Utoroshwaji wa dhahabu Wilayani Chunya nini kifanyike?

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
44,384
105,225
Kufuatia taarifa iliyotolewa tarehe 28/10/2023 katika Mkoa wa Mbeya wilaya ya Chunya.

Kuhusu wachimbaji kukutwa na vipande 160 vya dhahabu, walivyokuwa wakivitorosha kwenda kuuza nje ya mfumo rasmi.

Ni malalamiko ya wachimbaji wengi kuwa mfumo rasmi wa ununuzi wa dhahabu umekuwa na ushuru mkubwa sana ambao haumfaidishi mchimbaji.

Awali kabla ya mfumo huo rasmi kuja, wachimbaji walikuwa wanauza dhahabu zao sehemu yeyote ambayo wanaona kuna soko zuri la dhahabu.

Lakini tangu mfumo huu wa soko rasmi uletwe na serikali, wachimbaji wamekuwa wakiuziwa dhahabu zao kwa bei ndogo sana ukilinganisha na ile waliyokuwa wakiuza kabla ya mfumo huu kuja.

Zamani kabla ya mfumo rasmi kuingia dhahabu ya gram moja ilikuwa inauzwa hadi 200,000 huko kwenye masoko ya nje na mji.

Lakini serikali ilivyokuja na mfumo rasmi imewataka wachimbaji wauze gram moja kwa 130,000 kiasi ambacho kilionekana kuwa kidogo kisicho watosheleza baadhi ya wachimbaji.

Na kusababisha waanze kuvunja sheria kwa kutoka nje ya mji kuuza dhahabu kama njia ya magendo.

My take: Serikali iongeze bei ya ununuzi wa dhahabu kwenye mfumo rasmi wa soko lake, hii itapunguza wachimbaji kutorosha madini.
 
Mleta mada wewe ni mpotoshaji mkubwa sana. Kabla ya kuletwa masoko wachimbaji wadogo wa dhahabu walikuwa wanakadiriwa bei na watu wanaojulikana kama "makota" au madalali. Baada ya serikali kuleta masoko wachimbaji wadogo na wafanyabiashara wamekuwa na uhuru wa kuchagua mnunuzi mwenye bei nzuri. Hata hivyo bei elekezi huwa inatolewa na tume ya madini masokoni na inatokana na bei ya soko la Dunia ambayo benki kuu BOT huwa wanatoa bei hizo kulingana na bei ya siku. Wanachofanya ni kuweka punguzo au discount kidogo.
Kwa ufupi bei ya dhahabu katika GOLD SOUK nchini Dubai tofauti yake ni kidogo sana na bei anayopata mchimbaji huko Chunya.
Uzalendo unakosekana tu. Mtu yuko tayari amuuzie mhindi au atoroshe na serikali ikose mapato na anachekelea tu.
Ushauri wangu wachimbaji wadogo na wafanyabiashara watumie masoko hayo kwani ndio mkombozi wao. Ili mleta mada uamini ninachokieleza basi nenda maeneo ya migodi hasa ya dhahabu uone maendeleo ya wachimbaji wadogo wengi kabisa. Harrier na Kruger zinanunuliwa kama njugu. Lodges na petrol stations na majengo yanajengwa kama uyoga. Sababu kubwa ni masoko haya.
Serikali inakusanya maduhuli yake vizuri. Mathalan kabla ya masoko haya yaani kuanzia mwaka 2019 kurudi nyuma mchango wa sekta ya madini ulikuwa 3.4% lkn Baada ya kuanzishwa masoko kwa.sasa sekta ya madini inachangia 9.1% na lengo ni kufikia 10% ifikapo 2025. Na wachimbaji wadogo wanachangia 40% wakati kabla ya hapo walikuwa wanachangia 3% ya hiyo 3.4%.
Mleta mada ni mzushi kwamba bei ni 130,000 kwa gram wakati bei elekezi ni
TUME YA MADINI

TAREHE 02/11/2023:

BEI YA DHAHABU (TZS/gramu);

MASOKO YA MADINI

Bei ya Soko la Dunia 159,386.59

Bei ya Soko la Ndani 143,447.93

VITUO VYA UNUNUZI

Bei ya Soko la Dunia 159,386.59

Bei ya Soko la Ndani 140,260.20
 
Umeongea mengi yapo ambayo ya uhalisia yapo ambayo hayana uhalisia.

