Utajiri wa Ridhwani wamweka pabaya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajiri wa Ridhwani wamweka pabaya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, May 1, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280

  Adaiwa kuwa bilionea kwa mgongo wa Ikulu
  Na Mwandishi wetu - Tanzania Daima.


  RAIS Jakaya Kikwete anakabiliwa na kashfa nzito kutokana na utajiri wa mtoto wake, Ridhiwani. Sasa anatuhumiwa kuitumia Ikulu kumtajirisha mwanawe, ambaye anasemekana ni bilionea.

  Kwa nyakati mbalimbali, ukwasi wa mtoto huyo wa rais uliibuliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

  Katika moja ya mikutano yake ya hadhara hivi karibuni mkoani Tabora, Dk. Slaa alisema Ridhiwani amemaliza shule miaka michache iliyopita, lakini hivi sasa ni tajiri bilionea na kwamba ameupata utajiri huo katika mazingira ya kutatanisha.

  Jana Mtikila alizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Travertine, akidai Ridhiwani amegeuka bilionea kwa muda mfupi "kwa mgongo wa baba yake."

  Akibainisha zaidi uwezo wa kifedha wa kijana huyo, Mtikila alisema hivi karibuni mtoto huyo ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), aliingiza magari makubwa ya mizigo aina ya "semi trailer" zaidi ya 100 na kudai kuwa yanafanya kazi ya kusomba mizigo DRC na mengine ameyauza.

  Alidai pia mtoto huyo wa rais anamiliki makampuni ya ujenzi wa barabara na maeneo mengi ya ardhi kwa lengo la kujenga maghorofa ya kupangisha.

  "Huyu ni mtoto mdogo, kamaliza shule juzi, pesa za utajiri wote huu kazipata wapi?" alihoji Mtikila.
  Hata hivyo, wiki iliyopita, Ridhiwani alikaririwa na moja ya vyombo vya habari akisema kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano kwa Dk. Slaa kuonyesha kila anachomiliki.

  Kutokana na tuhuma hizo, Mtikila alimtaka Rais Kikwete naye ajivue gamba kwa kuonyesha mfano, vinginevyo ni uendawazimu kujivua gamba bila mkuu huyo wa nchi kujiuzulu urais na uenyekiti wa CCM.

  Huku akionekana kuwatetea Edward Lowassa (Monduli), Andrew Chenge (Bariadi Magharibi) na Rostam Aziz (Igunga), Mtikila alisema Kikwete anawachezea wana CCM na Watanzania kwamba ana nia ya kuwatimua makada hao kwa madai kuwa ni mafisadi wakati yeye ni mshirika wao.

  "Kikwete aanze kutoka yeye ndipo awanyoshee vidole hawa Mapacha Watatu alioshirikiana nao kwenye ufisadi wa EPA, Richmond na Dowans, vinginevyo anawadanganya Watanzania. Aanze yeye," alisema Mtikila.

  Alisema anashangazwa na Kikwete kuibuka na dhana ya kujivua gamba kwa kuwatosa marafiki zake watatu wakati chama hicho kina mafisadi lukuki.

  Mchungaji Mtikila pia aliorodhesha miradi ya ufisadi aliyomhusisha nayo Kikwete na watendaji wengine serikalini kuwa ni pamoja na IPTL, uuzaji wa iliyokuwa Benki ya NBC, Meremeta, Richmond, Dowans, EPA na nyingine, kwamba zinawahusu watendaji wengi na si mapacha watatu pekee.

  "Kikwete aliunda tume kubaini waliochota fedha za EPA na kutakiwa warudishe, lakini hadi sasa hatujui kina nani wamehusika, na kiasi gani cha fedha kilichorudishwa. Kama rais hahusiki na ufisadi huu, usiri wa nini?" alihoji Mtikila.

  Alisisitiza kuwa hana maana kuwa Lowassa, Rostam na Chenge ni wasafi, bali anataka orodha ya kuwatimua mafisadi wa CCM iwe kubwa, akiwamo Rais Kikwete kwani ndilo gamba kubwa kuliko yote.

  Kuhusu hatima ya CCM na kile alichokiita usanii wa kujivua gamba, Mchungaji Mtikila alisema chama hicho kina ugonjwa wa ‘Nambulila' ambao mgonjwa hufa na kuzikwa akijiona.

