SoC02 Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, ufanywe kwa ufanisi ili Serikali ipate takwimu kwa urahisi

Stories of Change - 2022 Competition

Mzee Wa Info_tz

New Member
Aug 31, 2022
4
5
Kumekuwa na Mfululizo wa Serikali ya Tanzania kudai Taarifa Mhimu za mwananchi anapotaka kupata huduma serikali ambazo kimsingi ni Mzigo kwa Mwananchi huyo, kuwa nazo kwa wakati anaohitaji kupata Huduma. Mfano unahitaji Kutibiwa kwa Njia ya Bima, Utadaiwa Cheti cha Kuzaliwa, cha serikali ya Mtaa, Ndoa au kingine Chenye Kuonyesha umezaliwa ndani ya Ardhi ya Tanzania.

Kwa Mfano, Zoezi ambalo liefanyika hivi Karibuni la Kuhesabu watu la Sensa ya Watu na Makazi, kuna Baadhi ya Maeneo kulikuwa na Ugumu wa wananchi kushiriki na Kugomea zoezi hilo ama kwa Kutojua umhimu au kudhani serikali haina Dhamira Njema katika uhesabuji wa watu, ndio maana hata Siku ya Mwisho Agosti 29, 2022 imefika Kulikuwa na asilimia 93% za waliohesabiwa.

Kungekuwa na Ufanisi Mzuri Katika Utoaji Vitambulisho vya Taifa, kusingehitaji nguvu Kubwa ya ukusanyaji wa Taarifa za watu au pengine kusingehitajika kabisa kuhesabu kwakuwa Taarifa Mhimu za wananchi zingeshaifikia serikali muda mrefu.

KIVIPI:

Kitambulisho Cha Taifa kikitolewa kwa Kila Mtanzania na kuondoa Kigezo cha Kutimiza Miaka 18, yale Madodoso ya Sensa yangejijibu Mle ndani. Mhimu ni ku ongeza taarifa ambazo mwenye kitambulisho cha Taifa atajaza. Ukiangalia ili kupata kitambulisho cha Taifa unatakiwa kuwa; Mtanzania mwenye umri usiopungua miaka 18, Kuwa na cheti cha kuzaliwa, Cheti cha kumaliza kidato cha Nne au cha Sita, Kadi ya mpiga kura, Bima ya afya, Pasipoti ya kusafiria, Kadi ya Mzanzibar mkazi (kwa mkazi wa Zanzibar).

Mtendaji wa Mtaa au Sheia atamthibitisha kwa kuweka mhuri kwenye fomu aliyoijaza.(Huyu huwajua watu wake hivyo anakiri kuwa ni wanastahili huduma Fulani)

UKiangalia hizo Taarifa Hapo Juu kwa Kiasi ndo hizo hizo kwenye sensa wanauliza.

MUHIMU KUJUA KWAMBA:


*Kitambulisho cha Taifa ni Mwananchi ndo anakifuatilia kwa Kuwa anajua hakuna huduma bila Kitambulisho.

*Kitambulisho cha Taifa Ukiweka sehemu ya Kujaza Taarifa za umiliki wa Mali Mwananchi atajaza kwa sababu anajua bila hicho hawezi kupewa huduma, hivyo ni rahisi serikali kupata Takwimu za kile inachokihitaji.

*Ikishaweka hizo Sehemu za kujaza Taarifa Muhimu, yanabaki tu mazingira ya kufanya Wananchi wake wa Huishe hizo taarifa wanapofanaya shughuli za Maendeleo.

Kwa Mfano ukishatoa Vitambulisho vya Taifa vyenye kila aina ya taarifa unaweka ulazima wa Kuhuisha Kama tunavyofanya Leseni za udereva, kwamba kila Baada ya Miaka Mitatu ili uendelee kupata huduma zako kwa kitambulisho cha Taifa lazima ujaze Taarifa za Mambo ya Maendeleo ambayo umeyafanya kwa Miaka Mitatu au ile itakayopendekezwa, Mwananchi anajaza Mwenyewe Kwa Usiri bila hata kuhojiwa na Mtu kama inavyofanyika na Sensa.

