Utendaji wa Fred Mpendazoe akiwa NEMC

ok nakubaliana na wewe kwamba mpendazoe ni mchafu, sasa unashauri asionge ubaya wa Mkapa au uchafu wowote?
Aliyeanzusha thread hii ni lazima ni mtu wa kutumwa na mafisadi.Haiingii akilini kwamba sasa Mpendazoe anaanza kushambuliwa baada ya kusema ukweli uliodhihiri katika ufusadi.
Kitu cha msingi ni kuelewa kuwa Mhe. Mkapa hachukiwi kama Mkapa , lakini ni mambo yanayoenda against the grain of good gevernance ambayo yamewakera waTanzania wengi.
Kurudisha Kiwira mikononi mwa Serikali is a step in the right direction.
Ni wazi kuwa Mpendazoe ni mtu aliye na msimamo mkali zaidi katika hili.
Sasa Philemon asiwe mwoga,kama anaushahidi wa ufisadi wa Mpendazoe si apeleke to kwa Hosea ili sheria ichukue mkondo wake?
Tunamkoma nyani tu awe wa bluu, kijani au kijivu
 
Hakika akina Serukamba wako wengi. Hayo ni mawazo mgando na kinafiki ya kukurupuka unapoguswa na matokeo yaku unaanza kusema ovyo kama mfa maji.
 
Hakika akina Serukamba wako wengi. Hayo ni mawazo mgando na kinafiki ya kukurupuka unapoguswa na matokeo yaku unaanza kusema ovyo kama mfa maji.

Serukamba!!!!
Serukamba!!!!

ukitaka kusikia Serukamba mbunge kijana anaongea Bungeni!!
we Gusa LOwaa na kapaaaaaaa , utamsikia tu!! huyo mbuge kijana sijawahi kumsikia akioongea kinyume na utetezi wa ufisadi hivi ana matatizo gani??

kwa bahati nzuri nimesikia bunge lijalo hana ubavu wa kurudi hata kwake wamechoka kuna kifaa kitanyakua kiti chake tena kwa tiketi ya Chama cha Mafisyundizi!!

Serukamba bye bye labda tafuta ajira kwa R and L and M.
 
....huyu ndie federick mpendazoe..akiwa mkurugenzi wa NEMC alitumika kama kikaragosi cha kuyachapa fimbo makampuni yaliyokuwa na ugomvi na mwenyekiti wake....

...akiwa pale NEMC ilikuwa kama vile uchafuzi wa mazingira nchi hii unafanyika karibu textiles peke yake...ukilala karibu, ukiamka karibu... na tv zinaporomosha!!

...akiwa NEMC kwa kuwa busy na makampuni adui hasi akasahau kupitia vema environmental impact assessment kwenye makampuni mengine kama Barrick na mengineyo hadi yakafunguliwa bila kuwa na mabwawa ya kuchuja adhari za zebaki kwenye maji kabla ya kuyaingiza kwenye mito......unaweza kufikiri ni jambo dogo ....lakini watu wamekufa na kupata ulemavu huko mara na kwenye migodi mingine ... kwa kuwa Frederick Mpendazoe alilala usingizi na NEMC yake ....

..viwanda vingi mijini kwa vijijiini vinatiririsha maji machafu havichukuliwi hatua .....tu waliochukuliwa hatua ni karibu kwa kuwa ni adui wa mwenyekiti wake.....

...hata yeye na mwenyekiti wake walipoondolewa NEMC kwa kuonekana wazi kuwa biased kwenye maamuzi yao .....hajaacha kuwa houseboy wake hadi leo...na kuendelea kuwakilisha mawazo ya bosi wake bungeni badala ya utashi wake binafsi na zaidi wa wapiga kura wake!!!!

...tupinge ufisadi kwa dhati ..lakini kamwe tusisukumwe na chuki binafsi!!!

Kaka nionavyo mimi haya makeke ya Mpendazoe hivi sasa yanapelekewa sana na joto la uchaguzi jimboni. Huyu jamaa mwaka 2005 alikaliwa kooni sana na katibu mkuuwa sasa wa umoja wa vijana MARTIN SHIGHELA. Alichofanya Mpendazoe ambaye wakati huo alikuwa mwanachama mzuri wa MTANDAO ni kuwaomba wakuu wa mtandao kumtuliza SHIGHELA amwachie nafasi hadi 2010. Na hilo likafanyika na SHIGHELA akatuliza mambo akiamini atapata muda wa kujitayarisha zaidi kiuongozi hadi wakati huo.

Tambua kuwa SHIGHELA ni mmoja wa vijana wachache waliojenga uaminifu mkubwa kwa JK na wakulu wa MTANDAO MATUMAINI.....ambao sasa upo katika vita kali na ya wazi na MTANDAO MASLAHI...

