Utajiri wa Ridhwani wamweka pabaya Kikwete

Status
Not open for further replies.
@Ritz... ni kweli uhsahidi ni muhimu sana kwenye hii matter, lakini je unadhani ni kwanini yeye mwenyewe hakanushi?? au je unadhani Mtikila hajawahi kumuita rostam fisadi??

Na kama unaishi bongo huhitaji ushahidi wa magazetini... things are there to be seen, so kama ridhiwani ni fisadi, yataonekana, ingawa bado naamini dogo kuna siku will come clean

very bad these days, maana information imekua so free sio kama enzi za mwalimu
 
jamani hili suala la utajili wa mtoto wa jk limekuwa linaibuliwa, mimi naomba nijulishwe utajili wake a.k.a mali alizonazo ili nami niweze kuchangia vizuri!

ana kituo cha mafuta big brother,baduel dodoma(afroil) wengine endelezeni hata rostam atatusaidia kwani hataki kufa peke yake.
 
Mpelekee Riz1 hii message inaweza kumsaidia kwa maisha yake ya baadaye

Tatizo lenu nyie Wachaga Wakiristo Chadema mnamuona Slaa Prophet wenu kila analosema ni la kweli, huwo upuuzi atuwezi kukubali toa ushahidi usilete porojo za kwenye mbege
 
Mtikila anapashwa atueleze kidogo kuhusu Mwananchi kampuni ya dhahabu na uhusiano wake na Mhe. Sinde Warioba. Pia, why now, why so soon, why very fast. Is it for 2015 wish?? Mie siamini katika kuadhibiana, kwani katika hilo hakuna chama cha kisiasa kitaweza kushinda. Ni vizuri tukajifunza sana kusu taratibu alizozichukua Nelson Mandela na Desmond TUTU. Nawatafuta wenye imani kama yangu ili tuwasaidie viongozi wa vyama vya siasa, waelezane ukweli, wakiri, waombe radhi na tuwasamehe. Hapo ndipo tutaanza vizuri. Kila mmoja aache dhambi na tusonge mbele wote tukiwa na furaha ya kweli. Kinyemechake itakuwa visa, kutafutana, kuoneshana ubabe na kukana makosa na kudai kuonewa. Mwisho wa yote ni vita ya wenyewe kwa wenyewe.
 
"...UMASIKINI NI DHAMBI..." JK Njerere, kwa kiwangio cha kutoa mfano wa kiasi cha fedha ambacho hakikidhi haja, inaonyesha ni kiasi gani unakumbwa na wimbi hili la kipato cha chini na ndicho unachoona ni kiasi kingi... mfano unaposema anatumia kama sh 50,000/- Ninasikitika kusema kwa thamani ya hela yetu na hali ya maisha hiki ni kiasi kidogo sana, usishangae kwa magari ya kifahari haitoshi hata kwa mafuta ya siku tu!

Hebu tuangalie mantiki ya uhakikia, unaposema fulani ni tajiri amejilimbikizia mali, lazima utaje angalau kwa wastani thamani ya mali yake ili tuelewe unamaanisha nini, ama sivyo hayo ni majungu tu...

Kama unaona gari na nyumba... nadhani utakuwa umeona ofisi yake iliyotengenezwa kwa umaridadi mkubwa basi hizo ni "proxy indicators" zinaweza kuwa na value kubwa kulingana na macho ya ko aundogo kuliko unavyofikiri, ni kwasababu tu amepangilia unmaridadi na kuchagua, basi thamani yake inaonekana kuwa kubwa....

Tunataka ushahidi na data, hapa sio jukwaa la michezo unaongea kwa kubahatisha au kubuni na watu watashangilia tu.. hapa ni vitu serious tunataka ushahidi na data


AMA SIVYO MODE FUTA HII THREAD HAINA MANTIKI
 
Ponda mali, kufa kwaja!! Katika mfumo wa kibepari kuwa na mali ndiyo lengo, umeipataje, ni matokeo. Na kwa nchi zetu za kiafrika ukiwa madarakani ukatoka huna mali nyingi wanajamii wanakushangaa! Mfumo mzima wa kijamii unamshawishi mtu kiongozi kuiba, "... amekuwa mkurugenzi kwa miaka ... lakini angalia hana kitu, atakufa maskini huyu!! haoni wenzake wanavyompita tuu! Sijui zake anafanyia nini ... yeye anasusa wenzie wanakula..." Huo ndo mfumo unaofanya viongozi wazidi kujilimbikizia mali huku masikini na wenye kipato kidogo wakiendelea kuwalamba miguu ili nao wamegewe au wakumbukwe katika ukwasi wa wakulu. The mass wanabaki kunung'unika bila kukemea wala kuchukua hatua (labda kwa kisingizio cha AMANI au huyu ni mwanetu, mtu wetu au trickle down ya utajiri inawatiririkia kidogo na kupoza kiu zao)
IT DOES NOT TAKE GREAT MEN TO DO GREAT THINGS BUT ONLY CONCENTRATED MINDS, AND SUCCESS SELDOM GOES TO THE TIMID WHO ARE EVER AFRAID OF THE CONSEQUENCES. THE TIME TO WAKE UP IS NOW, THE ROOSTER IS ON TH E ROOFTOP.
 
