Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 30,158
- 41,891
Nakataa kata kata. Si kweli.
Istoshe ukiona unafanya ibada zinazo tafuna watu huo sasa ndio Ushirikina (Satanism) sio Mila na Desturi.
Mila na desturi ni moja ya ibada za kishetani,kwasbb zinahusisha umwagaji damu,kafara( wengi) kupitia wanyama!!
Jambo lolote linakohusisha damu/kafara haijakishi ni damu ya wantama,ni ibada kamili.,tena ya kuabudu miungu wengine,
Ndo maana Mungu anachukizwa.... Soma kutoka 20:5
Ndo maana Yesu alifanyika kafara Ku replace hizo mambo,damu yake inalipa fidia ya hayo,ndo maana watu wanahubiriwa kuacha hizo mambo.(kwa kifupi,out of topic)
mshana jr
Mimi nachojiulizaga hizo kafara huwa zina uhusiano gani na utajiri? yani ni process gani inafanya mtu apate hayo mahela baada ya kumuua ndugu/jamaa yake.
Nimekupata aisee mangi! Hata sisi wachaga tunasemwa vibaya sababu ya bidii yetu na kujinyima.
Kumbe shetani anachagua kabila atiee!
Tatzo unafikiri masharti unapanga ww. Nenda ukapewe masharti magumu, sijui utalia na nani.
Masharti mengine sio kabsa Joh mbaya hakuna kurudi nyuma. Utajuta. Pigana ki halali tu.
We ngoja ukaambiwe mara moja kila mwezi lazma utinduliwe 0713. Unless unataka/unapenda ushenz huo.
Sijaelewa kwanini unaipenda mila ya kichaga ilhali ni sawa na uchawi tuu?
Binafsi nazipenda na kuziheshimu sana mila za wachaga
Hakuna utajiri wa halali na kama upo ngamia atapita kwenye tundu la sindano
Kuna tofauti kubwa kati ya mila na uchawi. Mila za kichagga si uchawi bali ni ibada flan za Miungu ya asili.
Zina madhara kama ukoo wenu una practice alaf we uache. Kama unaacha shikilia imani yako thabiti kama uko nje ndani kwa uroho wa mbege na nyama utapata shida sanaa. Wengi hawajui asili ya nyumba zao ndio maana wanateseka na kila wanachofanya hakifanikiwi.
Mchagga anayejielewa hawezi acha kufanya mila. Not exactly kila mwisho wa mwaka but in any major event of ur life (pia si lazma kuangusha ng'ombe au mbuzi. Unaweza tumia mbege au maziwa kufanyia ibada/sala hyo na majani flan yaitwayo " Masale" au " Isale ". Inategemea)
Kuna Mti wake special (Isale) wa ukoo/familia unaoteshwa kwenye eneo maalum ya nyumba yenu ni hapo ndio mnapo fanyia sala/ibada fupi kabla ya kuchinja au kumwagia mbege/maziwa kiasi flan kwenye Ardhi nyingine mna inywa.
Upo kabisa tena bila kupepesa macho.
'Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa'!
'Dhahabu na fedha ni Mali ya Bwana'
Tena Mungu anasema'mimi no Mungu nikupae utajiri'
Km we huwezi sio wote mkuu
mshana jr tumeona utajiri unaotoka na masharti ya umwagaji damu kama kafara, ukasema kuwa ile roho ya mtu unayoitoa ndiyo itakuwa kama muhuli wa utajiri wako kule kuzimu, je ! msharti ya ubakaji, au kuwaingilia nduguzo, wazazi au vichaaa, wajawazito yanahusiano gani, ebu nijibu niweze unganisha na lile ninalojua.Hapana kaka nikisema hivyo simaanishi zote kuna nyingine sikubaliani nazo
merengo90 hilo nalo ni muhuri unakumbuka bustani ya eden na tunda la mti wa kati? Unakumbuka maangamizi ya sodoma na gomora? Unakumbuka Samson na Delilah? Ukiacha damu muhuri mwingine ni ngonomshana jr tumeona utajiri unaotoka na masharti ya umwagaji damu kama kafara, ukasema kuwa ile roho ya mtu unayoitoa ndiyo itakuwa kama muhuli wa utajiri wako kule kuzimu, je ! msharti ya ubakaji, au kuwaingilia nduguzo, wazazi au vichaaa, wajawazito yanahusiano gani, ebu nijibu niweze unganisha na lile ninalojua.
Sijaelewa kwanini unaipenda mila ya kichaga ilhali ni sawa na uchawi tuu?
Kuna mmoja nikikua naambiwa ukiingia dukani kwake anakuona upo uchi nikabisha nikaenda na mazivu yangu nikanunua vitu wakati nataka kuondoka akanipatia nyongeza ya kiwembe nilibaki tu nashangaa.
Halafu akienda mdada yupo period anahudumiwa na Mke wake tu..usichezee mkinga na watu wanapanga foleni dukani kwake
Kwa uchunguzi wangu nimegundua kuwa watu wengi wenye hela/matajiri utajiri wao sio wa halali au wa kutoka jwa Mungu. Haijalishi awe ni mfanyabiashara au mfanyakazi wengi huwa wanakitu nyuma ambacho kinawapa huo utajiri kupitia hizo kazi au biashara wanazofanya.
ukianzia kwa wafanyabiashara, hawa ndo wanaongoza kwa sababu mwanzoni wakati unaanza biashara utapata faida kidogo basi na mtaji utakua taratibu nao. itafikia mahali utaona mtaji hauongezeki wala faida haikui sanasana unaanza kushuka. Hapo manaake uwezo wako wa kibinadamu umeishia hapo na hapo ndo huwa crossrod kwa wafanyabiashara wengi ambapo ili kusogea mbele au kupga hatua inabid uchagua moja kati ya Mungu au shetani. Wengi sana sana sana huchagua njia ya shetan kwa sababu huwa ni rahisi kwa macho hivyo huanza kwenda kwa waganga na wengne kujiunga na vikundi vya kishetan kulingana na ukubwa wa biashara yako na mahitaji yako. kumbuka haimaanishi kuwa ukijiunga huku ndo unaacha kufanya juhud, hapana.. juhud inaendelea pale pale sema unakua na busta ya kukunyanyua juu kwa spid ya ajabu. Unaweza ukatangaza kidogo watu wakajaa telee na kadhalika.
Kwa upande wa wafanyakazi, huku ndo kule ambapo wengi huwa wanalogana wao kwa wao kugombania cheo kazini. Kiuhalisia ukiachana na hii hali ambayo tunaiona kwa macho kuwa flani ni mtendaji kazi mzuri, huwa kuna nguvu nyuma inayobadilisha mwonekano wako mbele ya macho ya watu kiasi kwamba kila mtu anakua anatambua mchango wako kwa namna ya ajabu. Wafanyakazi wengi huwa wanalogezea kwa namna hii ili waonekane bora kuzid wenzao na huwa wanaendelea kufanya kazi vizuri tu. Hata wakati wa kuomba kazi, sio kila mtu hua anapata kazi kiuhalali. Wengi huwa wanaenda kwa waganga kupata mvuto ili wachaguliwe. Mara nyingi wafanyakazi hujificha wasionekane kama wanatumia mambo ya kishirikina kuliko wafanyabiashara. Taasisi nyingi za serikali na binafsi huwa unakuta mtu flan anakufa gafla , kumbe kashaangushwa na mwenzaje anayetaka hicho cheo. Kusoma au kuwa na PHD hakuusiani kivyovyote na iman ya kishirikina kwa maana hata maprofesa ni wachawi na vitu hvo viko katika pande mbili ambazo haziingiliani yaan mchana profesa usiku mchawi. Hivyo usijidanganye kuwa unapomuona mfanyakaz mwenzako pale ofisin ukajua ni elimu ndo imempa kile cheo. Mara nyingi hua ni hapana japaokua wapo wachache tena wachache sana wanaopata kwa style hiyo. ila wafanyakzi ni wanafiki sana na huwa wanakataa kukiri kuwa wengi wao wanatumia ushirikina kulinda kazi zao.
Mwisho nataka kusema kuwa Mali na fedha vyote hutoka kwa Bwana.. mtafute Bwana na vyote vitakuja maana ni vya ziada tuu!!!