Kitendo cha SHIGHELA kupewa ukatibu mkuu wa UVCCM ni wazi kimepandisha presha kubwa kwa MPENDAZOE kwani ni wazi JK anamjengea mazingira mazuri ya kuwa karibu na jimboni tofauti na wakati ule alipokuwa kule LINDI (kumbuka huko kuna MEMBE connection - MTANDAO MATUMAINI).

Kwa maoni yangu, yawezekana MPENDAZOE akachagua kujiunga na kundi la MASIHA FEKI wa CCM ili kujijengea ngome katika wanajamii haswa wale wa jimboni mwake. Na pia hivi sasa kama unavyoona ukishakuwa MASIHA FEKI na unakuwa na ngovu za MENGI hivyo pia unajijengea ULINZI kutokosolewa kwani yeyote atakayekukosoa ataambiwa kuwa NI ADUI WA "MAPAMBANO YA UFISADI" ama "ANATUMIWA NA MAFISADI".

Ukweli simjui MPENDAZOE kwa undani, lakini kwangu mimi hawa wote lao moja...Kulinda nafasi zao, kulinda maslahi ya CHAMA TAWALA na kuhakikisha wanalinda uhalali wa MFUMO FISADI kama WASHIKA DAU wake....(kumbuka hawa sio WADAU WENYEWE KAMA WALIVYO KINA LOWASSA)..

omarilyas
 
Hivi UKWELI una muda wake wa kukubalika?........tutajifunza lini kukubali ukweli hata kama ukweli huo unatumika kama weapon?
 
Kaka, Kwa kukiri kuwa humjui Mpendazoe, si jambo jema kwako hata kidogo. TAFAKARI. Inaashiria kitu si kizuri hata kidogo. Tutajadili.

Sisemi namjua sana Shigela, lakini huyu ni kijana makini na mtulivu sana, lakini kwa ufupi ni kwamba huyu ni mtuhumiwa mkuu wa kesi ya kughushi ambayo hadi sasa inachunguzwa na polisi. Siku anateuliwa kuwa DC alikuwa anatakiwa polisi kwa mahojiano na aliyetakiwa kumhoji anaitwa Suleiman Nyakulinga wa CID Makao Makuu, kitengo cha uhalifu wa nyaraka. Tatizo liko katika mfumo wetu wa uteuzi, amepanda kutoka DC sasa Katibu Mkuu, kesho atakuwa Waziri na huyooooo, ataangalia URAIS. Hii ni hatari sana.
 
Mimi siwaelewi wote wanaozungumziwa hapa isipokuwa naelewa kitu kimoja muhimu sana. Tanzania yetu kila sheria inatoka mdomoni mwa viongozi wa ngazi ya juu. Mwajiriwa yeyote wa serikali unatakiwa kutii amri hiyo hata kama Barricks wanaharibu mazingira lakini amri ni kutoa kibali itabidi utoe hicho kibali..
hjadi leo hii tunavyozungumza vita ya Ufisadi nchini walioondoka wengi ni Mabangusilo, wale watu wasiokuwa na hatia zaidi ya kufuata AMRI ya mkubwa... Mshikaji wangu kavuliwa wadhifa wake kutokana na kesi ya Tabata.. wengine ktk maswala ya benki na BoT na kadhalika ili mradi tu wale wakubwa waliotoa amri na ufisadi wote hawakuguswa...
Hivyo, ni vizuri sana kabla hatujamshutumu mtu mmoja ktk jambo fulani kupima uzito na nguvu ya mtu huyo ktk ufisadi. na amini maneno yangu hata wewe ungekuwa ktk nafasi yake yawezekana kabisa ukajikuta unafanya mabaya ambayo usingeweza kuyafanya kiutendaji - NDIVYO TULIVYO.
 
Kaka, Kwa kukiri kuwa humjui Mpendazoe, si jambo jema kwako hata kidogo. TAFAKARI. Inaashiria kitu si kizuri hata kidogo. Tutajadili.

Sisemi namjua sana Shigela, lakini huyu ni kijana makini na mtulivu sana, lakini kwa ufupi ni kwamba huyu ni mtuhumiwa mkuu wa kesi ya kughushi ambayo hadi sasa inachunguzwa na polisi. Siku anateuliwa kuwa DC alikuwa anatakiwa polisi kwa mahojiano na aliyetakiwa kumhoji anaitwa Suleiman Nyakulinga wa CID Makao Makuu, kitengo cha uhalifu wa nyaraka. Tatizo liko katika mfumo wetu wa uteuzi, amepanda kutoka DC sasa Katibu Mkuu, kesho atakuwa Waziri na huyooooo, ataangalia URAIS. Hii ni hatari sana.

very true Mkuu..........ninachojiuliza ni kwanini hii hali inaachwa ikiendelea.........ukishaingia kwenye lile bomba Mkuu ni rahisi sana ku-get away na alot of things..............unafikri watu kama hao wanakuwa vipi wanapoona mikataba ya ajabu ajabu ikipitishwa........
 