Hii inawezekana ikiwa kutakuwa na nia ya dhati katika utoaji wa Vitambulisho vya Taifa na Nia thabiti ya Kumsaidia Mwananchi. Kwa Mfano Wakati wa Uchaguzi Mkuu, Tume ya Uchaguzi NEC, hutumia Muda Mfupi Kuandikisha na Kugawa Vitambulisho vya Kupigia Kura kwa wananchi kwa Mfumo uleule ambao umekosa ufanisi kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA. (Tume huwaomba wenye umri wa Miaka Zaidi 18 waende kujiandikisha kwa hiari, ila Kwa Vitambulisho vya NIDA kuna Muundo Fulani wa Ulazima ili kupata huduma na wananchi wamekuwa wakifurika Kwenye ofisi za Halmashauri ili wapewe huduma na Matokeo yake wote Manayajua kuhusu Vitambulisho hivyo.

Kwa Kutumia Vitambulisho vya Taifa, vilivyoboreshwa kutaiwezesha serikali kujua wenye Akaunti za Benki, Wenye Nyumba, Wafanyabiashara, Wafanyakazi, Wakulima na Kila aina ya Mtu na shughuli yake bila hata kutembea Mtaani kuuliza.

Tena inaweza kuwekwa kisheria kuwa Kila mzazi akipata Mtoto ahakikishe anamuandalia Kitambulisho cha Taifa kama anavyofanya kwenye cheti cha kuzaliwa, hii itaisaidia serikali kujua idadi na jinsia ya watoto waliopo nchini kwa Kipindi husika na kupanga Mipango yake kwa ufanisi.

Yote Tisa, Kumi ili serikali iweze kupata Takwimu kirahisi lazima ikubali kuwa Ongeza watendaji wa Mamalaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA, Watendaji wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini RITA na watendaji wa Ngazi ya kata wenye weledi na Maarifa juu ya Mifumo ya Usajili. Nitazielezea Hapa;-

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA, inunue au (kuazima Mitambo ya Kutengenezea Vitambulisho Ndani ya Taasisi za serikali) na watoa nakala Laini au Ngumu wawe wengi( zinaweza Kuazimwa Mashine zile na Tume ya Uchaguzi NEC ambazo hutumika Mara chache Ndani ya Miaka mitano).

Zoezi la Kupata Namba au Nakala Ngumu ya Kitambulisho lifanye ama Siku hiyohiyo ya kuwaslisha Taaifa Kikamilifu au lisitumie Zaidi ya saa 48, kwani litakuwa limeweka Taarifa nyingi Nyeti za Mhusika na Mahali alipo, hivyo ni rahisi Kumpata ikiwa kuna Udanganyifu na Mamlaka zisiogope Kumnyang’anya na kuifungia namba ya kitambulisho yule Mdanganyifu.

Kuwepo kwa Ushirikiano Kati ya NIDA na Mamalaka za serikali za Mitaa kama walivyofanya RITA kwa kukasimisha Majukumu ya kuandikisha na kutoa Vyeti vya kuzaliwa. Kwa sasa Kupata cheti cha Mtoto cha kuzaliwa ni ndani Siku Moja, Anapewa namba na cheti Kama Kuna taarifa za ufuatiliaji baadaye RITA wanapiga simu kutaka Ufafanuzi.

NIDA waweke Mfumo kama unaotumiwa na serikali kutoa Namba za kufanyia Malipo. Kwa ku-program Mfumo utakaomuwezesha Afisa aliyeko Mkoani Kupata namba ya Kitambulisho Kwa Njia ya Mtandao na Kumpa yule mhusika na sio wao Watoe huko mkao Makuu ndipo zimfikie mhusika baada ya siku 14, au Kuwe na Vitabu kadhaa Vinavyopelekwa Kila Mkoa kwa ajili ya kuandikisha na kisha wao wazikusanye Takwimu, kutokea kwa wale waliokasimishwa Majukumu.

Kwa Mawazo Yangu, Serikali ikifanya hayo itasaidia kuweka Mabadiliko Makubwa katika Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa na kuifanya serikali ipate Takwimu zake Kirahisi. Natambua kunaweza kuwa na Utetezi wa Masuala ya Usalama wa Nchi kuwa Visitolewe kwa Ngazi ya mashinani, lakini usalama unatakiwa Uimarishwe na Vyombo vya Ulinzi na Usalama hasa Mikoa yenye wageni wengi kibiashara na wale wa Mipakani.

Kwako Mdau wa JF Stories of Change, Nawasilisha. Ikikupendeza Niunge Mkono kwa Kuipigia Kura yako.
 
Back
Top Bottom