Utata wa dhehebu lako katika kufunga ndoa

Utata wa dhehebu lako katika kufunga ndoa

Duuu hii inafanana na mshikaji wangu in short kama vile umemuongelea yeye. Ana mahusiano ya muda mrefu na binti wa kisabato tena muimba kwaya halafu jamaa Mkkkt. Jamaa wakati wakutaka kuvuta jumla ikawa noma akaamua kumjaza mimba ili walegeze msimamo lkn wapi. Hadi sasa wanavutana sijui ni mpaka lini.
Dah!
Hiyo kali sana.
Yaani binti yuko tayari kufanya uzinzi ndani ya mwamvuli wa dini yake, lakini hataki kufunga ndoa nje ya mwamvuli wa dini yake.

Yaani binti anatuambia kuwa, yuko tayari kwa uzinzi lakini hayuko tayari kwa ndoa.
Sasa mwanaume unataka kuoa huyo mwanamke ili iweje? Wa nini hasa? Una wazimu?
 
Yani hii ishu ya wasabato na madhehebu mengine kuoana ni changamoto sana.
Swali langu pia kwanini wakitaka kuoana kati ya RC, KKKT, TAG, EAGT au Pentekoste huwa hakuna shida.
Shida ni kwa wasabato tu?
Wala usishangae, issue ni mapokeo ya kiiimani baina ya dhehebu moja na lingine. Kama kuna 'gap' kubwa la kiimani ni ngumu sana 'ku-comprimise' baadhi ya mambo.

Binafsi siwashangai wasabato katika hilo, maana wanajua nini maana ya ndoa.
Kiasili ndoa ni taasisi ya Kiimani kwa 100%, hivyo kama imani za wahusika(wachumba) zinakinzana sana ni vyema ndoa hiyo isifungwe kabisa, maana ukilazimisha haya yatakuja kutokea...
1/Ndoa itakuwa kaburi la kuzika imani ya mmoja wapo kama sio wote.
2/Ugomvi usiokuwa na sababu utazuka kila mara na kuusuruhisha huo mgomvi.
3/Familia itapoteza dira ya kiimani.
 
Dah!
Hiyo kali sana.
Yaani binti yuko tayari kufanya uzinzi ndani ya mwamvuli wa dini yake, lakini hataki kufunga ndoa nje ya mwamvuli wa dini yake.

Yaani binti anatuambia kuwa, yuko tayari kwa uzinzi lakini hayuko tayari kwa ndoa.
Sasa mwanaume unataka kuoa huyo mwanamke ili iweje? Wa nini hasa? Una wazimu?
Kuna vitu vingine ni vya kushangaza na hizi imani zetu yani, sasa ukifikiria vizuri hapo ni kama kituko fulani
 
Maana yangu ni kwamba, kila mmoja akishajua kuwa wao ni wakristo, wako chini ya uongozi wa YESU kristo, wanamwomba YESU kristo kwa shida zao, wataondoa tofauti ya madhehebu yao. Na kama kweli wanapendana, basi, watafunga ndoa ya kikristo. Sidhani taratibu za ndoa kwa madhehebu mengi ya kikristo zinatofautiana, kwa sababu tunatumia kitabu kimoja kutuongoza.
Mkuu kuifunga hiyo ndoa sio kitu kirahisi hivyo kwa wasabato.
Kisabato ndoa...
1/Ni kati ya msabato na msabato tu.
2/Lazima ifungwe kisabato tu.

Hapo hakuna mjadala.
Kama mwanaume akikubali ifungwe kisabato, maana yake atapaswa aachane kwanza na KKKT, abatizwe kisabato na kupitia mafunzo maalum ya kisabato. Baada ya hapo ndio ndoa ifungwe. Sio jambo la 1+1=2, ni mchakato mrefu na unaochukua muda. Nadhani ni zaidi ya miezi sita hivi.

Kwenye Usabato hakunaga shortcut katika suala la kuoa na kuolewa.
 
Kuna vitu vingine ni vya kushangaza na hizi imani zetu yani, sasa ukifikiria vizuri hapo ni kama kituko fulani
Mkuu wala sio vitu vya kushangaza ila ni kwa sababu watu watuzijui vyema imani zetu tunazoziamini, hivyo tunashangaa sana ikifika wakati zikigeuka kuwa kikwazo katika uhuru wa maamuzi yetu. Na imani zote zina hizo 'obstacles' katika uhuru wa mtu binafsi. To believe is to pay to price. No price no faith.
 
