Utapeli kwenye uchawi na hatua za kuchukua

Utapeli kwenye uchawi na hatua za kuchukua

Nikiwa Alevel niliagizwa bank kulipia maji. Wakati natoka kuna dada akanidaka na kuanza kuniongelesha huku akiulizia sehemu niliyokuwa naifahamu. Nikamjibu napafahamu, akaniomba nimsindikize ili ampeleke kuna kaka alikuwa nae.

Nikawa nawasindikiza huku njiani tunazungumza. Yule kaka akaanza kujieleza kuwa ni mganga anatokea Tanga na mamno kibao. Mara yule kaka akaanza kuniuliza naishi wapi na najishughulisha na nini. Nikamwambia mie nipo nipo tu sina shughuli ya maana ni house girl kwa dada yangu.

Akaniomba kiganja aone anisomee nyota. Mara akaanza kuniambia nimelogwa na dada yangu kwa kunichimbia hirizi mlangoni ili nisiweze kuendelea na niendelee kuwa house girl wake. Nikajichekea kimoyomoyo maana dada yangu ndiye aliyekuwa ananisomesha🤣🤣

Mara akaniambia nimpe hela aniombee dua ili aondoe nguvu ya hiyo hirizi. Nikamwambia mie sina hata mia, akauliza mbona nimetoka benki? Ndio akili ikanijia hawa waliponiaona natoka benki walijua nina kibunda wanitapeli, kumbe nilikuwa na jero tu ya nauli🤣
 
Kuna siku nlikuwa Tanga, natembea mtaani nakuta watu wanakimbizana barabarani, kuna Jamaa kavaa kitambaa chekundu kichwani anakimbia vibaya mno yaani anaruka Tu mitaro mara anaruka katikati kwenye vijiwe vya watu yaani anakimbia Tu hovyo hovyo ikabidi sasa niulize, nikaambiwa Jamaa ameona jini au mnyama (kitu kama hicho kama sijasahau), ndo anakikimbiza hicho kitu na watu kibao wanamfuata nyuma Yake...Nikashangaa Sana.
Malizia basi, jini alikamatwa?
 
I bet ilikuwa CRDB Makumbusho😀
 
Uchawi haupo
Cc Nyani Ngabu
Utapeli unaohusisnyaniuchawi na uganga nchini Tanzania umekuwa ukichukua sura mpya, ambapo matapeli hutumia hofu, imani za kishirikina, na teknolojia kuwaibia wananchi. Kufikia Machi 2026, Jeshi la Polisi na mamlaka mbalimbali zimeongeza jitihada za kudhibiti vitendo hivi ambavyo mara nyingi huleta chuki na uvunjifu wa amani katika jamii.

Mbinu za Kawaida za Utapeli wa Kishirikina
Ramli Chonganishi na "Kamchape": Hii ni mbinu ambapo waganga feki hudai kutambua wachawi au vifaa vya uchawi kwenye makazi ya watu. Mara nyingi hulazimisha watu kutoa mifugo (kama ng'ombe) au fedha ili "kusafisha" nyumba, jambo ambalo limepigwa marufuku kisheria.

Utapeli wa Mitandao ya Simu:

Matapeli hujifanya waganga maarufu na kutuma ujumbe mfupi (SMS) au kupiga simu wakidai kumuona mhusika ana matatizo ya nyota, mikosi, au amelogwa. Huwataka wahanga kutuma fedha za "dawa" au "kafara" kupitia mitandao ya simu.
Chuma Ulete na Utajiri wa Haraka:

Matapeli huwahadaa wafanyabiashara kuwa fedha zao zinachukuliwa kishirikina (Chuma Ulete) na kuahidi kuwapa dawa za kuongeza mauzo au utajiri wa miujiza, hali inayopelekea watu kupoteza akiba zao kubwa

Kutumia Hofu ya Vifo au Maradhi:
Baadhi ya matapeli huwashawishi watu kuwa vifo au magonjwa kwenye familia yamesababishwa na ndugu wa karibu (kama wajane au vikongwe) ili wapate nafasi ya kutoza ada kubwa za "kinga".

Hatua za Kuchukua na Sheria

Ripoti Utapeli: Ikiwa umepokea ujumbe au simu ya kitapeli, unaweza kuripoti kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuandika neno UTAPELI na kutuma kwenda namba 15040.

Sheria ya Uchawi (Witchcraft Act):

Sheria nchini inakataza vitendo vya kishirikina vinavyosababisha hofu, madhara, au vifo. Jeshi la Polisi (kwa mfano mkoani Mwanza na Rukwa) limekuwa likiwakamata wanaojihusisha na "Kamchape" au mauaji yanayohusiana na imani hizi.

Waganga Waliosajiliwa:
Serikali inatambua waganga wa tiba asili waliosajiliwa tu. Ni muhimu kuepuka waganga wanaopiga ramli chonganishi ambazo ni kinyume na taratibu za Baraza la Tiba Asili.
 
Kuna siku nlikuwa Tanga, natembea mtaani nakuta watu wanakimbizana barabarani, kuna Jamaa kavaa kitambaa chekundu kichwani anakimbia vibaya mno yaani anaruka Tu mitaro mara anaruka katikati kwenye vijiwe vya watu yaani anakimbia Tu hovyo hovyo ikabidi sasa niulize, nikaambiwa Jamaa ameona jini au mnyama (kitu kama hicho kama sijasahau), ndo anakikimbiza hicho kitu na watu kibao wanamfuata nyuma Yake...Nikashangaa Sana.
Jini likimbizwe kwa miguu?😂 na binadamu!?🤣
 
Back
Top Bottom