Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi

Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi

Utajiri ni ile hali ya kumiliki mapesa mengi na kuwa na mali nyingi, utajiri ni mzuri kwa kuwa unakupa uwezo nguvu mamlaka sifa na umaarufu!kwa kifupi Utajiri ni kitu chema.

Watu wengi hutafuta utajiri kwa njia mbalimbali halali na haramu wao wanachotaka ni utajiri ili waweze kutimiza ndoto zao nyingi.

Sasa kuna wakati mtu hutafuta utajiri kwa njia za mkato hapa nazungumzia kwa njia za ushirikina na uchawi.

Utajiri huu ni mzuri na huja haraka lakini ukiwa na masharti mengi lakini kubwa likiwa ni kutoa kafara la damu kwa kuangamiza roho.

Unapoingia kwenye utajiri huu mwanzoni utafurahia na masharti utayaona mepesi lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda mambo hubadilika na tabu huanzia hapo.

Mwanzoni utaambiwa toa kafara la damu ya kuku baadae itakuja mbuzi, halafu itafuatia ng'ombe na mwishowe itakuja binadamu mmoja na hatimaye kwa makundi.

Hii yote ni kutaka kulinda utajiri wako usiporomoke na ukivunja masharti kila kitu kinaharibika .

Kuna pia masharti ya kujisaidia kulala kula kuvaa na hata matumizi ya vitu mbalimbali. Mwanzoni inakuwa ni rahisi tu kwenda sambamba nayo lakini mbeleni mambo hubadilika hasa pale watu wanapoanza kuhoji hiki au kile.

Wote tunajua jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi inavyoteketea kutokana na waganga wa kienyeji kuwaaminisha wateja wao kuwa viungo hivyo vikichanganywa na dawa nyingine huleta utajiri bahati nguvu na uwezo! Kuna zaidi ya waganga 300 kwenye mahabusu na Magereza mbalimbali wenye kesi zinazowahusisha na mauaji ya albino.

Jamani utajiri wa masharti ya namna hii haufai na mwishowe huwa na anguko kuu tunashuhudia visa vya kila aina kuhusiana na utajiri wa namna hii lakini kila uchao watu hawakomi kuendelea kuutafuta.

Hakika dunia inaumwa.

Wewe binafsi unao utajiri huo (unaodai wa kishirikina)?
 
Kwa uchunguzi wangu nimegundua kuwa watu wengi wenye hela/matajiri utajiri wao sio wa halali au wa kutoka jwa Mungu. Haijalishi awe ni mfanyabiashara au mfanyakazi wengi huwa wanakitu nyuma ambacho kinawapa huo utajiri kupitia hizo kazi au biashara wanazofanya.
ukianzia kwa wafanyabiashara, hawa ndo wanaongoza kwa sababu mwanzoni wakati unaanza biashara utapata faida kidogo basi na mtaji utakua taratibu nao. itafikia mahali utaona mtaji hauongezeki wala faida haikui sanasana unaanza kushuka. Hapo manaake uwezo wako wa kibinadamu umeishia hapo na hapo ndo huwa crossrod kwa wafanyabiashara wengi ambapo ili kusogea mbele au kupga hatua inabid uchagua moja kati ya Mungu au shetani. Wengi sana sana sana huchagua njia ya shetan kwa sababu huwa ni rahisi kwa macho hivyo huanza kwenda kwa waganga na wengne kujiunga na vikundi vya kishetan kulingana na ukubwa wa biashara yako na mahitaji yako. kumbuka haimaanishi kuwa ukijiunga huku ndo unaacha kufanya juhud, hapana.. juhud inaendelea pale pale sema unakua na busta ya kukunyanyua juu kwa spid ya ajabu. Unaweza ukatangaza kidogo watu wakajaa telee na kadhalika.
Kwa upande wa wafanyakazi, huku ndo kule ambapo wengi huwa wanalogana wao kwa wao kugombania cheo kazini. Kiuhalisia ukiachana na hii hali ambayo tunaiona kwa macho kuwa flani ni mtendaji kazi mzuri, huwa kuna nguvu nyuma inayobadilisha mwonekano wako mbele ya macho ya watu kiasi kwamba kila mtu anakua anatambua mchango wako kwa namna ya ajabu. Wafanyakazi wengi huwa wanalogezea kwa namna hii ili waonekane bora kuzid wenzao na huwa wanaendelea kufanya kazi vizuri tu. Hata wakati wa kuomba kazi, sio kila mtu hua anapata kazi kiuhalali. Wengi huwa wanaenda kwa waganga kupata mvuto ili wachaguliwe. Mara nyingi wafanyakazi hujificha wasionekane kama wanatumia mambo ya kishirikina kuliko wafanyabiashara. Taasisi nyingi za serikali na binafsi huwa unakuta mtu flan anakufa gafla , kumbe kashaangushwa na mwenzaje anayetaka hicho cheo. Kusoma au kuwa na PHD hakuusiani kivyovyote na iman ya kishirikina kwa maana hata maprofesa ni wachawi na vitu hvo viko katika pande mbili ambazo haziingiliani yaan mchana profesa usiku mchawi. Hivyo usijidanganye kuwa unapomuona mfanyakaz mwenzako pale ofisin ukajua ni elimu ndo imempa kile cheo. Mara nyingi hua ni hapana japaokua wapo wachache tena wachache sana wanaopata kwa style hiyo. ila wafanyakzi ni wanafiki sana na huwa wanakataa kukiri kuwa wengi wao wanatumia ushirikina kulinda kazi zao.

