Je, Mtazamo wa 50:50 si chanzo cha LGBTQ?

Joshua justine

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
792
1,007
Ulimwengu wote umekumbwa na taharuki kuu, Baada ya Joe Biden kusign bill ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja marekani nzima (awali ilikuwa ruhusa kwenye majimbo baadhi), mnamo Desemba ,2022; ghafula mke wake amepanda ndege mwezi February ,2023 kuzungukia Afrika nchi kadhaa akiwa na ajenda kadhaa moja wapo ni hiyo ya mambo yao ya LGBT!

Mambo yanaonekana kwenda kwa speed sana hali ni mbaya. Ni kweli hao watu wamekuwepo wengi kwa sasa lakini kuhalalisha jambo hilo kisheria ni swala lingine kabisa.

Lakini kama tunakuwa wepesi wa kusahau basi lazima tutapotea ama kupotezwa tu. Tukumbuke kuwa ni hawa hawa jamaa ndio walikuja na mambo yao ya 50:50, hapo mwanzoni, jambo lile tulilipokea maana lilikuwa ni malengo ya umoja wa mataifa na mpaka leo lipo kwenye malengo hayo, je hizo haki zaLGBT zenyewe ni katika kikao gani na charter ipi ya UN na kwa nini wasiifanyie kikao cha UN iwekwe kwenye millenium goal mbona wanaipitisha kimabavu mabavu tu!

Pongezi kwa viongozi wetu waliokuwa madarakani wakati ule, "za kuambiwa wakachanganya na za kwao", jambo lile likawa jema mpaka leo. Maana hiyo 50:50 tulichofanya tuliitafsiri within our context, kwa mazingira yetu , bila kuvunja tamaduni mila na desturi zetu. Tuliitumia kuwainua wanawake kiuchumi, kielimu na kijamii.

Kijamii tulitokomeza baadhi ya zile mila zilizowaletea mateso wanawake kama vile kurithiwa wajane ama ukeketaji .Tulibakiza utamaduni wetu wa kimamlaka palepale, mamlaka ya kifamilia yanayoanza kwa baba kisha mama na mwisho mtoto. Hapo tukawa tumevuka salama.

Lakini kadri muda ulivyosogea, na wanawake kuzidi kusaidiwa kisaikolojia na kiuchumi, kweli tumeona wanawake wakaongezeka kujiamini na kuingia katika nyanja mbalimbali , kielimu, kisiasa na katika biashara na uzalishaji. Until wakapona kabisa kisaikolojia na kujiamini na kusema kuwa sasa wanaweza bila hata kuwezeshwa, hapa sasa ndipo kosa linapoanzia, sasa tuanzie hapo.

Tukaanza kuona wanawake wanajiita single mothers, eti mwanamke akipata watoto tu hataki tena mtu juu yake kwa kuwa hata yeye anaweza kuwapeleka watoto shule na kuhakikisha wamekula nakulala vizuri. Sawa, yote hayo wanaweza lakini mambo hayo peke yake hayakamilishi maisha ya watoto wala ya mwanamke, vinginevyo MUNGU mwenyewe asingemlazimiaha Yusuph mumewe Mariamu awe baba wa kambo wa YESU KRISTO.

Jambo la malezi ni la MUNGU mwenyewe, hata kama mwanamke ana hela , psychology ya mtoto hasa wa kiume inahitaji sana anapokuwa awe anasikia sauti ya kiume na kupata malezi ya baba hata kama ni wa kambo. Angalia madhara yaliyojitokeza katika jamii mara baada ya hili wimbi la single mothers kushamiri miaka ya hivi karibuni, watoto wao wengi wa kiume ndio hao wasiojiidentify kati ya wao na watoto wa kike , and they think its a life style kufanya mambo ya LGBT.

Hiyo 50:50 ni jambo la MUNGU mwenyewe

MWANZO 1:28
Mungu alitumia neno " mkatawale " ,ina maana walikuwa hawatawaliani wao bali wanatawala pamoja , na mkaongezeke na kuutiisha. Hapo walikuwa wana hierachy kati yao maana Adam alitangulia kuumbwa na Eva aliumbwa kwa ajili ya Adam lakini haikuwa hierachy ambayo ni kali sana , it was very moderate. Utawala wa Adamu juu ya Hawa haukuwa kama unavyopaswa uwe hivi leo. Kwa hiyo kujifanya eti 50:50 inawezekana ni kutaka kurudi paleedeni na kukata rufaa ya hukumu ya MUNGU na kujifanya kama vile mwanamke hana makosa, yaani mwanamke kapata asvocate wake ambaye ni satan ndani ya illuminate na freemasonry. Sasa wanashindana na hukumu iliyowekwa juu yao baada yakuanguka wanadai ile 50:50 iliyokuwepo kabla ya kukoseakwao.

