Mpango kabambe; Taifa litambe

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
MPANGO KABAMBE; TAIFA LITAMBE!

Anaandika, Robert Heriel
Mastermind

Ilisemwa taifa ili liendelee linahitaji mambo makuu manne,
i) Watu
ii) Ardhi
iii) Siasa Safi
iv) Uongozi Bora.
Hayo yalikuwa mawazo ya Mwl. Nyerere. Watu wapo, Ardhi Ipo, sina uhakika kwenye Siasa Safi na Uongozi Bora.

Taifa lolote ili liendelee ni lazima liwe na Sera, sheria, mipango na mikakati mizuri ya Kutumia Rasilimali zake vizuri kwaajili ya Maendeleo ya wananchi waliopo na kizazi kinachokuja.

Katika mipango na malengo ni sharti iwepo mipango ya muda mfupi, mipango ya muda wa Kati, na mipango ya muda mrefu. Mipango ya muda mfupi muda wake ni miaka 5-10, mpango WA muda wa Kati ni miaka 15- 50, Wakati mipango ya muda mrefu ni miaka 50 - 100 ambapo inahusisha Zama au kizazi kimoja mpaka vinne.
Mipango na malengo ndio huunda Sera na sheria za nchi.

Huwezi kuunda Sera na Baadhi ya sheria kama hujaweka mipango na malengo ya kitaifa Kwa muda Fulani.
Taifa lisilo na mipango na malengo ni kama taifa la Ngedere, hurukiarukia mambo kama ngedere arukiavyo matawi ya miti.

Mipango ya muda mrefu ambayo itaunda Sera na Ilani za muda mrefu hizo ni sharti zifuatwe na kila Kiongozi atakayeingia madarakani bila kujali mtazamo na Maoni yake. Ni vizuri Kiongozi Kabla hajaingia madarakani afanyiwe vetting ya kutosha ili kuona kama ata-fit nafasi hiyo au Laa.
Mipango ya muda mfupi ianishwe na iwe na mahusiano ya moja Kwa moja na mipango ya muda mrefu.

Taifa katika Kutumia Rasilimali zake lazima liweke Rasilimali hizo katika makundi anuai. Hiyo pia itatumika Kwa Rasilimali Watu, serikali lazima iwatenga Watu katika makundi yake Sahihi ili kuweza kuwatumia katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa. Sio kila MTU anaweza kuwa Rais au mwanasiasa kama ilivyo katika majukumu mengine.

Matumizi ya Rasilimali Watu pamoja na Rasilimali Ardhi yataaamua taifa letu liwe taifa la namna gani. Taifa ili liendelee lazima liwekeze katika Raia wake, kuwekeza Kifikra, kimwili, kihisia na Kiroho lakini pia kuwekeza kwenye Ardhi. Utumiaji na utunzaji wa Ardhi pamoja na mazingira lazima iwe sehemu ya mipango katika kuiendeleza nchi.

Rasilimali Watu imegawanyika katika kategoria kadhaa kama ifuatavyo;
1. Jinsia na jinsi
2. Umri

Watu hawa ili waishi wataongozwa na mambo makuu mawili,
1. Elimu
2. Imani (Dini), Mila, desturi na tamaduni

Elimu itahusu mambo ya Akili katika Kutumia, kutunza, kudhibiti, kuepuka athari Mbaya za matumizi ya Rasilimali. Wakati Imani, Mila, desturi, na tamaduni itahusu zaidi Maadili, mahusiano ya MTU na mtu au MTU na mazingira yake.

Hii ni kusema, Taifa kama taifa katika kulifanya LITAMBE lazima lihakikishe linaweka iwe moja Kwa moja au Kwa kificho mizizi yake katika suala la Elimu na Imani za Watu ili kuliendeleza taifa Hilo. Imani, Mila na desturi pamoja na tamaduni ndio hujenga Uzalendo katika Nchi. Mtu hawezi kuwa Mzalendo kama Hana Imani, au desturi, Mila au tamaduni ya taifa lake.

Mtu akishakuwa MTU wa Mila, desturi na tamaduni hawezi kuwa jizi na mhujumu uchumi wa Taifa lake kwani atakuwa MTU wa miiko. Ni ngumu Sana MTU kuwa Mkristo au muislam kindakindaki katika bara la Afrika alafu akawa Mzalendo Kwa taifa lake. Hiyo itakuwa maajabu ya Dunia. Hii ni Kwa sababu MTU anaongozwa na Akili yake(Elimu yake) na kile anachokiamini(dini, mila, desturi na tamaduni yake).

Muafrika sio Mzungu au myahudi mpaka aamini katika desturi na Imani za biblia, wala muafrika sio muarabu mpaka aamini katika mambo ya Quran. Hiyo pekee inaweza kueleza kuwa mataifa ya kiafrika bado yatabaki gizani Kwa Karne mbili mpaka tatu zijazo ikiwa yataendelee kushika Mila, desturi na tamaduni zisizowahusu.

Uzalishaji wa Mali msingi wake Mkuu ni Elimu na Mila na desturi.

Mpango KABAMBE wa kitaifa katika taifa letu lazima uzingatie Aina ya Watu waliopo na Yale yanayowaongoza.

Ikiwa kuna kiongozi yoyote anataka taifa hili liendelee itampasa afuate kile nikisemacho, sio Kwa kuhangaika kupoteza muda kuyaleta Maendeleo Kwa nguvu Bali kujenga Dini, Imani, desturi, Mila na utamaduni WA taifa letu ambao utatutambulisha kama taifa. Hivyo ndivyo taifa linavyojengwa na kama litahitaji kudumu Kwa muda mrefu. Kisha Elimu inayohusiana na mazingira yanayotuzunguka itolewe Kwa Watu wote ndani ya nchi kulingana na mazingira husika.

