Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
Tanzania & Romania Zatia Saini Mikataba ya Ushirikiano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis wakati wakishuhudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo iliyotiwa saini na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, na Waziri wa nchi wa masuala ya Dunia na Mikakati ya Kidiplomasia wa Romania Mhe. Traian - Laurentiu Hristea kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, 17 Novemba, 2023.
"Uhusiano wa Romania na Tanzania ulianza May 1964 yaani mwezi mmoja tu baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Romania imekuwa Mbia wetu kama Nchi na kama Nchi Mwanachama wa Umoja wa Ulaya hivyo ni dhamira yetu kuendelea kudumisha umoja huu" - Rais Samia Suluhu Hassan
"Tumezungumzia wigo wa kuongeza ufadhili wa masomo hususani kwenye fani za Udaktari na Ufamasia, pia katika kudumisha uhusiano Romania imekubali kwa mwaka huu kutoa nafasi 10 za masomo kwa Watanzania katika maeneo tutakayoyachagua" - Rais Samia Suluhu Hassan