Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Safi Munkari.
Huyo jamaa alimvamia huyu dem kwa style ya kujifanya matawi ya juu.Maana huwezi kusema anapenda hela na uponae.Maana ishara za wapenda hela unaziona mapema.

Huyo nae Hapo Juu anajidai Kizungu eti No money No Honey,kwa tafsiri yangu Hakuna pesa hakuna asali.Sasa we nani atakupa asali bure hata huko tabora wanakovuna inabidi ununue.au sijui amekosea thread huyu au mie nime over understanda(kizungu kidogo kumtisha)

Kwa ufupi inategemea na ulivyomvamia na malengo yako kwake.
 
Mimi saa nyingine kwa dada zetu hawa naona ni umaskini wa mawazo(kifikra)..kutotambua thamani ya mwanamke zaidi kuliko pesa......inashangaza sana mtu anakukimbia kisa una hela....ila bado anataka attension yako na anataka um-mle though yupo na mtu mwenye hela alzo kimbila...ndo mana nasema ni umaskini wa mawazo tu wakati mwingine....

Kweli kabisa...
 
Mmmmh lakini too much

Mkuu niliwahi kuambiwa kuwa "yaani unakuja unanigegeda unanichafua tu na leo ni mara yako ya mwisho"

Umaskini umenikosesha msichana niliyempenda sana lkn I have to give her some kudos maana alinivumilia mwezi mzima akidanganyika na suti zangu kama nina pesa ahahahahaha!

Mapenzi bila hela hayapo!
 
Enzi za mwaalim, mapenzi yalikuwa yakienda bila pesa.lakin siku hiz WIZI MTUPU. Utakuta eti ukimtongoza 2 mdada 1st time atakuliza hivi unafanyia wapi kaka? Kesho utasikia,'kaka niongezee ela kwenye simu yangu....nasema wizi mtupu,ni kuliana tu ela...lakin pia mh angalia walvyo pia mwonekano wake.mfano dada kapiga jeans kali, tishet matata, cm ya laki 8 we unayo ya elf 30!! Akikuomba ela unashangaa tenaaa? Wanawake wa sasa si wa zaman, wanataka shekel kaka.ila tafuta asietaka gharama kubwa, na alie tayari kuiolewa ndo hatataka gharama kubwa
 
Jamani hii statement 'pesa ndo kila kitu' inajihidhirisha wazi wazi kwenye maisha yetu ya kila siku, nimekumbuka tukio moja la hivi karibunii ndo nikaikumbuka tena hii statement.

Tukio lenyewe ni ile skendo ya daidomo na uyowa, nilichoshangaa baada ya skendo ile sikusikia reaction yoyote toka kwa peni, itakumbukwa ndo kwanza alikuwa aingia kwenye mahaba motomoto na daidomo lakini jamaa bila aibu akamsaliti live tena within such short period of their relationship.

My take: mapenzi na pesa haviwezi kutenganishwa, hivyo ipo haja ya kuhamasisha vijana wa kiume kusakanya pesa kwa udi na uvumba ili ku-sustain relationships zao, iwe ndoa au urafiki to wa boyfriend na girlfriend, vinginevyo relationships zao zintakuwa majangaaa!! Am I right??????

Jamani kuna some more examples zinazoshabihiana na uzi wangu, here we go!
[h=1]Kwanini wanasoka wa Tanzania hawatoki kimapenzi na celebrities wa kike?[/h]
By Israel Saria on August 5, 2013
ZUNGUKA kumbi zote za disko. Hautamuona mwanasoka yoyote wa Tanzania amemshika kiuno mwanamke maarufu (celebrity) katika fani yoyote maarufu kuanzia, filamu, muziki hadi siasa. Na sio hao tu, wanasoka wa Tanzania wanaishi dunia tofauti na wanawake wenye hadhi za juu (high Personalities female).

Wakati David Beckham akihangaika na Victoria Adams, Cristiano Ronaldo akihangaika na mwanamitindo wa Kirusi, Irina Shayk, hali ni tofauti kwa mwanasoka wa Tanzania. Ni nadra kwenda katika klabu ya usiku (Nightclub) na kumkuta Nadir Haroub ‘Cannavaro' akiwa katika mtoko na Mwanamitindo Flavian Matata. Unajua kwa nini?
Baada ya kazi ni wakati wa… (Photo credit: kikuyumoja)

Kuna sababu nne kubwa. Kwanza ni umaskini unaowakabili. Hawapo katika kiwango cha kushindana kifedha na mastaa wa fani nyingine ndani ya nchi. Wakati mwanamuziki Diamond anaweza kuingiza sh 30 milioni kwa shoo za mwezi mmoja, inamchukua Mrisho Ngassa miaka miwili ya kusaini mkataba mpya ndipo apate fedha hizo.

Wema Sepetu hawezi kwenda kwa Mrisho Ngassa. Atakimbilia kwa Diamond kwa sababu anajua wanaweza kuagiza chochote wanachojisikia katika hoteli yoyote ya hadhi ya nyota tano bila ya hofu.