Mwisho nataka kusema kuwa Mali na fedha vyote hutoka kwa Bwana.. mtafute Bwana na vyote vitakuja maana ni vya ziada tuu!!!
 
SISI wakinga hatutumii uchawi bali maarifa tu. Kwanza utakubaliana na mimi kwamba wakinga ni wachapa kazi, hili halina ubishi it is there for all to see.
Wakinga sio wahongaji, wakinga hawavai nguo za bei mbaya, hawanunui magari ya kutanulia, hawanywi pombe za matanuzi, hawali nyama, wakisafiri hawali njiani maana kuna ule mkate wao wa kikinga ambao husafiri nao, kanisani wanatoa kiasi kidogo tu. Kwanini wasilimbikize mali ? Hutegemei kuona tajiri mbondei kwasababu tabia zao ni kinyume kabisa na za wakinga. Kama kuna mtu alishawahi kuona tajiri wa kibondei aingie pm nimtumie vocha anipigie.

kama hawaendeshi magari,hawali nyama,hawavai vizuri,hawendi vacation,hawa enjoy .hiyo pesa haina maana.mi nawaona ni masikini.siyo matajiri. Tajiri unaogopa kula nyama? Ha ha ha h..
 
Mamantilie ndio wanatulisha uchafu mwingi sana anadanganywa na mganga wake kuwa ukitaka uvute wateja wengi pikia chakula maji uliyoogea bila sabuni, basi utakuta mama na mdishi mkubwa wa maji hadi bafuni akifika huko atajitumbukiza mzimamzima na kujisugua na kujifyokonyoa mpaka kwenye naniliu halafu akitoka hapo maji yale machafu na uchafu wote ule ndio atayatumia kupikia vyakula na utakuta watu wamepanga msururu kwenye chakula chake wakikisifia kuwa ni kitamu sana HERI WANGEJUA
Teh teh teh mbavu zangu...eti kujifyokonyoa naniliu haa haa JF!
 
Kwani naomba kuuliza hivi uhusiano wa pesa na hivyo vitu ni UPI?
Yaani kifo cha kiumbe hai na mie kuwa tajiri ni process gani inafanyika?
 
Mamantilie ndio wanatulisha uchafu mwingi sana anadanganywa na mganga wake kuwa ukitaka uvute wateja wengi pikia chakula maji uliyoogea bila sabuni, basi utakuta mama na mdishi mkubwa wa maji hadi bafuni akifika huko atajitumbukiza mzimamzima na kujisugua na kujifyokonyoa mpaka kwenye naniliu halafu akitoka hapo maji yale machafu na uchafu wote ule ndio atayatumia kupikia vyakula na utakuta watu wamepanga msururu kwenye chakula chake wakikisifia kuwa ni kitamu sana HERI WANGEJUA

Nimehisi kutapika (kinyaa kikuu) ......Daaaah

Mwanzo na mwisho kula kwenye migahawa uchwara. Lol
 
Kuna vitu huwa vinafanyika mpaka mtu kuwa tajiri ndio mana unaambiwa utoe kafara ya damu unapokwenda kwa mganga japo kuna utajiri mwingine unaweza kuupata bila kutoa damu ila nao huitaji ujasiri wa hari ya juu
 
Mkuu huyu hawajui wakinga anawasikia,atuulize tuliokua nao na kuishi nao

Kuna mmoja nikikua naambiwa ukiingia dukani kwake anakuona upo uchi nikabisha nikaenda na mazivu yangu nikanunua vitu wakati nataka kuondoka akanipatia nyongeza ya kiwembe nilibaki tu nashangaa.
Halafu akienda mdada yupo period anahudumiwa na Mke wake tu..usichezee mkinga na watu wanapanga foleni dukani kwake
 
tang'ana;
Sijui ni mimi tu sikukuelewa. Huamini nini katika uchawi? Huamini kuwa kuna uchawi au huamini kutajirika kiuchawi? Vyote hivyo vipo kwani hata vitabu vitakatifu vimeandika habari za uchawi na wachawi.
Pia usiache kuamini kuwa kuna mali zinapatikana kiuchawi ila tatizo lake ni kuwa, mali zile ni za mda mfupi nazo hupotea na kukuacha katika aibu kuu.
Mali za kichawi hazirizishwi mtu mwingine. Ukifa na kila kitu chafa na weye. Kafara hutolewa kila siku, kama bungeni ndo usiombe. Watu waliwahi kwenda kuweka vitu mle kiasi kwamba hata cct camera zile hazikumshika jamaa akiwa kazini. Si wakumbuka enzi za Mh. Six??? Uchawi upo, na wachawi wapo ila they live for a short tyme na hizo raha zao.
Utajiri wa kweli hauji kwa kujinyima wala kwa uchawi ila kwa kukaa sawa sawa na mapenzi ya Mungu akubariki kwani ametuahidia baraka.
Wapo watu tunawajua, hawaruhusiwi kuvaa suruali, viatu, kulala kwenye nyumba zao ikifika saa 12 jioni ni mwisho wake kuingia ndani ya nyumba aliyoijenga. Kuna mwingine jirani yetu tu hapa, saa 11 alfajiri, lazima akanye njia panda kila siku. Mateso gani haya jamani??
Tafuta kwa njia nzuri na utatajirika tuuu. Mungu anipe utoshelevu na amani vyanitosha

