Ukimuuliza msichana swali hili "je ni aina gani ya mwanaume unaependa aje kuwa mumeo wa ndoa?"Atakujibu hivi "napenda mwanaume yeyote nitakaejaaliwa na Mungu, awe anajiheshimu, mwenye kujua thamani yangu na kunithamini, awe na mapenzi ya kweli pia awe mwanaume aliye kamilika kuhusu pesa na mali hayo anajua Mungu"
Huo unaitwa uongo mkamilifu kwa maana hili neno (mwanaume aliyekamilika) wanawake humaanisha kuwa ili uwe mwanaume wa kweli lazima uwe na uwezo wa kutia mimba mtoto wa watu.
Lakini uwezo wa kutia mimba hautoshi kukufanya wewe kuitwa mwanaume, bali uwanaume wako hutokana na pesa uliyonayo. Maana hata mbuzi zinatia mimba, ila kwa kuwa hazimiliki pesa ndio maana hautakuta mbuzi zimeoana.
Vijana wengi hukimbilia kujimarisha katika huduma ya ndoa na kusahau majukumu ya familia.Mwanamke anaposema kuwa anahitaji mwanaume aliye kamilika anakuwa anakudanganya na kukupoteza.
Aminini nawaambia kuwa starehe ya usiku mmoja haiwezi kumfanya mwanamke akavumilia shida kwa miaka mi5. Ila hata kama humridhishi mpenzi wako na una pesa, ataenda kuzini nje ila jioni atarudi ndani kwa ajili ya pesa uliyonayo.
Sifa kuu ya wewe kuitwa mwanaume wa kweli ni uwezo wa kupata pesa basi, maana hawa wanawake wa leo bila pesa hata uwe na nguvu za kuvuta meli ni kazi bure. Kwanini hamjiulizi kuwa mbona siku hizi kuna ndoa za mababu na mabinti wadogo? Sasa wewe kijana shinda sana gym ukijenga mwili ili kumvutia mkeo mtarajiwa, halafu jibu utalipata baadae kuwa ni kipi kinamtuliza mwanamke kati ya pesa na mazoezi yako.
[HASHTAG]#Acheni[/HASHTAG] ujinga,tafuteni pesa#