Mwanadamu anayesubiri shilingi 30 milioni baada ya misimu miwili ana tofauti kubwa na mwanadamu anayesubiri shilingi 30 milioni baada ya wiki tatu. Kwa Ulaya na kwingineko, hali ni tofauti. Wanasoka wameingia katika soko la ushindani wa kimaisha na wasanii na mastaa wengine kutokana na mapato makubwa wanayotapata ndani ya fani zao, na katika matangazo ya biashara.
David Beckham, Kanye West na Tom Cruise wote wanaweza kununua nyumba katika mtaa mmoja wa Beverly Hills, ni wazi kwamba wote wapo katika nafasi sawa ya kutoka kimapenzi na Kim Kardashian bila ya kujali kama Kanye West amemuwahi.
Lakini pia sababu ya pili ya msingi inayowanyima fursa wanasoka wetu ni makuzi waliyopitia ambayo yamewanyima fursa katika elimu na tabia ya kujiamini katika maisha yao. Wengi wao wamekosa uwezo wa kujiamini, kujitawala kifikra na kujiamulia mambo kwa uhuru. Utaongea nini mezani na mrembo anayejiamini huku akinywa Savannah yake taratibu.
Wakati pesa likiwa tatizo la kimsingi, bado upeo wa fikra kichwani ni tatizo jingine linalokusumbua ukikaa na mrembo aliyemaliza chuo kikuu au IFM miaka sita iliyopita. Unahitaji kuwa zaidi ya Jerry Tegete. Zaidi ya mabao, una nini mezani. Pesa au elimu?
Zaidi ya yote haya. Wanasoka wa Tanzania wametoka Ghetto. Ni wachache waliotokea katika familia zinazoeleweka kwa sababu mchezo wa soka bado unabakia na taswira kuwa ni mchezo wa kihuni na ni watu wa hali ya chini.
Zao linatoka katika picha hii iliyopo kuhusu soka, lazima litamtoa mwanasoka ambaye kichwa chake kwa asilimia nyingi kinafikiria uhuni na kushindwa kujiamini katika fursa zilizopo. Mwanasoka aliyetoka katika familia isiyoeleweka hawezi kujipa hadhi sawa na ya kujiamini mbele ya Mwanamitindo anayefanya kazi zake London, Paris, Milan na kwingineko na ambaye amelelewa katika familia njema.
Mpaka wanasoka wa Tanzania watakapoanza kutoka nje ya mipaka yao na kuelimika nadhani watajipa nafasi nzuri ya kuanza kutoka kimapenzi na celebrities wa kike. Ni kwa sababu wakiwa nje watakuwa kama wako darasani huku wakielimika na kujiongezea uwezo mkubwa wa kujiamini.
Nje, wanasoka wanafundishwa jinsi ya kujiamini, jinsi ya kuongea, jinsi ya kujitawala na jinsi ya kujipenda. Na zaidi ya yote watalalia paundi nyingi na Dola ambazo zitajikuta zikiongea zaidi kuliko midomo yao!

source:http://www.tanzaniasports.com/featu...ia-hawatoki-kimapenzi-na-celebrities-wa-kike/
 
Ulimbukeni fanya kazi kwa bidii basi sio eti sababu ya penzi uliona wapi penzi la kweli likinunuliwa kama sio kutafuta dhahama.mnajidanganya sana nyie.
 
Ukiwa na hela ukakosa penzi utajifariji na mjengo mkali mashine za kutembelea mishoping na mambo kama hayo!!!

Pesa chweee na penzi ligome weeeeee!!!!!

Masela tupige kazi saaaanaaa kupata chedar mengine yatajipanga
 
mkuu hapo kwa red inaweza tokea kweli?
 
Ulimbukeni fanya kazi kwa bidii basi sio eti sababu ya penzi uliona wapi penzi la kweli likinunuliwa kama sio kutafuta dhahama.mnajidanganya sana nyie.

of course siyo kwa sababu ya penzi, ila tukubali kuwa ni ngumu ku-sustain penzi bila pesa
 
Jamani hii statement 'pesa ndo kila kitu' inajihidhirisha wazi wazi kwenye maisha yetu ya kila siku, nimekumbuka tukio moja la hivi karibunii ndo nikaikumbuka tena hii statement.

Tukio lenyewe ni ile skendo ya daidomo na uyowa, nilichoshangaa baada ya skendo ile sikusikia reaction yoyote toka kwa peni, itakumbukwa ndo kwanza alikuwa aingia kwenye mahaba motomoto na daidomo lakini jamaa bila aibu akamsaliti live tena within such short period of their relationship.

My take: mapenzi na pesa haviwezi kutenganishwa, hivyo ipo haja ya kuhamasisha vijana wa kiume kusakanya pesa kwa udi na uvumba ili ku-sustain relationships zao, iwe ndoa au urafiki to wa boyfriend na girlfriend, vinginevyo relationships zao zintakuwa majangaaa!! Am I right??????
Mkuu umejuaje kuwa ni pesa ndio iliyomfanya huyo peni asifanye chochote kwa diamond?
 
Mkuu umejuaje kuwa ni pesa ndio iliyomfanya huyo peni asifanye chochote kwa diamond?

aaaha, ndo tetesi zilizozagaa mujini mkuu, hebu twambie wewe sababu unayoifahamu basi
 
aaaha, ndo tetesi zilizozagaa mujini mkuu, hebu twambie wewe sababu unayoifahamu basi
Umejibu vyema mkuu kama ni tetesi sawa, ila kama hakuna ushahidi wa moja kwa moja tunaweza sema kutokureact kunaweza sababishwa na mambo mengi ikiwemo hilo 1.pesa pia, 2. mtu anavyochukulia jambo lenyewe 3. Tukokujiamini kama akiondoka pale atakwenda wapi. 4. Bahati ya kuwa na mtu maarufu 5. Mshininikizo ya wazazi au walezi au yeyote. 6 N.K
 
Back
Top Bottom