kuhusu "evolution na akili zetu!
 
Wanabodi,

Hili ni angalizo tuu kuhusu utumbuaji majipu wa rais Magufuli, sio kila mtumbuliwa ni jipu, wengine wanatumbuliwa kwa circumstances tuu, wengine wanatumbuliwa for political capitalisation tuu na wengine kweli ni majipu hivyo wanatumbuliwa kihalali.

Hili la kuwatumbua watu maprofession tena wenye weledi wa hali ya juu katika professionals zao for political capitalization, ni udhalilishaji wa hali ya juu wa professional za watu.

Hii ni kufuatia tetesi ya utumbuaji mwingine wa maprofessionals unaotarajiwa kufanywa na Mhe. rais any moment from now.


Nasisitiza Tanzania ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima tuwe wakweli kwa kuacha kuingiza siasa kwenye taaluma za watu, kama gharama za uzalishaji umeme per unit ni Kubwa kuliko tozo ya umeme, ukweli ni kwamba umeme lazima upende bei tutake tusitake, hili la Tanesco kuendelea kulishwa kwa spoon feed na serikali huku ikilazimishwa kuuza umeme kwa bei ya hasara, sio sustainable na ni short lived! .

Ili Tanzania tuweze kupiga hatua za kweli za maendeleo na kusonga mbele ni kwanza lazima tuwe wakweli, na pili tuache siasa kwenye kila kitu! .

Let's stop politicizing everything, politicians do politics and leave professionals Alone! .
Heri ya Mwaka Mpya.
Paskali
Pascal Mayalla
Ulitaka Umeme upande bei sio?
 
Huyu anatakiwa atumbuliwe kabisa waache kula pesa za mafisadi na kuja kusingizia professional...........

Sasa hivi kuna gesi inazalisha umeme,Tanesco wamefunga Luku karibu kwa watumia 75% sasa hasara inatoka wapi?.........

Wakati mtu akitaka kuunganishiwa umeme ananunua nguzo,vifaa vyote kama mita ananunua sasa hizo garama zinatoka wapi......

Mchawi ni Tanesco wenyewe waliokubali kusaini mikataba mibovu kama kuwalipa watu Milioni 400 kwa siku...........

Huyu mkurugenzi huwezi sema hana maslahi wakati umeme ukipanda na tozo yao kama EWULA inapanda pia....

Hawa ndio walisababisha mafuta ya taa yapande bila sababu eti uchakachuaji...

Uchakachaji unathibitiwa kwa kupandishwa mafuta ya taa?.......

Halafu kichekesho pesa wanayokusanya yote kwenye mafuta,umeme maji ni pesa ya kugawana tu kula kwenye vikao,posho na kuandaa press kwa ajili ya kutoa matamko......

Huyu anatumwa na wezi na wanyonyaji wenye kampuni za kufua umeme tuwe wa kweli hapa Rais akichukua hatua wala siwezi shangaa............

Haya ndio majipu........
Hiyo mikataba haina influence ya wanasiasa?
 
Pascal Mayalla
Ulitaka Umeme upande bei sio?
No sikutaka umeme upande bei, bali Tanesco na Ewura ni taasisi ya serikali yenye serikali ambayo ni regulatory yenye mandate yake, autonomy yake na independence yake ambapo serikali ina jicho na mkono wake pale kwa mtindo wa eyes on hands off, serikali kujua kila kilichokuwa kinafanyika hatua kwa hatua, lakini maamuzi yalipofikiwa kwa kufuata taratibu zote ndipo serikali hiyo hiyo inaibuka na eyes on hands on kusimamisha.

Ningekuwa mimi bosi wa Tanesco na Ewura, ningeziandika barua za kumbwagia kazi yake jana ile ile ili Jumatatu asubuhi angezikuta mezani kwake kuliko kusubiri kutumbuliwa kwa aibu na udhalilishaji.