Mambo mengine kuumiza vichwa bila sababu kwani tangu mwanzo mnapoanza ukiona mambo hayaendi si unaacha unaendelea na safari? Kuna dada mmoja alipata msabato yeye ni RC na dingi ni mkali balaa ikabidi wafunge huko Roman Catholic baada ya kwenda kwao mbona walifunga upya kabisa kama ndiyo wanachumbiana ni her ya nusu shari
 
Wasabato wasumbufu sana atamsumbua mpaka kwenye watoto yan akimbie mbioo ndefu tena Ashukuru Mungu saiv mapema keshaona dalili
 
Wasabato tuwaache waolewe na wasabato wenzao. Ndio imani yao inavyo sisitiza siku zote. Na kamwe hawawezi kurahisisha hilo kisa tu kuwaridhisha hao wachumba wa madhehebu mawili tofauti. Na katika hili tusiwahukumu wasabato kwa msimamo wao bali tuwapongeze maana wamekubali kusimamia kile kile wanachokiamini.

Na katika maisha ya ndoa, kufunga ndoa(harusi) ni jambo moja dogo sana, issue ni kuweza kuishi na msabato kama wewe sio muumini wa kisabato. Ama wewe ni msabato uende kuishi na mtu ambaye sio msabato. Embu waza haya..
-Siku ya kuabudu.
-Vyakula.
-Vinywaji.
-Mavazi. Nk
 
Ila izi imani na dini inatakiwa watu wawe na mipaka nazo kwakweli mana namna hii dhehebu linapokuwa ni kikwazo cha kukosa mwenza, hatari sana
 
Aisee hiyo mpya tena, kufunga ndoa mara mbili tena?
 
Asante kwa ushauri mzuri ndugu
 
Kwa kukushauri tu, mwambie atafute mtu wa KKKT au dhehebu lolote la Kikristo, Ndoa na Msabato ni pasua kichwa, Msabato hachangamani na Mkristo yoyote, nimeshuhudia mateso makubwa ya ndoa a Msabato na Mkristo (Catholic, KKKT, Mlokole) Kuoa ni mara moja tu na ukikosea ni kila kitu
MADE IN TARIME, RORYA , MAJITA and UPARENI
 
Wasabato wasumbufu sana atamsumbua mpaka kwenye watoto yan akimbie mbioo ndefu tena Ashukuru Mungu saiv mapema keshaona dalili
Na wasumbufu kweli ni afadhali akaacha mapema kuliko akaingia hivyo atajutia
 
Ila izi imani na dini inatakiwa watu wawe na mipaka nazo kwakweli mana namna hii dhehebu linapokuwa ni kikwazo cha kukosa mwenza, hatari sana
Mkuu ngoja nikupe ufafanuzi mzuri hapa, halafu utaelewa vizuri Concept kati ya Ndoa na Imani.

1/Ndoa ni taasisi ya Kiimani kwa 100%. Huwezi kuitenganisha ndoa na imani yako. Mitazamo yote ya ndoa iliyopo leo duniani imetafsiriwa kutoka kwenye maandiko ya kiimani. Kuanzia kwenye Uhindi, Ukristo, Uislamu nk.

2/Ndoa ni mapatano baina ya watu wawili tu, na patano hilo linaweza kuhalalishwa kisheria, kiimani au Kijamii. Sasa vijana waliochumbiana wenyewe, waamue wao wenyewe kwanza wanataka kuhalalisha(kuubariki) uhusiano wao wa kindoa katika misingi ipi ya kiimani. Kama wameshindwa kuafikiana katika hilo sasa, usitegemee kama wataweza kuishi kwenye ndoa kwenye uhalalisho huo. Ni vyema wakajiuliza kama kuna ulazima wa wao kuishi pamoja(kuoana)

3/Imani yako ni zaidi ya ndoa yako, hivyo hupaswi kuilazimisha Imani yako iifuate ndoa yako maana haiwezekani, ila unaweza kuilazimisha ndoa yako ifuate imani yako maana inawezekana.
 
Ndoa ni jambo la kimila, hakuna verse yoyote kwenye Biblia Takatifu inayotoa muongozo kwamba ndoa ni LAZIMA ifungwe kanisani, hizo ni taratibu za Kanisa na taratibu za Kanisa sio LAZIMA ziwe taratibu za Mungu. Mkishindwa kuungana kimila huko kanisani mnapoteza muda tu.
 
The Spirit of Prophecy consistently counsels against marriage between “the believer and the unbeliever” and further cautions against uniting with fellow Christians who have “not accepted the truth for this time.”—5T 364. Marriages are more likely to endure, and family life to fulfill the divine plan, if husband and wife are united and are bound together by common spiritual values and lifestyles. For these reasons the Church strongly discourages marriage between a Seventh-day Adventist and a member of another religion and strongly urges its pastors not to perform such marriages.

The Church recognizes that it is the prerogative of each individual member to make the final decision relative to the choice of a marriage partner. However, it is the hope of the Church that if the member chooses a partner who is not a member of the Church, the couple will realize and appreciate that the Seventh-day Adventist pastor, who has covenanted to uphold the principles outlined above, should not be expected to perform the marriage.

Hii ni sehemu ya maelezo ya kanuni ya kanisa la Waadventista Wasabato. Hapo hakuna ndoa itakayofungwa kwa kifupi tu
 
Back
Top Bottom