Utumbuaji: Tuache Siasa Kwenye Professionalism, Sio Kila Mtumbuliwa ni Jipu!

No sikutaka umeme upande bei, bali Tanesco na Ewura ni taasisi ya serikali yenye serikali ambayo ni regulatory yenye mandate yake, autonomy yake na independence yake ambapo serikali ina jicho na mkono wake pale kwa mtindo wa eyes on hands off, serikali kujua kila kilichokuwa kinafanyika hatua kwa hatua, lakini maamuzi yalipofikiwa kwa kufuata taratibu zote ndipo serikali hiyo hiyo inaibuka na eyes on hands on kusimamisha.

Ningekuwa mimi bosi wa Tanesco na Ewura, ningeziandika barua za kumbwagia kazi yake jana ile ile ili Jumatatu asubuhi angezikuta mezani kwake kuliko kusubiri kutumbuliwa kwa aibu na udhalilishaji.

Hili la kupanda umeme hakuna kitu ambacho Prof. Muhongo na rais Magufuli walikuwa hawajui kwa sababu maamuzi yoyote ya kuomba kupandisha umeme yanatoka kwenye bodi ambapo bodi zote zina waserikali, mtu wa ikulu, ambao wote waliripoti hivyo wanajua kila kitu bali kudhalilishana tuu


Paskali
Wote hao wazinguaji tu hakuna aliye serious.
 
Kwenye uzi huu, nilizungumzia kuhusu utuaji wa majipu wa rais Magufuli, mtu yoyote, no matter how good s/he is, akiisha tumbuliwa tuu, anageuka jipu!.

Hoja yangu hapa ni sio kila mtumbuliwa ni jipu.
Angalia hapa nimesema nini kuhusu Wizara ya Viwanda.

Wanabodi

Rais Magufuli ameamua kuibadili nchi yetu na kuijenga Tanzania ya Viwanda. Tanzania ya Viwanda haiwezi kujengwa kwa kauli ya “Tunajenga Tanzania ya Viwanda”. Tanzania ya viwanda vya ukweli, itajengwa kwa strategies na sio kwa kauli. Huwezi kujenga Tanzania ya Viwanda bila Blue Prints na SMART Objectives, Ni Maneno Mengi, Viendo Vichache. Hivyo hata ukimteua malaika mwenyewe kabisa kutoka mbinguni kuja kuongoza wizara ya Viwanda ili kujenga Tanzania ya Viwanda bila ya blue print yoyote, utaishia kumtumbua!.

Hili la Tanzania ya Viwanda bila Blue Print, nimelisema hapa
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!.

Jee Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu au Vitu?- Wachumi Tusaidieni, Magufuli Analisaidia Taifa au Ataliangamiza?.

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!

P
Masikini Waziri Kakunda, kateuliwa Waziri wa Viwanda, kakuta hakuna blue print yoyote ya Tanzania ya viwanda, within his six months kaitengeneza na imekamilika, ilikuwa inasubiri tuu baraka za baraza la mawaziri, izinduliwe....

Hebu msikilizeni hapa,

Kakunda was dam good.
msikilize hapa







halafu mtu kama huyu, ametumbuliwa, just like that!, to be honest, I'm not very sure if we all determined and we know for sure what we want.

God Bless Tanzania.
Mungu mbariki rais wetu Magufuli, aweze kutufikisha kwenye nchi ya ahadi.

P
 
Hakuna Jambo linalodhorotesha Utumishi wa umma nchini Kama hii style yakutumbuana kila siku. Viongozi wa nchi wameacha kutafuta suluhu ya matatizo ya wananchi badala yake wamejikita kutumbua kila siku na bila hoja ya msingi. Clip ikirushwa mtandaoni tayari mtu amefukuzwa kazi bila kujali uhusika wake.

Lakini pia utaratibu huu umeligharimu taifa fedha nyingi sana ambazo zingeweza kusaidia kufanyika kwa shughuli nyingine zakulisaidia taifa.

Kumtumbua mtu kunaambatana na kumlipa maslahi yake na kama alikuwa mwajiriwa wa kudumu serikalini anarejea kazi yake ya awali bila kushuka kwa mshahara wake Jambo linalopelekea mtu kulipwa fedha nyingi kwa majukumu yasiyolingana na mshaara.

Wananchi wamekuwa wakishangilia lakini wakumbuke anayetumbuliwa analitia taifa hasara kwa kulipwa benefits za cheo alichokuwa nacho pamoja na gharama nyingine ikiwemo kusafirisha familia na mizigo kurejea eneo lake la makazi au kituo Cha kazi kwa wale wanaorejea ofisi zao za awali.

Wanaharakati nao pia wamekuwa wakipiga kelele kushangilia na kufurahia, wanasiasa vilevile na wasomi kwa jumla.

Kiwango Cha uteuzi na utumbuaji Tanzania ni kikubwa kwa miaka mitano iliyopita nadhani kuliko Taifa lolote Duniani. Je watu wanaoteuliwa Wana sifa? Kama Wana sifa je, anayetengua ana sababu zakutengua au nikufurahisha adhara?

Kwa mfumo huu unaoendelea ,ni mteule gani wa Rais atakayekuwa na courage yakusimama na kuongoza wakati anajua akitumbuliwa jamii inamzomea? Kwanini viongozi wasiwe unpopular kulinda cv zao? Leo hii kwa style inayoendelea kama tungepewa nafasi yakuwatumbu Marais kwa mapungufu yao tungekuwa na Marais wangapi?

Nadhani ni wakati wakusema kutumbua No la sivyo wanaotumbbuliwa watiwe hatiani ili wakose stahiki zao na kuliepusha Taifa na gharama za mishahara mikubwa ya watendaji wanaorudi kukaa benchi huku wakinufaika na marupurupu ya vyeo vyao
Naunga mkono hoja, na hili hata mimi niliwahi kulisema hapa
P.
 
Back
Top Bottom