Utata wa dhehebu lako katika kufunga ndoa

Utata wa dhehebu lako katika kufunga ndoa

Leo ni mara ya kwanza kuingia kwenye hili jukwaa wadau, nategemea ushauri wa maana juu ya hili jambo.

Iko hivi kuna kijana wangu anaomba ushauri kuhusu tatizo linalomsumbua yeye ni mkristo wa dhehebu la KKKT na ana mchumba wake ni msabato, sasa mda unazidi kwenda kijana anataka kufunga ndoa.

Kijana akatoa wazo kwa binti kwamba ndoa inatakiwa ifungwe kanisani KKKT na baada ya ndoa binti ataendelea na dhehebu la kisabato.

Sasa binti amegoma kabisa, binti nae kasema hawezi kufunga ndoa KKKT anataka ndoa ifungwe kanisani sabato na baada ya ndoa kamruhusu kijana aendelee na dhehebu la KKKT.
Sasa ubishano upo kwenye wapi ndoa ifungwe kati ya Kanisani KKKT au sabato, na imefika hatua kwamba endapo mmoja atakataa kukubali mawazo ya mwenzie wanasema bora mahusiano yaishe.

Sasa wadau mnaushauri gani ili kuweza kuwanusuru huyu kijana pamoja na huyo mchumba wake.
Nimewashauri kuhusu ndoa ya kiserikali, ila wote hawako tayari kwa ndoa ya kufungwa serikalini.

Je mnamshauri nini huyu kijana na mchumba wake ili waweze kufanikisha mipango yao ya kufunga ndoa pamoja?
Tatizo ni kukumbatia imani zilizopandikizwa na wakoloni ili watutawale vyema na kwa ujinga wetu tumeshaamini na kule kwao hawanaga maupuuzi kama haya . Wao ndoa ni dakika 5 tu kwao na maisha yanaendelea
 
Hapo hakuna kitu ila ni mapokeo tu yanayo tusumbua.maana mkkkt alianzia uwaki nk.akafundishwa imani ya ukkkt.na msabato alianzia pass finder akaja assa na ss tucasa.

~Wasichelewe wafungie ndoa popote hati ya ndoa,yakanisa,udini hamufanyi mtu aingie mbinguni hakuna tiketi hapo.tiketi pekee ni kuokoka,utakatifu na dhabihu ya msalaba wa YESU tu
 
Unanitisha ndugu, una maana gani unaposema wasabato sio wakristo na wakati nao pia wanatumia biblia?
Kutumia biblia siyo sababu..

Mosi....Wasabato hawaamini Utatu Mtakatifu
Wasabato wanapinga ufufuko wa Yesu...Ref, kitabu cha Mama EGW nabii wao kinachoitwa Investigative Judgement....

Pili Wasabato wana biblia yao mpya inajulikana kama "the clear Word Bible"
 
Sijakuelewa ndugu una maana gani kusema tumtafutie atheists waliokomaa?,
Na kwa uelewa wangu najua atheists ni aina ya watu wasio amini uwepo wa Mungu
Hao watu wenu wana 'wehu' wa kiimani nadhani kwa sababu hawako exposed kwa fikra tofauti na walizomezeshwa na michungaji yao. Kwo watafutie atheists wawape changamoto mpya. In a long run watajifunza kukompromise mambo ya dini pia.
g
 
We mwambie amkubalie kwamba watafungia sabato, huku kwa siri akifanya mchakato ya KKKT, siku ya siku, demu yupo ndani ya shela, ambadilikie kwamba ndoa ni KKKT, hataki, basi, avue gwanda.
 
nkikumbuka walivyotaka kusafir bila visa hata passport sijashangaa sana
hahaaaa! wale ni dogmatists, na kawaida ya dogmatist ni kuongozwa na set za principles ambazo hawezi kwenda nje yazo. huamini kuwa yule asie enenda sawa na principle zao ni mkosefu/mdhambi/adui, tena yule ambaye ni extreme dogmatist aweza hata kujustfy kifo kwa mkosefu/mdhambi/adui..............
 