  "Wapangwa wana ugonjwa unaitwa Nambulila. Ni ugonjwa unaotokana na tego la mke. Mtu akitembea na mke wa mtu anaupata na anapokufa, anawaona watu wanavyomlilia, wanavyomuingiza kwenye kaburi, lakini hana uwezo wa kusema, hivyo anazikwa akiwa hai, akiona kila kitu. Ndivyo ilivyo CCM, inakufa ikijiona. Hii ndiyo Nambulila," alisema Mtikila.

  Alisema usanii wa kujivua gamba hauwezi kuinusuru CCM kwani ni dhana ya uendawazimu yenye lengo la kuwaghilibu Watanzania.

  Sambamba na hilo, Mtikila aliwataja mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye, Joseph Warioba na Cleopa Msuya, kuwa ni miongoni mwa watu wachache wasafi ndani ya CCM.

  Alipobanwa kueleza usafi wa Sumaye wakati miaka sita iliyopita alipata kumtaja kwamba ni fisadi namba moja, Mtikila alikiri kutoa kauli hiyo na kuongeza kwamba baada ya kufuatilia walibaini kashfa dhidi yake zilikuwa za uongo na zilipikwa ili kumrahisishia Kikwete njia ya kuwa rais.

  "Kweli niliwahi kumtaja kama fisadi namba moja, tulipofuatilia tulibaini kwamba haikuwa sahihi na ndiyo maana leo namtaja kama mmoja ya viongozi wachache wasafi," alisema.

  Aliwataka wana CCM kutobeza ushauri wa viongozi hao wachache wasafi na kutolea mfano wa Warioba na Sumaye walivyoshambuliwa na UVCCM walipotoa mawazo yao.

  Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka !

   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Ha ha haaaaaaaaaaaaaaaa


  tanzania daima
  chadema
  na mapacha watatu ni kundi moja?
   
 3. z

  zamlock JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  yan huyu dogo awezi kumiliki kodi za watanzania kiasi hicho na hizo gari zitakuwa zimeingia hata azijalipiwa ushuru ni magumashi tu ushenzi mtu alafu baba yk anataka kutuchakachua katiba yani nina hasira sana na huyu dogo
   
 4. x

  xman Senior Member

  #4
  May 1, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtoto huyo nazani alama za nyakati hajazisoma vizuri, amuulize mtoto wa mubarak kinachomtokea sasa hivi,,
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,883
  Likes Received: 83,366
  Trophy Points: 280
  Mali hizo ni za Baba mtu ambazo kwa sasa ziko katika jina la mwanae na pindi atakapomaliza awamu yake ya pili 2015 basi si ajabu zikahamishwa na kuwa katika jina la Baba. Ridhiwan hajafanya kazi wala biashara yoyote ile kwa muda mrefu kiasi cha kuweza kuwa na mali inayosadikiwa kwamba ina thamani ya bilioni moja na ndiyo maana mpaka sasa amepata kigugumizi kutokana na ombi la Dr Slaa la kumtaka atoe maelezo ya jinsi alivyopata mali yote hiyo katika kipindi kifupi sana toka amalize masomo yake.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,348
  Trophy Points: 280
  Hivi andunje Ridhiwani ana tubilioni tungapi vile???
   
 7. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #7
  May 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Kikwete akitoka madarakani ni ametoka kimoja..
  kwa hiyo huu ndo muda wake wakujibandikizia
  kwa kupitia familia yake..

  nasisi tunachofanya ni kuongea
  na kukasirika lakini hakuna action yeyote..
  hii itapotelezewa muda si mrefu...
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  May 1, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Sijui huyu Mtikila hizi nyeti huwaga anazitoa wapi tu.
   
