ukikaidi utapigwa2
JF-Expert Member
- Feb 24, 2015
- 16,286
- 31,675
boss hiyo ni imani yako tu.
wakinga wanatafuta hela mahali popote na wanaishi maisha ya kujibana ndio maana wanakuwa na mali pale wanapozipata.
matumizi mabaya ya kile kidogo unachopata yanakufanya usifanikiwe hata kidogo.
mkinga asubuhi anakunywa chai nyumbani, mchana analetewa chakula kutoka nyumbani, jioni anaenda kula nyumbani kwa nini asiwe na hela?
dukani kwake yupo yeye na mkewe ndio wauzaji akiweka msaidizi basi ni ndugu yake.
kwani wangapi wameenda kwa waganga na bado biashara zikagoma/kuanguka?
siku zote hata kwa anayetegemea mshahara, matumizi mazuri ya anachopata ndio mafanikio yake.
sio mtu kila siku asubuhi anaamkia supu ya kuku, mchana nyama choma na jioni kitimoto na bia juu.
huyu hawezi kufanikiwa.
mkuu umenigusa