Hili la kupanda umeme hakuna kitu ambacho Prof. Muhongo na rais Magufuli walikuwa hawajui kwa sababu maamuzi yoyote ya kuomba kupandisha umeme yanatoka kwenye bodi ambapo bodi zote zina waserikali, mtu wa ikulu, ambao wote waliripoti hivyo wanajua kila kitu bali kudhalilishana tuu


Paskali
 
kwanini mkulu hakupinga toka mwanzo na badala yake akuje kumuunga bw.muongo sasa?hakuona mchakato wa vikao kutoka mwanzo na nia ya EWURA Ku raise cost?.Inaweza kuwa political move ya kufufua the deadly influence of someone above!. ndo yaleyale ya wamachinga toka mwanzo wanavunjiwa vibanda mtu fulani anakuja kutoa tamko la kusitisha eviction ya marching guys....
 
Kwahili Mara ya kwanza nakuunga mkono JPM....[HASHTAG]#wale[/HASHTAG] wanaokaa kwasemeji zao watakupinga# ongeza nafasi ktk kitengo cha utumbuaji nije kusaidia ...sihitaji salary just volunteer tu.
 
No sikutaka umeme upande bei, bali Tanesco na Ewura ni taasisi ya serikali yenye serikali ambayo ni regulatory yenye mandate yake, autonomy yake na independence yake ambapo serikali ina jicho na mkono wake pale kwa mtindo wa eyes on hands off, serikali kujua kila kilichokuwa kinafanyika hatua kwa hatua, lakini maamuzi yalipofikiwa kwa kufuata taratibu zote ndipo serikali hiyo hiyo inaibuka na eyes on hands on kusimamisha.

Ningekuwa mimi bosi wa Tanesco na Ewura, ningeziandika barua za kumbwagia kazi yake jana ile ile ili Jumatatu asubuhi angezikuta mezani kwake kuliko kusubiri kutumbuliwa kwa aibu na udhalilishaji.

Hili la kupanda umeme hakuna kitu ambacho Prof. Muhongo na rais Magufuli walikuwa hawajui kwa sababu maamuzi yoyote ya kuomba kupandisha umeme yanatoka kwenye bodi ambapo bodi zote zina waserikali, mtu wa ikulu, ambao wote waliripoti hivyo wanajua kila kitu bali kudhalilishana tuu


Paskali

Hakuna mdau yoyote aliyeshirikishwa halafu akakubali bei ipande.Wadau wote walikataa wakati wakuchukua maoni at EWURA CCC. Sasa final huyu mkurugenzi mkuu wa ewura akafanya maamuzi ya kukubaliana na Tanesco kupandisha umeme against maoni ya wadau. Fatilia mambo ndio mje kuanzisha thread hapa na sio kukurupuka tuu.
 
Mkuu unamaana aache kutumbua watu waovu ETI KWA KUWA NI WATAALAMU?
Naona umepotoka labda kwa sababu ya wingi wa majipu.Majipu ni mizigo kwa taifa
Majipu sio tu kuwafuta kazi labda tungewafungulia mashtaka ya kuhujumu uchumi na ingebainika dawa ingekuwa kuwafilisi na kuwanyonga.
 
Mods huu uzi uunganishwe na ule uzi wa Magufuli au la sivyo nyuzi zetu zilizounganishwa zifumuliwe na kurejeshwa kuwa nyuzi zinazojitegemea....

EWURA wana sifa moja tu....kupandisha bei ya umeme na mafuta.....

Bwana @Pasco na aliyekutuma uje kumtetea hebu njooni na evidence ya kiasi halisi cha gharama ya kuzalisha unit moja ya umeme.

Mtueleze ni lini hizi production costs zilipanda?

Ni kipi kilichopandisha hizo production costs??

Production costs zilipanda kwa kiwango cha asilimia ngapi?

Upandishwaji wa asilimia 8 unamaanisha nini vs ule wa aslimia 18??

Tanesko haipati ruzuku yoyote kutoka serikali kuu??

Madeni yaliyolipwa kwa Tanesko kwa kiwango kikubwa kutoka taasisi za umma kama hospitali yametumiwaje??

Fedha inayokatwa kwenye mauzo ya luku kwenda EWURA inatumika kwa ajili ya nini haswa??? Uongezekaji wa bei ya umeme au mafuta unawafaidishaje EWURA and specifically mabosi wa EWURA?


Mwisho kabisa....tuwekee CV za hao mabosi wa EWURA tuone weledi wao katika Electricity pricing ili kweli uwe na angle ya kuwatetea kama proffesionals.
 
Back
Top Bottom