Utapeli kwenye uchawi na hatua za kuchukua

Utapeli kwenye uchawi na hatua za kuchukua

Maluweluwe ya Macho (Optical Illusions) ni hali ambapo unachokiona ni tofauti na uhalisia.
Hii hutokea wakati ubongo wako unapotafsiri vibaya taarifa unazopokea kutoka kwenye macho.
Hizi ni "mbinu" ambazo mara nyingi hutokana na ubongo kujaribu kuelezea uhalisia kulingana na vitu au mifumo unayoijua, au hitaji lake la kujaza taarifa zinazokosekana.

Aina za Kawaida za Maluweluwe ya Macho

Maluweluwe ya Kiuhalisia (Literal Illusions):
Haya hutengenezwa kwa kuunganisha picha nyingi ndogo ili kuunda picha moja kubwa ambayo inaonekana tofauti na vitu vilivyoiunda.

Maluweluwe ya Kifiziolojia (Physiological Illusions):
Haya hutokea wakati mfumo wa uoni wa ubongo unachochewa kupita kiasi na mwanga, mwendo, au rangi, na kuufanya uone vitu kama vile picha zinazobaki machoni baada ya kuangalia kitu (afterimages) au mwendo kwenye picha ambayo haisogei.

Maluweluwe ya Kitambuzi (Cognitive Illusions):
Haya yanategemea kile ambacho akili yako isiyo na fahamu (subconscious mind) inafikiria na jinsi inavyohusianisha vitu kulingana na uzoefu wako wa awali kuhusu ulimwengu.

Optic illusions (mauzauza) | Page 27 | JamiiForums Optic illusions (mauzauza)
Safi sana
 
Ukitaka kupata mganga hodari na wa kweli anzia mkoani kigoma,burundi, DRC,Congo Republic,Central Africa Rebublic, huko ndiko kuna waganga wa ndagu za mali, ukitaka kulogwa nenda tabora,mwanza,simiyu geita,sumbawanga,mpanda nk.
Kuna sehemu hivi inaitwa lamadi uyo mganga anaupiga mwingi adi unamwagika

Nilipelekwa na jamaa yangu yule mzee alinionesha kwenye kioo ma ex zangu wote mpaka leo uwa siamin nahc nimawenge tu
 
Lakini hatuoni wakikimbizwa sehemu wanazokaa matajiri, sehemu zenye maisha duni ndio utakuta wataalamu wanakusanya watu na kukimbiza majini.
imani ya kuwepo kwa uchawi na mapepo haiwahusu masikini tu. Ingawa mara nyingi matukio haya huzungumziwa zaidi katika mazingira ya kimasikini, dhana hizi zipo katika matabaka yote ya jamii kutokana na sababu zifuatazo:
  • Tofauti ya malengo: Wakati masikini wanaweza kuhusisha uchawi na matatizo ya afya au ukosefu wa riziki, matajiri au watu wenye vyeo mara nyingi huhusishwa na kutafuta nguvu za giza kwa ajili ya kulinda utajiri, kupata madaraka, au kuwashinda wapinzani wao

  • Aina ya huduma: Watu wenye uwezo wa kifedha mara nyingi hutafuta huduma hizi kwa siri zaidi ("high-end" services) kulinganisha na masikini ambao matukio yao huonekana wazi katika mazingira ya umma au nyumba za ibada.
 
Kuna siku tapeli la uganga wa kienyeji lilikuja shuleni na msafara mkubwa wa wanakijiji eti kuja kutoa majini na vifaa vya kichawi vilivyowekwa shuleni. Mkuu wa shule hakuwepo wakaingia ofisini, ghafla wakatoka mbio wakidaia wanakimbiza majini. Awali tuliwagomea wasifanye utapeli wao shuleni ila wanakijiji wakakomalia wakisema ni lazima shule yao isafishwe. Mara wakadai jini moja limekimbia mbali wasikoweza kufika, wakakimbia kuelekea nyumba za walimu, wakarudi mbio kurudi shuleni wakikimbiza jini, wakarirukia kama kumbikumbi na kulikamata chini ya mti wakifukua ardhi wakaibua pembe ya ng'ombe iliyofunikwa kitambaa chekundu na kudai ni jini. Tusioamini hayo mambo tulionekana kwa wanakijiji kuwa tunazuia shule isitolewe vitu vya kichawi. Tuliona kama wanamchafua mkuu wa shule kuwa ni mshirikina na ameweka ushirikina wake shuleni wakidai shule haifaulishi kwa sababu kuna ushirikina. Ilibaki kidogo tumjulishe mkurugenzi wa wilaya achukue hatua kwa kuwajulisha polisi kuwa shule imevamiwa na mganga tapeli
 