 9. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Du.........sumaye, msuya miongoni mwa watu wachache wasafi ktk ccm.......mbona mnatuchanganya, au ndio sumye for 2015,
   
 10. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Ha! ha! ha! ha! ha! ha! haaah!
  Mie simo! Vijana wa CCM Pwani walisema ni zamu yao kula. Wengine mnapaswa ku-shut up!
  Mungu Mkubwa! Sijui kwa nini Dingi yangu hajachangamkia urais enzi za ujanja wake! Bila shaka ningekuwa na utajiri kama huo wa kuingiza malori 100. Ningepewa u-Fisadi Toto kama Ridhiwan hata wananchi msingeniona kwenye siasa.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Usishangae hivyo, nchi hii wenye uchungu nayo ni wengi, ikiwa ni pamoja na walio karibu na Mkulu mwenyewe wanaona kila anachokifanya. Tatizo vyombo vya usalama havina hulka ya kuweka mambo hadharani kama umoja wa wanawake kutoa sri ni dhambi, ila wanaweza tumia nja ambazo zinawalinda.
  Watu walio mashujaa kama Mtikila na Slaa wanamegewa habari hizo, ndo maana unaona wahusika na ufujaji wa mali hawawafungulii mashtaka na wanajua wapi siri zinakovujia na wakithubutu mengi yatavujishwa na vithibitisho.

  Angalia siri za Wikileaks mkulu amefyata mkia kabisa na haongelei cho chote kuhusu hilo na aliyetoa siri anapeta tu. Na kama jamaa ni mwanachama wa umoja wa wanawake anaogopwa kama ukimwi.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,883
  Likes Received: 83,366
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni wale TAKUKURU ambao wanafuata wezi wa kuku tu na kuwabana sana na hupewa vifungo vya mvua nyingi tu, lakini mafisadi wa mabilioni ya EPA, Richmond/Dowans, BoT, Kiwira, Kagoda, Meremeta, rada n.k. hakuna wa kuwagusa wanaendelea kula kuku zao kwa mrija...labda yaliyotokea Tunisia na Egypt yako njiani hapo ndipo watajua kwamba watu wamechoshwa na ufisadi.
   
 13. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mtikila - ni mwendawazimu

  Cleopa Msuya - Tunaomba maelezo ya nini kilichotokea 12/04/XX pale Morogoro (kweli wewe ni msafi)

  Joseph Sinde Warioba - Sina comment - Uwaziri Mkuu wako uliishia kwa Mke! Strange!

  Frederick Sumaye - What are you UP TO?

  Tanzania Daima - Why are you becoming the Voice of "triplets"?

  I feel Like Shooting someone - cold blood!
   
 14. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #14
  May 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Nadhani kuna madharau ya hali ya juu hapa kwetu (TZ)
  wameona hatufanyi kitu tunachofanya ni kuongea tuuu
  ndo maana wanaendelea kufanya wafanyalo..
  Na Kikwete madarakani mmhh imekula kwetu....
  kama wanavyosemaga action speak louder than words ...
  mpaka tuanze kuongea kwa vitendo ndio tutasikika otherwise tunapigia mbuzi debe..
   
 15. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtikila kasign check nyingine toka kwa Rostam,. we subiri wakivurugana Rostam hakawii kulopoka kilichojiri nyuma ya pazia
   
 16. kui

  kui JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 6,478
  Likes Received: 5,146
  Trophy Points: 280
  Hii sasa ni kufuru, 100 whaat? and these are just some of his bussinesses we know, what bout those we don't know? yaani Tz kuna watoto wa shule bado wanakaa chini na kuandikia miguuni na kisha they're not even sure if they're going to have anything to eat when they go back home, and what are these tyrants doing??!!!

  This's when I really, really miss Mwalimu!
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  May 1, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Cuzoooooooo...what up? don't be a stranger
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,883
  Likes Received: 83,366
  Trophy Points: 280
  Wealth accumulation through corruption

   
 19. m

  mubi JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Ndiyo maana hawataki katiba mpya aaah. Tutashinikiza iwepo katiba mpya yenye manufaa kwa wote, isiyo pendelea upande mmoja tu. Punde itakapopatikana tutawabana watasota kama tunavyosota sasa.
   
 20. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kinachoboa zaidi kuna wajinga fulani wanaendelea kutetea ccm na kuanzisha matawi ya ccm nje ya nchi! Hapo ndipo unaona akili ya watu. Upumbavu na ujinga mwingi umejaa kichwani. Leo hii tunaibiwa LIVE wajinga wanafungua matawi ya ccm nje ya nchi?
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...