HANGAYA THE CHIEF
JF-Expert Member
- Sep 10, 2021
- 329
- 947
Katiba ya JMT ibara ya 109 (2) inampa Rais mamlaka ya kuteua Jaji Kiongozi na Majaji wengine wa Mahakama kuu, Muhimili huu wa utoaji haki unatakiwa kuwa huru katika kutekeleza shughuli zake hiyo ibara ya 107B imetamka bayana kuwa mahakama zote zitakuwa huru pasipo kuingiliwa na muhimili wowote. Uhuru wa Mahakama ni pamoja na watoa huduma wake yaani majaji wanapashwa wawe huru, hivyo katiba ibara 110 imewahakikishiria muda wa kukaa kazini na kutekeleza shughuli zao kwa uhuru.
Hivyo pamoja na kuwa na nguvu ya uteuzi ibara109 (2), kuondolewa katika shughuli za ujaji lazima ibara 110 (5) au ibara 110 (5) visomwe kwa pamoja na ibara na ibara ndogo 7, au ibara ndogo ya 6 na 8. kulingana na mazingira.
Kwa kifupi, maana ya mahakama kuwa huru ni watendaji wake kuwa na uhakika wa kazi zao (security of tenure)
Je, uteuzi wa Feleshi ni kuondolewa kazini?
kwa haraka haraka unaweza kuona kala shavu, lakini kimsingi kaondolewa kazini kwa maana sio jaji tena (kwa hiyo anatoka kwenye muhimili wa mahaka ) na kwenda muhimili mwingine yaani serikali.
Nini maana ya uteuzi wake?
Maana ya uteuzi huu ni kwamba ukomo wa majaji kukaa kazini (security of tenure) uko chini ya Rais, anaweza kuteua na kutengua majaji wakati wowote anaotaka.
Nini maana yake kwa Muhimili wa Mahakama?
Muhimili wa mahakama hauko Huru, kwa sababu sasa majaji wataogopa kufanya shughuli zao za utoaji haki kwa uhuru kwa sababu wana mamlaka ya utenguzi, (no security of tenure is guranteed).
Maoni yangu?
Mosi, uteuzi wa Jaji Feleshi kuwa Mwanasheria Mkuu ni kinyume cha Katiba na kuingilia Uhuru wa mahakama kwa maana ya watendaji wake (kuteuliwa kushika nyadhifa zingine tofauti na shughuli zao)
Mahakama iachwe huru, tunawatanzania zaidi ya mililion 60 tupanue wigo kuona kama wapo wanaofaa.
Pili, wanaomshauri Mheshimiwa Rais wetu mpendwa, tumieni taaluma zanu vizuri kwa malengo mapana ya nchi yetu
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE