Utata wa dhehebu lako katika kufunga ndoa

Utata wa dhehebu lako katika kufunga ndoa

Kwa kuwa wote ni waumini wa biblia takatifu nawaambia kabisa hapo hakuna uchumba wala nini. Wameongozwa na matamaa yao ya kimwili sasa wanajua wazi kuwa hakuna popote watapata suluhisho. Si mchungaji wa KKKT au Sabato ataifunga hiyo ndoa.
Kwa kuwa wote wanaiamini biblia takatifu wasome 2 Kor. 6 : 14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa.....
Kati yao ni nani anaamini sawa sawa na mwenzake?? Hakuna. Basi hawatafanikiwa bali wanapotezeana muda.
Wazo la kimwili; Kijana ajitahidi amtotoe huyo binti. Atalainika tu

Wasabato hawaamini Biblia bali sehemu ya Biblia, kwa kifupi hakuna ndoa hapo zaidi ya mateso ya baadae
 
Wasabato wanaamini wao ndio walioteuliwa na Mungu kwa ajili ya kuingia mbinguni

Wakristo wengine ni wakosaji au kafiri(mataifa) kama vile ni uzao wa shetani hivyo hawaruhusiwi kushirikiana nao katika masuala ya IMANI
Duuh, kama ni kweli basi hii ni hatari aisee
 
Leo ni mara ya kwanza kuingia kwenye hili jukwaa wadau, nategemea ushauri wa maana juu ya hili jambo.

Iko hivi kuna kijana wangu anaomba ushauri kuhusu tatizo linalomsumbua yeye ni mkristo wa dhehebu la KKKT na ana mchumba wake ni msabato, sasa mda unazidi kwenda kijana anataka kufunga ndoa.

Kijana akatoa wazo kwa binti kwamba ndoa inatakiwa ifungwe kanisani KKKT na baada ya ndoa binti ataendelea na dhehebu la kisabato.

Sasa binti amegoma kabisa, binti nae kasema hawezi kufunga ndoa KKKT anataka ndoa ifungwe kanisani sabato na baada ya ndoa kamruhusu kijana aendelee na dhehebu la KKKT.
Sasa ubishano upo kwenye wapi ndoa ifungwe kati ya Kanisani KKKT au sabato, na imefika hatua kwamba endapo mmoja atakataa kukubali mawazo ya mwenzie wanasema bora mahusiano yaishe.

Sasa wadau mnaushauri gani ili kuweza kuwanusuru huyu kijana pamoja na huyo mchumba wake.
Nimewashauri kuhusu ndoa ya kiserikali, ila wote hawako tayari kwa ndoa ya kufungwa serikalini.

Je mnamshauri nini huyu kijana na mchumba wake ili waweze kufanikisha mipango yao ya kufunga ndoa pamoja?
Huyo binti hajampenda tu kijana. Ukipendwa raha sana. Yaani hayoyote ni kitu kidogo sana. Kwani KKKT wanaabudu shetani???????. Mshauri binti aachane na ulimbukeni wa dini.
 
Kwa kawaida ndoa hufungwa kanisani kwa kijana wa kiume, ila katika hili km wasipokubalina ktk hili ni dalili sio tu wao watapata shida ila watawachanganya hata watoto wao, ikiwa MUNGU atawabarikia na uzao
 
Wasabato wanaamini wao ndio walioteuliwa na Mungu kwa ajili ya kuingia mbinguni

Wakristo wengine ni wakosaji au kafiri(mataifa) kama vile ni uzao wa shetani hivyo hawaruhusiwi kushirikiana nao katika masuala ya IMANI
Imani ya kuwa wewe ni bora kuliko wenzako ni ujinga uliopitiliza
 
Huyo binti hajampenda tu kijana. Ukipendwa raha sana. Yaani hayoyote ni kitu kidogo sana. Kwani KKKT wanaabudu shetani???????. Mshauri binti aachane na ulimbukeni wa dini.
Umemaliza...whats the problem kufungia ndoa kanisani kwa mwenzio wote mkiwa wakristo??
Dini zenyewe zmekuja na meli afu mtu ana complicate htr
 
Wasabato ni wasumbufu na ukipata mwanamke msabato lazma akomae uhamie sabato lasivyo huwez mpata.nikama wamelishwa imani kali sanaa.Yote katka yote mwambie jamaa achane nae atafute wa dhehebu lake kwani asipofanya hivyo ananunua ugomvi na mvurugano wa familia yao hasa watoto watakao zaliwa."wanawake wasabato=pasua kichwa"
 
Huyo binti hajampenda tu kijana. Ukipendwa raha sana. Yaani hayoyote ni kitu kidogo sana. Kwani KKKT wanaabudu shetani???????. Mshauri binti aachane na ulimbukeni wa dini.
Asante kwa ushauri
 
Kwa kawaida ndoa hufungwa kanisani kwa kijana wa kiume, ila katika hili km wasipokubalina ktk hili ni dalili sio tu wao watapata shida ila watawachanganya hata watoto wao, ikiwa MUNGU atawabarikia na uzao
Asante kwa ushauri
 
Umemaliza...whats the problem kufungia ndoa kanisani kwa mwenzio wote mkiwa wakristo??
Dini zenyewe zmekuja na meli afu mtu ana complicate htr
Kuna mijitu ya ajabu sana hapa duniani. Mwishowasiku mwanaume ata ghairi kuwowa.

Yaani dini ndo mshindwe kuwa pamoja. Binti apimwe akili kwa kweli
 
Back
Top Bottom