Kuna watu wananishangaza sanaaa eti wanakuambia wana muamini Mungu yet hawatambui uwepo wa shetani (uchawi). Ni unafiki tu. Wakati misahafu ina muelezea Ibilisi in and out.

Ndio maana hata kwenye hesabu kuna hasi na chanya.

Mtu yeyote aliyeishika dini vilivyo ana uelewa wa shetani na uchafu wake wote. Unatatua vp tatzo (nguvu za giza) kama huelewi zinavyo function ?? Otherwise utakubaliana na mada ya mshana jr fika. Tusifanyane watoto humu.
 
Last edited by a moderator:
zipompa

Thank you.
Nilikua mbishi sanaaa mpaka nlivyo shuhudia Moshi huko kwa macho yangu ni shida ndugu.

There are lots of things going on in the spiritual world. Mila za kichagga ni very powerful na ukifanya masihara wataanguka watu utashangaa na macho yako kama sio kudhurika.

Yupo Aunty yangu flan alitoka nnje ya ndoa akashika mimba nnje na mtu mwingine akamdanganya mmewe ni yake. Yule mtoto wa nnje alivyozaliwa kwenye ile nyumba yao. Kulitokea balaa.

Watoto wengine wa ile nyumba ilikua full kuumwa, hospital ugonjwa hauonekani vitimbi kibao, watu wametoa pesa kibao kutibia. Babu yetu wa ukoo akabutuka akasema ile mimba sio ya nyumba yetu (ukoo wetu) ndio maana.

Mwanamke kubanwa akakubali cz watoto wale wengine wangeweza dhurika kwa kiasi kikubwa. Ikafanywa mila kile kichanga kikarudishwa kimila kwenye ukoo wao (baba yake). Watoto siku mbili nyingi wakapona wote.

Kuna makabila haya dhulumiwi watajua tu, kuweni makini mnapo oa / kuolewa.
 
Last edited by a moderator:
Mamantilie ndio wanatulisha uchafu mwingi sana anadanganywa na mganga wake kuwa ukitaka uvute wateja wengi pikia chakula maji uliyoogea bila sabuni, basi utakuta mama na mdishi mkubwa wa maji hadi bafuni akifika huko atajitumbukiza mzimamzima na kujisugua na kujifyokonyoa mpaka kwenye naniliu halafu akitoka hapo maji yale machafu na uchafu wote ule ndio atayatumia kupikia vyakula na utakuta watu wamepanga msururu kwenye chakula chake wakikisifia kuwa ni kitamu sana HERI WANGEJUA

Hilo ni kweli kabisa hawa mama ntilie ni noma kuna huyo mmama yeye Yale maji ya kutawaza kila asubuhi au mkojo wana changanya kwenye msosi au ile ya ble.... Ana chaganya kwenye misosi yake.Mteja akila una shangaa tumbo linamsumbua kila Mara plasi na aliyonenea inakua mkosi mtupu. Cha msingi before eating mtu asali kwa imani yake.
 
Na kwenye haya masharti kuna
-ya kulala na mamaako/babaako/mwanao
-kulala na mtoto mdogo/mchanga.ndio maana kuna habari nyingi sana za watu kubaka vitoto vidogo kabisa tena vingine vya miezi tuu

Hyo ya kulala na mzazi inatumiwa sana hadi na wasanii wakubwa wa kibongo aisee ushirikina ni hatari sana kwa kweli. Ubaya vitu vya kishetani havidumu kabisa hata utimize masharti lazma siku viku geuke wewe.
Kuna baba mmoja alienda kwa mganga kusaka utajiri mganga akaangalia nyota ya wana ukoo akamwambia mtoe ndugu flani na flani na mwanawe akawa tahira. Yeye huyo baba akamuua ndugu yake kwa siri watu wakajua kapotea.
Huyo baba alikua tajiri wa kutisha mijumba magari siku kakosea masharti vyote vilipotea kuanzia magari kuungua nyumba utajiri wote ukawa kwishney. Nowadays kafulia hatari.
Ushirikina ni mbovu siku kikibuma unaumia na ndugu umewapoteza.
 
Senior Boss mila za kichaga usipofata ka ni ukoo lazma uangamie bila kupenda watu kuenda kinyume na miiko ya kikoo na familia bora hyo kuliko kutoa mikafara.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom