Huu ujinga ndiyo unafanya muendelee kuwa maskini..we endelea kuimba masharti masharti wenzako wanatoboa!!
acha kulisha watu ujinga wewe!!
That's all you can say...!!! Watu wa aina yako hawakosekani popote pinga kwa hoja tuone kama utaweza
Naona wasengenyaji mko kwenye kikao....hii dhana ni kazi sana kuiprove,inafanya watu wawe wavivu
Haya yote ni maneno ya mkosaji
Kiyoya hili jambo la kutafuta utajiri wa haraka limeitafuna jamii vibaya sana asilimia kubwa sana ya wafanyabiashara wanafanya haya mamboNajua kuna msalaba na tasbihi sasa huku kuvaa Mabangili,mapete makubwa sometimes mikono yote tena yenye tochi,namba 1111111(chale) ya nini kama sio ushirikina
boss hiyo ni imani yako tu.
wakinga wanatafuta hela mahali popote na wanaishi maisha ya kujibana ndio maana wanakuwa na mali pale wanapozipata.
matumizi mabaya ya kile kidogo unachopata yanakufanya usifanikiwe hata kidogo.
mkinga asubuhi anakunywa chai nyumbani, mchana analetewa chakula kutoka nyumbani, jioni anaenda kula nyumbani kwa nini asiwe na hela?
dukani kwake yupo yeye na mkewe ndio wauzaji akiweka msaidizi basi ni ndugu yake.
kwani wangapi wameenda kwa waganga na bado biashara zikagoma/kuanguka?
siku zote hata kwa anayetegemea mshahara, matumizi mazuri ya anachopata ndio mafanikio yake.
sio mtu kila siku asubuhi anaamkia supu ya kuku, mchana nyama choma na jioni kitimoto na bia juu.
huyu hawezi kufanikiwa.
Utajiri ni mmoja tu ndugu,hakuna wa ushirikina wala wa nini...umeshafatilia maaharti mengine wanayopewa hao watafuta utajiri kwa waganga,mwisho utakuta masharti hayo yanawarudisha kulekule kwenye kufanya kazi kwa bidii na si kwenda kulala miguu juu kusubiri hela zitoke hewani...waganga ni wajanja..hutakiwi kuamini wanachosema hata waseme wangapi