Augustino Fanuel Massongo
JF-Expert Member
- Dec 23, 2016
- 1,279
- 665
Brother hapa umenena point ya msingi sana ambayo huwa mara nyingi baada ya maamuzi ya Ikulu huwa ninajiuliza sana, inakuwaje michakato ya kiutendaji imo ndani ya kanuni,sera au scheme of work na watendaji wanaanza mchakato hatua kwa hatua wakati mwingine kwa taarifa na matangazo ya kusudio la utekelezaji wa jambo fulani hatua zote hizi Ikulu inakaa kimya tu mfano suala la sherehe za siku ya ukimwi duniani (kitaifa),sherehe za kuzima mwenge nk matukio yote haya yalikuwa ndani ya kalenda ya utendaji ya serkali lakini maandalizi yalifanywa watu wakatumiwa mialiko na siku moja kabla ya utekelezji ikulu inatoa tamko la kusitisha na hata kuwataka waalikwa wengine kurejesha fedha za ushiriki nk tena katika language inayowaonyesha kama wamezipata fedha hizo kwa hila.Zoezi la kupandisha bei ya umeme hupitia hatua kadhaa ambazo huhusisha mamlaka husika ikiwemo EWURA kutangaza hadharani kusudio la kufanya hivyo haya yote yalizingatiwa na Ikulu ikawa kimya kwa ninI wasingewazuia?zaidi ya yote kwanini Ikulu isitoe MWONGOZO nini inataka na nini hakitakiwi ili watendaji wa serikali nk wajue wazi kuwa yako mambo yakiutendaji ambayo yalikuwa halali (TRADITIONAL) katika serikali zilizopita ila sasa hayatakiwi tena."Politics is everything but everyhing is not politics and making everything politics,amount to make everything a failure".
Katika hili la kuzuia kupanda kwa bei ya umeme kwa umbumbu na ujinga wetu,tunasifia maamuzi haya ya wanasiasa lakini hatujiulizi chanzo cha haya yote ni nini na hii shirika limefikaje hapa lilipo leo hii.
Alafu hivi huu mchakato wa kupandisha bei ya umeme ulikuwa wa siri?
Mbona serikali haikusitisha mapema huu mchakato wa kupandisha bei ambao umetumia fedha za serikali(EWURA) na badala yake wanasubiri dakika za mwisho?
Huku si kutafuta sifa za kisiasa tu?
Hivi tunastahili kupongeza hapa?
of
Sometimes huwa nawaza sana kuhusu "evolution na akili zetu!