@Ritz... ni kweli uhsahidi ni muhimu sana kwenye hii matter, lakini je unadhani ni kwanini yeye mwenyewe hakanushi?? au je unadhani Mtikila hajawahi kumuita rostam fisadi??

Na kama unaishi bongo huhitaji ushahidi wa magazetini... things are there to be seen, so kama ridhiwani ni fisadi, yataonekana, ingawa bado naamini dogo kuna siku will come clean

very bad these days, maana information imekua so free sio kama enzi za mwalimu

Mtikila alishawahi kusema Rostam Fisadi kama unakumbuka baada ya kusema Rostam alifanyaje?
 
Mali hizo ni za Baba mtu ambazo kwa sasa ziko katika jina la mwanae na pindi atakapomaliza awamu yake ya pili 2015 basi si ajabu zikahamishwa na kuwa katika jina la Baba. Ridhiwan hajafanya kazi wala biashara yoyote ile kwa muda mrefu kiasi cha kuweza kuwa na mali inayosadikiwa kwamba ina thamani ya bilioni moja na ndiyo maana mpaka sasa amepata kigugumizi kutokana na ombi la Dr Slaa la kumtaka atoe maelezo ya jinsi alivyopata mali yote hiyo katika kipindi kifupi sana toka amalize masomo yake.

Bil1 tu mkuu? Mbona hiyo ni pesa ya nyanya tu sokoni!
 
Wakuu,mbona watoto wa Mkapa hawajawahi kutuhumiwa kuiba fedha za umma!vipi huyu fisadi mtoto?ana jeuri gani?
 
Kwa kiongozi yeyote mwenye kujali haki na utawala wa kidemokrasia ni lazima atakanusha au kukubali hili na kulitolea ufafanuzi kwa sababu linamgusa moja kwa moja.

Rais ni first Citizen.Kama kweli anapiga vita ufisadi,sasa ni wakati mwafaka kabisa wa kuonyesha kwa vitendo na pengine kama ridhiwani anamiliki kweli hicho kiasi,basi atoe ufafanuzi ili vijana wengine wa kitanzania watumie hiyo mbinu kujikwamua kutoka katika Lindi la Umaskini

Si Rais anasema ana nia njema na Watanzania?si ana nia njema na Taifa hili?Si ana uchungu na taifa na umaskini wa watanzania unamsikitisha?Hili swala linahitaji Maelezo ya kina,kamwe wasifikirie kukana Tuhuma bila maelezo na au kutishia gazeti au watu walioibua Tuhuma hizi.ni wajibu wa Jk kuwaeleza watanzania ukweli,ni haki ya watanzania kujua.Otherwise,huu ni moto ambao hataweza kuuzima,Vijana wa Tanzania wamechoka,hii nchi si bustani ya watawala na familia zao
 

Adaiwa kuwa bilionea kwa mgongo wa Ikulu
Na Mwandishi wetu - Tanzania Daima.


RAIS Jakaya Kikwete anakabiliwa na kashfa nzito kutokana na utajiri wa mtoto wake, Ridhiwani. Sasa anatuhumiwa kuitumia Ikulu kumtajirisha mwanawe, ambaye anasemekana ni bilionea.

Kwa nyakati mbalimbali, ukwasi wa mtoto huyo wa rais uliibuliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

Katika moja ya mikutano yake ya hadhara hivi karibuni mkoani Tabora, Dk. Slaa alisema Ridhiwani amemaliza shule miaka michache iliyopita, lakini hivi sasa ni tajiri bilionea na kwamba ameupata utajiri huo katika mazingira ya kutatanisha.

Jana Mtikila alizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Travertine, akidai Ridhiwani amegeuka bilionea kwa muda mfupi “kwa mgongo wa baba yake.”