Labda niulize swali kwa mdau, sabato na kkkt wana muabudu nani??" Naomba majibu ili nitoe ushauri wangu, maana mimi naamini wakiristo wote wana muabudu Yesu, nakama sipo sahihi niweke sawa hapo.
 
Hapo hakuna kitu ila ni mapokeo tu yanayo tusumbua.maana mkkkt alianzia uwaki nk.akafundishwa imani ya ukkkt.na msabato alianzia pass finder akaja assa na ss tucasa.

~Wasichelewe wafungie ndoa popote hati ya ndoa,yakanisa,udini hamufanyi mtu aingie mbinguni hakuna tiketi hapo.tiketi pekee ni kuokoka,utakatifu na dhabihu ya msalaba wa YESU tu
Asante kwa ushauri, ila una maana gani unaposema KKKT ilianzia kwenye uwaki n.k na pia kwanini unasema usabato ulianzia katika pass finder na akaja assa?
 
Kutumia biblia siyo sababu..

Mosi....Wasabato hawaamini Utatu Mtakatifu
Wasabato wanapinga ufufuko wa Yesu...Ref, kitabu cha Mama EGW nabii wao kinachoitwa Investigative Judgement....

Pili Wasabato wana biblia yao mpya inajulikana kama "the clear Word Bible"
Asante kwa maelezo mazuri ndugu, sikuwa najua hizi habar kuhusu wasabato kwa kweli
 
Hao watu wenu wana 'wehu' wa kiimani nadhani kwa sababu hawako exposed kwa fikra tofauti na walizomezeshwa na michungaji yao. Kwo watafutie atheists wawape changamoto mpya. In a long run watajifunza kukompromise mambo ya dini pia.
g
Nimekuelewa ndugu, asante kwa ushauri
 
We mwambie amkubalie kwamba watafungia sabato, huku kwa siri akifanya mchakato ya KKKT, siku ya siku, demu yupo ndani ya shela, ambadilikie kwamba ndoa ni KKKT, hataki, basi, avue gwanda.
Asante kwa ushauri, ile we noma mdau yani unataka kijana abadilishie gia angani siku ya kuoa...!!!!
 
hahaaaa! wale ni dogmatists, na kawaida ya dogmatist ni kuongozwa na set za principles ambazo hawezi kwenda nje yazo. huamini kuwa yule asie enenda sawa na principle zao ni mkosefu/mdhambi/adui, tena yule ambaye ni extreme dogmatist aweza hata kujustfy kifo kwa mkosefu/mdhambi/adui..............
Hizi imani ni hatari sana yani
 
Ushauri wangu ni huu, waachane tu, hakuna sababu ya wao kuoana. WHY?
Dalili ya mvua ni mawingu, kama kila dalili inaonyesha misimamo yao ya kiimani inakinzana hata mahali pa kufungia ndoa, hiyo inatoa picha pana kuwa ndoa yao itakuwa pasua kichwa. Heri nusu shari kuliko shari kamili. Walipofikia inatosha, wasilazimishe mambo. WAACHANE tu.
 
Labda niulize swali kwa mdau, sabato na kkkt wana muabudu nani??" Naomba majibu ili nitoe ushauri wangu, maana mimi naamini wakiristo wote wana muabudu Yesu, nakama sipo sahihi niweke sawa hapo.
Mimi ninavyojua KKKT na wasabato wote wanaamini katika Yesu Kristo, ila kwa mujibu wa maelezo ya wadau wengi naona imani ya wasabato ni zaidi ya ukristo
 
Hayoyote Ni makampuni ya wazungu ,, laiti kama kungekuwa ni Dini ya mungu wangetekeleza amri ya mungu ktk swala zima la ndoa
 
Back
Top Bottom