Huwezi ukajenga nchi mkiwa mnatofauti kubwa ya kiutamaduni, kumaanisha ninyi sio Wamoja. Na Sifa mojawapo ya taifa ni UMOJA. Leo akiongoza muislam upande wa Wakristo wataona hayo sio Maendeleo, na akiongoza mkristo upande wa Waislam watasema hayo sio Maendeleo.

Zingatia Maendeleo sio majengo wala miundombinu, Maendeleo ni mtizamo na Imani waliyonayo Watu.

Sio ajabu Kwa Wazungu Haki Sawa na Haki za ushoga kwao ni Maendeleo lakini Kwa wenye utamaduni tofauti wanaona sio Maendeleo. Demokrasia Kwa wengine ni Maendeleo huku Kwa wengine sio Maendeleo.

Ni lazima kama taifa tuweke Mpango KABAMBE tutakaoupenyeza katika vizazi vyetu polepole Kwa awamu awamu mpaka utakapotimia.

Jinsi ya kufanya:
1. Mitaala ya Elimu kuanzia Elimu ya msingi na Sekondari ibadilishwe,
2. Ziundwe Dini Mpya zenye Mila na desturi za Kitanzania.
Dini hizi zipewe Promo kubwa,
Dini hizi zitafundisha pia asili yetu kama Watanzania, miiko na Maadili yetu.

Kwa vile litakuwa Jambo jipya upinzani utakuwa ni mkali hasa wale wenye hizi dini za kigeni kama Wakristo na Waislam, lakini hiyo haitazuia ikiwa itatumika Akili nzuri.

3. Vyombo vya habari vidhibitwe katika kutangaza mambo yasiyo ya kizalendo, mambo ya kuigaiga

4. Neno Demokrasia liwe na udhibiti na litolewe maana kulingana na Mila na desturi zetu. Msingi wa neno Demokrasia usiwe Kutoka Nchi za kigeni. Uchorwe Mstari wa mwanzo wa demokrasi na mpaka wake.
Na ielezwe kinagaubaga kuwa mambo haya yanademokrasia Kwa kiwango hiki lakini mambo haya hayatakuwa na demokrasia kabisa.

5. Haki za binadamu ni Kwa maadili Mema pekee. Hakunaga Haki za binadamu Kwa Wasio na Maadili. Unapovunja Haki yako au Haki ya mwenzako lazima na wewe Haki yako ivunjwe. Watu wafundishwe kujiheshimu na kuheshimu wengine huo ndio utu na Haki za binadamu. Mtu asiyeuheshimu mwili wake au miili ya wengi naye hatakuwa na Haki ya kuheshimiwa na atadhibitiwa Kwa nguvu zote.

6. Uvamizi Kwa mataifa mengine lazima utekelezwe
Kwani tusipovamia bila Shaka tutavamiwa. Tusipoeaendesha basi tutaendeshwa. Sasa tutaamua tuvamie Kwa namna ipi, Kwa nguvu au Kwa Akili. Tusipotumia Rasilimali zao basi watatumia za kwetu. Hivyo ni lazima tufanye uamuzi sahihi ambao unajulikana.

Taikon naamini katika Uvamizi wa mataifa mengine kama sehemu ya kujilinda na kujihami kama Taifa.
Hii itatengeneza fursa Kwa Watu wetu kuwa pamoja zaidi kuliko tukikaa vivihivi kibwanyenye. Tutapunguza pia matatizo yetu ya ndani Kwa kiwango kikubwa endapo tutatumia mbinu hii kuvamia wengine.

Lakini tukisubiri kuvamiwa tutaongeza matatizo ya Watu wetu ndani ya nchi kama vile ukosefu wa Fursa za Ajira, kufanywa watumwa na vibarua, kunyonyana wenyewe Kwa wenyewe hasa Watawala kuwaibia wananchi wao.

Kuvamia mataifa mengine itafungua masoko pia ya Mazao yetu tunayoyalima hapa lakini yanakosa solo, Hii inapelekea Vijana wetu kukata tamaa na mambo ya kilimo kwani wanaona hakilipi.

Subiri Kwanza, Taikon kwani unaelezea vitu gani? Mbona kama unaandika mambo mengi yasiyo na Mbele wala nyuma!

Hapana, nilikuwa naelezea sehemu ya Mpango KABAMBE, TAIFA LITAMBE.

Acha nipumzike SASA!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ziundwe dini mpya.....hahah

Naam ziundwe Dini Mpya.
Kama hizi za kigeni zilivyoundwa nasi tuunde za kwetu.
Zitakazobeba uhalisia wetu, Mila, desturi, miiko na Wahusika wetu.

Hakunaga Mzalendo Duniani aliyekataa Mila na desturi na Dini zake za Asili. Haijawahi na haitokuja kutokea
 
Naam ziundwe Dini Mpya.
Kama hizi za kigeni zilivyoundwa nasi tuunde za kwetu.
Zitakazobeba uhalisia wetu, Mila, desturi, miiko na Wahusika wetu.

Hakunaga Mzalendo Duniani aliyekataa Mila na desturi na Dini zake za Asili. Haijawahi na haitokuja kutokea
Zumaridi ameshatekeleza
 
Back
Top Bottom