Jambo hilo lilikuwa jema wakati ule akini sio katika ulimwengu kama huu tulionao, ni jambo lililokuwa sahihi katika ulimwengu msafi, wa bustani ya Edeni, ulimwengu usio na watu wa kumuwazia mambo maovu mwanao ,ulimwengu usio kuwa na media za kujaribu akili za vijana.

It means wangekuwa na social media basi zingehubiri neno la MUNGU tu. Hiyo hamsini kwa hamsini, sio kitu kinachotekelezeka kwa sasa maana ni MUNGU mwenyewe aliyekibadiriaha baada ya makosa ya Adamu na hawa mkewe pale pale bustanini, baada ya kuanguka dhambini, anguko lililosababishwa na Hawa , agizo likabadirika, katikamojawapo ya adhabu kwa mwanamke ikawa ni kutawaliwa na mumewe.

MWANZO. 3: 16
Hii iliamnatana na adhabu nyingine kama kuzaa kwa uchungu , Je wanawake hawazai kwa uchungu mpaka leo? Wawafanye basi wasizae kwa uchungu kama wao ni wamiliki wa hiyo science kweli! Katika sayansi yote wameshindwa kutengeneza kitu mbadala cha kufanya mtu azae lakini asione uchungu, Na wamegundua kuwa ili mtu azae ni lazima aone uchungu tu, na ndio maana hata wao wanamuongezea uchungu ikibidi haiwezekani kuzaa bila ya uchungu yaani kuwepo na kama ganzi fulani. Wao wanajua kuwa jambo hilo wameshindwa lakini hawasemi maanawanajua wakipublicize watawafumbia watu macho juu ya uweza wa MUNGU katika neno lake hapo alipotoa adhabu hiyo, na wao hawataki kumkiri MUNGU.

Badala yake wanawadanganya wanawake wanawapasua pasua hovyo hovyo na kuwatolea watoto madirishani badala ya mlangoni ! Madhara yake kiroho ni makubwa na kisaikolojia kwa watoto hao na kwa mama zao. Wamama wa visu hawa sio imara hata katika malezi ya watoto wao kama wamama walioona uchungu, maana "uchungu wa mwana aujuae mzazi"

Hatukatai wanawake kuwa na maendeleo lakini ni lazima wafanye hivyo wakiwa aware kuwa wao wako chini ya authority, maana yake ni kama wanataka kujikomboa kabisa kabisa chini ya Neno walilotamkiwa pale bustanini, adhabu ile itaiaha msimu wa mke na mume utakapoisha, yaani mwisho wa maisha haya na kule katika maisha ya milele. Kwa sasa mwanamke anaruhusa zote za kutenda mambo makubwa awezavyo lakini ni katika hali ya kujitambua kuwa yeye bado ni nani chini ya mwanaume.

MITHALI. 31: 11-12
Mambo yote yanaanzia kwa kuwa na adabu zote, wema wote na utiifu kwa mumewe ndipo huyu mwanamke anaendelea kufanya mambo makubwa ya biashara, ujasiriamali n.k kama unavyoona ukimsoma huyo mke mwema hapo katika mistari inayofuata.

Mwanamke huyo hapati kiburi eti kwa sababu na yeye anaweza kufanya mambo makubwa basi eti sasa amekuwa yeye badala ya mwanaume, na jambo hili lina madhara pia hata katika malezi maana watoto wanajifunza hapo hapo na wao.

MITHALI 31: 28
Tusijidanganye wala tusidanganyame mzizi wa tatizo lote la kimaadili kwa watotto wetu na mambo yote ya LGBT yanaanzia kwenye familia zilizotoka kwenye ile family manual ya MUNGU mwenyewe. Jambo hilo limeshawashinda hao wanaolileta kwetu. Huko kwao sasa hivi watoto wanashoot watu hovyo, wanakula madawa ya kulevya hovyo, ni vichaa. Hawana furaha ya maisha tena, huwezi kumlea mtoto, mtoto anadai haki za kujifanyia anavyotaka wakati NENO la MUNGU linasema mtoto ana uninga ndani yake sasa hiyo dunia yake hajaijua bado anajiamuliaje mambo hayo anayotaka, its a confusion goin on there.

Wale sio wazungu wa zamani, hao sasa ni mashetani, tusipokunali na kulielewa hilo tukadhani wanayotuletea leo ni kama vile zamani walipotuletea dini basi tutaangamia. Wazungu wa leo wao wenyewe ibilisi alishawaweza, hawasambazi tena habari njema, wanasambaza habari za lusifa; ushoga, usagaji, kushindana na mpango wa MUNGU wa familia, magonjwa n.k ndio wazungu wa leo.

