mitindo huru
JF-Expert Member
- Apr 26, 2016
- 1,610
- 1,601
- Thread starter
- #161
Nimekuelewa vizuri sana ndugu na asante sana kwa maelezo mazuri.Mkuu ngoja nikupe ufafanuzi mzuri hapa, halafu utaelewa vizuri Concept kati ya Ndoa na Imani.
1/Ndoa ni taasisi ya Kiimani kwa 100%. Huwezi kuitenganisha ndoa na imani yako. Mitazamo yote ya ndoa iliyopo leo duniani imetafsiriwa kutoka kwenye maandiko ya kiimani. Kuanzia kwenye Uhindi, Ukristo, Uislamu nk.
2/Ndoa ni mapatano baina ya watu wawili tu, na patano hilo linaweza kuhalalishwa kisheria, kiimani au Kijamii. Sasa vijana waliochumbiana wenyewe, waamue wao wenyewe kwanza wanataka kuhalalisha(kuubariki) uhusiano wao wa kindoa katika misingi ipi ya kiimani. Kama wameshindwa kuafikiana katika hilo sasa, usitegemee kama wataweza kuishi kwenye ndoa kwenye uhalalisho huo. Ni vyema wakajiuliza kama kuna ulazima wa wao kuishi pamoja(kuoana)
3/Imani yako ni zaidi ya ndoa yako, hivyo hupaswi kuilazimisha Imani yako iifuate ndoa yako maana haiwezekani, ila unaweza kuilazimisha ndoa yako ifuate imani yako maana inawezekana.
Kuna kitu nimeongeza kutoka kwenye maelezo yako
tena bora wote wa mwelekeo mmoja majumba tofauti tuu