Akibainisha zaidi uwezo wa kifedha wa kijana huyo, Mtikila alisema hivi karibuni mtoto huyo ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), aliingiza magari makubwa ya mizigo aina ya “semi trailer” zaidi ya 100 na kudai kuwa yanafanya kazi ya kusomba mizigo DRC na mengine ameyauza.

Alidai pia mtoto huyo wa rais anamiliki makampuni ya ujenzi wa barabara na maeneo mengi ya ardhi kwa lengo la kujenga maghorofa ya kupangisha.

“Huyu ni mtoto mdogo, kamaliza shule juzi, pesa za utajiri wote huu kazipata wapi?” alihoji Mtikila.
Hata hivyo, wiki iliyopita, Ridhiwani alikaririwa na moja ya vyombo vya habari akisema kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano kwa Dk. Slaa kuonyesha kila anachomiliki.

Kutokana na tuhuma hizo, Mtikila alimtaka Rais Kikwete naye ajivue gamba kwa kuonyesha mfano, vinginevyo ni uendawazimu kujivua gamba bila mkuu huyo wa nchi kujiuzulu urais na uenyekiti wa CCM.

Huku akionekana kuwatetea Edward Lowassa (Monduli), Andrew Chenge (Bariadi Magharibi) na Rostam Aziz (Igunga), Mtikila alisema Kikwete anawachezea wana CCM na Watanzania kwamba ana nia ya kuwatimua makada hao kwa madai kuwa ni mafisadi wakati yeye ni mshirika wao.

“Kikwete aanze kutoka yeye ndipo awanyoshee vidole hawa Mapacha Watatu alioshirikiana nao kwenye ufisadi wa EPA, Richmond na Dowans, vinginevyo anawadanganya Watanzania. Aanze yeye,” alisema Mtikila.

Alisema anashangazwa na Kikwete kuibuka na dhana ya kujivua gamba kwa kuwatosa marafiki zake watatu wakati chama hicho kina mafisadi lukuki.

Mchungaji Mtikila pia aliorodhesha miradi ya ufisadi aliyomhusisha nayo Kikwete na watendaji wengine serikalini kuwa ni pamoja na IPTL, uuzaji wa iliyokuwa Benki ya NBC, Meremeta, Richmond, Dowans, EPA na nyingine, kwamba zinawahusu watendaji wengi na si mapacha watatu pekee.

”Kikwete aliunda tume kubaini waliochota fedha za EPA na kutakiwa warudishe, lakini hadi sasa hatujui kina nani wamehusika, na kiasi gani cha fedha kilichorudishwa. Kama rais hahusiki na ufisadi huu, usiri wa nini?” alihoji Mtikila.

Alisisitiza kuwa hana maana kuwa Lowassa, Rostam na Chenge ni wasafi, bali anataka orodha ya kuwatimua mafisadi wa CCM iwe kubwa, akiwamo Rais Kikwete kwani ndilo gamba kubwa kuliko yote.

Kuhusu hatima ya CCM na kile alichokiita usanii wa kujivua gamba, Mchungaji Mtikila alisema chama hicho kina ugonjwa wa ‘Nambulila’ ambao mgonjwa hufa na kuzikwa akijiona.

“Wapangwa wana ugonjwa unaitwa Nambulila. Ni ugonjwa unaotokana na tego la mke. Mtu akitembea na mke wa mtu anaupata na anapokufa, anawaona watu wanavyomlilia, wanavyomuingiza kwenye kaburi, lakini hana uwezo wa kusema, hivyo anazikwa akiwa hai, akiona kila kitu. Ndivyo ilivyo CCM, inakufa ikijiona. Hii ndiyo Nambulila,” alisema Mtikila.

Alisema usanii wa kujivua gamba hauwezi kuinusuru CCM kwani ni dhana ya uendawazimu yenye lengo la kuwaghilibu Watanzania.

Sambamba na hilo, Mtikila aliwataja mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye, Joseph Warioba na Cleopa Msuya, kuwa ni miongoni mwa watu wachache wasafi ndani ya CCM.

Alipobanwa kueleza usafi wa Sumaye wakati miaka sita iliyopita alipata kumtaja kwamba ni fisadi namba moja, Mtikila alikiri kutoa kauli hiyo na kuongeza kwamba baada ya kufuatilia walibaini kashfa dhidi yake zilikuwa za uongo na zilipikwa ili kumrahisishia Kikwete njia ya kuwa rais.

“Kweli niliwahi kumtaja kama fisadi namba moja, tulipofuatilia tulibaini kwamba haikuwa sahihi na ndiyo maana leo namtaja kama mmoja ya viongozi wachache wasafi,” alisema.