Uatupasa tuelewe kuwa msimu tunaoishi sasa ni uleule wa kuitumikia adhabu iliyotolewa bustanini edeni , ndio maana mwanadamu bado anakifa kifo cha mwili japo roho itaiahi kwa kumuamini KRISTO. ASIWADANGANYE MTU HATA AGANO JIPYA BADO ADAMU NI ADAMU NA HAWA NI HAWA VINGINEVYO MWAFWA.

1 KORONTHO 11:8
1TIMOTHEO. 2:11-13
 
U-LGBTQ upo kabla hata ya Yesu kuzaliwa, miaka hiyo ya Ibrahimu. Ukitaka kupata chanzo inabidi urudi nyuma hadi wakati huo.
 
Kazi kwenu wale mnaokurupuka kupinga ushoga, mkiambiwa ukweli mnaanza kuhisi wenzenu ni wanachama wa hicho chama cha kubanjuana
 
Kazi kwenu wale mnaokurupuka kupinga ushoga, mkiambiwa ukweli mnaanza kuhisi wenzenu ni wanachama wa hicho chama cha kubanjuana
usodoma umeanza kitambo
Ila haukuwahi kuwa Public na kuungwa mkono kama ilivyo leo
Watu wanapinga sababu adhabu yake ilifanyika hapa hapa duniani
 
sisi tunapinga ushoga wewe unaunga mkono?
kwa mujibu wa biblia ulawiti ni dhambi, sasa kama ni dhambi unataka kufahamu nini msimamo wangu kuhusu ushoga? Jibu ni siungi mkono ushetani huo ila kuvunja haki za mashoga kuishi ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria zetu
 
50/50 ni mpango wa watu wasiojielewa.
Mungu hakukosea kumuumba mwanamke kama msaidizi, na baada ya uasi pale Eden, Mungu alimlaani mwanamke, akamwambia Umelaaniwa, Utazaa kwa Uchungu, na Utatawaliwa na Mmeo.

50/50 ni mpango wa shetani
Ushoga ni mpango wa Shetani pia maana ukishavunja familia kama taasisi ni rahisi kuendesha watu maana watoto hawatalelewa kimaadili.

Hadi sasa lengo la shetani limetimia na linatimia
 
Huu ni uongo mkubwa sana, hakuna bill yoyote Joe Biden aliyosaini ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja USA. Bunge la Marekani halijawahi kupitisha muswaada wa aina hiyo , masuala ya ndoa bado yako chini ya mamlaka za majimbo.
 
Huu ni uongo mkubwa sana, hakuna bill yoyote Joe Biden aliyosaini ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja USA. Bunge la Marekani halijawahi kupitisha muswaada wa aina hiyo , masuala ya ndoa bado yako chini ya mamlaka za majimbo.
Hizi sio zama za kubishana kibwege , tafuta mitandaoni, ukashangae kama huna habari , we unadhani hii movement duniani inatokea wapi,
 
50/50 ni mpango wa watu wasiojielewa.
Mungu hakukosea kumuumba mwanamke kama msaidizi, na baada ya uasi pale Eden, Mungu alimlaani mwanamke, akamwambia Umelaaniwa, Utazaa kwa Uchungu, na Utatawaliwa na Mmeo.

50/50 ni mpango wa shetani
Ushoga ni mpango wa Shetani pia maana ukishavunja familia kama taasisi ni rahisi kuendesha watu maana watoto hawatalelewa kimaadili.

Hadi sasa lengo la shetani limetimia na linatimia
Sasa hivi hawa ma feminist(wanawake) wanataka kuchuana na musclinity(wanaume)
Kama unavyoona sahv mwanamke anataka 50/50,mwanamke anataka apewe uhuru zaidi kwa mwanaume,
Kuna force kubwa inatokea kati ya nwanaume na mwanamke na hiyo inaleta majibizano,kuvurugana maana hakuna kuelewana
Ndomana watu wanaishia kuuana

Ovs
 
Sahv hawa ma feminist(wanawake) wanataka kuchuana na musclinity(wanaume)
Kama unavyoona sahv mwanamke anataka 50/50,mwanamke anataka apewe uhuru zaidi kwa mwanaume,
Kuna force kubwa inatokea kati ya nwanaume na mwanamke na hiyo inaleta majibizano,kuvurugana maana hakuna kuelewana
Ndomana watu wanaishia kuuana

Ovs
Kama waamini Biblia utaona kabisa lengo la Mungu haikuwa uwepo usawa, alimuweka Mwanamke kama msaidizi.

Ili shetani afanikiwe lengo lake ni lazima watu wakorofishane
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom