Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,719
Hii ni moja ya mbinu zinazotumiwa na matapeli mtandaoni. Mara nyingi hujitangaza kwenye mitandao ya kijamii wakionesha bidhaa, kisha huomba utume malipo kabla ya kukupatia bidhaa. Baada ya kupokea fedha, hupotea au kuacha kujibu simu na ujumbe.
Soma > Kuweni Makini na Dar Expart Sales na utapeli wa Pesa Mtandaoni
- Je, unawezaje kujilinda?
Hakiki utambulisho wa muuzaji kabla ya kutuma fedha.
Soma maoni na uzoefu wa wanunuzi wengine.
Epuka kutuma malipo kamili kabla ya kuthibitisha uhalali wa biashara.
Tumia njia salama za malipo na uhifadhi kumbukumbu za miamala.
Soma > Kuweni Makini na Dar Expart Sales na utapeli wa Pesa Mtandaoni