Sioni connection ya masuala ya NEMC na ufisadi wa Mkapa uliowekwa wazi na watu mbalimbali akiwemo Mpendazoe. Ni dhahiri kwamba hii post ina chuki binafsi ndani yake. Alichosema Mpendazoe Bungeni ni ukweli mtupu. Kwamba makosa aliyoyafanya Mkapa yanatakiwa yasafishwe mahakamani basi! Asikurupuke mtu mwingine yeyote na kusema eti Mkapa ni clean!
 
PM unaanza kufulia...vipi na wewe umekuwa manyerere...be Tanzanian na mkweli...leo mpendazoe umekumbushwa kwamba yupo kisa kaongelea Mkapa..be serious...babu yako kaezeka vigae nini?
 
very true Mkuu..........ninachojiuliza ni kwanini hii hali inaachwa ikiendelea.........ukishaingia kwenye lile bomba Mkuu ni rahisi sana ku-get away na alot of things..............unafikri watu kama hao wanakuwa vipi wanapoona mikataba ya ajabu ajabu ikipitishwa........
na hii silaha ya kuwabeba watu walio iba ilitumiwa sana na mkapa katika kuwafunga mdomo wazee wa shirecu na nyanza, maana aliwaachia au kuwalegezea kamba ili na yeye akifanya hiyo mikataba ya madini wakawa hawana cha kusema, maana mafaili yao yapo takukuru
 
Tatizo kubwa la wezi wakiguswa hujibu hoja kwa kusema, "Hata anayetupigia kelele za mwizi na yeye mwizi", walianza kwa Mwakyembe, ambaye sasa kanyamaza na wao wamemuacha. Ni mbinu ya kunyamazishana. Mpendazoe hakuwa issue, lakini sasa kwa kuwa kaanza kusema, ameanza kuianikwa. Why PM kama ulijua anasababisha watu kufa katika migodi ukanyamaza? Na wewe PM ni muuaji maana ulinyamazia hadi atajwe MKapa ndio umseme Mpendazoe. Nadhani hii mada ni kutaka kuzima hoja. Mimi napinga na nitapinga mpaka mwisho hii tabia ya kujibu mapigo. Bahati nzuri Slaa alipambana lakini alianza kuandamwa kwamba na yeye ni mwizi, Zitto naye aliandamwa sana wakati wa Buzwagi na wengine wengi. Tuseme mambo wakati mwafaka si mpaka mtu alipue jambo ndio tumuandame.

Nilishwahi kusema hapa, hata ikitokea mwizi ama mtuhumiwa mkuu wa kesi yoyote akitoa siri ya wezi, tuache kukamata wezi kwa sababu eti aliyetoa siri ni mwizi!??? Hapana. Mbinu za kipelelezi zinatuambia kwamba mtoa taarifa za uhalifu hata akiwa mhalifu, fanyia kazi taarifa kwanza na mara nyingi taarifa za mhalifu, awe ametubu ama bado ni mhalifu, huwa na ukweli mwingi zaidi. JF isitumike kukatisha watu tamaa. JF akiwamo PM wamekuwa wakisema sana kuhusu Mkapa, sasa Mpendazoe kakosea?

Mkuu,
Unachoongea hapo juu si hoja yenye nguvu dhidi ya maelezo ya PM. Unapo-deal na issues mbalimbali katika uso wa dunia ni lazima uwe na approaches tofauti ili upate mafanikio. Katika hili PM hakuhitaji afahamu aliyokuwa anayafanya Mpendazoe huko nyuma akiwa NEMC at that time. Kinachojitokeza ni kuwa unaweza kuyajua hayo leo kutokana na kufanya utafiti. I believe PM katika utafiti wake amegundua tatizo la msingi katika sakata la uchafuzi wa mazingira kule Mara limetokana na kutokuwajibika kwa watendaji wa NEMC hususan Mpendazoe. kwa hiyo basi jina la Mpendazoe ni sehemu ya historia ambayo imeshawekwa katika maafa yanayoendelea kuwapata wananchi mbalimbali hasa wale wa Mara. Kama umekuwa unafuatilia current issues, utagundua kwamba hili swala liko bungeni sasa hivi kwa maana hiyo ni wajibu wetu sisi kaka wananchi pia tufuatilie kwa makini, na kujua kulikoni???.
Tusimtazame mtu uso na kumuonea haya, kama huna data basi fanya utafiti wako juu ya hili suala na wewe uweze kuchangia kikamilifu juu ya tatizo la wananchi wa Mara.
 
Back
Top Bottom