Utata wa dhehebu lako katika kufunga ndoa

Utata wa dhehebu lako katika kufunga ndoa

Kwa Sababu hatuelewani kwa hilo suala la wapi tufunge ndoa
Mosi: anaweza kuwa hataki tu kuolewa na Mimi so akatumia kigezo cha dini kukomalia ishindikane, n.a. ukiamua kukubali ni mwanzo wa kuonyesha udhaifu kwa Tabia za wadada wa kiafrica, ataendelea kukubadilikia kila uchwao.
Pili: Mimi huwa nikiona kitu kinakuwa na dalili za kushindikana, naairisha maana kama anakupenda kweli hawezi kukupinga au ww huwezi kumpinga
Tatu; tukikomaa tukafunge Kwa Dc baada ya ndoa mtasalije? Nani atamfuta nani au kila mtu kivyake, ibada za nyumbani je? Watoto wataenda wapi, mtaonekanaje kwa watoto
Kiujumla ni mwanzo wa mtafaruku, achilia mbali ratiba za ibada na maombi ya usiku sijui kwa walokole na blabla nyingine
Asante kwa uzoefu wako, na pia kwa ushauri wako
 
Leo ni mara ya kwanza kuingia kwenye hili jukwaa wadau, nategemea ushauri wa maana juu ya hili jambo.

Iko hivi kuna kijana wangu anaomba ushauri kuhusu tatizo linalomsumbua yeye ni mkristo wa dhehebu la KKKT na ana mchumba wake ni msabato, sasa mda unazidi kwenda kijana anataka kufunga ndoa.

Kijana akatoa wazo kwa binti kwamba ndoa inatakiwa ifungwe kanisani KKKT na baada ya ndoa binti ataendelea na dhehebu la kisabato.

Sasa binti amegoma kabisa, binti nae kasema hawezi kufunga ndoa KKKT anataka ndoa ifungwe kanisani sabato na baada ya ndoa kamruhusu kijana aendelee na dhehebu la KKKT.
Sasa ubishano upo kwenye wapi ndoa ifungwe kati ya Kanisani KKKT au sabato, na imefika hatua kwamba endapo mmoja atakataa kukubali mawazo ya mwenzie wanasema bora mahusiano yaishe.

Sasa wadau mnaushauri gani ili kuweza kuwanusuru huyu kijana pamoja na huyo mchumba wake.
Nimewashauri kuhusu ndoa ya kiserikali, ila wote hawako tayari kwa ndoa ya kufungwa serikalini.

Je mnamshauri nini huyu kijana na mchumba wake ili waweze kufanikisha mipango yao ya kufunga ndoa pamoja?

yani uzito wa ndoa uko kwenye kanisa gani ifungiwe na sio aina gani ya maisha wamejipanga kuishi, watafute vipi vipato, wana maono gani na mipango gani ya maendeleo. kama wako tayari kuacha mahusiano kisa kanisa, basi hamna ndoa apo.. na ata waki ingia kwenye ndoa watakua na maamuzi magumu yenye kukwaruzana kila siku.. la kwanza mtoto kazaliwa abatizwe wapi? huo ugomvi wanarudi kwa wazazi tena..

nimesahau kwanza wasabato hawanywi coca, jamaa mwendo wa maji tu mezani. sijui kwenye mgegedo, wana masharti yapi..

wanatakiwa waone ndoa ni kubwa zaidi ya kanisa lipi wafungie. they should be worried of other more important things.
 
Una maana gani kusema mioyo yao iko mbali sana?
Maana yangu ni kwamba, kila mmoja akishajua kuwa wao ni wakristo, wako chini ya uongozi wa YESU kristo, wanamwomba YESU kristo kwa shida zao, wataondoa tofauti ya madhehebu yao. Na kama kweli wanapendana, basi, watafunga ndoa ya kikristo. Sidhani taratibu za ndoa kwa madhehebu mengi ya kikristo zinatofautiana, kwa sababu tunatumia kitabu kimoja kutuongoza.
 
Kwa wasabato itabidi Jamaa abatizwe kwa wasabato ndo taratibu za ndoa ziendelee
 
Wataftieni atheists waliokomaa wachallenge imani zao kwanza. Akili zitawakaa sawa tu
Sijakuelewa ndugu una maana gani kusema tumtafutie atheists waliokomaa?,
Na kwa uelewa wangu najua atheists ni aina ya watu wasio amini uwepo wa Mungu
 
Duuu hii inafanana na mshikaji wangu in short kama vile umemuongelea yeye. Ana mahusiano ya muda mrefu na binti wa kisabato tena muimba kwaya halafu jamaa Mkkkt. Jamaa wakati wakutaka kuvuta jumla ikawa noma akaamua kumjaza mimba ili walegeze msimamo lkn wapi. Hadi sasa wanavutana sijui ni mpaka lini.
Hii nimeona seheemu
 
Huyo mwanamke amfate mumewe akafungie kkkt then arudi kwenye dhehebu lake
 
yani uzito wa ndoa uko kwenye kanisa gani ifungiwe na sio aina gani ya maisha wamejipanga kuishi, watafute vipi vipato, wana maono gani na mipango gani ya maendeleo. kama wako tayari kuacha mahusiano kisa kanisa, basi hamna ndoa apo.. na ata waki ingia kwenye ndoa watakua na maamuzi magumu yenye kukwaruzana kila siku.. la kwanza mtoto kazaliwa abatizwe wapi? huo ugomvi wanarudi kwa wazazi tena..

nimesahau kwanza wasabato hawanywi coca, jamaa mwendo wa maji tu mezani. sijui kwenye mgegedo, wana masharti yapi..

wanatakiwa waone ndoa ni kubwa zaidi ya kanisa lipi wafungie. they should be worried of other more important things.
Asante kwa ushauri ndugu, ila umeniacha hoi ulipo sema wasabato hawanyi coca
 
Maana yangu ni kwamba, kila mmoja akishajua kuwa wao ni wakristo, wako chini ya uongozi wa YESU kristo, wanamwomba YESU kristo kwa shida zao, wataondoa tofauti ya madhehebu yao. Na kama kweli wanapendana, basi, watafunga ndoa ya kikristo. Sidhani taratibu za ndoa kwa madhehebu mengi ya kikristo zinatofautiana, kwa sababu tunatumia kitabu kimoja kutuongoza.
Nimekuelewa ndugu
 
Back
Top Bottom