Utajiri wa Ridhwani wamweka pabaya Kikwete

Status
Not open for further replies.
Jakaya nakuomba na ninamwomba Mungu pia uweze kupata ufahamu wa kuona kesho yako kwani watanzania watakupitisha njia moja mara mbili.Ninapata hofu siku utakapo HASIWA kama mbuzi dume angalau upate uchungu ambao labda ndio utakaoufananisha na machungu iliyo mioyoni mwa Watanzania dhidi yako.
 
Na mali zake nyingi za bwana mdogo ameshirikiana na aliyekuwa mweka hazina wa bagamoyo aliyetimuliwa ukimtafuta kwa peke ake huwezi kumpata

Adaiwa kuwa bilionea kwa mgongo wa Ikulu
Na Mwandishi wetu - Tanzania Daima.


RAIS Jakaya Kikwete anakabiliwa na kashfa nzito kutokana na utajiri wa mtoto wake, Ridhiwani. Sasa anatuhumiwa kuitumia Ikulu kumtajirisha mwanawe, ambaye anasemekana ni bilionea.

Kwa nyakati mbalimbali, ukwasi wa mtoto huyo wa rais uliibuliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

Katika moja ya mikutano yake ya hadhara hivi karibuni mkoani Tabora, Dk. Slaa alisema Ridhiwani amemaliza shule miaka michache iliyopita, lakini hivi sasa ni tajiri bilionea na kwamba ameupata utajiri huo katika mazingira ya kutatanisha.

Jana Mtikila alizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Travertine, akidai Ridhiwani amegeuka bilionea kwa muda mfupi “kwa mgongo wa baba yake.”

Akibainisha zaidi uwezo wa kifedha wa kijana huyo, Mtikila alisema hivi karibuni mtoto huyo ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), aliingiza magari makubwa ya mizigo aina ya “semi trailer” zaidi ya 100 na kudai kuwa yanafanya kazi ya kusomba mizigo DRC na mengine ameyauza.

Alidai pia mtoto huyo wa rais anamiliki makampuni ya ujenzi wa barabara na maeneo mengi ya ardhi kwa lengo la kujenga maghorofa ya kupangisha.

“Huyu ni mtoto mdogo, kamaliza shule juzi, pesa za utajiri wote huu kazipata wapi?” alihoji Mtikila.
Hata hivyo, wiki iliyopita, Ridhiwani alikaririwa na moja ya vyombo vya habari akisema kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano kwa Dk. Slaa kuonyesha kila anachomiliki.

Kutokana na tuhuma hizo, Mtikila alimtaka Rais Kikwete naye ajivue gamba kwa kuonyesha mfano, vinginevyo ni uendawazimu kujivua gamba bila mkuu huyo wa nchi kujiuzulu urais na uenyekiti wa CCM.

Huku akionekana kuwatetea Edward Lowassa (Monduli), Andrew Chenge (Bariadi Magharibi) na Rostam Aziz (Igunga), Mtikila alisema Kikwete anawachezea wana CCM na Watanzania kwamba ana nia ya kuwatimua makada hao kwa madai kuwa ni mafisadi wakati yeye ni mshirika wao.

“Kikwete aanze kutoka yeye ndipo awanyoshee vidole hawa Mapacha Watatu alioshirikiana nao kwenye ufisadi wa EPA, Richmond na Dowans, vinginevyo anawadanganya Watanzania. Aanze yeye,” alisema Mtikila.

Alisema anashangazwa na Kikwete kuibuka na dhana ya kujivua gamba kwa kuwatosa marafiki zake watatu wakati chama hicho kina mafisadi lukuki.

Mchungaji Mtikila pia aliorodhesha miradi ya ufisadi aliyomhusisha nayo Kikwete na watendaji wengine serikalini kuwa ni pamoja na IPTL, uuzaji wa iliyokuwa Benki ya NBC, Meremeta, Richmond, Dowans, EPA na nyingine, kwamba zinawahusu watendaji wengi na si mapacha watatu pekee.

”Kikwete aliunda tume kubaini waliochota fedha za EPA na kutakiwa warudishe, lakini hadi sasa hatujui kina nani wamehusika, na kiasi gani cha fedha kilichorudishwa. Kama rais hahusiki na ufisadi huu, usiri wa nini?” alihoji Mtikila.

Alisisitiza kuwa hana maana kuwa Lowassa, Rostam na Chenge ni wasafi, bali anataka orodha ya kuwatimua mafisadi wa CCM iwe kubwa, akiwamo Rais Kikwete kwani ndilo gamba kubwa kuliko yote.

Kuhusu hatima ya CCM na kile alichokiita usanii wa kujivua gamba, Mchungaji Mtikila alisema chama hicho kina ugonjwa wa ‘Nambulila’ ambao mgonjwa hufa na kuzikwa akijiona.

“Wapangwa wana ugonjwa unaitwa Nambulila. Ni ugonjwa unaotokana na tego la mke. Mtu akitembea na mke wa mtu anaupata na anapokufa, anawaona watu wanavyomlilia, wanavyomuingiza kwenye kaburi, lakini hana uwezo wa kusema, hivyo anazikwa akiwa hai, akiona kila kitu. Ndivyo ilivyo CCM, inakufa ikijiona. Hii ndiyo Nambulila,” alisema Mtikila.

Alisema usanii wa kujivua gamba hauwezi kuinusuru CCM kwani ni dhana ya uendawazimu yenye lengo la kuwaghilibu Watanzania.

Sambamba na hilo, Mtikila aliwataja mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye, Joseph Warioba na Cleopa Msuya, kuwa ni miongoni mwa watu wachache wasafi ndani ya CCM.

Alipobanwa kueleza usafi wa Sumaye wakati miaka sita iliyopita alipata kumtaja kwamba ni fisadi namba moja, Mtikila alikiri kutoa kauli hiyo na kuongeza kwamba baada ya kufuatilia walibaini kashfa dhidi yake zilikuwa za uongo na zilipikwa ili kumrahisishia Kikwete njia ya kuwa rais.

“Kweli niliwahi kumtaja kama fisadi namba moja, tulipofuatilia tulibaini kwamba haikuwa sahihi na ndiyo maana leo namtaja kama mmoja ya viongozi wachache wasafi,” alisema.

Aliwataka wana CCM kutobeza ushauri wa viongozi hao wachache wasafi na kutolea mfano wa Warioba na Sumaye walivyoshambuliwa na UVCCM walipotoa mawazo yao.

Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka !

 
Hatuko nchi ya kufikirika@ibange.hao kina rachel,mbona atleas chenge suala la rada lilijieleza wazi,lowasa ,richmond ilimfanya yeye mwenyewe ajiuzuru,aziz kagoda,si tuliona document kuhusu wakurugenzi wa kagoda kuwa watu wake wa karibu.
Ndo maana nikasema wenye evidence ya kuhusu riz watubandikie hapa
 
Hatuko nchi ya kufikirika@ibange.hao kina rachel,mbona atleas chenge suala la rada lilijieleza wazi,lowasa ,richmond ilimfanya yeye mwenyewe ajiuzuru,aziz kagoda,si tuliona document kuhusu wakurugenzi wa kagoda kuwa watu wake wa karibu.
Ndo maana nikasema wenye evidence ya kuhusu riz watubandikie hapa
 
Ha ha haaaaaaaaaaaaaaaa


tanzania daima
chadema
na mapacha watatu ni kundi moja?
hilo halina ubishi gazeti la tanzania daima leo lina makala kibao kuwatetea mapacha watatu huenda hili gazeti limeanza kupata ruzuku kutoka kwa mapacha watatu
 
Hatimaye yale yaliyobashiriwa sasa yametimia. Ilizungumzwa huko nyuma kwamba hawa mapacha watatu wataanza kampeni ya nguvu ya kuchafua watu kwa stori za uongo ili hatimaye wote waonekane wamechafuka kama mkakati wao wa kubaki CCM kwa vile ni dhahir kwamba hawana pa kwenda kwa vile ni mzigo na hawana mvuto.

Kwa wenye akili na wanaoweza kufanya utafiti mdogo tu watagundua kwamba habari hizi hazina hata chembe ya ukweli kwa vile dhamira yake ilikuwa ni kutekeleza shabaha yao na kwa bahati nzuri kwao, haijakosa uungwaji mkono wa watu ambao ama hawajui mlolongo wa mbinu chafu za kujinasua.

Mtikila tunamfahamu, baada ya kupoteza relevance yake kwa jamii sasa amekuwa ni kama jeshi la kukodiwa ili aweze kuishi mjini.

Ndiye huyu huyu aliyekwenda kusaini petty cash voucher kwa Rostam kupata hela ya kuishi na akabana mpaka alipoumbuliwa. Leo anamuomba radhi Sumaye baada ya kutuhubiria watz juu ya uchafu wake huyu jamaa.


Tulishadokeza huko nyuma kwamba sasa hivi watatumika hata wale wenye mvuto na heshima mbele ya jamii ili kuwanasua mapacha hawa.

Tumeona Dr. akipaza sauti kwa vitu ambavyo tunajua havina ukweli. Haya ni matokeo ya hawa jamaa kujibanza kwa CDM ili wanusurike na panga hili la shaba linalowakabili.

Tanzania Daima sasa hivi ni sehemu ya Habari Corporation katika kuimba mapambio ya kuwasifu na kuwatakasa mafisadi hawa.

Tutayaona na kuyasikia mengi katika kipindi hiki cha kujaribu kurejesha gamba lakini ukweli ni kwamba jamaa ni LAZIMA WAONDOKE na hakuna msaada wa propaganda na upotoshaji wowote utakaosaidia kuwaondoa jamaa katika shida hii.

Ni mzigo wa sumu ambao ni lazima utokomezwe, naihurumia CDM inavyojaribu kujiua kwa kukumbatia wale wale iliyokuwa inawapigia kelele.
mkuu kuna kila dalili luwa chadema walishalambishwa si bure
 
yan huyu dogo awezi kumiliki kodi za watanzania kiasi hicho na hizo gari zitakuwa zimeingia hata azijalipiwa ushuru ni magumashi tu ushenzi mtu alafu baba yk anataka kutuchakachua katiba yani nina hasira sana na huyu dogo
nani wakumlipsha kodi wakati serikali ipo mikononi mwao. Sisi tulie tu, Tusimuudhi mtoto wa mfalme.
 
Mtikila - ni mwendawazimu

Cleopa Msuya - Tunaomba maelezo ya nini kilichotokea 12/04/XX pale Morogoro (kweli wewe ni msafi)

Joseph Sinde Warioba - Sina comment - Uwaziri Mkuu wako uliishia kwa Mke! Strange!

Frederick Sumaye - What are you UP TO?

Tanzania Daima - Why are you becoming the Voice of "triplets"?

I feel Like Shooting someone - cold blood!

Una kitu cha kuandika sijui kwanini unaogopa? Hapo upo wewe na keyboard yako tu.
 
Napenda sana utajiri... Lakini si kwa style ya huyu dogo
nasi tunapenda ukweli daima si kupindisha mlichokuwa mnasimamia siku zote leo ukisoma tanzania daima ndio utajua unafiki wa hiki chama
 
Jamani hii inakera sana!!! ni lini tutachukua hatua?? wakati ni huu ! kama tumeshindwa kidemokrasia basi tujipange KULIANZISHA!!! kwani naona tunapoteza nguvu na muda mwingi kudiscuss ishu hizi hizi!!! jamani tuamke angalua hapa kwetu napo pawe na sifa za DAFUR watakao salimika wataongoza njiiiii na tutakao potea historia itatukumbuka. Kumbukeni KIAZI LAZIMA KIFUKIWE NDIO KIOTE!!
 


Na Mwandishi wetu - Tanzania Daima.



Huku akionekana kuwatetea Edward Lowassa (Monduli), Andrew Chenge (Bariadi Magharibi) na Rostam Aziz (Igunga), Mtikila alisema Kikwete anawachezea wana CCM na Watanzania kwamba ana nia ya kuwatimua makada hao kwa madai kuwa ni mafisadi wakati yeye ni mshirika wao.

Sambamba na hilo, Mtikila aliwataja mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye, Joseph Warioba na Cleopa Msuya, kuwa ni miongoni mwa watu wachache wasafi ndani ya CCM.


SOURCE: TZDaima; tumeshuhudia gazeti hili siku za karibuni wakijaribu sana kuwasafisha hawa mafisadi. Na huyu Mtikila aliwahi kufadhiliwa sana na RA katika shughuli za kanisa lake.

Nashangaa hivi Sumaye ameoga sabuni kiasi gani hadi akawa msafi?​
 
Sijui makongoro na Madaraka Nyerere wanajisikiaje wakipata habari kama hizi? je wanasema dingi yao hakuwa mjanja au?
 
KIKWETE KUBALI AU KATAA KUHUSU UTAJIRI WA HUYO BWANA MDOGO MTOTO WAKO,NCHI HII SIO KILA MTAWALA LAZIMA AWE BILLIONEA,UNARUDISHA NYUMA JUHUDI ZETU ZA KUREKEBISHA NCHI YETU,USIPOCHUKUA HATUA NILIZOKUSHAURI UTAONA MATOKEO YAKE:bored::bored::bored::bored:

Jamani hili suala la utajili wa mtoto wa JK limekuwa linaibuliwa, mimi naomba nijulishwe utajili wake a.k.a mali alizonazo ili nami niweze kuchangia vizuri!
 
Miafrika bana..yaani mtu anapewa dhamana ya uongozi na watu wake, kisha anashirikiana na maponjoro kuwaibia watu wake mafukara waliompa dhamana ya kuwaletea maendeleo.
hakuna kitu kibaya kama kuwa mnafiki leo gazeti la tanzania daima linawatetea mapacha watatu wakati huo huo linaongelea kuhusu utajiri wa rizwan
 
ushahidi please.na pia tunataka mtikila nae atoe ushahidi juu ya ufisadi wa viongozi wa cdm na cdm kama chama kijitete wakikaa kimya itakuwa ni kweli
 
Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom