Kufutwa kwa leseni ya utafiti wa madini pl/6973/2011 iliyokwisha muda mwaka 2020, baada ya agizo la Doto Biteko kupuuzwa

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,828
21,460
Wananachi wa Kijiji cha Itumbi, Kata ya Matundasi, kwa ujumla wao, wakishirikiana na wachimbaji wa madini wadogo wanaomba Mh Waziri wa Madini kupitia Tume ya Madini , kuifuta leseni ya utafiti PL 6973/2011 inayomilikiwa na kampuni ya Dondoro Minerals Limited.

Leseni hiyo ya utafiti, ilitolewa na Serikali ya Tanzania mwaka 2007 na ilikwisha muda wake mwaka 2020 na sasa ni miaka mitatu tangu kumalizika muda wake na haijafutwa.

Wananachi na wachimbaji wadogo, wamekuwa wakiteseka muda mrefu,kuomba leseni hiyo ambayo imekwisha muda wake ifutwe kwa sababu zifuatazo:

i. Ukubwa wa leseni ni Sq.km 7.9 ambapo ndani ya leseni hiyo ya utafiti wanachi wamejenga mji , na mji umekuwa mkubwa na sasa ni makazi ya watu tena ya kudumu.

ii. Kuna taasisi nyingi za serikali zilizojengwa ndani ya leseni hiyo ya utafiti vikiwemo, shule, chuo cha madini, kituo cha polisi, miradi ya umeme REA,vituo vya afya na stand ya mabasi.

iii. Kuna huduma za kijamii, mfano maeneo ya makaburi ya kuzikia watu, makanisa na misikiti.

iv. Kuna biashara nyingi zimejengwa ndani ya leseni hiyo ambapo ni vituo vya mafuta, nyumba za kulala wageni, nyumba za kupanga watu na makazi mengi ya watu.

v. Vituo vya kuchenjulia dhahabu na midodi ya makampuni ya watu binasfi na wachimbaji wadogo.

vi. Eneo hilo lote lenye leseni ya utafiti lilisha gawiwa leseni ndogo za wachimbaji wadogo na Tume ya Madini.

vii. Aliyekuwa Wazri wa Madini Dotto Biteko alitembelea Itumbi mwaka 2022 na kuhutumbia wananchi na wachimbaji wadogo kwenye mkutano ule alihaidi kuwa leseni hiyo itaifuta, ila hadi leo leseni hiyo haijafutwa na Dotto Biteko amepanda cheo na kuwa Naibu Waziri Mkuu ila bado leseni haijafutwa.

viii. Kutokufutwa kwa leseni hii ya utafiti pia kumwezuia miradi ya maji safi na salama, kutokuwepo eneo la Matundasi na Itumbi.

ix. Kilio hiki , Mbunge wa CCM jimbo la Chunya na Lupa wamekipigia kelele kufutwa kwa leseni hii ya utafiti ambayo muda wake umeisha,pamoja na Diwani wa Kata ya matundasi ila Tume ya Madini imekuwa haifuatilii wala kuichukulia kama jambo muhimu .

Kwa maelezo haya hapo juu, tunamuomba Mh Rais , Mama yetu mpendwa atusaidie ,ili leseni hii ya utafiti ambayo haifanyi utafiti na imeisha muda wake ifutwe ili wananchi waweze kufanya shughuli za kimaendeleo ndani ya Wilaya ya chunya na mkoa wa Mbeya.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

MWANACCM, KIJIJI CHA ITUMBI, KATA YA MATUNDASI, WILAYA YA CHUNYA ,MKOA WA MBEYA.
 
Kumbe ni ya chama chenu pelekeni kwenye vikao vya chama sw. Takataka tu
 
Back
Top Bottom