Utamaduni wetu - are we sure ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utamaduni wetu - are we sure ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mag3, Dec 16, 2008.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Baba yangu alinitembelea hapa Dar es Salaam kwenye miaka ya 90. Alifika kipindi ambapo kulikuwepo na mashindano ya kumtafuta 'Miss Tanzania'. Bahati mbaya ni wakati huo kulitokea malumbano kuhusu mavazi ya vimwana hawa wakiwa jukwaani kwamba hayaendani na mila zetu !! Kwa kuwa shindano lilikuwa likionyeshwa 'live' kwenye TV kwa aibu niliamua kubadilisha 'channel' nikihofia baba kuchukizwa na vimwana walivyovaa. Lo, nilishangaa babu aliponikataza nisifanye hivyo na nikagundua anafuatilia kwa makini sana kilichokua kinaendelea.

  Baada ya onyesho kwisha nilitaka sana kujua kwa nini mzee wangu aliyekua na umri karibu miaka 100 afuatilie jambo kama hilo. Akasema, " Mwanangu hilo onyesho limenikumbusha mengi wakati wa ujana wangu kabla ya kuja hawa wazungu. Nashukuru kuwa sasa mnaamka na kuanza kuzienzi mila zetu na desturi ambazo wao waliziita za kishenzi " Nilipomweleza kuwa hayo anayoyaona yanapigwa vita kuwa si utamaduni wetu na tunaiga tu, alihamaki na kunitaka nimpeleke kwa huyo mhuni anayesema hivyo. Alisisitiza kuwa ni hao wazungu ndio walikuwa wanaiga utamaduni wetu.

  Ingefaa tuwe tunafikiria mara mbili kabla ya kukurupuka kuponda tamaduni zetu wenyewe na kuziita za kigeni. Huu ni mfano moja tu na naomba wenye mifano mingine kama hii watuhabarishe.
   
 2. m

  mnyama Member

  #2
  Dec 17, 2008
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hili swala la mila na utamaduni wetu huwa lina nipa mashaka sana. Unapoongelea utamaduni na mila za watanzania hasa unaongelea nini? Tanzania ina zaidi ya makabila 100 ambayo kila moja lina mila na utamaduni wake. Sasa utamaduni na mila za watanzania ni zipi? na zimekuwa documented wapi? tunapongelea utamaduni tunamaanisha mwenendo mzima wa maisha kuanzaia vyakula, mavazi, ujenzi wa nyumba, namna ya kufanya na kusherekea vitu mbali mbali kama harusi, jando, misiba etc.

  Kwa swala la mavazi, sote tunajua kuwa jamii zetu nyingi kabla ya kuja haya mavazi ya kisasa walivaa ngozi au mavazi yaliyotengenezwa kwa nyazi na magome ya miti. Mavazi haya yalifunika sehemu za siri tu huku yakiacha mwili mzima wazi.

  Katika kabila letu la wakurya wasichana wanapofanyiwa tohara, walikuwa wakizunguka uchi kijiji kizima huku ngoma zikipigwa. Leo tunaambiwa kuvaa bikini siyo utamaduni wetu, Kuvaa nguo fupi siyo utamaduni wetu, hii mimi naona haijakaa sawa.

  Wizara inayohusika na mambo ya utamaduni ni vyema ikatoa mwongozo sahihi ya utamaduni wa mtanzania katika nyanja mbali mbali kama nilivyozitaja hapo juu.

  Kwa sasa kusema kweli tumepotea na tumechanganyikiwa. Baadhi ya tamaduni za kiarabu ndo zinageuzwa kuwa utamaduni wa watanzania, mfano wanawake kuvaa nguo zinazofunika sehemu kubwa ya miili yao etc.
   
Loading...