Wakuu,
Habari za mchana,
Nadhani ni mara ya tatu hivi kupost katika jukwaa hili, lakini ni msomaji mzuri sana wa post humu, kiasi ambacho huwa ninatafuta thread ambayo sijaiipitia na kuambulia patupu nashukuru kwa elimu muafaka ninayopata hapa inanisaidia sana.
Leo nimediriki kusema jambo ambalo nimejifunza katika relationship pamoja na kusoma hapa na kwingineko. Haya ni mawazo yangu, wewe una yako pia, jambo ni kwamba wanawake walio wengi wanaweka pesa kuwa ni priority namba moja katika kumchagua mchumba.
Unakuta mwanamke anakutana na mpenzi mwenye upendo wa kweli kabisa bila kificho na yuko tayari kuwa naye kwa lolote na hata kusaidia anajitahidi kwa kadri ya uwezo wake, tena hata kujinyima mwenyewe, lakini kwasababu msaada anaotoa wa materials haumtoshi mdada anaamua kumtosa jamaa na kumtafuta mwenye kumtosheleza kipesa, badala ya kuchukuliana naye na kumthamini mwenzake kwa upendo alionao kwake, na kumtia moyo ili upendo uzidi kujengeka na kutengeneza maisha yenye uthabiti baadaye, mwanamke atamtafutia sababu ya kumwacha mwanamme ati kisa pesa.
Je hao wenye pesa si walikuwa hawana pesa mwanzo? Lakini wakazitafuta na zikapatikana,na je ulichangia chochote katika pesa za huyo unayemshobokea? Kwanini usikomae na jamaa kuanzia chini mpaka juu? Na je mshikaji aliyejijenga tayari kuliko mshikaji wako umempenda kwa sababu ya mali zake au yeye mwenyewe tu?
Je hiyo ndiyo maana halisi ya upendo? unachokitaka hasa ni ni kutoka kwa mwanaume? Je ni pesa au upendo wa dhati? Je mwanaume asiyekuwa na pesa hawezi kuwa na upendo wa dhati? Je huyo aliye na pesa siku mambo yakienda mrama utafanyaje? Maana pesa ni maua.Je mwanaume akikupa pesa tena nyingi ndio anakupenda sana? Hebu soma biblia yule mwanamke mjane aliyetoa dinari moja na kuwazidi wale matajiri waliotoa mamilioni kwa thawabu mbinguni. Kwasababu alitoa kwa moyo kile kidogo alicho nacho.
Mwisho migogoro inaanza kutokea kwenye ndoa, kwasababu umuhimu wa upendo wa dhati unadhihirika na inakuwa hakuna lingine zaidi ya kujuta, unasikia anatimizia mahitaji lakini ana nyumba ndogo, mara analala baa, mara upendo umepungua.
Nimalizie kwa kusema, upendo wa dhati ni muhimu kuliko pesa, kama umempata mpenzi lakini anakupenda kwa dhati, usimdharau kwa sababu mambo yake hayako sawa, mthamini kwa ule upendo wake wa dhati, ipo siku utaona thamani yake.jenga naye maisha, mtie moyo, shikamana naye na mungu atawabariki wote hakika.
Asanteni sana na samahani kwa urefu wa thread.