CCM imemteua Dk Asha Rose- Migiro, kuwa Katibu Mkuu wake kuchukua nafasi ya Dk. Emanuel Nchimbi, Mgombea Mwenza wa Mama Samia.
Aidha Chama hicho kimemteua Kenani Kihongosi, Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi.
Mabadiriko haya ni ya Kimkakati zaidi kuelekea Uchaguzi Mkuu;
1: Dk. Asha- Rose Migiro.
Ni Kada wa CCM ambaye amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na kuiletea heshima kubwa nchi yetu Kimataifa.
Ikumbukwe kuwa kwa sasa CCM inabebwa na wanawake. Dk. Asha Rose- Migiro anaenda kuleta ushawishi kwa wanawake ambao kwa kiasi kikubwa ni miongoni mwa kundi linalolamikia hali ya mambo na mwenendo wa CCM na Serikali yake kwa ujumla.
2: Kenani Kihongosi.
Ni kijana anayepandishwa haraka haraka ndani ya CCM kwa malengo maalum. Sote tunajua vema kuwa karibu robo tatu ya wapiga kura waliojiandikisha kupiga kura ni vijana. Kundi hili linaongoza kulalamika dhidi ya utendaji wa CCm na Serikali yake kwa ujumla.
Kenani Kihongosi anaenda kutumika kama chambo cha CCM kushawishi vijana wakapige kura ukizingatia kuwa hata ndani ya Chama hiki Kuna wanaoimba wimbo wa CHADEMA wa No reform, no election.
3: Tahadhali kutokana na Humphrey Polepole kulisanua kuwa kuna liwaya linalounganisha INEC, CCM na NIDA.
Katika Press yake ya mwisho, Humphrey Polepole alisema CCM wanaiba kura Kwa mfumo wa li-waya lililounganishwa katika Taasisi hizo tatu.
Kama tuhuma hizi ni za kweli, basi huenda Chama hiki sasa kina tafuta njia mbadala ya kupata kura kwani li-waya hilo huenda lisiwasaidie walau kwa kipindi hiki.
Hata hivyo, kutokana na hali ya mambo na mfumo wa CCM hii ya Sasa, mwelekeo wa Serikali ijayo na Mwamko wa wengi ndani ya CCM na jamii nzima kwa ujumla kuelekea 2030, wawili Hawa yaani Dk. Asha Rose- Migiro na Kenani Kihongosi huenda wakatenguliwa mara baada tu ya malengo ya waliowateua kukamilika. Tuombe uzima.