Stories of Change - 2022 Competition

Shida Masuba

Member
May 30, 2016
6
4
Utawala ni uongozi ambao unakuwa madarakani katika kipindi fulani, utawala huu unaweza kutokana na kuchaguliwa, kurithi kama ilivyo katika baadhi ya nchi kama Korea Kaskazini ama mapinduzi.

utawala bora no utawala unaozingatia misingi ya haki, taratibu na kanuni kwa mujibu wa sheria ambazo nchi imejiwekea.


Utawala bora nchini Tanzania unaweza kutazamwa katika mambo yafuatayo:

1. Demokrasia; Tanzania ni nchi ya Demokrasia ambayo inafuata mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1992, na hivyo kuruhusu vyama vingi kushiriki katika uchaguzi mkuu wa viongozi wa serikali kuu na serikali za mitaa. Utawala bora katika demokrasia ni Pamoja na kuheshimu mawazo yanayokinzana na mtazamo wako kama kiongozi na kuyafanyia kazi kwa namna ambayo itaweka thamani ya utu, na kuimarisha amani Kwa njia ya maridhiano, na majadiliano. Jambo ambalo lilijidhihirisha dhahiri katika uongozi wa Hayati Benjamin W. Mkapa, na Jakaya M. Kikwete. Katika awamu ya tano utawala bora ulishuka kwa sababu hakukuwa na Uhuru wa kujieleza, upinzani ulionekana ni uadui. Haya yalidhihirika wazi kupitia matukio mbali mbali yaliyotendeka, ikiwemo kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani na mikutano ya ndani ya vyama hivyo kuzuiliwa . Naamini na ninatumaini kuwa utawala wa sasa utazingatia hilo juu ya demokrasia ya nchi hii.

2. Ushiriki wa Wananchi katika maamuzi ambayo huanzia kwenye sanduku la kura, ushirikishwaji katika maamuzi. Nchini mwetu utawala bado hili halijatazama kwa kina. Miongoni mwa mambo ambayo yanadhirisha ni msuguano kuhusu uhitaji wa katiba mpya. Ni muhimu utawala ukaelewa kuwa katiba ni mwongozo wa sheria za nchi ambazo kila raia anaongoza, anapewa haki na kuadhibiwa kwayo. Hivyo ni muhimu kuridhia mapendekezo ya wananchi katika urekebishaji wa katiba

3. Uchumi wa taifa na mwananchi. Utawala bora ni lazima usimamie uchumi wa nchi na wa mwananchi mmomoja kwa kuhakikisha mwananchi anawekewa mazingira rafiki ya kiuchumi. Lakini Tanzania kwa sasa tunaweza kusema kuwa kuna changamoto kubwa kwa sababu utawala unaona changamoto za kiuchumi mwananchi anaweza kuzibeba. Tukiangazia tozo, za muamala, kwenye simu, tozo za majengo, wapangaji wengi wanaumia na mfumo wa ulipaji kwa njia ya luku, huku wasio na umeme huko vijijini hawalipii huduma hiyo kwa sababu hawatambuliki na mfumo wa kieletroniki wa luku.


Raslimali, Tanzania tuna raslimali nyingi, kwa mfano madini. Utawala bora lazima uzilinde raslimali hizo kwa manufaa ya taifa. Katika nchi yetu tuna madini ya kila namna. Nashauri kuwa serikali ifungue kampuni itakayohusika na utengenezaji wa Vito na bidhaa nyingine zitokanazo na madini ili kuongeza thamani ya madini sanjari na kukuza uchumi wa taifa. Tunaweza kumuenzi Muamar Gaddafi katika usimamizi wa raslimali zetu.

Upande wa utalii, nchi yetu ina vivutio vingi ambavyo havijaendelezwa na hivyo kutofikiwa na watalii vya kutosha. Utawala bora no pamoja na kuhakisha vyanzo vya mapato vinasimamiwa kwa umakini mkubwa. Kwa mfano wilayani Rungwe kuna mlima Rungwe, maporomoko ya Kaporogwe, ziwa kisibha nk. Maeneo haya yanavutia sana lakini miundombinu ndiyo changamoto kubwa. Sehemu hizi zikiboreshwa zitakuwa chanzo kikubwa cha mapato. Tukiachana na Rungwe, kuna Kyela kuna sehemu inaitwa Kilambo kuna chemichemi ya majimoto. Lakini eneo hilo ni kama limetelekezwa. Njia haishawishi mgeni kufika hapo. Lakini ni utalii mzuri eneo lenye utajiri wa magadi pia

4. Utawala bora una jukumu kuhakikisha chakula kinapatikaba nchini kwa kununua mazao kutoka kwa wakulima na kuweka kwenye ghala za serikali, ziada ndiyo huruhusiwa kuuzwa nje wakiwa wamejihakikishia uwepo wa chakula. Hili litapunguza mfumuko wa bei za vyakula usio na mpangilio. Mbali na hilo serikali yenye utawala bora huzingatia mahitaji makuu ya jamii. Mfano: mafuta ya kula na sukari, tunaweza kuweka mikakati maalumu ya kuboresha kilimo cha miwa na alizeti katika mikoa inayolima ipewe kipaumbele na kuwezeshwa kwenye pembejeo ili kuongeza tija na kiwango cha upatikanaji wa bidhaa hizo.

5. Biashara, utawala bora huhakikisha mfanyabiasha anawapatia mahitaji muhimu wafanyakazi na wakulima wanafikiwa na huduma kwa wakati na iwezekanvyo. Jamii inanufaika na uwepo wake kwa maana ya mazingira ya biashara, vibali na fedha zenyewe. Kuhakikisha fedha zinapatikana katika benki za biashara ili wananchi wafikiwe nazo kwa Urahisi. Sanjari na hilo kuhakikisha mzunguko wa fedha uko thabiti katika jamii kwa thamani inayoendana na maisha ya wakati huo.

Fauka utawala bora unajikita katika kuhakikisha changamoto za jamii zitatuliwa kwa kuweka mazingira wezeshi kwa raia wake, kuwekeza fedha katika benki za biashara ili wananchi wafikiwe kiurahisi, fedha kuwa katika mzunguko mzuri. Sanjari na hilo kuweka vyanzo vya mapato vingi ambavyo havimwelemei mwananchi.
 
Back
Top Bottom