Kabla ya huu mfumo wa masoko kuletwa kulikuwa na wanunuaji wa dhahabu waliokuwa wanaitwa "madigara"

Hawa wanunuzi walikuwa ni wale mataita wamjini wenye hela zao.

Miaka ya nyuma wakati kuna wanunuaji wachache ndio kulikuwa na hiyo dhana ya kujipangia bei.

Lakini ushindani ulipoongezeka hapo ndio wanunuzi walipokuja na bei tamanishi kuwavutia wauzaji.

Kusema kuwa soko rasmi linanunua dhahabu kwa bei nzuri inayowafutahisha wachimbaji sio kweli.

Ndio maana wachimbaji wanawakwepa brokers waliohalalishwa na serikali kununua dhahabu kisha wanaenda kuuza kwa mataita kimagendo.

Wanajua wakifika kule watauziwa kwa bei kubwa ambayo itawafaidisha.

Na hao mataita wakikusanya mzigo mkubwa wanakwepa kuuza kwenye soko rasmi kwasababu haiwalipi kimaslahi kama wangeenda kuuza nje ya mji.
 
Mleta mada wewe ni mpotoshaji mkubwa sana. Kabla ya kuletwa masoko wachimbaji wadogo wa dhahabu walikuwa wanakadiriwa bei na watu wanaojulikana kama "makota" au madalali. Baada ya serikali kuleta masoko wachimbaji wadogo na wafanyabiashara wamekuwa na uhuru wa kuchagua mnunuzi mwenye bei nzuri. Hata hivyo bei elekezi huwa inatolewa na tume ya madini masokoni na inatokana na bei ya soko la Dunia ambayo benki kuu BOT huwa wanatoa bei hizo kulingana na bei ya siku. Wanachofanya ni kuweka punguzo au discount kidogo.
Kwa ufupi bei ya dhahabu katika GOLD SOUK nchini Dubai tofauti yake ni kidogo sana na bei anayopata mchimbaji huko Chunya.
Uzalendo unakosekana tu. Mtu yuko tayari amuuzie mhindi au atoroshe na serikali ikose mapato na anachekelea tu.
Ushauri wangu wachimbaji wadogo na wafanyabiashara watumie masoko hayo kwani ndio mkombozi wao. Ili mleta mada uamini ninachokieleza basi nenda maeneo ya migodi hasa ya dhahabu uone maendeleo ya wachimbaji wadogo wengi kabisa. Harrier na Kruger zinanunuliwa kama njugu. Lodges na petrol stations na majengo yanajengwa kama uyoga. Sababu kubwa ni masoko haya.
Serikali inakusanya maduhuli yake vizuri. Mathalan kabla ya masoko haya yaani kuanzia mwaka 2019 kurudi nyuma mchango wa sekta ya madini ulikuwa 3.4% lkn Baada ya kuanzishwa masoko kwa.sasa sekta ya madini inachangia 9.1% na lengo ni kufikia 10% ifikapo 2025. Na wachimbaji wadogo wanachangia 40% wakati kabla ya hapo walikuwa wanachangia 3% ya hiyo 3.4%.
Mleta mada ni mzushi kwamba bei ni 130,000 kwa gram wakati bei elekezi ni
TUME YA MADINI

TAREHE 02/11/2023:

BEI YA DHAHABU (TZS/gramu);

MASOKO YA MADINI

Bei ya Soko la Dunia 159,386.59

Bei ya Soko la Ndani 143,447.93

VITUO VYA UNUNUZI

Bei ya Soko la Dunia 159,386.59

Bei ya Soko la Ndani 140,260.20
Hebu tuweke Makato ya kodi
Inayokatwa kwenye hiyo 143,000 mkuu

Ova
 
Back
Top Bottom