Kuna wale wanaotuma meseji kuwa wanaunganisha vijana na ufrimasoni wakati freemason wa ukweli wanasema wao hawatafuti wanachama wao kwa njia hizo. Unaambiwa utume elfu hamsini uungwe chapchapu bila kutoa kafara. Mara wabandike matangazo yao kwenye mistimu wakidai wanaunganisha watu kwenye chama kubwa, freemason iwatajirishe wapate fedha nyingi na kumiliki mali kama majumba na magari ya kifahari.
 
Umaskini, elimu na kukosa maarifa huku wengi wakitaka shortcut
 
Kuna siku tapeli la uganga wa kienyeji lilikuja shuleni na msafara mkubwa wa wanakijiji eti kuja kutoa majini na vifaa vya kichawi vilivyowekwa shuleni. Mkuu wa shule hakuwepo wakaingia ofisini, ghafla wakatoka mbio wakidaia wanakimbiza majini. Awali tuliwagomea wasifanye utapeli wao shuleni ila wanakijiji wakakomalia wakisema ni lazima shule yao isafishwe. Mara wakadai jini moja limekimbia mbali wasikoweza kufika, wakakimbia kuelekea nyumba za walimu, wakarudi mbio kurudi shuleni wakikimbiza jini, wakarirukia kama kumbikumbi na kulikamata chini ya mti wakifukua ardhi wakaibua pembe ya ng'ombe iliyofunikwa kitambaa chekundu na kudai ni jini. Tusioamini hayo mambo tulionekana kwa wanakijiji kuwa tunazuia shule isitolewe vitu vya kichawi. Tuliona kama wanamchafua mkuu wa shule kuwa ni mshirikina na ameweka ushirikina wake shuleni wakidai shule haifaulishi kwa sababu kuna ushirikina. Ilibaki kidogo tumjulishe mkurugenzi wa wilaya achukue hatua kwa kuwajulisha polisi kuwa shule imevamiwa na mganga tapeli
Tusioamini hayo mambo tulionekana kwa wanakijiji kuwa tunazuia shule isitolewe vitu vya kichawi.😂
 
Waganga nuksi. Miaka ya nyuma sana, kabla utandawazi haujangia, nikiwa bado mdogo nilikwenda kumsalimia mjomba wangu. Alikuwa na mgonjwa na akaamua kumpeleka kwa mganga wa kienyeji. Mganga alianza kwa kupiga ramli, ili kujua kinachomsibu mgonjwa. Mbele yake kulikuwa na kibuyu kidogo, kina shanga nyingi, hirizi na manyoya na juu amepachika kijiti ambacho kimeingia ndani ya kibuyu. Mjomba akaambiwa akae mbele. Kibuyu kikaanza kuzungumza kwa sauti ndogo kama mtoto ''logwa, logwa, ndugu, ndugu, Tini, Tini''. Mganga akatoa tafsiri kuwa kimesema amelogwa na ndugu yake anaitwa Martin. Kibuyu kuweza kuzungumza ilikuwa ni ajabu kweli kweli. Fast foward baada ya kukua na kupata akili nikahisi mganga aliweka spika ndogo ndani ya kibuyu halafu aka-connect kwa waya chini kwa chini na kulikuwa na mtu mwengine chumba kingine alikuwa anazungumza,
Na inawezekana hawa waganga wakawa wanawasiliana maana unaweza ukaenda kupiga ramli kwa waganga tofauti ila unakuta unaambiwa tatizo lile lile.
 
Back
Top Bottom