Aliwataka wana CCM kutobeza ushauri wa viongozi hao wachache wasafi na kutolea mfano wa Warioba na Sumaye walivyoshambuliwa na UVCCM walipotoa mawazo yao.

Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka !


Sumaye sio msafi kiasi hicho,ila ukilinganisha na akina Rostam,Lowasa,Kikwete etc.,he is okay!
 
Mtikila - ni mwendawazimu

Cleopa Msuya - Tunaomba maelezo ya nini kilichotokea 12/04/XX pale Morogoro (kweli wewe ni msafi)

Joseph Sinde Warioba - Sina comment - Uwaziri Mkuu wako uliishia kwa Mke! Strange!

Frederick Sumaye - What are you UP TO?

Tanzania Daima - Why are you becoming the Voice of "triplets"?

I feel Like Shooting someone - cold blood!
Mkuu unataka kusema Cleopa Msuya anahusika na nini mwaka huo kule Morogoro?
 
Jmn ukwasi wa jk na familia yake ni mkubwa sana zaidi mnavyofikilia. Me jana tu jmoc nimeenda mkuranga kuangalia kma naweza kupata kajieneo ka kufanya kilimo kwanza kwa vitendo, nimekosa maana nimekuta kuna muwekezaji ameingia ubia na mama salma na kuchukua eneo zuri kwajili ya kujenga hotel eneo ni kubwa sanaaa!
tukaenda eneo jingine tukakuta wanasema wanajenga kiwanda kikubwa sana cha saruji nazan EA nzima,kama sijakosea humu ndani nilionaga watu walisema kwamba huyo mwekezaji ana ties na Jk.

Kali zaidi kuna eneo ndo lilikua zuri zaidi ya yote hapo ni eka kma 500 hv ya ardhi nzuri kweli kweli yote niliambiwa na mtendaji wa hilo eneo ni ya mama salma kikwete!na pia tukaenda mpk nyumban hapo tukamkuta baba yake salama tukamsalimia! Sasa kma mkuranga tu wana ukwasi wa ardhi kiasi hichi unazan maeneo mwengine wanafanyaje kwa mfn? Naumia sana mana nchi yangu tanzania tunaijenga wote wanaila wachache tena hawaili wanakomba, hakuna kula mbakishie baba
 
Tatizo lenu nyie Wachaga Wakiristo Chadema mnamuona Slaa Prophet wenu kila analosema ni la kweli, huwo upuuzi atuwezi kukubali toa ushahidi usilete porojo za kwenye mbege


......hizi propaganda hizi ....hazina maana kabisa ..kwani kuna watu nchi hii wanayo haki na wengine wanatakiwa wawe wasindikizaji tu...people......kauli yako ya kibaguzi inafanana na ile ya vijana wa bagamoyo...
 
mimi nahisi tuchukue hatua dhidi ya haya mambo maneno matupu hayana maana

Tunaliwa na watu wachache tena mazuzu ambao hawana hata maana
 
Jmn ukwasi wa jk na familia yake ni mkubwa sana zaidi mnavyofikilia. Me jana tu jmoc nimeenda mkuranga kuangalia kma naweza kupata kajieneo ka kufanya kilimo kwanza kwa vitendo, nimekosa maana nimekuta kuna muwekezaji ameingia ubia na mama salma na kuchukua eneo zuri kwajili ya kujenga hotel eneo ni kubwa sanaaa!
tukaenda eneo jingine tukakuta wanasema wanajenga kiwanda kikubwa sana cha saruji nazan EA nzima,kama sijakosea humu ndani nilionaga watu walisema kwamba huyo mwekezaji ana ties na Jk.

Kali zaidi kuna eneo ndo lilikua zuri zaidi ya yote hapo ni eka kma 500 hv ya ardhi nzuri kweli kweli yote niliambiwa na mtendaji wa hilo eneo ni ya mama salma kikwete!na pia tukaenda mpk nyumban hapo tukamkuta baba yake salama tukamsalimia! Sasa kma mkuranga tu wana ukwasi wa ardhi kiasi hichi unazan maeneo mwengine wanafanyaje kwa mfn? Naumia sana mana nchi yangu tanzania tunaijenga wote wanaila wachache tena hawaili wanakomba, hakuna kula mbakishie baba

Halafu watu wakiandika hapa jamvini kwamba huyu Mama ni fisadi basi watatoka watetezi wa mafisadi na kumtetea kwa nguvu zao zote. Hizo pesa anazojengea hotel kazitoa wapi? Kwa biashara ipi? kama siyo ufisadi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom