analysti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 731
- 615
Utajiri ni ile hali ya kumiliki mapesa mengi na kuwa na mali nyingi, utajiri ni mzuri kwa kuwa unakupa uwezo nguvu mamlaka sifa na umaarufu!kwa kifupi Utajiri ni kitu chema.
Watu wengi hutafuta utajiri kwa njia mbalimbali halali na haramu wao wanachotaka ni utajiri ili waweze kutimiza ndoto zao nyingi.
Sasa kuna wakati mtu hutafuta utajiri kwa njia za mkato hapa nazungumzia kwa njia za ushirikina na uchawi.
Utajiri huu ni mzuri na huja haraka lakini ukiwa na masharti mengi lakini kubwa likiwa ni kutoa kafara la damu kwa kuangamiza roho.
Unapoingia kwenye utajiri huu mwanzoni utafurahia na masharti utayaona mepesi lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda mambo hubadilika na tabu huanzia hapo.
Mwanzoni utaambiwa toa kafara la damu ya kuku baadae itakuja mbuzi, halafu itafuatia ng'ombe na mwishowe itakuja binadamu mmoja na hatimaye kwa makundi.
Hii yote ni kutaka kulinda utajiri wako usiporomoke na ukivunja masharti kila kitu kinaharibika .
Kuna pia masharti ya kujisaidia kulala kula kuvaa na hata matumizi ya vitu mbalimbali. Mwanzoni inakuwa ni rahisi tu kwenda sambamba nayo lakini mbeleni mambo hubadilika hasa pale watu wanapoanza kuhoji hiki au kile.
Wote tunajua jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi inavyoteketea kutokana na waganga wa kienyeji kuwaaminisha wateja wao kuwa viungo hivyo vikichanganywa na dawa nyingine huleta utajiri bahati nguvu na uwezo! Kuna zaidi ya waganga 300 kwenye mahabusu na Magereza mbalimbali wenye kesi zinazowahusisha na mauaji ya albino.
Jamani utajiri wa masharti ya namna hii haufai na mwishowe huwa na anguko kuu tunashuhudia visa vya kila aina kuhusiana na utajiri wa namna hii lakini kila uchao watu hawakomi kuendelea kuutafuta.
Hakika dunia inaumwa.
Mimi hii post naiangalia kwa mtazamo hasi kwakuwa mantiki yake ni kutuaminisha kuwa ni kweli utajiri wa ushirikina upo ila una masharti magumu. Katika kipindi hiki ambacho tuna pambana na imani POTOFU kwamba kumuua albino kunaleta utajiri au bahati, si kipindi cha kuwaeleza watu kuwa ukimuua albino utatajirika isipokuwa masharti yatakuwa magumu zaidi baadae.
Imani hizi huitwa POTOFU kwakuwa si kweli kwamba kumuua albino kutakufanya ufanikiwe ktk mipango yako.
Ndugu mshana, huoni kwamba post yako yaweza kuwahamasisha watu kutafuta utajiri kwa masharti yawayo yoyote yale ilhali si kweli.
Ndugu mshana hujagundua kuwa makabila au jamii zinazosifika kwa utajiri , nyingi husifika kwa ubahili pia???
Angalia WACHAGGA, WAKINGA, WAPARE....Makabila haya yanasifika kwa kufanikiwa ktk biashara, lakini pia yanasifika sana kwa Ubahili.
Ningependa kuwafahamisha wana JF ya kwamba, Hakuna kitu kinaitwa Utajiri wa ushirikina wenye masharti magumu, ila ili uwe tajiri lazima uzingatie "MASHARTI YA UJASILIAMALI" ambayo kimsingi ndiyo huitwa masharti ya kishirikina.
Nakuhakikishia ndugu Mwana JF, Fanya kazi kwa bidii, kuwa mbunifu, usiwe arrogant, fanya matumizi yale ya muhimu tu, epuka anasa, hakika utafanikiwa bila hata kuongeza kiungo cha albino au kumuua mtoto wako.
Acha kuua ndugu, acha kuua mtoto, acha kuua ALBINO. zingatia masharti ya Ujasiliamali, na utafanikiwa.