The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 836
Chama tawala nchini Tanzania, CCM, kimehitimisha mchakato wa uteuzi wa wagombea wake wa ubunge kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, ambapo matokeo yake yameibua mshangao baada ya baadhi ya majina makubwa kuachwa nje na sura mpya kuteuliwa.
Katika mabadiliko hayo, aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ametajwa kugombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini. Makonda, ambaye mwaka 2020 alijaribu bila mafanikio Jimbo la Kigamboni, safari hii aliongoza kura za maoni kwa kura 9,056 na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) imempitisha kuwa mgombea.
Msanii wa muziki anayefahamika kwa jina la Baba Levo (Clayton Revocatus Chipando) naye ameteuliwa katika Jimbo la Kigoma Mjini. Hii ni baada ya kumaliza wa pili kwenye kura za maoni nyuma ya mbunge anayemaliza muda wake, Kirumbe Ng'enda.
Lakini miongoni mwa waliokosa nafasi ni Ummy Mwalimu, aliyewahi kuwa Waziri wa Afya. Hata baada ya kuongoza kura za maoni kwa kura 5,750 katika Jimbo la Tanga Mjini, jina lake limekatwa na nafasi yake kuchukuliwa na Kassim Mbaraka.
Aidha, wanasiasa waliokuwa wapinzani na maarufu kama wabunge wa zamani wa Chadema, Esther Matiko na Esther Bulaya, wamerejea kupitia CCM. Matiko ameteuliwa kugombea Jimbo la Tarime Mjini, huku Bulaya akiwania tena Jimbo la Bunda Mjini, licha ya kushika nafasi ya tatu kwenye kura za maoni
Mtoto wa waziri Mkuu wa zamani, hayati Edward Lowassa, Fredrick Lowassa naye ameachwa katika jimbo mla Mondoli aliloliongoza katika kipindi kilichopita.
Uteuzi huu wa mwisho unakuja wakati Tanzania inajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba, ambapo wapinzani wanatarajiwa kujaribu kurejesha nguvu baada ya miaka kadhaa ya siasa yenye changamoto.
Kwa wachambuzi, hatua ya CCM kuwatumia sura mpya na kuwarejesha wanasiasa waliokuwa upinzani inaweza kuwa mkakati wa kupanua wigo wa chama hicho hasa kwenye majimbo ya mijini ambayo kwa muda mrefu yalikuwa ngome za upinzani.
Mbali na kutangaza wagombea kupitia majimbo majimbo 272 yakiwemo 222 ya Tanzania Bara na 50 ya Tanzania Zanzibar, pamoja na wajumbe wa Baraza la wawakilihii Zanzibar, uteuzi mkubwa wa kushangaza ni aliyewahi kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN)Dkt. Asha Rose Migiro kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM akichukua nafasi ya Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye amekuwa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM.
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imemteua Migiro ambaye aliwania urais katika uchaguzi wa ndani CCM mwaka 2015 na kuingia tatu bora. Si jina lililotarajiwa wala kutajwa kurejea katika siasa za wakati huu.
Katika kile kinachoonekana kuleta sura mpya, Kenani Kihongosi, Mkuu wa mkoa wa Arusha, ameteuliwa kuwa katibu Mkuu, Itikadi, uenezi na mafunzo wa chama hicho kuchukua nafasi ya Amos Makalla aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa huo.