Story of Change Utofauti computer developer vs programmer vs coder [Kiswahili]

Nijosnotes

Member
Aug 1, 2021
49
125
Habari wana JF

Leo nina mada fupi juu ya utofauti wa kazi za hawa watu watatu tajwa hapo juu kwenye kichwa cha habari katika sekta ya TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) .

Mada hii itachochea wale ambao wanahitaji kuwa na uelewa wa maswala ya TEHEMA na pia kwa wale walio ndani ya gemu watapata kutambua vizuri ubobezi wao.

Twende moja kwa moja kuziangalia tofauti zao...

Coder (Computer coder)
Capture.PNG

Code kwa kutumia PYTHON programming Language


Huyu ni mtu anayejua jinsi yakuandika lugha ambayo mashine (kompyuta) inaelewa, lugha hii inafanya kazi ya kuiambia kompyuta nini cha kufanya. Lugha hii imezoelekea kwa jina la kingereza kama "programming language" .

Programming languages zipo nyingi mfano baadhi ni:- C,C++, Javascript, Java, Python, HTML, CSS, PHP n.k ....... ambapo hizi languages (lugha) zinakufanya uweze kuandika codes zitakazo amrisha kompyuta kufanya jambo fulani unalokusudia.

Mara nyingi Coder anachukua maelezo toka kwa programmer/developer, anachofanya nikutumia lugha anayojua kuiambia mashine(kompyuta) kazi anayotaka ifanye.

Coder wakati mwengine anaitwa junior programmer kwasababu, kwa karne ya sasa Coder amechanganywa kwenye shughuli za programmer. Macoder walikuepo zamani ambapo mtu ilikua inatosha tu kujua kuandika Code unaweza kupata kazi, lakini kulingana na ukuaji wa teknolojia unahitaji ujuzi zaidi yakuandika Code tu.

Coder mara nyingi huwa anazalisha kitu kinachoitwa program, program ni mjumuisho wa codes..

Programmer (computer programmer)
Huyu ni mtu anayeweza kufanya zaidi ya kuandika Code tu, anahusika na kuandaa program kuanzia muonekano ( Design & Architecture), tabia (features) na kuandika code pia.

Programmer anakazi ya kuchukua mawazo na changamoto kwenye jamii kisha kuzitafutia utatuzi kwa kutumia program za kompyuta.

Ingewezekana mtu kujikita tu zaidi katika programming na kuandaa muonekano na tabia ya program pasipo kuandika code, lakini kwa karne ya sasa ilikupata kazi inabidi ujue kuandika code pia.

programmer mara nyingi pia anazalisha program ama anaweza kushiriki kuunda Software/Application.

Developer (Computer Developer)
Huyu ni zaidi ya programmer anakwenda mbali zaidi mpaka kufanya biashara (
kunadi Software aliyo develop), Huyu anatambua nini anafanya kuanzia mwanzo kabisa yanikuanzia wazo la kuandika hiyo program mpaka mwisho inavyoingia sokoni.

Huyu anafanya kazi kubwa yakumuelekeza programmer nini cha kufanya (kama watakua ni watu wawili tofauti). Kwasababu wakati mwengine developer ndo huyohuyo programmer. Developer inatakiwa pia ajue kuandika code.

Unaweza kuwa umeona picha ni kwanini kampuni kubwa za teknolojia zinakua na timu kubwa ya watu wanaoandika code/ wanaofanya programming, kwasababu kunakua na shughuli za ziada kufanya zaidi ya kuandika code tu.

Developer huwa anazalisha Software/Application.

HITIMISHO
Kuna Software engineer pia, huyu ni mtu aliyefunzwa vyote development, programming na coding na zaidi ya hapo anaelimu nyingine ya ujasiriamali, ujuzi wakazi zingine za TEHAMA, anafunzwa nidhamu pia kazini na mambo mengine yakijamii kama utawala bora. Haya mafunzo mara nyingi yanapatikana chuo.

Lakini kuwa coder/programmer/developer sio lazima uende chuo unaweza kupata mwalimu akakufundisha ama unaweza kujifunza mwenyewe kwa kusoma vitabu, kuangalia youtube videos ama kununua kozi mtandaoni.

NB: Kama umependezwa na mada hii, husisahau kubonyeza kamshale ka kuvote hapo chini👇

code.jpg
 
Upvote 3

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom